Kombe la Dunia: Argentina waifunga Ufaransa kwa mikwaju ya penati katika fainali ya kusisimua
Lionel Messi ameiongoza Argentina kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia baada ya kuifunga Ufaransa kwa mikwaju ya penalti katika mechi ya kusisimua katika historia ya michuano hiyo.
Argentina walionekana kupoteza kombe hilo, baada ya Kylian Mbappe kufunga mabao mawili katika dakika 10 za mwisho na kupelekea sare katika dakika za nyongeza, baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Messi na Angel di Maria kuwafanya Waargentina hao kuwa mbele kwa mabao 2-0 katika mchezo kipindi chakwanza.
Messi alirejesha uongozi wao katika kipindi cha nyongeza, kabla ya Mbappe kuwashangaza Wamarekani Kusini tena kwa mkwaju wa penalti na kujipatia hat-trick ya kwanza katika fainali ya Kombe la Dunia tangu 1966.
Lakini kipa wa Argentina Emiliano Martinez aliokoa penati ya Kingsley Coman na Aurelien Tchouameni kisha akakosa bao, na kumruhusu Gonzalo Montiel kufunga bao la ushindi na kuzua matukio ya ajabu.
Messi aliyebubujikwa na machozi afikia kilele cha maisha yake katika mchezo wa soka.
Atakumbukwa daima kwa kuandikisha historia baada ya kufunga bao lake la saba kwenye Kombe la Dunia la 2022, mabao mengi zaidi kwa mchezaji yeyote wa Argentina kwenye mashindano hayo, akimpita Mario Kempes mnamo 1978 (mabao sita).
Soma: