Milipuko huku wanajeshi wa Uganda wakipambana na wanamgambo nchini Somalia

Kundi la Al-Shabab linasema limewaua makumi ya wanajeshi lakini madai hayo hayajathibitishwa.

Moja kwa moja

  1. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu kwa leo

  2. Papa Francis aondoka katika hadhira ya Ijumaa kwa homa

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Papa Francis amejiondoa katika hadhira yake ya Ijumaa baada ya kuugua homa, msemaji wa Vatican amesema.

    Matteo Bruni aliwaambia waandishi wa habari kuwa kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki anajisikia vibaya. Hata hivyo, hakutoa maelezo zaidi.

    Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 86 amekumbwa na matatizo mengi ya kiafya katika miaka ya hivi karibuni.

    Mnamo Aprili, alikaa siku kadhaa hospitalini baada ya kuugua maambukizi ya njia ya kupumua

    "Kutokana na homa, Papa Francis hakujitokeza mbele ya hadhira asubuhi ya leo," Bw Bruni alisema akijibu swali la mwandishi wa habari. Haikuwa wazi kama Papa atahudhuria hadhira ya faragha siku ya Jumamosi.

  3. Urusi inapeleka silaha za nyuklia nchini Belarus

    Urusi siku ya Alhamisi ilianza mpango wa kupeleka silaha za kinyuklia huko Belarus, ambaye kiongozi wake alisema vichwa vya kivita vya nyuklia tayari viko kwenye harakati, katika uwekaji wa kwanza wa mabomu kama hayo kwa Kremlin nje ya Urusi tangu kuanguka kwa Umoja wa Soviet mnamo 1991.

    Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilishutumu mpango huo wa kupeleka silaha hizo, lakini ilisema kuwa Washington haina nia ya kubadilisha msimamo wake kuhusu silaha za kimkakati za nyuklia au kuona dalili zozote kwamba Urusi inajiandaa kutumia silaha za nyuklia.

    Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema Marekani na washirika wake wanapigana vita vya wakala vinavyozidi kupanuka dhidi ya Urusi baada ya mkuu wa Kremlin kutuma wanajeshi nchini Ukraine miezi 15 iliyopita.

    Mpango wa uwekaji nyuklia ulitangazwa na Putin katika mahojiano na televisheni ya serikali mnamo Machi 25.

    "Magharibi ya pamoja kimsingi yanaendesha vita ambavyo havijatangazwa dhidi ya nchi zetu," waziri wa ulinzi wa Putin, Sergei Shoigu, alisema katika mkutano na mwenzake wa Belarus mjini Minsk, kulingana na wizara ya ulinzi ya Urusi.

    Rais wa Belarus Alexander Lukasjenko alisema kuwa silaha za kimkakati za nyuklia tayari ziko kwenye harakati kulingana na agizo lililotiwa saini na Putin, ingawa hakukuwa na uthibitisho wa hilo kutoka kwa Kremlin yenyewe.

    "Harakati za silaha za nyuklia tayari zimeanza," Lukashenko aliwaambia waandishi wa habari huko Moscow, ambapo alikuwa akihudhuria mazungumzo na viongozi wengine wa mataifa ya zamani ya Soviet.

  4. Rwanda: Jinsi mtoro mmoja kati ya wanaosakwa kwa mauaji ya halaiki alivyopatikana amejificha Cape Town

    .

    Chanzo cha picha, Hawks (South Africa)

    "Ilikuwa operesheni kubwa na ya muda mrefu" msemaji wa polisi Brigedia Thandi Mbambo anaiambia BBC, kuhusu kukamatwa kwa mtoro wa kwanza kati ya wanne waliokuwa wakisakwa zaidi nchini Rwanda kwa mauaji ya halaiki mwaka 1994 siku ya Jumatano.

    Fulgence Kayishema, 61, "ametumia vitambulisho vingi vya uongo, na wakati wa kukamatwa kwake alipatikana akijiita Donatien Nibashumba", Brig Mbambo anasema.

    Alikuwa akitafutwa kwa madai ya kuhusika moja kwa moja na mauaji ya Watutsi zaidi ya 2,000 katika kanisa katoliki na kutumia tingatinga kuangusha kanisa hilo na kuwazika ndani baadhi ya watu baada ya juhudi za kuliteketeza kanisa hilo huku watu wakiwa ndani kushindikana.

    Kasisi wa kanisa hilo likiwa na watu, Athanase Seromba, alihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka wa 2008.

    Kayishema mwendesha mashtaka wa zamani wa eneo hilo magharibi mwa Rwanda, "alikuwa akifanya kazi kama kibarua katika shamba kubwa" huko Paarl karibu kilomita 60 magharibi mwa Cape Town.

    "Wakati anakamatwa, alikuwa anakaa peke yake, familia yake iko Cape Town, kuna mambo fulani ambayo yatachunguzwa, lakini alikuwa anakaa peke yake shambani." Brig Mbambo alisema.

    Vyama vya manusura wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda vimeelezea kuridhishwa na kukamatwa kwa Kayishema na kutaka haki ichukue mkondo wake.

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kukamatwa kwa Kayishema "kunatuma ujumbe mzito kwamba wale wanaodaiwa kufanya uhalifu huo hawawezi kukwepa haki".

    Polisi wa Afrika Kusini waliongoza uchunguzi na operesheni iliyoanza mwaka 2022 iliyohusisha polisi na mamlaka kutoka Canada, Eswatini, Msumbiji, Rwanda, Marekani na Uingereza ili kumpata mshukiwa.

    "Vyombo vyote hivyo vililazimika kuchukua jukumu la kujumuisha taarifa zote pamoja hadi hatimaye wakawa na uhakika wa 100% kuwa huyu ndiye mtu wanayemtafuta" Brig Mbambo anasema.

    Anaongeza kuwa mshukiwa alifanikiwa kuja na kukaa Afrika Kusini kwa kutumia vitambulisho bandia na "kuishi maisha ya utulivu sana shambani, akijaribu kuhakikisha kuwa hakuna anayemjua yeye ni nani."

    Siku ya Ijumaa, Bw Kayishema anatarajiwa kufikishwa mahakamani mjini Cape Town kuhusu sheria za uhamiaji na ilani ya Interpol akisubiri kupelekwa Rwanda, polisi walisema kwenye tovuti yake.

    Soma zaidi:

  5. ‘Mackenzie alitumia genge lililojihami kwa silaha kuwaua waumini waliochukua muda mrefu kuaga dunia’ - Waziri

    .

    Chanzo cha picha, You Tube

    Maelezo ya picha, Paul Mackenzie

    Kiongozi wa wa kanisa la kufunga hadi kufa huko Kilifi Paul Mackenzie alitumia genge lililomiliki vifaa butu kuwaua baadhi ya waumini waliochukua muda mrefu kufa na wale waliobadilisha mawazo yao wakati wa kufunga , alisema Waziri wa masuala ya ndani nchini Kenya Kindiki Kithure.

    Kiongozi huyo anasema magenge hayo yaliomiliki silaha yalijenga vibanda karibu na makaburi ya waliofariki na kula chakula cha lishe bora huku wakiwataza waumini waliokufa njaa.

    Ugunduzi wa makaburi ya halaiki mwezi uliopita umelishangaza taifa katika kile kilichotajwa kuwa mauaji ya msitu wa Shakahola.

    Maafisa wa polisi wanaamini kwamba miili mingi ni ya waumini wa kanisa la Mackenzie anayedaiwa kuwaagaiza kufunga hadi kufa.

    Huku njaa ikidaiwa kuwa chanzo kikuu cha vifo hivyo, baadhi ya waathiriwa wakiwemo Watoto , walinyongwa , kupigwa hadi kufa, kufunikwa pua na mdomo, kulingana na mwanapatholojia mkuu Johannsen Oduor.

  6. Mahakama ya juu Nigeria yatupilia mbali kesi ya kutaka kumuondoa rais mteule Bola Tinubu

    w

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mahakama ya Juu nchini Nigeria imetupilia mbali kesi ya kutaka kumuondoa rais mteule Bola Tinubu na mgombea mwenza wake Kashim Shettima kama wagombea urais na makamu wa rais wa chama tawala cha All Progressives Congress (APC) katika uchaguzi wa rais wa Februari 2023.

    Kesi hiyo iliyowasilishwa Julai mwaka jana na chama cha upinzani cha Peoples Democratic Party ilidai kuwa uteuzi wa Bw. Shettima kama mgombea mwenza wa Tinubu ulikuwa unakiuka katiba ya Nigeria.

    Hata hivyo, jopo la wanachama watano wa mahakama ya juu zaidi mnamo Ijumaa liliamua kwamba kesi hiyo haina mashiko.

    Majaji walisema kuwa Peoples Democratic Party haikuwa na uwezo wa kuanzisha kesi hiyo kwa vile sio mwanachama wa APC.

    Kulikuwa na woga na wasiwasi mbele ya hukumu ya kihistoria ya Mahakama ya Juu Chama cha upinzani kilikuwa kimesema kuwa uteuzi wa Shettima kugombea nafasi ya makamu wa rais na kiti cha useneta wa Borno - wakati huo huo - ulikiuka sheria.

    Lakini Jaji Adamu Jauro ambaye alitoa uamuzi mkuu, alibainisha kuwa PDP ilikuwa inaingilia masuala ya ndani ya chama kingine na akapiga faini ya N2 milioni (kama dola 4,300) juu yake.

    Uamuzi wa Mahakama ya Juu sasa umeliweka suala hilo mahali pazuri na inaonekana kutoa muhuri wa mahakama wa kuidhinisha kuapishwa kwa rais mteule Bola Ahmed Tinubu na Makamu wa Rais mteule Kashim Shettima.

    Wanatarajiwa kuapishwa Jumatatu Mei 29 wakati rais Muhammadu Buhari atakapoondoka madarakani baada ya kumaliza muhula wa nne wa nne.

  7. Nyati, mamba kuzifurusha familia za Msumbiji

    .

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Serikali nchini Msumbiji inawapa makazi watu walioathirika na mashambulizi ya wanyamapori

    Zaidi ya familia 1,000 zinatazamiwa kuhama makazi yao katikati mwa Msumbiji kufuatia mashambulizi ya wanyama pori.

    Mkuu wa utawala wa eneo hilo katika wilaya ya Marromeu katika jimbo la Sofala alisema serikali ya eneo hilo itahamisha familia 1,500 zilizotishiwa na mashambulizi hayo.

    Henriqueta de Rosário alisema mamlaka imerekodi vifo vya watu watatu kutokana na mashambulizi ya wanyamapori katika robo ya kwanza ya mwaka huu.

    Nyati kutoka Hifadhi Maalum ya Marromeu katika delta ya mto Zambezi wamevamia maeneo ya makazi na kuwalazimu wakazi kuhamia visiwa vya mto huo.

    Hata hivyo, wanapotafuta hifadhi visiwani humo, wanakabiliwa na tisho la kushambuliwa na mamba.

    "Mgogoro kati ya mwanadamu na wanyamapori ni ukweli unaokua" alisema Bi Rosário, akiongeza kuwa watu wengi walitishiwa.

    Alisema kuwa takriban watu 400 tayari walikuwa wamejiandikisha kwa ajili ya mpango wa makazi mapya ya hiari ili kuondoka katika eneo hilo.

  8. Msumbiji inapendekeza kupunguzwa kwa mishahara kwa maafisa wakuu

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Hatua hiyo pia inalenga kushughulikia wasiwasi kuhusu malipo ya haki

    Baraza la mawaziri la Msumbiji limeidhinisha mswada unaopendekeza kupunguzwa kwa mishahara ya mawaziri, manaibu waziri, makatibu wa majimbo na wabunge huku serikali ikikabiliana na mswada wa mishahara kupanda.

    Waziri wa Fedha na Uchumi Max Tonela siku ya Alhamisi alisema pendekezo hilo pia lilikuwa linataka kushughulikia maswala ya mishahara ya wajumbe wa mabunge ya majimbo, ambayo alisema yanakinzana na kanuni za malipo ya haki.

    Bw Tonela alisema baadhi ya mishahara yao ni ya juu zaidi kuliko ile inayolipwa watendaji wengine na wataalamu waliobobea.

    Hakuonyesha kiasi cha kupunguzwa kilichopendekezwa.

    Mapunguzo hayo ya mishahara hayatatumika kwa watumishi wa umma ambao mishahara yao ilirekebishwa chini ya Kiwango cha Malipo Pamoja (TSU) kilichoidhinishwa mwaka huu.

    Hatua hiyo inajiri takriban wiki mbili baada ya Shirika la Fedha la Kimataifa IMF kuangazia haja ya serikali kupunguza matumizi ya mishahara ya umma.

    Mswada wa mishahara utawasilishwa bungeni kwa mjadala kabla ya kupitishwa kuwa sheria.

  9. Rwanda na Ukraine zatia saini mkataba wa ‘mashauriano ya kisiasa’

    kk

    Chanzo cha picha, Ikulu/Rwanda

    Rwanda na Ukraine jana zilitia saini mkataba wa maelewano kuhusu "mashauriano ya kisiasa" na kujadili maeneo mengine ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, tovuti inayounga mkono serikali ya New Times iliripoti.

    Mkataba huo ulitiwa saini na waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Vincent Biruta, na mwenzake wa Ukrania, Dmytro Kuleba, baada ya wawili hao kufanya mkutano wa pande mbili.

    Kuleba alikuwa nchini Rwanda kwa ziara ya siku moja katika ziara yake ya pili barani Afrika ambayo pia imemkuta akitembelea Morocco na Ethiopia.

    "Tunakusudia kuongeza ushirikiano katika biashara, uwekaji digitali, anga, ujenzi, elimu, na dawa.

    Ukraine itafungua ubalozi nchini Rwanda," Kuleba alinukuliwa akisema. Kulingana na wizara ya mambo ya nje ya Ukrane, Kuleba na Biruta pia walijadili fomula ya amani ya Ukraine, usalama wa chakula barani Afrika, mauzo ya nafaka ya Kiukreni kupitia Bahari Nyeusi na mpango wa kibinadamu wa Nafaka Kutoka Ukraine.

    Kuleba baadaye alikutana na Rais wa Rwanda Paul Kagame na akakariri "nia kubwa" ya Ukraine katika kuendeleza uhusiano na Rwanda kwa kuzingatia kuheshimiana na manufaa.

  10. Roketi ya Urusi yashambulia kliniki ya matibabu ya Ukraine

    .

    Chanzo cha picha, TELEGRAM/SERHIY LYSAK

    Takriban mtu mmoja ameuawa na wengine 15 kujeruhiwa, wakiwemo watoto wawili, katika shambulio la kombora kwenye kliniki ya matibabu huko Dnipro mashariki mwa Ukraine.

    Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alithibitisha kutokea kwa shambulio hilo na kusema mamlaka inajitahidi kuwaokoa wengine kutoka hospitalini.

    Alisema mamlaka zote muhimu zilihusika katika misheni ya kusafisha.

    Hapo awali, gavana wa eneo hilo, Serhiy Lysak, alisema mji huo ulishambuliwa Alhamisi usiku.

    "Ulikuwa usiku mgumu sana. Kulikuwa na sauti kubwa - adui alianzisha mashambulizi makubwa katika eneo hilo kwa makombora na ndege zisizo na rubani," Bw Lysak alisema.

    Baadaye alithibitisha watoto wawili waliojeruhiwa walikuwa wavulana wenye umri wa miaka mitatu na sita.

    Bw Zelensky alichapisha video ya jengo la zahanati iliyoharibiwa ambayo ilionyesha wazima moto kwenye eneo la tukio na moshi ukifuka kutoka kwa jengo hilo.

    "Magaidi wa Urusi kwa mara nyingine tena wanathibitisha hali yao ya wapiganaji dhidi ya kila kitu cha utu na uaminifu," alisema.

    Pia unaweza kusema:

  11. Milipuko huku wanajeshi wa Uganda wakipambana na wanamgambo nchini Somalia

    M

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kundi la al-Shabab leo Ijumaa asubuhi lilifanya shambulizi dhidi ya kituo cha wanajeshi wa Uganda cha Kikosi Umoja wa Afrika (ATMIS) katika wilaya ya Bulla Mareer, eneo la Lower Shabelle nchini Somalia.

    Shambulio hilo lilianza muda mfupi baada ya sala ya asubuhi.

    Lilianza na mlipuko mkubwa, unaoaminika kuwa gari la vilipuzi.

    Buulo Mareer iko takriban kilomita 110 kutoka mji mkuu, Mogadishu.

    Wakazi waliripoti kuwa baada ya mlipuko huo mkubwa, milipuko miwili zaidi ilisikika katika kambi hiyo, kabla ya mapigano kuanza kati ya wanajeshi wa Uganda na washambuliaji

    Al-Shabab walisema wameteka kambi hiyo na kuua makumi ya wanajeshi wa ATMIS, lakini madai hayo hayajathibitishwa.

    ATMIS inasema vikosi vyake kwa sasa vinatathmini hali ya usalama katika eneo hilo lakini hakuna kauli iliyotolewa na serikali ya Somalia kuhusiana na shambulio hilo.

    Msemaji wa jeshi la Uganda Felix Kulayigye ameliambia gazeti la Daily Nation la Kenya kwamba wanajeshi wanachunguza shambulio hilo.

    Aliwalaumu "waasi wa kigeni" kwa uvamizi huo bila kutoa maelezo zaidi.

    Kiwango cha uharibifu uliosababishwa na shambulio hilo bado hakijajulikana.

    Raia wamesalia ndani ya nyumba zao na licha ya baadhi ya risasi zilizofyatuliwa kugonga nyumba zao, hakuna uharibifu ulioripotiwa.

    Baadhi ya wakazi wa Bulo Mareer waliambia BBC kwamba walisikia sauti za helikopta zikipaa juu ya jiji hilo.

    Pia unaweza kusoma:

  12. Wakili wa Nigeria apigwa faini kwa kutaka kusitisha kuapishwa kwa Tinubu

    Ambrose Owuru alitaka mahakama kubatilisha ushindi wa Bw Tinubu

    Chanzo cha picha, Bola Tinubu/Twitter

    Mahakama nchini Nigeria imemtoza faini aliyekuwa mgombea urais katika uchaguzi wa 2019 kwa kuwasilisha kesi ya kusitisha kuapishwa kwa Rais mteule Bola Tinubu tarehe 29 Mei.

    Mahakama iliamuru Ambrose Owuru, wakili, kulipa $87,000 (£80,000) kwa kufuata kesi ya "ajabu" na "isiyo na maana". Bw Owuru, ambaye aligombea na kushindwa katika uchaguzi wa urais wa 2019, alikuwa ameitaka mahakama iamuru aapishwe kama rais badala ya Bw Tinubu.

    Wakili huyo, ambaye hakushiriki uchaguzi wa urais wa 2023, alidai alishinda uchaguzi wa urais wa 2019 lakini alinyimwa ushindi wake isivyo haki.

    Ikitupilia mbali kesi hiyo mnamo Oktoba 2019, Mahakama ya Juu ilieleza kuwa ni matumizi mabaya ya mchakato wa mahakama.

    Baada ya Bw Tinubu kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa 2023, Bw Owuru aliwasilisha kesi nyingine kutokana na ukweli wa kesi yake ya 2019.

    Jopo la watu watatu wa Mahakama ya Rufaa katika mji mkuu Abuja walitupilia mbali kesi hiyo katika uamuzi ulioafikiwa siku ya Alhamisi.

  13. Ilichukua miaka 54 mtu huyu kupata shahada yake ya kwanza

    Baada ya kustaafu kutoka taaluma ya sheria ya miaka 35, Arthur Ross aliamua kuwa ni wakati wa kurejea shuleni na kumaliza shahada yake ya kwanza

    Chanzo cha picha, UBC

    Zaidi ya miongo mitano baada ya kuanza masomo yake, hatimaye Arthur Ross alipita jukwaani katika Chuo Kikuu cha British Columbia (UBC) siku ya Alhamisi kupokea Shahada yake ya Sanaa.

    Bw Ross, 71, alisema huenda yeye ndiye "mwanafunzi aliyekuwa na uelewa wa polepole zaidi" katika chuo kikuu cha Vancouver. Pia anaweza kuwa mwenye uelewa wa polepole zaidi duniani.

    Ilimchukua miaka 54 haswa kumaliza shahada yake ya kwanza- miaka miwili zaidi ya mmiliki wa Rekodi ya Dunia ya Guinness, Robert FP Cronin, ambaye alianza shahada yake ya baiolojia katika Chuo Kikuu cha Princeton mnamo 1948 na kuhitimu mnamo 2000.

    Lakini Bw Ross alisema hana haraka ya kudai taji lake la rekodi ya dunia. Thawabu ya kweli, alisema, ilikuwa maarifa ambayo aliweza kupata kupitia madarasa yake.

    "Nilitaka tu kujifunza kwa sababu nilitaka kujua," Bw Ross aliambia BBC wiki hii. Shauku hiyo ya kujifunza, alisema, ndiyo iliyomtia moyo kumaliza shahada yake baada ya miaka hii yote.

  14. Marekani yamuwekea vikwazo mkuu wa kundi la Wagner la Urusi nchini Mali

    Marekani imeitaja Wagner kama shirika la uhalifu la kimataifa

    Chanzo cha picha, Reuters

    Marekani imemuwekea vikwazo raia wa Urusi ambaye inasema ni kiongozi wa operesheni ya kundi la mamluki la Wagner nchini Mali.

    Marekani imesema Ivan Maslov alikuwa mtu muhimu katika shughuli za kimataifa za Wagner.

    Imesema Wagner huenda inatumia uwepo wake nchini Mali kuficha juhudi za kupata silaha na vifaa vya kijeshi kwa ajili ya vita dhidi ya Ukraine.

    Pia ilishutumu kundi la Urusi kwa kusambaza makombora ya kutungulia ndege kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka nchini Sudan.

    Mapema mwaka huu, Marekani iliitaja Wagner kama shirika la uhalifu la kimataifa. Kundi hilo limekuwa likiisaidia serikali ya kijeshi ya Mali kupambana na waasi wa Kiislamu.

    "Uwepo wa Kundi la Wagner katika bara la Afrika ni nguvu ya kudhoofisha utulivu kwa nchi yoyote ambayo inaruhusu kupelekwa kwa rasilimali za kikundi katika eneo lao huru," Idara ya Hazina ilisema katika taarifa.

    Unaweza pia kusoma;

  15. Afrika Kusini haitaingizwa katika ushindani wa 'nchi zenye nguvu'- Ramaphosa

    Rais alisema nchi yake inatishiwa kuchukuliwa hatua

    Chanzo cha picha, South Africa presidency/ Twitter

    Maelezo ya picha, Rais alisema nchi yake inatishiwa kuchukuliwa hatua

    Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anasema nchi yake itaendelea kupinga wito wa kuachana na sera yake huru ya mambo ya nje na isiyofungamana na upande wowote.

    Akizungumza siku ya Alhamisi kwenye sherehe za Siku ya Afrika huko Krugersdorp, magharibi mwa Johannesburg, Bw Ramaphosa alisema bara la Afrika mara nyingi linaingizwa kwenye migogoro nje ya mipaka yake.

    "Afŕika Kusini haijaingizwa na haitaingizwa katika mashindano kati ya mataifa yenye nguvu duniani.

    Tutadumisha msimamo wetu kuhusu utatuzi wa amani wa migogoro popote pale migogoro hiyo inapotokea,” Rais Ramaphosa alisema.

    Uhusiano wa Afrika Kusini na Marekani, mshirika mkuu wa kibiashara, umekuwa mbaya tangu Pretoria ilipochukua msimamo usiofungamana na upande wowote katika vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.

    Hili lilichochewa na matamshi ya hadharani ya hivi karibuni ya yaliyotolewa na balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini, Reuben Brigety, kwamba nchi hiyo ilikuwa imeiuzia Urusi silaha.

    Rais Ramaphosa alikubali kuchunguza madai hayo lakini akasema hakuna ushahidi thabiti wa kuunga mkono madai hayo.

    Katika hotuba yake ya Alhamisi, rais alisema nchi, ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini, "zinatishiwa kuadhibiwa" kwa kufuata "sera huru ya kigeni" na kwa kupitisha msimamo wa kutofungamana na upande wowote.

    Hata hivyo, hakutaja adhabu hizo au ni nani anayezitisha.

    Rais Ramaphosa alisema bara hilo lina kumbukumbu chungu za mataifa makubwa ya kigeni kuendesha "vita vya uwakilishi katika ardhi ya Afrika".

    Serikali ya Afrika Kusini pia iko chini ya shinikizo la kuchukua uamuzi juu ya Rais wa Urusi Vladimir Putin, ambaye anatazamiwa kuzuru nchi hiyo baadaye mwaka huu.

    Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetoa kibali cha kukamatwa kwake kuhusiana na mzozo wa Ukraine.

    Pia unaweza kusoma:

    • Mzozo wa Ukraine: Afrika Kusini inamtaka Putin asihudhurie mkutano wa BRICS ili wasimkamate- Ripoti
    • Afrika inaongoza juhudi za amani kati ya Urusi-Ukraine - Ramaphosa
    • Kwa nini jeshi la wanamaji la Afrika Kusini linajiunga na Urusi na China kwa mazoezi?
  16. Mkuu wa uhandisi wa Twitter ajiuzulu baada ya hitilafu za uzinduzi wa kampeni ya DeSantis

    Kuingia kwa Bw DeSantis katika kinyang'anyiro cha 2024 kwa Ikulu kulikumbwa na hitilafu za kiufundi.

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Uzinduzi wa kampeni ya Bw DeSantis katika kinyang'anyiro cha urais wa Marekani 2024 ulikumbwa na hitilafu za kiufundi.

    Mkuu wa uhandisi kwenye Twitter anasema anaondoka kwenye kampuni hiyo siku moja baada ya uzinduzi wa kampeni ya urais wa Marekani ya Ron DeSantis kwenye jukwaa hilo kukumbwa na hitilafu za kiufundi.

    Foad Dabiri aliandika kwenye ujumbe: "Baada ya kufanya kazi Twitter kwa karibu miaka minne, niliamua kuondoka hapo jana."

    Kuingia kwa Bw DeSantis katika kinyang'anyiro cha kuwania Ikulu ya White House kulikumbwa na matatizo huku mtandao wa Twitter ukiendelea kuharibika.

    Zaidi ya 80% ya wafanyikazi wa kampuni hiyo wamefutwa tangu Bwana Musk alipoinunua.

    Bw Dabiri, ambaye alikuwa Mhandisi Mkuu katika kitengo cha ukuaji wa mtandao wa Twitter, alisema katika ujumbe wake wa Twitter "amekumbwa na hitilafu kubwa mara mbili" katika kampuni hiyo, kabla na baada ya kununuliwa na bilionea huyo mwaka jana.

    Bw Dabiri hakubainisha ni kwa nini aliamua kuacha kazi Twitter, na ikiwa ilihusiana na matatizo ya tukio la DeSantis kwenye jukwaa hilo.

    Hakujibu ombi la BBC la kutaka maoni yake.

    Twitter haikutoa taarifa kuhusu kujiondoa kwa Bw Dabiri ilipoulizwa na BBC.

    Hata hivyo, Bw Dabiri alisema: "Nimejifunza mengi kwa kufanya kazi na @elonmusk, na nimepata mafunzo kuona jinsi kanuni na maono yake yanavyounda mustakabali wa kampuni hii."

  17. 'Nilifanya nini?' Mvulana wa miaka 11, aliyepigwa risasi na polisi Marekani

    CARLOS MOORE, COCHRAN LAW FIRM

    Chanzo cha picha, CARLOS MOORE, COCHRAN LAW FIRM

    Mvulana mwenye umri wa miaka 11 ambaye alipigwa risasi na afisa baada ya kuita polisi kuomba msaada ameruhusiwa kutoka hospitalini, familia yake inasema.

    Polisi wa Mississippi walifika nyumbani kwa Aderrien Murry siku ya Jumamosi wakijibu simu ya kukabiliana na ghasia nyumbani iliyopigwa na mvulana huyo, kisha kumpiga risasi kifuani, kulingana na mama yake.

    Baada ya kupigwa risasi anasema kijana alimuuliza "nilifanya nini?"

    Afisa aliyehusika amepewa likizo ya lazima huku uchunguzi ukiendelea.

    Ofisi ya Upelelezi ya Mississippi inaendesha uchunguzi kuhusu tukio hilo.

    Mvulana huyo kwa sasa anapata ahueni nyumbani baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya eneo hilo, ambako alipatiwa matibabu ya mapafu zilizoathiriwa, mbavu zilizovunjika na ini lililochanika.

    Mamake, Nakala Murry, ameomba afisa huyo afutwe kazi na kushtakiwa.

    Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu nje ya Ukumbi wa Jiji la Indianola, alisema baba wa mtoto wake mwingine alifika nyumbani kwao mapema Jumamosi asubuhi na kuanz akuzua "vurugu", ndiposa alimuomba mwanawe kuwaita polisi.

    Afisa wa Indianola alipofika, Bi Murry baadaye aliambia CNN, "alikuwa na bunduki ambayo ilikuwa tayari kupigwa na kuamrisha kila mtu aliyekuwa ndani ya nyumba kutoka nje.

    Mtoto wake alipopiga kona kutoka ukumbini, afisa huyo alifyatua risasi na kumpiga Aderrien kifuani, alisema.

    "Maneno yake yalikuwa: 'Kwa nini umenipiga risasi? Nimefanya nini?' na kuanza kulia," Bi Murry alisema. "Hili sio haki. Hii sio sawa."

    Anasema alijaribu kumsaidia mwanawe asipoteze damu nyingi lakini mikiono yake ililowa damu.

    Afisa huyo pia alimsaidia kwa huduma ya kwanza, hadi madaktari walipofika.

  18. Mzozo wa Sudan: Raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 85 atelekezwa kando ya ubalozi wa Uingereza

    Sholgami

    Chanzo cha picha, Familia ya Sholgami

    Raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 85 nchini Sudan alipigwa risasi na walenga shabaha na mkewe akafa kwa njaa baada ya kuachwa wajitegemea na ubalozi wa Uingereza nchini Sudan, familia yao imeambia BBC News Arabic.

    Abdalla Sholgami aliishi na mke wake mwenye umri wa miaka 80, Alaweya Rishwan, kando ya mkabala na balozi wa Uingereza mjini Khartoum.

    Lakini licha ya wito wa mara kwa mara wa kuomba msaada, mmiliki wa hoteli ya London hakuwahi kupewa usaidizi wa kuondoka Sudan, hata wakati timu ya kijeshi ya Uingereza ilipotumwa kuwahamisha wafanyakazi wa kidiplomasia.

    Badala yake, wanandoa hao wazee waliambiwa waende kwenye uwanja wa ndege ulioko kilomita 40 nje ya Khartoum - ambayo ingemaanisha kuvuka eneo la vita - ili kupanda ndege ya kuwahamisha.

    Ofisi ya mambo ya nje ya Uingereza ilikiri kwa BBC kwamba hali ya Sholgamis ilikuwa "ya kusikitisha sana" lakini ikaongeza kuwa "uwezo wetu wa kutoa usaidizi wa kibalozi ni mdogo sana na hatuwezi kutoa usaidizi wa kibinafsi ndani ya Sudan".

    Eneo kidiplomasia la Khartoum limeshuhudia mapigano makali tangu mzozo huo ulipozuka tarehe 15 Aprili.

    Vurugu hizo zilichochewa na mzozo wa madaraka kati ya washirika wa zamani - viongozi wa jeshi la kawaida na vikosi maalum vya kijeshi (RSF).

    Siku chache tu baada ya mzozo kuibuka familia ilianza kuwasiliana na ubalozi wa Uingereza.

    Ubalozi huo ulihamishwa kwa usaidizi wa Jeshi la Uingereza na Jeshi la Wanahewa la Kifalme zaidi ya wiki moja baada ya mapigano kuanza.

    Pia unaweza kusoma:

  19. Hujambo na karibu.