EAC yamtaka kiongozi wa DR-Congo kuheshimu mamlaka ya jeshi la kikanda

Katibu Mkuu wa EAC Peter Mathuki anasema ukosoaji wa jeshi la EAC haukuwa na msingi

Moja kwa moja

  1. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu kwa leo

  2. Papa Francis aonya wanyama wasiwe kipenzi na kuchukua nafasi ya watoto Italia

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kuanzisha familia nchini Italia imekuwa kitu kinachohitaji "juhudi kubwa" ambayo ni matajiri pekee wanaweza kumudu, Papa Francis ameonya.

    Akihutubia mkutano kuhusu mzozo wa idadi ya watu wa Italia, alisema wanyama wanachukua wanafasi ya watoto katika kaya nyingi.

    Pia jukwaani walikuwepo vijana kadhaa, wakiwa wamevalia fulana wakisema "tunaweza kufanya hivi" - wakimaanisha kuwashawishi watu kupata watoto zaidi.

    Italia ina moja ya viwango vya chini vya uzazi katika EU na idadi ya kuzaliana imepungua chini ya 400,000 mwaka jana - kiwango kipya cha chini zaidi.

    Katika hotuba yake mjini Roma, Papa alisema kupungua kwa kiwango cha kuzaliana kunaashiria ukosefu wa matumaini katika siku zijazo, huku vizazi vichanga vikilemewa na hali ya kutokuwa na uhakika, udhaifu na hali ya hatari.

    "Ugumu wa kupata kazi thabiti, kodi ya juu na mishahara haitoshi ni matatizo halisi," alisema.

    Akionya kwamba wanyama wamekuwa kipenzi na wanachukua nafasi ya watoto katika baadhi ya kaya, Papa alisimulia jinsi mwanamke mmoja alivyofungua begi lake na kumtaka "abariki mtoto wake".

    Hakuwa mtoto badi mbwa mdogo.

    "Nilipoteza uvumilivu wangu na nikamwambia: kuna watoto wengi ambao wana njaa, na unaniletea mbwa?" Aliongeza, na kusababisha waliokuwa karibu kupiga makofi.

    Viwango vya kuzaliana vinapungua katika maeneo mengi - kama vile Japan, Korea Kusini, Puerto Rico na Ureno.

  3. Afrika Kusini yajaribu kurejesha uhusiano na Marekani katikati ya mzozo wa madai ya kuuzia Urusi silaha

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Afrika Kusini inatafuta kurejesha uhusiano wake na Marekani, huku kukiwa na mzozo wa kidiplomasia kuhusu madai ya kuiuzia Urusi silaha.

    Balozi wa Marekani Reuben Brigety amedai meli ya Urusi ilikuwa imesheheni risasi na silaha mjini Cape Town Desemba mwaka jana.

    Madai hayo yalizua mgogoro wa kidiplomasia na Afrika Kusini imesema haina rekodi ya mauzo ya silaha yaliyoidhinishwa.

    Lakini serikali pia ilisema inathamini uhusiano "wa kirafiki, wenye nguvu, na wenye manufaa kwa pande zote" na Marekani.

    Jpo linalochunguza madai hayo limeanzishwa, Rais Cyril Ramaphosa alithibitisha Alhamisi.

    BBC inaelewa kuwa nyuma ya pazia serikali inasikitishwa zaidi – na imekasirishwa na kile ambacho baadhi wanakiona kuwa Marekani inajaribu kutumia nguvu kwa Afrika Kusini ili ikubaliane nayo juu ya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine "kwa njia yoyote ile".

    Soma zaidi:

  4. Erling Haaland na Sam Kerr washinda tuzo za Chama cha Waandishi wa Soka

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Picha: Sam Kerr ashinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka kwa Wanawake mnamo 2022

    Mshambulizi wa Manchester City Erling Haaland na Sam Kerr wa Chelsea wamechaguliwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka kwa wanaume na wanawake na Chama cha Waandishi wa Soka (FWA).

    Haaland wa Norway amefunga mabao 51 hadi sasa katika msimu wake wa kwanza akiwa na City.

    Kati ya hayo, 35 yamekuwa kwenye Ligi Kuu, akivunja rekodi ya ligi hiyo ya kufunga mabao mengi zaidi kwa msimu mmoja.

    Mshambulizi wa Australia Kerr ndiye mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka kwa Wanawake katika miaka mfululizo.

    Amefunga mabao 26 katika mechi 34 za klabu msimu huu, yakiwemo 10 kwenye Ligi Kuu ya Wanawake.

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alizoa kura mara mbili zaidi ya Rachel Daly wa Aston Villa aliyeshika nafasi ya pili, ambaye ndiye mfungaji bora wa WSL akiwa na mabao 20.

    Mchezaji mwenza wa Kerr wa timu ya Chelsea Lauren James alikuwa wa tatu.

    Kwa tuzo ya wanaume, Haaland mwenye umri wa miaka 22 alipata 82% ya kura huku Bukayo Saka wa Arsenal na Martin Odegaard wakikamilisha tatu bora.

    Pia unaweza kusoma:

  5. Mamlaka ya Marekani yalegeza sheria za uchangiaji damu kwa wapenzi wa jinsia

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) imepunguza vikwazo vyake vinavyowazuia wapenzi wa jinsia moja na wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia zote mbili kutoa damu.

    Shirika hilo, mnamo 2015, liliondoa marufuku ya maisha ya michango ya damu kutoka kwa wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao, lakini miongozo yake ya uchangiaji imekuwa ikikosolewa kwa miaka mingi.

    Sera ya hivi punde zaidi ya FDA inazingatia kutathmini wafadhili wote kwa vigezo sawa huku ikichunguza shughuli za hivi majuzi, ikiwemo hatari kubwa inayotokana na ngono.

    Chanzo cha hatua hiyo ya hivi sasa ni Uingereza na Canada.

    Nchi zote mbili, mnamo 2021 na 2022 mtawalia, ziliruhusu michango kutoka kwa wanaume ambao wamefanya ngono na wanaume wengine katika miezi mitatu iliyopita.

    Lakini mabadiliko ya sheria yanatumika tu kwa wale ambao wamekuwa na mwenzi yule yule wakati wa ngono katika kipindi hicho.

    Wale ambao wamekuwa na wapenzi wapya au wengi, na ngono ya sehemu ya nyuma, katika muda wa miezi mitatu iliyopita hawastahiki kutoa damu.

    FDA pia inapendekeza kwamba wale wanaotumia pre-exposure prophylaxis (PRrEP)dawa za kupunguza makali ya VVU au post-exposure prophylaxis (PEP) - dawa zinazotumiwa kuzuia maambukizi ya VVU - lazima waahirishe uchangiaji wa utoaji damu.

    Shirika hilo lilisema utumiaji wa dawa hizi unaweza kuchelewesha kugunduliwa kwa VVU na hivyo basi, kupata matokeo hasi ya uwongo katika kipimo cha uchunguzi.

    Wapenzi wa jinsia mojanchini Marekani na wenye kushiriki mapenzi ya jinsia mbili walipigwa marufuku kutoa damu mwaka wa 1983, kwani hofu na taarifa potofu juu ya kuenea kwa VVU/UKIMWI zilienea.

  6. Mmoja wa Simba wazee zaidi Kenya auawa kwa mkuki

    .

    Chanzo cha picha, Lion Guardians/Facebook

    Maelezo ya picha, Loonkiito alidungwa mikuki na wanakijiji waliokuwa wanawinda mifugo

    Mmoja wa Simba wazee zaidi Kenya amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 19, mamlaka imesema.

    Simba huyo dume kwa jina Loonkiito, alichomwa mkuki na wafugaji wa eneo hilo katika kijiji cha Olkelunyiet Jumatano usiku wakiwa wanawinda mifugo.

    Kijiji hicho kinapakana na Mbuga ya Kitaifa ya Amboseli - nje kidogo ya mji mkuu, Nairobi.

    Msemaji wa Shirika la Huduma ya Wanyamapori nchini (KWS) Paul Jinaro aliambia BBC kwamba simba huyo alikuwa mzee na dhaifu na alirandaranda katika kijiji hicho kutoka mbugani kutafuta chakula.

    Bw Jinaro hakuweza kuthibitisha ikiwa ni simba mzee zaidi nchini lakini amebainisha kuwa ni "mzee sana".

    Lion Guardians, shirika la uhifadhi, lilisema Loonkiito ndiye simba dume mzee zaidi katika mfumo wake wa ikolojia na pengine barani Afrika.

    "Alikuwa ishara ya uthabiti na maisha marefu," shirika hilo lilisema katika taarifa.

    Paula Kahumbu ni mhifadhi wa wanyamapori na ofisa mtendaji mkuu wa shirika la WildlifeDirect, Paula Kahumbu alisema amehuzunishwa na mauaji ya simba huyo na kutaka hatua zichukuliwe ili kulinda wanyamapori nchini.

    "Hiki ndicho kitovu cha mzozo kati ya binadamu na wanyamapori na tunahitaji kufanya zaidi kama nchi kuwalinda simba, ambao wanakabiliwa na kutoweka," Bi Kahumbu aliambia BBC.

    Pia unaweza kusoma:

  7. Habari za hivi punde, Mahakama Pakistan yaamuru Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan asikamatwe

    Pakistan

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mahakama nchini Pakistan imeamuru aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Imran Khan anapaswa kuachiliwa kutoka kizuizini na asikamatwe tena kwa angalau wiki mbili.

    Mahakama ya Juu ya Pakistan imesema kwamba kukamatwa kwa waziri mkuu wa zamani Imran Khan kwa tuhuma za ufisadi wiki hii ni kinyume cha sheria. Mahakama iliamuru Bw Khan aachiliwe mara moja.

    Mawakili wake walidai kuwa kukamatwa kwake kutoka kwa majengo ya mahakama huko Islamabad siku ya Jumanne ilikuwa kinyume cha sheria.

    Takriban watu 10 wameuawa na wengine 2,000 kukamatwa kutokana na maandamano ya ghasia nchini humo tangu aliposhikiliwa.

    Khan aliwaambia waandishi wa habari kwamba "alitekwa nyara" kutoka majengo ya Mahakama Kuu ya Islamabad siku ya Jumanne na hakukuwa na sababu ya kumkamata.

    "Nilitekwa nyara," alisema kabla ya kusikilizwa kwa kesi yake katika mahakama hiyo. “Na nilipochukuliwa, ndipo nilipoonyeshwa hati ya kukamatwa kwangu. Je, hii ni sheria ya wapi? Wanajeshi waliniteka nyara. Polisi wako wapi? Sheria iko wapi? Inaonekana kama sheria ya kijeshi imetangazwa hapa," alisema.

  8. Ukraine yadai kukomboa maeneo huko Bakhmut baada ya Urusi kukanusha

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Ukraine inasema kuwa imetwaa tena eneo la Bakhmut, hatua ambayo ni nadra baada ya miezi kadhaa ya Urusi kuendelea kukalia maeneo katika mji huo wa mashariki.

    Naibu Waziri wa Ulinzi Hanna Malyar alisema vikosi vya Ukraine vilisonga mbele kilomita mbili (maili 1.2) katika wiki moja.

    Madai hayo yanaashiria mabadiliko ya kasi katika eneo la Bakhmut - lakini kwa upana zaidi, hakuna ushahidi wa wazi wa uvamizi unaotarajiwa kutoka upande wa Ukraine.

    Urusi imekanusha ripoti Ukraine kutwaa maeneo, baada ya madai ya pande zote mbili.

    "Matangazo ya mtu binafsi kwenye Telegram kuhusu 'mafanikio' katika sehemu kadhaa vitani hayalingani na ukweli," wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema.

    "Hali jinsi kwa jumla katika eneo maalum la operesheni ya kijeshi iko chini ya udhibiti," iliongeza, ikitumia neno la Urusi linalomaanisha ‘uvamizi’.

    Wakati vita vikali na vya umwagaji damu vikiendelea, Bakhmut imekuwa muhimu - ingawa wataalam wengi wanatilia shaka thamani yake ya kimbinu.

    Katika chapisho kwenye mtandao wa Telegraph, Bi Malyar alisema Bakhmut imekuwa eneo lengwa na lenye umuhimu kwa Urusi.

    Alishutumu Kremlin kwa kudai ushindi wa uwongo na wakati huo huo ikiwa pia inaeneza uwongo juu ya uhaba wa silaha na risasi.

    Akielezea "hali halisi" katika wiki iliyopita, Bi Malyar alidai Urusi ilipata hasara kubwa ya wanajeshi, kwani Ukraine ilipata mafanikio ya kupiga hatua ya kilomita 2 bila kupoteza nafasi yoyote.

    Siku ya Alhamisi, Yevgeny Prigozhin, mkuu wa kundi la mamluki la Wagner linalopigana upande wa Urusi, alishutumu wanajeshi wa kawaida wa Urusi kwa kuacha wazi sehemu walizokuwa wako huko Bakhmut.

    Na wanablogu wa kijeshi wa Urusi waliripoti maendeleo ya yaliyopigwa na Ukraine au mienendo ya wanajeshi katika maeneo kadhaa.

    Pia unaweza kusoma:

  9. Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Tanzania Bernard Membe aaga Dunia

    membe

    Chanzo cha picha, MEMBE/TWITTTER

    Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani na aliyewahi kuwa mgombea Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo mwaka 2020, Bernard Membe, amefariki dunia.

    Bw. Membe amefariki akiwa katika Hospitali ya Kairuki, Jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mfupi.

    Bernard Membe alihudumu katika nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Mwaka 2007 hadi 2015.

    Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameelezea kusikitishwa kwake na kifo cha Bw. Membe.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  10. EAC yamtaka kiongozi wa DR-Congo kuheshimu mamlaka ya jeshi la kikanda

    Peter Mathuki alisema ukosoaji wa jeshi la EAC haukuwa na msingi

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Peter Mathuki alisema ukosoaji wa jeshi la EAC haukuwa na msingi

    Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imemtaka kiongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuheshimu hatua ya mataifa ya kikanda ya kupeleka vikosi katika jaribio la kuleta utulivu katika maeneo ya mashariki mwa nchi yake.

    Siku ya Jumanne Rais Félix Tshisekedi, alishutumu jeshi la Afrika Mashariki kwa kutofanya kazi yake, akionya huenda likaombwa kuondoka nchi humo kufikia Juni.

    Pia alishutumu jeshi hilo kwa kushirikiana na waasi wa M23.

    Katibu Mkuu wa EAC Peter Mathuki alisema hajapokea mawasiliano yoyote kuhusiana na malalamiko ya Bw Tshisekedi, akisema masuala yoyote yatakayoibuliwa yatajadiliwa na wakuu wa nchi za EAC.

    "Naomba tuheshimu na kuami ni wanachama wa mkutano wa [EAC] kwa sababu najua wana nia ya kutatua suala hili," Bw Mathuki aliambia NTV ya Uganda siku ya Alhamisi.

    Mkuu huyo wa EAC hapo awali aliambia kituo cha redio cha Ufaransa RFI kwamba ukosoaji wa kikosi hicho haukuwa na msingi.

    "Kusema kwamba jeshi la kikanda halifanyi lolote, kwa muda mfupi kama huo, si sawa," alisema, ingawa alikiri kwamba kasi ya kuleta utulivu DR Congo "inaweza isiwe vile tulivyotarajia"

    Ukosoaji wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo dhidi ya jeshi la Afrika Mashariki umekuja siku moja baada ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Sadc) kuidhinisha kupelekwa kwa wanajeshi mashariki mwa nchi hiyo.

    Ramani

    Maelezo zaidi:

  11. Sarafu ya Afrika Kusini yashuka thamani baada ya Marekani kuishutumu kwa kuipatia Urusi silaha

    Sarafu ya Afrika Kusini

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Randi ya Afrika Kusini ilianguka siku ya Alhamisi dakika chache baada ya balozi wa Marekani kuishutumu nchi hiyo kwa kutoa silaha na risasi kwa Urusi.

    Sarafu hiyo ilipoteza zaidi ya senti 30 ya thamani yake dhidi ya dola, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

    Hii ilikuwa randi dhaifu zaidi tangu mwaka 2020.

    Balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini Reuben Brigety alisema silaha na risasi zilipakiwa kwenye meli ya Urusi iliyotia nanga katika kambi ya jeshi la majini ya Simon's Town mjini Cape Town mwezi Disemba mwaka jana.

    Ripoti hiyo ilizua hofu kwamba Marekani itachukua hatua za kiuchumi dhidi ya Afrika Kusini.

    Ofisi ya rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ilisema kutakuwa na uchunguzi huru kuhusu tuhuma hizo, utakaoongozwa na jaji mstaafu

  12. Wapinzani wa Sudan wakubali kulinda raia lakini si kusitisha mapigano

    Sudan

    Chanzo cha picha, AFP

    Pande mbili zinazozozana nchini Sudan zimetia saini makubaliano ya kuwalinda raia na misaada, lakini hazikuweza kukubaliana kuhusu kusitisha mapigano.

    Mazungumzo hayo yaliyofanyika katika bandari ya Saudia ya Jeddah huku Saudia na Marekani ikishiriki, yameelezwa na wanadiplomasia wa Marekani kuwa magumu, huku pande hizo mbili zikiwa bado "mbali mbali".

    Wanajeshi wa Sudan na Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF) waliahidi kuruhusu msaada na kuwaruhusu watu kukimbia maeneo ya mapigano.

    Bado wanajadili mapendekezo ya usitishaji vita wa siku 10 na utaratibu wa kuufuatilia, kutokana na kushindwa kwa usitishaji mapigano hapo awali.

    Inatarajiwa kwamba ingesababisha mazungumzo juu ya mwisho wa muda mrefu wa uhasama. Siku ya Alhamisi, mji mkuu wa Sudan, Khartoum, ulikumbwa na mapigano zaidi lakini hali kwa ujumla ilikuwa shwari kuliko ilivyokuwa siku moja kabla.

    Unaweza kusoma;

  13. Elon Musk asema amemteua Mkuu mpya wa Twitter

    f

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Elon Musk amesema kwamba amempata Mtendaji Mkuu mpya wa kuongoza Twitter.

    Alitangaza habari hizo kwenye mtandao wa kijamii, alioununua mwaka jana kwa $44bn (£35.2bn). Bw Musk hakumtaja Mkuu mpya wa tovuti hiyo lakini alisema "yeye" angeanza baada ya wiki sita, ambapo atakuwa Mwenyekiti Mtendaji na afisa mkuu wa teknolojia.

    Amekuwa chini ya shinikizo la kutaja mtu mwingine kuongoza kampuni na kuzingatia biashara zake nyingine. Mwaka jana, baada ya watumiaji wa Twitter kumpigia kura ya kumtaka aachie ngazi katika kura ya maoni mtandaoni, alisema: "Hakuna anayetaka kazi hiyo ambaye anaweza kuIweka Twitter hai."

    Hata hivyo, ijapokuwa Bw Musk alikuwa amesema angekabidhi majukumu, haikuwa wazi ni lini au hata ikiwa ingefanyika.

    Hisa za Tesla ziliongezeka baada ya tangazo. Hapo awali Bw Musk alishtumiwa na wenye hisa kwa kuitelekeza Tesla baada ya kuchukua Twitter na kuharibu chapa ya kampuni hiyo ya magari.

  14. Urusi yakanusha maendeleo ya vikosi vya Ukraine kwenye mstari wa mbele

    Muonekano wa hivi karibuni wa angani wa jiji lililoharibiwa la Bakhmut

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Muonekano wa hivi karibuni wa angani wa jiji lililoharibiwa la Bakhmut

    Wizara ya ulinzi ya Urusi imekanusha ripoti za vyanzo vinavyounga mkono Urusi kwamba wanajeshi wa Ukraine wamepiga hatua katika mstari wa mbele mashariki mwa Ukraine.

    Yevgeny Prigozhin, mkuu wa kikundi cha mamluki cha Wagner kinachopigana upande wa Urusi, alishutumu wanajeshi wa kawaida wa Urusi kwa kuacha maeneo karibu na Bakhmut.

    Wanablogu wa kijeshi wa Urusi waliripoti maendeleo ya Kiukreni au harakati za askari katika maeneo kadhaa siku ya Alhamisi.

    Rais wa Ukraine awali alisema ilikuwa mapema mno kuanza mashambulizi dhidi yake.

    "Kwa [kile tulichonacho tayari] tunaweza kwenda mbele na, nadhani, kufanikiwa," Rais Volodymyr Zelensky alisema katika mahojiano na watangazaji wa huduma za umma ambao ni wanachama wa Eurovision News, kama BBC.

    "Lakini tungepoteza watu wengi. Nafikiri hilo halikubaliki. Kwa hivyo tunahitaji kusubiri.

    Bado tunahitaji muda zaidi." Shambulio linalotarajiwa linaweza kuwa la mwisho katika vita, na kuchora tena mstari wa mbele ambao, kwa miezi kadhaa, umebaki bila kubadilika.

    Pia litakuwa mtihani muhimu kwa Ukraine, ikiwa na hamu ya kuthibitisha kwamba silaha na vifaa ambavyo imepokea kutoka Magharibi vinaweza kusababisha mafanikio makubwa katika uwanja wa vita.

    Katika taarifa yake, wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema: "Matangazo ya mtu binafsi kwenye Telegram kuhusu 'mafanikio' kwenye maeneo kadhaa kwenye mstari wa mbele hayalingani na ukweli."

    "Hali ya jumla katika eneo maalum la operesheni ya kijeshi iko chini ya udhibiti," iliongeza. Kwa mujibu wa Bw Prigozhin, hali "pembeni" huko Bakhmut, jiji lililoharibiwa katikati ya mapigano ya umwagaji damu kwa miezi kadhaa, "ilikuwa ikistawi kulingana na hali mbaya zaidi iliyotabiriwa".

    Mwandishi wa habari wa vita wa Urusi anayeiunga mkono Kremlin Sasha Kots alidai kuwa uvamizi wa Kyiv uliokuwa ukitarajiwa sana umeanza.

    Vifaru vya Ukraine vilikuwa kwenye barabara ya pete ya Kharkiv kuelekea mpaka na Urusi, alisema, akinukuu vyanzo "vinavyoaminika".

    Madai yake hayangeweza kuthibitishwa kwa kujitegemea.

  15. Hujambo na karibu.