Marais wa Afrika walivyojikwatua Marekani

Rais Barack Obama aliwaandalia marais wa Afrika dhifa ya jioni na picha hizi ni dhihirisho ya kilichojiri

Wajumbe wamekusanyika katika kongamano la viongozi wa Afrika mjini DC kwa mkutano mkubwa wa aina yake kuwahi kufanyika nchini humo. Mkutano wa kwanza ulikuwa kati ya Rais waziri wa mambo ya nje John Kerry na Rais Joseph Kabila. Mkutano wenyewe unakamilika Alhamisi
Maelezo ya picha, Wajumbe wamekusanyika katika kongamano la viongozi wa Afrika mjini DC kwa mkutano mkubwa wa aina yake kuwahi kufanyika nchini humo. Mkutano wa kwanza ulikuwa kati ya Rais waziri wa mambo ya nje John Kerry na Rais Joseph Kabila. Mkutano wenyewe unakamilika Alhamisi
Mkutano huo unalenga kuimarisha uhusiano kati ya Afrika na Marekani ili kuongeza nafasi za uwekezaji
Maelezo ya picha, Mkutano huo unalenga kuimarisha uhusiano kati ya Afrika na Marekani ili kuongeza nafasi za uwekezaji
Makampuni ya Marekani yameahidi kutoa dola bilioni 14 za uwekezaji barani Afrika katika sekta za kawi na miundo mbinu. Hii ni kauli ya Rais Barack Obama
Maelezo ya picha, Makampuni ya Marekani yameahidi kutoa dola bilioni 14 za uwekezaji barani Afrika katika sekta za kawi na miundo mbinu. Hii ni kauli ya Rais Barack Obama
Rais Obama, pia aliwaandalia dhifa ya jioni viongozi hao katika Ikulu ya White house
Maelezo ya picha, Rais Obama, pia aliwaandalia dhifa ya jioni viongozi hao katika Ikulu ya White house
Rais wa Cameroon Paul Biya na mkewe Chantal walikuwa miongoni mwa wageni waalikwa
Maelezo ya picha, Rais wa Cameroon Paul Biya na mkewe Chantal walikuwa miongoni mwa wageni waalikwa
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir aliwapungua mkono waliokuwa wamefika katika hafla hiyo katika White house
Maelezo ya picha, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir aliwapungua mkono waliokuwa wamefika katika hafla hiyo katika White house
Rais wa Gambia Yahya A.J.J Jammeh, pia aliwaamkua wandishi wa habari waliofika alipowasili katika White House na mkewe Zineb Jammeh
Maelezo ya picha, Rais wa Gambia Yahya A.J.J Jammeh, pia aliwaamkua wandishi wa habari waliofika alipowasili katika White House na mkewe Zineb Jammeh
Rais wa Ghana John Mahama alizungumzia swala la kupanua miradi ya kawi katika mkutano wa awali. Bwana Mahama alihudhuria dhifa hiyo na mkewe Lordina Dramani Mahama.
Maelezo ya picha, Rais wa Ghana John Mahama alizungumzia swala la kupanua miradi ya kawi katika mkutano wa awali. Bwana Mahama alihudhuria dhifa hiyo na mkewe Lordina Dramani Mahama.
Wageni hatimaye waliandaliwa sehemu maalum ya maankuli hayo baada ya siku iliyojaa shughuli si haba
Maelezo ya picha, Wageni hatimaye waliandaliwa sehemu maalum ya maankuli hayo baada ya siku iliyojaa shughuli si haba
Mkewe Rais Obama , Michelle Obama alimsaidia mumewe kuwaandalia wageni. Hapa anawachangamkia wageni wake akiwemo mwenyekiti wa tume ya Afrika Nkosazana Dlamini Zuma.
Maelezo ya picha, Mkewe Rais Obama , Michelle Obama alimsaidia mumewe kuwaandalia wageni. Hapa anawachangamkia wageni wake akiwemo mwenyekiti wa tume ya Afrika Nkosazana Dlamini Zuma.
Muimbaji Lionel Richie ndiye aliwatumbuiza wageni
Maelezo ya picha, Muimbaji Lionel Richie ndiye aliwatumbuiza wageni