Rais ataka dini ya Kiislamu ikubaliane na mfumo wa nchi yake

Rais Xi Jinping wa China amewataka viongozi kuongeza juhudi katika kanuni ya kuoanisha Uislamu katika mwelekeo na dini za nchi hiyo

Moja kwa moja

  1. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu ya moja kwa moja kwa hii leo.

  2. Rwanda: Kesi ya mshukiwa wa mauaji ya kimbari ya mwaka 94 yaanza kusikilizwa,

    Beatrice Munyenyezi
    Maelezo ya picha, Beatrice Munyenyezi

    Nchini Rwanda, mahakama ya mji wa Huye kusini mwa nchi hiyo imeanza kusikiliza rasmi kesi dhidi ya Beatrice Munyenyezi, mshukiwa wa mauaji ya kimbari ya mwaka 94.

    Munyenyezi ameshtakiwa kwa makosa ya mauaji dhidi ya Watutsi na kuwa na jukumu kubwa katika ubakaji dhidi ya wanawake wakati wa mauaji ya kimbari - yeye amekanusha mashtaka hayo.

    Beatrice Munyenyezi alitimuliwa na Marekani mwaka jana baada ya kutumikia kifungo cha miaka 10 jela kwa kosa la udanganyifu.

    Mwandishi wa BBC Yves Bucyana anasema Beatrice Munyenyezi ameshtakiwa kwa makosa 5 ya mauaji ya kimbari, kuhimiza watu kufanya mauaji hayo na ubakaji wa wanawake.

    Kwa mujibu wa ushahidi wa upande wa mashtaka, Munyenyezi aliungana na wanamgambo Interahamwe kuweka vizuizi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Butare, akieleza kuwa Watutsi walipaswa kuuawa, hasa wale wanaosoma chuo kikuu - na kwamba alikuwa akitoa wito kwa wanamgambo kuwabaka wanawake kabla ya kuwaua.

    Munyenyezi ameelezwa mahakamani kuwa mwanamke aliyekuwa hatari katika kipindi cha mauaji na akifahamika kwa jina la ‘komando’ na kwamba yeye binafsi alimuuwa mtawa mmoja ambaye kwanza alitoa amri ya kubakwa kisha akamuua kwa kutumia bastola.

    Yeye amejitetea kwamba waliotoa ushahidi huo hawakumfahamu vizuri akielezea mahakamani kuwa Ushahidi wao unakinzana - huku mmoja akidai kwamba mtawa huyo aliuliwa kwenye kizuizi mwingine alidai aliuliwa hotelini.

    Alisema kwamba kamwe hakusoma katika chuo kikuu kilichopo mjini Butare kama walivyodai mashahidi akisisitiza kwamba hata hakuhitimu elimu ya sekondari na kwamba wakati wa mauaji ya kimbari alikuwa mjamzito pia akiwa na mtoto mchanga kiasi kwamba hangeweza kushughulika na vitendo vya mauaji.

    Munyenyezi mwenye umri wa miaka 52 ni mke wa Arsène Shalom Ntahobali - ambaye, yeye na mama yake Pauline Nyiramasuhuko aliyekuwa waziri wa usawa wa jinsia na ustawi wa jamii mwaka 1994, wote wametiwa hatiani kwa mauaji ya kimbari na Mahakama ya Kimataifa ya Arusha na wanazuiliwa huko Arusha.

    Soma zaidi:

  3. Linapokuja suala la ufisadi hakuna aliye juu ya sheria - Ruto

    Naibu Rais wa Kenya William Ruto
    Maelezo ya picha, Naibu Rais wa Kenya William Ruto

    Naibu Rais wa Kenya William Ruto anasema hajasikitishwa na kwamba Rais Uhuru Kenyatta hamuungi mkono anapojitokeza kuwania urais.

    Bw Ruto aliambia BBC kuwa alikuwa akigombea kama mtu anayejitegemea katika kura ya Agosti 9 na inalenga kutatua matatizo ya nchi ikiwa ni pamoja na gharama ya juu ya maisha na ufisadi “Ni [Rais Kenyatta] ambaye alijitolea yeye binafsi na kwa watu. ya Kenya kwamba angeniunga mkono.

    ‘’Lakini pia mimi ni mtu ninayeelewa kuwa yeye ni mtu mzima na anaweza kubadilisha mawazo yake, siwezi kumlaumu.’’

    Bw Ruto pia alitetea jinsi alivyodhihirisha kampeni yake kuwa ya walalahoi.

    “Nimekuza taaluma yangu kuanzia chini, bila chochote. Na nimepanda pole pole na kujifunza njia ngumu kufikia hapa nilipo leo.’’

    ‘’Ninaamini kwamba ninatoa fursa kwa watu wengine wenye asili kama yangu, na kuna mamilioni ambayo ni wengi’’

    Kuhusu rushwa, naibu rais alisema atashughulikia ufisadi uliokithiri ndani ya siku zake za kwanza madarakani.

    ‘’Tunataka hali ambayo hata kama rais ni fisadi apelekwe mahakamani kama ilivyo katika nchi nyingine hakuna aliye juu ya sheria.’’

    Soma zaidi:

  4. Wakenya ni wazuri katika kusimulia hadithi - mwandishi aliyeshinda tuzo

    Idza Luhumyo ni Mkenya wa tano kushinda tuzo hiyo ya fasihi
    Maelezo ya picha, Idza Luhumyo ni Mkenya wa tano kushinda tuzo hiyo ya fasihi

    Mwandishi Idza Luhumyo, ambaye ametoka tu kushinda Tuzo ya Caine ya uandishi wa Kiafrika, amesema kwamba yeye na Wakenya wenzake ‘’ni wazuri sana katika kusimulia hadithi [na] tuna tamaduni zinazoelezeka sana’’.

    Katika mahojiano na kipindi cha Newsday cha BBC, alidokeza kwamba hii inaweza kuwa sababu iliyomfanya sasa kuwa Mkenya wa tano kushinda tuzo hiyo ya kifahari ya fasihi, ambayo ilitangazwa Jumatatu jioni.

    Hadithi yake fupi, ‘Five Years Next Sunday,’ inafanza kwa maelezo mazuri ya nywele:

    ‘’Nywele zangu mtindo wa locs zina miaka mitano tu. Zinatiririka, kama maji. Zimejaa na ni nyeusi. Ninakataza mtu yeyote kuzigusa.Ninatumia kitambaa cheusi kuwafunika. Na jinsi zinavyojikunja, na jinsi zilivyo nzito, hunielemea na matarajio ya robo yangu.’’

    Pili, mhusika mkuu, ana uwezo wa kuita mvua kupitia nywele zake na hadithi inazingatia chaguzi anazopaswa kufanya kwa sababu hiyo.

    ‘’Tulichopenda kuhusu hadithi ilikuwa ofisi isiyoeleweka ya mhusika mkuu, ambaye ametengwa na bado anashikilia hatima ya jamii yake katika nywele zake,’’ mwenyekiti wa jopo la majaji mwandishi wa riwaya wa Nigeria Okey Ndibe alisema.

    Luhumyo aliambia BBC kwamba ‘’alifurahi’’ kushinda Tuzo ya Caine na aliona ushahidi kana kwamba hadithi yake ‘’inasikika’’ kwa watazamaji.

    Kuhusu hatua yake inayofuata, alisema sasa ana mpango wa kuandika riwaya.‘’Natumai utakuwa unasikia kutoka kwangu katika miaka michache,’’ alisema, ‘’lakini kwa sasa ninafurahia wakati huu.’’

  5. Eneo la Kramatorsk huko Ukraine lalipuliwa

    Meya wa eneo athibitisha kutokea kwa mlipuko

    Chanzo cha picha, Oleksandr Goncharenko

    Maelezo ya picha, Meya wa eneo athibitisha kutokea kwa mlipuko

    Meya wa jiji la Kramatorsk, Alexander Goncharenko ametangazwa kutokea kwa mlipuko mbaya zaidi na katika eneo hilo.

    Kulingana na yeye, kuna wahasiriwa, wazima moto na waokoaji waliopo kwenye eneo la tukio.

    Kwenye video, ambayo imechapishwa na mkuu wa utawala wa Donetsk Pavel Kirilenko, mwili mmoja wa marehemu, vyumba viwili katika jengo la makazi na magari kadhaa yaliharibiwa.

    Mkuu wa Donetsk OVA, Pavlo Kyrylenko, alisema kwamba Warusi hapo awali walipiga sehemu ya kati ya Kramatorsk kwa makombora ya angani.

    ‘’Kwa sasa, tumethibitisha kifo cha mtu mmoja. Moto ulizuka katika majengo ya makazi ambayo yalikuwa kwenye kitovu cha shambulio hilo,’’ aliandika kwenye Facebook.

    Tangu mwaka 2014 Kramatorsk ni kituo cha utawala cha mkoa wa Donetsk na idadi ya watu wapatao 150 elfu.

    Mnamo Aprili 8, watu 56 ambao walikuwa wakijiandaa kuhamishwa waliuawa baada ya kombora la Tochka-U kupiga kituo hicho, hata hivyo Urusi inakanusha kutekeleza shambulizi hilo.

    Soma zaidi:

  6. Marekani yatekeleza shambulizi la bomu nchini Somalia

    Jeshi la Marekani limewaua wapiganaji 2 wa Al Shabaab

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Jeshi la Marekani limewaua wapiganaji 2 wa Al Shabaab

    Jeshi la Marekani limewaua wapiganaji 2 wa Al Shabaab baada ya shambulio la anga kusini mwa Somalia, kulingana na Kamandi ya Marekani ya Afrika.

    Majeshi ya Marekani yalikuwa yakisaidia wakati wa operesheni ya majeshi ya Somalia.

    Shambulio hili limetokea katika kijiji cha Labikus eneo la Juba ya Chini nchini Somalia, na ni shambulio la pili ambalo Marekani imetekeleza nchini Somalia tangu Rais Joe Biden atangaze kuwa mamia ya wanajeshi wake wanaondoka Somalia.

    Kamandi ya Marekani ya Afrika (Africom) ilisema kuwa shambulio hilo la bomu lilitekelezwa wakati Al-Shabaab iliposhambulia vikosi vya Somalia.

    Uharibifu uliosababishwa na shambulio hilo haujajulikana, lakini Africom ilisema kuwa hakuna raia aliyejeruhiwa na shambulio hilo.

  7. Ukraine: Mke wa Rais yupo Marekani kwa mikutano ya ngazi ya juu

    Ziara ya Olena Zelenska mjini Washington inakuja baada ya karibu miezi mitano ya vita nchini Ukraine

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Ziara ya Olena Zelenska mjini Washington inakuja baada ya karibu miezi mitano ya vita nchini Ukraine

    Mke wa rais wa Ukraine, Olena Zelenska, yuko Marekani kwa mfululizo wa mikutano ya ngazi ya juu na kuhutubia Bunge la Congress.

    Ziara yake inakuja miezi minne baada ya mumewe, Rais Volodymyr Zelensky, kutoa hotuba ya mtandaoni kwa Congress, akishinikiza kupata vifaa zaidi vya kijeshi.

    Bi Zelenska alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken Jumatatu na anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenzake Jill Biden siku ya Jumanne, Ikulu ya White House ilisema.

    Anatarajiwa kuzungumza bungeni Capitol Hill siku ya Jumatano.

    Pambano hilo la Jumanne litakuwa mara ya pili kwa wanawake hao wawili kukutana, baada ya Dk. Biden kufanya ziara isiyotarajiwa nchini Ukraine mwezi Mei.

    Baada ya karibu miezi mitano ya vita vya Urusi nchini Ukraine, Kyiv ina nia ya kutafuta msaada zaidi wa kijeshi na uungwaji mkono wa kisiasa kutoka Marekani.

    Bunge tayari imeidhinisha karibu $40bn (£33bn) kama msaada kwa Ukraine ambao unatarajiwa kuwasilishwa kikamilifu mwishoni mwa Septemba.

    Siku ya Jumatatu, Bi Zelenska pia alikutana na Samantha Power, mkuu wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani.

    Shirika hilo limetoa mabilioni ya dola kusaidia serikali ya Ukraine kwa mahitaji ya kibinadamu, pamoja na kufanya kazi ya kukabiliana na uhaba wa chakula duniani uliochochewa na vita vya Urusi.

    Soma zaidi:

  8. Rais ataka dini ya Kiislamu ikubaliane na mfumo wa nchi yake

    Rais Xi Jinping wa China

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Rais Xi Jinping wa China

    Rais Xi Jinping wa China amewataka viongozi kuongeza juhudi katika kanuni ya kuoanisha Uislamu katika mwelekeo na dini za nchi hiyo ili kuendana na jamii ya kisoshalisti inayoshikamana na Chama cha Kikomunisti nchini China.

    Rais Xi Jinping alitembelea eneo lenye matatizo la Xinjiang ambako vikosi vya usalama vya China vimekuwa vikiendesha operesheni ya kuwadhibiti Waislamu wa Uyghur kwa muda.

    China inaaminika kuwafunga zaidi ya watu milioni moja wa Uyghur na Waislamu wengine huko Xinjiang, eneo kubwa la kaskazini-magharibi mwa China ambalo ni makazi ya watu wanaojiita waturuki.

    Serikali imekosolewa kwa kufanya ukiukaji wa haki za binadamu katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na kazi ya kulazimishwa na ubakaji.

    Soma:

  9. Wagombea wenza wanne Kenya kushiriki mdahalo wa kitaifa leo

    th

    Chanzo cha picha, File

    Wagombea wanne watachuana kwenye mdahalo wa wagombea wenza wa urais unaotarajiwa kufanyika leo jioni jijini Nairobi,Kenya .

    Wakenya wanasubiri kwa hamu mdahalo huo utakaoshirikisha kwa mara ya kwanza wagombea watatu wa kike wanaowania nafasi ya pili ya juu serikalini

    Mdahalo huo utaendeshwa katika madaraja mawili huku ule wa kwanza ukishirikisha wagombeaji ambao walipata chini ya asilimia 5 katika viwango vya umaarufu huku mdahalo wa pili utashirikisha wagombea waliopata zaidi ya asilimia 5 katika tafiti za maoni za hivi majuzi.

    Mjadala huo utafanyika kuanzia saa kumi na moja jioni hadi saa 10 usiku kwa saa za huko.

  10. Punguzo la bei ya Unga lazua maswali mengi kuliko afueni

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Tangazo la wizara ya Kilimo nchini Kenya kwamba bei ya unga wa mahindi itapunguzwa kwa wiki nne kutoka shilingi 230 hadi shilingi 100 siku 20 kabla ya uchaguzi mkuu limezua maswali mengi kuhusu afueni .

    Wengi hasa mitandaoni wamehoji nia ya serikali wakati huu ikizingatiwa kwamba wananchi wengi wamekuwa wakilalamikia bei ya juu ya unga kwa wiki kadhaa sasa bila kupata matumaini ya msaada wowote kutoka kwa upande wa serikali .

    Punguzo hilo ambalo ni la takriban asilimia 60 litadumu kwa wiki nne tun a huenda bei ikarejea kuwa ile ya juu baada ya mpango huo wa ruzuku kati ya wizara ya kilimo na wasagaji nafaka kuisha.Mpango wenyewe haujawekwa wazi na duru zinaarifu haujakamilishwa lakini utafanikishwa . Tathmini katika sehemu nyingi za kuuza bidhaa huo inaonyesha bei haijapunguzwa .

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Ruka X ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 2

    Ruka X ujumbe, 3
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 3

    Ruka X ujumbe, 4
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 4

    Ni siasa ama serikali imewahurumia wananchi?

    Mpango huo wa ruzuku ya mahindi hasa wakati huu wa kampeni umechukuliwa na baadhi kama hatua ya Rais Kenyatta, ambaye anamuunga mkono Raila Odinga wa Azimio la Umoja-kuwashawishi wa piga kura wakati huu ambapo wengi wamekuwa wakilalamikia gharama ya juu ya maisha.

    Serikali pia imeondoa tozo zote zinazotozwa kwa mahindi kutoka nje ya nchi.

    Wasagaji watawauzia wauzaji begi ya pakiti 12 za unga wa mahindi wa kilo 2 kwa Sh1,080, ambayo ina maana ya Shilingi 90 kwa pakiti.Serikali nayo itawafidia Sh1,120 kwa pakiti 12 za unga, au Sh93 kwa moja.

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Naibu Rais William Ruto amemshutumu Rais Uhuru Kenyatta kwa kucheza siasa na unga wa mahindi baada ya serikali kuchukua hatua zitakazopunguza bei ya bidhaa hiyo .

    Akihutubia mikutano ya kando ya barabara jijini Nairobi, ambayo ina wapiga kura milioni 2.4, Dkt Ruto alisema Mkuu wa Nchi aliingilia tu kuchukua hatua hiyo kama chombo cha kampeni kwa sababu uchaguzi umekaribia.

    "Hii ni serikali ile ile ambayo hapo awali ililaumu bei ya juu juu ya bidhaa kwa vita vya Ukraine na Urusi. Vita bado vinaendelea, kwa nini uliwaacha Wakenya wateseke kwa muda mrefu hivyo?” Ruto alihoji

    “Nimesikia wakisema watapunguza gharama ya unga. Mwenyekiti wa Azimio (One Kenya Coalition) ndiye Rais na Raila (Odinga) ndiye anayepeperusha bendera. Ni tofauti gani unaweza kutarajia kutoka kwake? Serikali inataka kupunguza bei ya unga kwa sababu uchaguzi umekaribia,” aliongeza.

  11. Nusu ya wakazi wa Somalia wana njaa kutokana na ukame

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Ukame mbaya zaidi katika miongo minne unaendelea katika Pembe ya Afrika.

    Shirika la Mpango wa Chakula Duniani linasema hadi watu milioni 20 nchini Kenya, Ethiopia na Somalia wako katika hatari ya njaa ifikapo mwisho wa mwaka.

    Somalia inabeba mzigo mkubwa na nusu ya watu sasa wanaokumbwa na njaa.

    Mamia kwa maelfu ya watu wanaondoka makaazi yao vijijini Somalia na kuelekea kwenye kambi za wakimbizi wa ndani.

    Mashamba yao ni tupu, mazao yamefeli , na mifugo iliyokufa imetapakaa kando ya barabara. Huu ndio ukame mbaya zaidi katika muongo uliopita kulingana na wataalam, na njaa inakaribia.

    Kuna maelfu ya watoto ambao hawajasindikizwa katika kambi. Ndugu wakubwa wamechukua nafasi ya wahudumu, kwani baba zao wamekwenda mijini kutafuta chakula, na akina mama wamekwama hospitalini ambapo kiwango cha utapiamlo kiko juu sana.

    Vifo sasa vinaripotiwa. Katika kituo kimoja huko Baidoa, angalau watoto 26 walikufa kati ya Mei na Juni, kulingana na rekodi.

  12. Hatimaye Kenya yapata Dhahabu baada ya ushindi wa Faith Kipyegon katika mbio za 1500m

    TH

    Chanzo cha picha, AFP

    Bingwa mara mbili wa Olimpiki, Faith Kipyegon wa Kenya alishinda taji lake la pili la mbio za mita 1500 kwenye ubingwa wa riadha dunia mapema leo na kuipa Kenya dhahabu yake ya kwanza katika mashindano hayo.

    Kipyegon, ambaye hapo awali alishinda dhahabu ya dunia mwaka wa 2017 pamoja na fedha mbili kutoka 2015 na 2019, alitawala mbio hizo kuanzia mwanzo hadi mwisho, akitumia muda wa ushindi wa dakika 3 na sekunde 52.96.

    "Nimefurahi sana kutwaa tena taji leo kwa sababu nililazimika kufanya bidii kulifanikisha. Ushindani ulikuwa mkali, lakini nilikuwa nimejitayarisha vyema kwa vita," Kipyegon alisema baada ya ushindi wake.

    Alipoteza taji la dunia kwa Mholanzi Sifan Hassan wakati wa Mashindano ya Riadha ya Dunia ya Doha ya 2019.

    Tangu wakati huo ameshindwa mara moja tu na Hassan kwenye mbio za Diamond League huko Florence mwaka jana.

  13. Joto kali la Ulaya linaelekea kaskazini

    th

    Chanzo cha picha, AFP VIA GETTY IMAGES

    Ulaya Magharibi inakabiliwa na hali ya joto huku wimbi la joto kali likielekea kaskazini.

    Nchini Ufaransa na Uingereza ilani za joto kali zilitolewa huku kaskazini mwa Uhispania ikirekodi halijoto ya 43C (109F) siku ya Jumatatu.

    Moto wa nyika nchini Ufaransa, Ureno, Uhispania na Ugiriki umewalazimu maelfu ya watu kuhama makazi yao.

    Uingereza inatarajiwa kushuhudia siku yake yenye joto kali zaidi na wataalam wanasema sehemu za Ufaransa zinakabiliwa na "apocalypse ya joto".

    Sehemu kadhaa za Ufaransa zilishuhudia siku zao za joto kuwahi kutokea huku mji wa magharibi wa Nantes ukirekodi nyuzijoto 42C, ofisi ya taifa ya hali ya hewa ilisema.

    Moto wa nyika katika siku za hivi majuzi umewalazimu zaidi ya watu 30,000 kukimbia, huku makazi ya dharura yakiwekwa kwa ajili ya kuwahamisha.

    Gironde, eneo maarufu la watalii kusini-magharibi, limepigwa vibaya sana, huku wazima moto wakipambana kudhibiti moto ambao umeharibu karibu hekta 17,000 (ekari 42,000) za ardhi tangu Jumanne iliyopita.

    "Wazo linalonijia kichwani ni kwamba, ni mnyama mkubwa," Jean-Luc Gleyze, rais wa mkoa wa Gironde alisema kuhusu moto huo.

  14. Natumai hujambo .Karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo