Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Urusi yashambulia miji kadhaa ya Ukraine

Wanajeshi wa Urusi wameshambulia majumba kadhaa katikati ya mji wa Kharkiv , na kuwaua watu watano huku 13 wakijeruhiwa , kulingana na maafisa wa Afya katika eneo hilo.

Moja kwa moja

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena hapo kesho majaaliwa.

  2. Mashahidi wasikilizwa katika kesi ya mshukiwa wa mauaji ya Rwanda Wenceslas Twagirayezu,

    Chumba maalum cha mahakama kuu ya Nyanza kimeanza kusikiliza mashahidi katika kesi ya mauaji ya kimbaridhidi ya Wenceslas Twagirayezu

    Twagirayezu alirejeshwa Rwanda na nchi ya Denmark mwaka 2018 kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kimbari katika maeneo 7 tofauti katika jimbo la zamani la Gisenyi, mashitaka ambayo anakanusha.

    Mashahidi 9 waliosikilizwa leo ni wa upande wa mashitaka.

    Shahidi mmoja kwa jina la Nsengiyumva, mfungwa wa mauaji ya kimbari, ameonekana kujichanganya katika kauli zake mara akisema kwamba mtuhumiwa alishiriki katika mashambulio dhidi ya watutsi waliokimbilia katika chuo kikuu cha Mudende yalitokea kabla ya ndege ya aliyekuwa Rais Habyalimana kudunguliwa ,mara nyingine akisikika akisema kuwa shambulio katika eneo hilo lilifanyika baada ya ndege kudunguliwa.

    Shahidi mwingine Gasenge Ethienne alieleza kuwa yeye alikuwa alijipatia umaarufu kwa kuuwa watutsi na kwamba alihusika katika kila shambulio lililofanywa kuwauwa watutsi katika maeneo 7 tofauti ya Gisenyi huku akisisitiza kushirikiana na Bwana Wenceslas Twagirayezu.

    Mara kwa mara alikabiliana na Twagirayezu mahakamani wakati Twagirayezu aliposema kwamba hamfahamu.

    Shahidi huyo amesema:”Hebu niangalie vizuri ,nikumbuke vizuri ,nilikuwa mwanamgambo maarufu nikitembea kwa miguu pana kutokana na kuugua funza’’

    Shahidi huyo alionyesha picha ya mshukiwa huyo anayotembea nayo popote anapokwenda. Picha hiyo imezua mabishano makali mahakamani.

    Shahidi huyo amesema kwamba alipata picha hiyo kutoka kwa familia ya mshukiwa wakimuomba awasaidie kumuondoa kwenye orodha ya washukiwa wakuu wa mauaji ya kimbari wanaosakwa na Rwanda wakati huo akiwa nchini Denmark.

    Twagirayezu alisema mahakamani kuwa ‘’ni jambo la kusikitisha kwamba bado kuna watu wenye mamlaka ya kusingizia wengine kwamba walihusika na mauaji ya kimbari’’

    Mashahidi wote wanasema kwamba Wenceslas Twagirayezu mwenye umri wa miaka 54 alikuwa na ushawishi katika kundi la wanamgambo Interahamwe waliohusika na mauaji dhidi ya watutsi kwa kufanya mashambulizi katika maeneo tofauti ya jimbo la zamani la Gisenyi

    Jumanne mahakama itaanza kusikiliza mashahidi 4 wanaomtetea Bwana Twagirayezu.

  3. Mafuriko ya KwaZulu-Natal: Afrika Kusini kutuma wanajeshi 10,000

    Jeshi la Afrika Kusini linasema linawapeleka wanajeshi zaidi ya 10,000 kusaidia katika shuguli za misaada na uokoaji kufuatia mafuriko mabaya yaliyosomba baadhi ya maeneo ya jimbo la KwaZulu-Natal wiki iliyopita.

    Zaidi ya watu 440 wamefariki, na msako unaendelea kwa ajili ya kuwasaka watu wengine 63 ambao bado hawajulikani walipo.

    Baadhi yao walisombwa na mito iliyofurika na maporomoko ya ardhi.

    Serikali imeitakanga KwaZulu-Natal eneo la mkasa.

    Maafisa wameyaelezea mafuriko kama mabaya kuwahi kuilikumba jimbo hilo.

    Waziri mkuu wa KwaZulu-Natal Sihle Zikalala amesema kuwa karibu nyumba 4,000 ziliangamia huku zaidi ya 8,000 zikiharibiwa, nyingi kati yake katika mji wa mwambao wa Durban na maeneo yanayouzingira.

  4. Bunge la somalia lashambuliwa na makombora

    Takriban watu saba, wakiwemo walinzi wa bunge wamejeruhiwa katika shambulio la makombora katika jengo la Bunge la Somalia mjini Mogadishu leo ​​asubuhi.

    Haya yanajiri huku wabunge wapya waliochaguliwa wakikutana ili kupanga tarehe za uchaguzi wa maspika na manaibu wao wa mabunge hayo mawili.

    Wabunge kutoka bunge la Somalia walikuwa wakijadili uchaguzi wa maspika wa mabunge yote mawili wakati kombora lilipotua kwenye lango la jengo la bunge maarufu kama Villa Hargeisa.

    Shambulio hilo lilisimamisha mkutano huo, na kusababisha hofu kubwa miongoni mwa wabunge waliohudhuria mkutano huo.

    Uchaguzi wa rais wa Somalia uliocheleweshwa kwa muda mrefu unaonekana kukaribia, huku wabunge wapya wakiidhinisha taratibu za uchaguzi wa Maspika wa mabunge ya juu na ya chini utakaofanyika tarehe 26 na 27 Aprili.

    Waziri mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Rooble amelaani shambulizi hilo na kusema kuwa hii inaweza kuwa kikwazo kwa mchakato wa uchaguzi.

    Uchaguzi usio wa moja kwa moja wa bunge la Somalia umekuwa ukiendelea kwa takriban mwaka mmoja, baada ya kukosa makataa muhimu yaliyowekwa kukamilisha uchaguzi wa wabunge na urais ambao umecheleweshwa kwa zaidi ya mwaka mmoja.

    Al-Shabab, kundi tanzu la al-Qaeda nchini Somalia lilidai kuhusika na shambulio hilo, na mara kwa mara hufanya mashambulizi ya mabomu mjini Mogadishu na kwingineko nchini Somalia kama sehemu ya kampeni yake ya kuiangusha serikali kuu.

    Mwezi uliopita, kundi hilo lililenga kituo cha uchaguzi katikati mwa Somalia, na kumuua mbunge aliyekuwa akizungumza na wagombea wengine.

    • Uchaguzi wa Somalia: Nchi ambayo watu hawapigi kura
    • Wanajeshi wa Kenya wauawa Somalia: Usiri unaozunguka vifo hivyo
    • Somalia, Ujinsia na mimi: Kuwa mpigapicha katika Mogadishu
  5. Vita vya ukraine: Walinzi wa Mariupol watapigana hadi mwisho anasema Waziri mkuu

    Walinzi wa mji uliozuingirwa wa Mariupol watapigana hadi mwisho dhidi ya vikosi vya Urusi, amesema Waziri mkuu wa Ukraine Denys Shmyhal.

    Mji huo wa bandari bado haujaanguka licha ya kauli ya mwisho kutoka kwa Moscow inayowataka wapiganaji wa mwisho wa Ukraine waliobakia mjini humo wajisalimishe, alisema.

    Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alisema Urusi imechagua kuiporomosha ardhini Mariupol.

    Maafisa wa eneo hilowalisema vikosi vya Urusi vimetangaza kuwa vitamzuwia yeyote kuingia au kutoka mjini humo.

  6. Picha zinazoonyesha uharibu uliosababishwa na makombora ya Urusi katika shambulio la Lviv

    Watu saba wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa baada ya Urusi kufanya shambulio la kombora katika ngome ya kijeshi ya Ukraine iliyopo Lviv.

    Na hizi ndizo picha za matukio kuhusu shambulio hilo:

  7. 'Mane alikuwa na matatizo ya kimwili'

    Akizungumza kumuhusu Sadio Mane na ushindani kutoka kwa Luiz na Diaz, Meneja wa Liverpool Jugen Klopp amesema: "Nimemfahamu Sadio kwa karibu miaka sita, na kulingana na ninavyomfahamu hajawahi kuhitaji ushindanibora zaidi ya ubora wake. Sina uhakika kama kumleta Luis kuliathiri sehemu ya mechi yake. Lakini kucheza safu ya kati kunamfaa pia vyema sana Sadio''.

    "Sadio alikuwa maumivu ya mwili tangu aliporejea kutoka katika michezo ya AFCON. Hakuweza kutumia mwili wake mkubwa wa kimwili kila baada ya siku chache. Kabla ya mechi dhidi ya Manchestere City, Nilifikiria hilo, inaonaekana kama kimwili Sadio hakuwa sawa na ndio maana alicheza mechi kama alivyocheza ."

  8. Saudi Arabia yalaani walioichoma Qurani

    Serikali ya Saudia imewalaani Waswidi wenye itikadi kali walioichoma kwa "makusudi’’ Qurani Takatifu, ikisema kuwa ililenga kuchochea mapigano na , ghadhabu miongoni mwa Waislamu.

    Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu , Wizara ya mambo ya nchi za nje ilisisitizia umuhimu wa mazungumzo, kuamimiana na ushirikiano.

    Taarifa hiyo pia ilisisitizia juu ya kuwepo kwa haja ya kupambana na chuki na ubaguzi yenye misingi ya dini na itikadi kali.

    Saudi Arabia pia imetoa wito wa kumalizwa kwa ghasia za kidini katika miji mitakatifu.

    Watu watatu wamejeruhiwa katika mji mkuu wa Uswidi, Norrkoping, baada ya polisi kufyaa risasi wakati wa ghasia zilizotokea baada ya kuchomwa kwa Qurani, maandamano yaliyoibuka katika miji kadhaa mwishoni mwa juma.

  9. Simba mguu mmoja nusu fainali Shirikisho

    Kocha wa timu ya soka ya Orlando Pirates Mandla Ncikazi amemshutumu muamuzi wa mchezo kati yao na Simba sports club ya Tanzania kwa kuwanyima penati ya wazi na kisha baadaye kuwapatia wapinzani wao penati iliyowapatia ushindi.

    Sambamba na tuhuma hizo pia aliwatuhumu waWatanzania kuwatendea kama wanyama na kuuliza iwapo Simba wakienda Afrika kusini wa wafanyie hivyo hivyo.“Kila tulikopita tunafanywa kama wanyama na kupokea matusi”

    Akiongea na waandishi wa habari baada ya mchezo kocha huyo raia wa Afrika kusini alisema matumizi ya VAR hayakufanyika, licha ya kuwepo kwa mfumo huo ambao ulikuwa unatumika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.

    Simba iliibuka na ushindi wa goli moja bila ambalo linaitanguliza mguu mmoja kwenye nusu fainali kabla Kombe la Shirikisho la mchezo wa marudiano ambao utapigwa huko Afrika kusini mwishoni mwa juma.

    Katika mchezo wa Dar es salaam Simba iliruhusiwa kujaza uwanja na mashabiki walijitokeza kwa wingi wao .

    kwa mujibu wa Afisa habari wa Simba, mashabiki zaidi ya elfu hamsini walihudhuria uwanjani kushuhudia mtanange huo.

    Miaka ya hivi karibuni Simba imekuwa hatari inapocheza kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Benjamin Mkapa ambao unauwezo wa kuchukua mashabiki elfu sititini.

  10. Waukraine wanne wauawa wakijaribu kukibilia mji wa mashariki- Mkuu wa kikanda

    Raia wanne wameuawa kwa kupigwa risasi na mmoja kujeruhiwa walipokuwa wakijaribu kuukimbia mji wa Kreminna, kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Luhansk Serhiy Haidai.

    Alisema jeshi la Urusi liliwafyatulia risasi kwa raia waliokuwa wakijaribu kuondoka kwa gari wao wenyewe.

    Hakutakuwa na korido za kibinadamu kwa raia wa Ukraine wanaokimbia vita kwa siku ya pili mfululizo, baada ya Ukraine na Urusi kushindwa kukubaliana juu ya mipango.

    Haidai alionya watu katika taarifa akisema: "Usitoke mafichoni. Usijaribu kuondoka Kreminna peke yako! Ni hatari!"

    Alisema Warusi "walimechukua udhibiti" wa mji huo na mapigano yanaendelea, akiongeza kuwa "kuwahamisha watu kutoka mji huo hauwezekani tena".

    Kwa upande wake naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Iryna Vereshchuk alisema: Hakutakuwa na njia ya kuwaondoa raia katika maeneo yaliyoathiriwa kwa siku ya pili mfululizo baada ya maafisa wa Ukraine kushindwa kukubaliana kuhusu njia za kibinadamu.

  11. Urusi yadai kushambulia ngome 315 za Ukraine usiku kucha

    Vyombo vya habari vya serikali ya Urusi vinaripoti kuwa jeshi lake lilishambulia jumla ya malengo 315 nchini Ukraine usiku kucha na miji kadhaa ikishambuliwa Jumatatu.

    Wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema kuwa imeharibu maghala manne ya silaha na vifaa vya kijeshi nchini Ukraine usiku kucha kwa makombora ya Iskander, kombora la masafa mafupi, shirika la habari la TASS linaripoti.

    "Makombora ya anga ya juu yaliharibu vituo 16 vya kijeshi vya Ukraine usiku wa kuamkia leo," msemaji wa wizara ya ulinzi ya Urusi Igor Konashenkov alisema.

    Aliongeza kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi iliwaangusha wapiganaji wawili wa Ukraine.

    BBC haijafanikiwa kuthibitisha madai haya.

    Hata hivyo Yuri Sak - mmoja wa washauri wa waziri wa ulinzi wa Ukraine, ambaye yuko magharibi mwa Ukraine - amekuwa akizungumza na BBC kuhusu mashambulio katika mji wa Lviv.

    "Kilichotokea leo ni kitu cha kutisha kwa sababu hili ni shambulio kubwa la kombora [dhidi] ya miundombinu ya kiraia," aliambia kipindi cha Leo cha BBC Radio 4.

  12. Maafa na majeruhi yaripotiwa Lviv bada ya shambulio la makombora

    Watu sita wameuawa na wanane kujeruhiwa mjini Lviv baada ya makombora kushambulia vituo vya kijeshi na kituo cha kutolea huduma ya matairi ya gari katika mji wa magharibi mwa Ukraine asubuhi ya leo, gavana wa eneo hilo Maksym Kozytsky amethibitisha.

    Mtoto mmoja alikuwa miongoni mwa waliokufa, alisema.

    Mamlaka ya Ukraine katika eneo la kusini la Dnipropetrovsk pia iliripoti milipuko kadha siku ya Jumatatu, na kusema baadhi ya makombora hayo yalipiga maeneo karibu na kituo cha reli na vituo vingine vya reli.

    Kwa mujibu wa Mamlaka ya Anga ya Magharibi, makombora manne yalipiga Lviv, na kuacha vifaa vikiwa vimeharibiwa vibaya, na moto uliozuka kutokana na mapigo hayo bado unaendelea kuzimwa.

    BBC haijaweza kuthibitisha madai haya.

    Unaweza pia kusoma

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  13. Ni nini kilitokea kwenye meli ya kivita ya Urusi iliyozama?

    Picha ambazo hazijathibitishwa za meli ya kivita ya Urusi iliyoshambuliwa kwa makombora - inayodaiwa kuzama Moskva - zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii.

    Lakini tunafahamu nini kuhusu kuzama kwa meli hiyo?

    Moskva ilikuwa sehemu muhimu ya mkakati wa jeshi la majini la Urusi nchini Ukraine - meli ya kivita ya wafanyakazi 510 ambayo ilikuwa ya tatu kwa ukubwa katika meli zinazofanya kazi za Moscow, ikiwa na safu ya silaha za kupambana na meli na manowari, pamoja na ulinzi mkali.

    Kwa hivyo Ukraine iliposema kuwa imezamisha Moskva kwa kutumia makombora yake ya Neptune, tukio hilo lilionekana kuwa ushindi mkubwa na muhimu kiishara.

    Lakini Urusi ina ilikuwa na maelezo tofauti kuhusu tukio hilo. Inadai kuwa mlipuko wa risasi ndani ya ndege ulisababisha moto, na meli ilizama ilipokuwa ikivutwa kurudi bandarini.

    Urusi pia inasema wafanyakazi wote waliondolewa salama.

    Ilichapisha video siku ya Jumamosi ikonyesha baadhi ya wafanyakazi wakiwa salama.

    Unaweza pia kusoma

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  14. Urusi inakamilisha uundaji wa 'kundi la fujo': Ukraine

    Vikosi vya jeshi la Urusi vinakamilisha kuunda kundi lenye vurugu katika eneo la Oparesheni ya Mashariki, vikosi vya jeshi vya Ukraine vimesema katika taarifa zao za kila siku. Hiki ndicho kingine walichosema:

    • Wanajeshi wa Urusi wameendelea na vizuizi vidogi vidogo huko Kharkiv.
    • Huko Donetsk, makombora yameendelea kurushwa katika ameneo ya makazi ya Siversk na Pokrovsk.
    • Majaribio ya Urusi ya kuvamia Novotoshkivsk, Popasna huko Luhansk na Avdiyivka na Maryinka huko Donetsk hayakufaulu.
    • Wanajeshi wa Urusi bado wanajaribu kuingia kwenye mipaka ya kiutawala ya Kherson.

    BBC haijafankiwa kuthibitisha maelezo haya.

  15. Ukraine yakaidi makataa ya Mariupol huku Kharkiv ikishambulia kwa makombora

    Maafisa wa Ukraine wamekataa matakwa ya vikosi vya Urusi kuwa watetezi wa mji wa Mariupol wanapaswa kuweka chini silaha zao.

    Waziri Mkuu Denys Shmyhal alisema katika mahojiano na ABC kwamba vikosi vya Ukraine ambavyo bado viko mjini "vitapigana hadi mwisho".

    Wanajeshi wa Kikosi cha Azov bado wamejificha kwenye jengo kubwa la chuma la Azovstal, lakini Urusi imetoa njia salama kwa wale wanaojisalimisha.

    Kuteka mji mzima kunaonekana kama zawadi kuu ya kimkakati kwa Urusi, na kuiacha ikidhibiti eneo kubwa la kusini na mashariki mwa Ukraine.

    Wakati huo huo mjini Kharkiv, mashambulizi ya mabomu yanaendelea, huku takriban watu watano wakiuawa na 13 kujeruhiwa.

    Moto unasemekana kutanda katika jiji lote. Mwandishi wa BBC Joe Inwood aliyeko Dnipro anasema ving'ora vya mashambulizi ya anga katika eneo la mashariki mwa Ukraine vimetoka kwa hapa na pale hadi karibu mara kwa mara.

    Unaweza pia kusoma

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  16. Urusi inapanga kuuangamiza mji wa Mariupol - waziri wa Ukraine

    Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine anasema mji wa Mariupol "haupo tena".

    Mji wa bandari wa kusini-mashariki umeharibiwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya Urusi tangu vita kuanza karibu miezi miwili iliyopita.

    Dmytro Kuleba aliambia kipindi cha Face the Nation cha chombo cha habari cha CBS siku ya Jumapili kwamba wanajeshi wavamizi "wameamua kuharibu jiji hilo kwa gharama yoyote ile ".

    Huku hayo yakijiri mshauri wa Meya wa Mariupol anasema kuwa majeshi ya Urusi yanatoa "pasi maalum" tkwa wale waliosalia mjini humo.

    Petro Andriushchenko - ambaye kwa sasa hayupo jijini lhumo lakini anaangazia habari za eneo hilo - alitoa madai hayo kupitia Telegram Jumapili, akishirikisha mtandaoni picha inayoonekana kuwaonyesha watu wakiwa wamepanga foleni.

    "Mamia ya raia wanapanga foleni kupata pasi, wale ambao hawtaitikia wito huo watatizika kutoka wilaya moja hadi nyingine, au kutembea mtaani,"aliandika.

    Andriushchenko alipendekeza kwamba vikosi vya uvamizi labda vilikuwa vinakusanya habari juu ya, au kuchuja, wale waliosalia katika jiji.

    BBC haijathibitisha madai ya afisa huyo.

    Urusi inadai kuwa na udhibiti wa sehemu kubwa ya jiji hilo, huku watetezi wa Ukraine wakiripotiwa kuzuiliwa katika eneo kubwa la viwanda linaloitwa Azovstal steelworks.

    Maafisa wa Urusi walijitolea kuokoa maisha ya wanajeshi hao ikiwa watajisalimisha siku ya Jumapili - toleo ambalo lilipuuzwa.

  17. Urusi yashambulia miji kadhaa ya Ukraine

    Karibu katika habari zetu za moja kwa koja kuhusu matukio ya Ukraine huku bara Ulaya likiamka alfajiri.

    Huu hapa mkusanyiko wa matukio ya hivi punde:

    Wanajeshi wa Urusi wameshambulia majumba kadhaa katikati ya mji wa Kharkiv , na kuwaua watu watano huku 13 wakijeruhiwa, kulingana na maafisa wa Afya katika eneo hilo.

    Mji huo uliopo kaskazini mashariki, karibu na mpaka wa Urusi umeharibiwa vibaya na mashambulio ya awali ya Urusi.

    Mwandishi wa BBC Joe Inwood aliyepo mjini Dnipro anasema kwamba ving’ora vinasikika mara kwa mara mashariki mwa Ukraine, kutoka Kharkiv hadi katika maeneo kama vile Zolote, kijiji kilichopo katika jimbo la mapambano la Donbas.

    Mji wa kusini wa Mykolaiv na maeneo yaliopo karibu yalishambuliwa na Urusi kulingana na gavana Vitaliy Kim aliyeambia BBC. Vikosi vya Ukraine katika eneo hilo vimezuia majaribio ya Urusi ya kusonga mbele hadi katika mji wa Bandari wa Odesa.

    Waziri mkuu wa Ukraine Denys Shymhal anasema kwamba mji wa Mariupol ulioharibiwa na mashambulio bado haujatekwa na kwamba vikosi vya Ukraine vilivyopo katika eneo hilo vitapigana kufa kupona.

    Urusi ilikuwa imewapatia makataa wapiganaji katika eneo hilo kusalimu amri ili kuokoa maisha yao – ombi ambalo limepuuziliwa mbali.

    Jenerali mwengine wa Urusi ameuawa katika makabiliano – naibu kamanda wa jeshi la nane Meja jenerali Vladimiri Frolov.

    Mwisho wa mwezi Machi, maafisa wa Ulaya walisema kwamba Urusi ilikuwa imepoteza majenerali wake saba katika vita hivyo kufikia sasa.Urusi haijathibitisha idadi hiyo.

    Wanajeshi 40 wa majini wa Urusi pia wanadaiwa kufariki, huku makumi ya wengine wakijeruhiwa na wengine kutoweka baada ya meli ya kivita ya Moskva kushambuliwa na makombora ya Ukraine.

    Hadi kufikia sasa wizara ya ulinzi nchini Urusi haijatoa tamko kuhusu walioathirika.

    Unaweza pia kusoma

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  18. Natumai hujambo. Ni asubuhi nyengine ambapo ulimwengu unaendelea kusherehekea siku kuu ya pasaka. Nasi hapa BBC tunaendelea kukupasha na matukio tofauti duniani na hususan yale ya kule Ukraine