Polisi wanaamini kwamba Robin amejiua akiwa nyumbani kwake mjini California.
Maelezo ya picha, Simanzi limetanda nchini Marekani kufuatia kifo cha muigizaji Nguli Robbin Williams
Maelezo ya picha, Salamu za rambi rambi zimeendelea kumiminika kufuatia kifo cha Williams, ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka sitini na sita.
Maelezo ya picha, Polisi wanaamini kwamba Robin amejiua yeye mwenyewe akiwa nyumbani kwake katika mji wa Carlifonia.
Maelezo ya picha, Gwiji wa utengenezaji filamu Steven Spielberg amefafanua kwamba Williams alikua na kipaji cha namna ya kipekee katika sanaa ya uchekeshaji na alikua ni muigizaji maarufu sana .
Maelezo ya picha, Naye Rais wa Marekani Barack Obama alimuelezea Williams kwamba katika uchekeshaji wake alikua akigusa maisha ya watu.
Maelezo ya picha, Robin Williams katika uhai wake alikua maarufu sana na mcheshi katika kipindi cha runinga kilichojulikana kama 'Mork and Mindy' kabla hajageukia katika tasnia ya filamu kama ya Good Morning Vietnam na pia alikua ni mshairi na mashairi yake yalikua ya kuvunja mbavu.