Wizara ya Ulinzi ya Urusi yasema inadhibiti jaribio la uvamizi wa Ukraine

Wizara ya Ulinzi ya Urusi inasema wanajeshi wake "wanaendelea kudhibiti jaribio la uvamizi" la vikosi vya Ukraine katika eneo la Kursk.

Muhtasari

  • Wizara ya Ulinzi ya Urusi yasema inadhibiti jaribio la uvamizi wa Ukraine
  • Zelensky athibitisha kwamba wanajeshi wa Ukraine wanapambana ndani ya Urusi
  • Programu ya kupunguza vifo vya tembo yazinduliwa nchini India
  • Kamala Harris asema vifo vya raia ni 'vingi sana' Gaza
  • Miili yote yapatikana baada ya watu 62 kufariki katika ajali ya ndege ya Brazil

Moja kwa moja

Lizzy Masinga

  1. Maporomoko ya udongo katika eneo la kutupa taka Uganda yaua watu 12

    Jalala

    Chanzo cha picha, AFP

    Takribani watu 12 sasa wameripotiwa kufariki dunia baada ya kutokea maporomoko ya udongo katika eneo kubwa la kutupa taka katika mji mkuu wa Uganda, Kampala.

    Waokoaji wanaendelea kuchimba uchafu huo kwa matumaini ya kupata manusura zaidi baada ya maporomoko hayo yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha kwa wiki kadhaa.

    Jalala la Kiteezi lenye ukubwa wa ekari 36 (hekta 14) ndilo pekee linalohudumia Kampala nzima, jiji ambalo linakadiriwa kuwa na watu milioni nne.

    Mamlaka za jiji zimeripotiwa kujaribu kutafuta eneo jipya kwa miaka mingi.

    Kilima kikubwa kilichoundwa na mrundikano wa takataka kiliporomoka Ijumaa usiku, na kufunika nyumba kwenye ukingo wa eneo hilo wakati wakazi walikuwa wamelala, linaripoti shirika la habari la Reuters.

    Siku ya Jumamosi, idadi ya waliofariki ilitolewa kuwa wanane, wakiwemo watoto wawili.

    Msemaji wa polisi wa Kampala Patrick Onyango aliambia AFP siku ya Jumapili kwamba miili minne zaidi imetolewa, huku watu 14 wakiokolewa.

  2. Wizara ya Ulinzi ya Urusi yasema inadhibiti jaribio la uvamizi wa Ukraine

    silaha

    Chanzo cha picha, Viacheslav Ratynskyi/Reuters

    Wizara ya Ulinzi ya Urusi inasema wanajeshi wake "wanaendelea kudhibiti jaribio la uvamizi" la vikosi vya Ukraine katika eneo la Kursk.

    Inasema "jaribio za vikundi vya maadui wanaotembea kupenya kwenye magari ya kivita ndani kabisa ya eneo la Urusi" yamezimwa.

    Wizara hiyo inataja maeneo matatu katika eneo la Kursk, kuanzia kati ya 25km (maili 15) na 30km (maili 19) kutoka mpaka na Ukraine, ambapo inasema vikosi vya Ukraine vilipigwa.

    Inaongeza kuwa Ukraine ilipoteza wanajeshi 230 na magari 38 ya kivita katika saa 24 zilizopita.

    Madai ya Urusi hayajathibitishwa. Ripoti hii ni sawa na ile iliyotolewa siku zilizopita.

  3. Zelensky athibitisha kwamba wanajeshi wa Ukraine wanapambana ndani ya Urusi

    Magari ya mizinga

    Chanzo cha picha, RUSSIAN DEFENCE MINISTRY HANDOUT/EPA-EFE

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekiri kwa mara ya kwanza kwamba jeshi lake linaendesha mashambulizi ya kuvuka mpaka ndani ya eneo la Kursk magharibi mwa Urusi.

    Katika hotuba yake ya video Jumamosi jioni, Bw Zelensky alisema jeshi la Ukraine lilikuwa likipambana kwenye "eneo la wavamizi".

    Kyiv ilianzisha mashambulizi ya kushtukiza siku ya Jumanne, na kusonga mbele kwa kasi zaidi ya kilomita 10 (maili sita) ndani ya Urusi ,uvamizi mkubwa zaidi tangu Moscow kuanza uvamizi nchini Ukraine mnamo Februari 2022.

    Huko Ukraine, mji mkuu wa Kyiv na mikoa mingine kadhaa ilikumbwa na shambulio la ndege isiyo na rubani ya Urusi mapema Jumapili, maafisa wa eneo hilo walisema.

    Katika hotuba yake, Rais Zelensky aliwashukuru "wapiganaji" wa Ukraine na kusema kuwa amejadili kuhusu operesheni hiyo nchini Urusi na kamanda mkuu wa jeshi la nchi hiyo Oleksandr Syrskyi.

    Unaweza kusoma;

  4. Programu ya kupunguza vifo vya tembo yazinduliwa nchini India

    Tembo

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Jimbo la Assam nchini India limeanzisha programu ya simu ya mkononi inayolenga kupunguza vifo vinavyosababishwa na tembo.

    Programu ya Haati itawaonya watu kukaribia makundi ya tembo ili kuwaruhusu kuondoka njiani.

    Assam ina mojawapo ya idadi kubwa ya tembo nchini India na idadi kubwa ya tembo na vifo vya binadamu vinavyosababishwa na mwingiliano wao.

    Wahifadhi wanasema tembo wanazidi kuwa wakali huko Assam kwa sababu makazi yao yanapungua, na hata korido zao za asili zinavamiwa.

    Takribani watu 1,701 waliuawa na tembo nchini India kutoka 2020 hadi 2024, kulingana na data rasmi iliyotajwa na Hindustan Times mnamo Machi.

    Programu iliyoanzishwa huko Assam imetengenezwa na Aaranyak, shirika la bioanuwai kaskazini-mashariki mwa India.

    Pia inawawezesha waathiriwa na jamaa zao kuomba fidia kutoka kwa serikali ya mtaa katika visa vya majeraha au kifo kutokana na kushambuliwa na wanyama.

    Aaranyak pia imezindua kitabu cha mwongozo kuhusu uzio unaotumia nishati ya jua ambao unaweza kuwazuia tembo. Kulingana na shirika la usaidizi la wanyamapori WWF, kuna tembo wasiopungua 50,000 wa Asia waliosalia porini.

    Unaweza kusoma;

  5. Kamala Harris asema vifo vya raia ni 'vingi sana' Gaza

    Athari za mashambulizi

    Chanzo cha picha, MAHMOUD ZAKI/EPA-EFE/REX/Shutterstock

    Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amelaani kupoteza maisha ya raia katika shambulio la anga la Israel dhidi ya jengo la shule huko Gaza siku ya Jumamosi.

    Zaidi ya watu 70 waliuawa katika jengo lililokuwa likiwahifadhi Wapalestina waliokimbia makazi yao, mkurugenzi wa hospitali moja ameiambia BBC.

    Bi Harris alisema raia "wengi sana" wameuawa "bado tena" na akasisitiza wito wa makubaliano ya kutekwa nyara na kusitishwa kwa mapigano, akirejea maoni yaliyotolewa na Ikulu ya Marekani.

    Msemaji wa jeshi la Israel amesema shule ya al-Taba’een "inatumika kama kituo cha kijeshi cha Hamas na Islamic Jihad", jambo ambalo Hamas inakanusha.

    Akizungumza katika kampeni huko Phoenix, Arizona, Bi Harris alisema Israel ilikuwa na haki ya "kuwafuata Hamas" lakini pia ina "jukumu muhimu" ili kuepuka madhara kwa raia.

    Shambulio la anga la Jumamosi limekosolewa na mataifa yenye nguvu ya Magharibi na kikanda, huku Misri ikisema ilionesha kuwa Israel haina nia ya kufikia usitishaji vita au kumaliza vita vya Gaza.

    Fadl Naeem, mkuu wa Hospitali ya al-Ahli ambako wengi wa majeruhi walipelekwa, alisema karibu waathiriwa 70 walitambuliwa saa chache baada ya shambulio hilo, huku mabaki ya wengine wengi yakiwa yameharibika vibaya kiasi kwamba utambuzi ulikuwa mgumu.

    Jeshi la Israel lilisema "limewashambulia haswa magaidi wa Hamas wanaoendesha shughuli zao ndani ya kituo cha udhibiti wa Hamas kilichowekwa katika shule ya al-Taba'een".

    Taarifa ya Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) na Shirika la Usalama la Israel ilisema "takribani magaidi 19 wa Hamas na Islamic Jihad" "walitokomezwa" katika shambulio hilo.

    Msemaji wa IDF Adm Daniel Hagari alisema "dalili mbalimbali za kijasusi" zinaonesha "uwezekano mkubwa" kwamba kamanda wa Kikosi cha Kambi Kuu cha Islamic Jihad, Ashraf Juda, alikuwa katika shule ya Taba'een ilipopigwa. Alisema bado haijabainika iwapo kamanda huyo aliuawa katika shambulio hilo.

    Unaweza kusoma;

  6. Miili yote yapatikana baada ya watu 62 kufariki katika ajali ya ndege ya Brazil

    Eneo la ajali

    Chanzo cha picha, EPA

    Miili yote imepatikana katika eneo la ajali ya ndege katika jimbo la São Paulo nchini Brazil na kusababisha vifo vya watu wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo, mamlaka imethibitisha.

    Timu zilikuwa zikifanya kazi kutafuta na kutambua waathirika wa janga hilo baada ya turboprop ya injini-mbili inayoendeshwa na shirika la ndege la Voepass kushuka katika mji wa Vinhedo.

    Idadi ya waliojeruhiwa mpaka Jumamosi ilikuwa imefika 62.

    Voepass lilisema hapo awali kwamba ATR 72-500 ilikuwa na abiria 57 na wafanyakazi wanne kati ya Cascavel katika jimbo la kusini la Paraná hadi uwanja wa ndege wa Guarulhos katika jiji la São Paulo. Lakini baadaye ilithibitisha kuwa kulikuwa na abiria mwingine ambaye hajulikani alipo kwenye ndege hiyo.

    Picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilionesha ndege ikishuka wima, ikizunguka huku ikianguka.

    Jimbo la São Paulo lilisema lilihitimisha operesheni yake ya kuondoa miili ya waathirwa kutoka eneo hilo saa 18:30 saa za ndani (22:30 BST) siku ya Jumamosi.

    Iliongeza kuwa miili hiyo, wanaume 34 na wanawake 28, walikuwa wakihamishiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha polisi katika mji wa São Paulo, ambapo watatambuliwa na kukabidhiwa kwa familia.

    Wawili kati ya waathiriwa, nahodha na afisa mkuu, tayari wametambuliwa, serikali ilithibitisha.

    Hapo awali, Capt Maycon Cristo, msemaji wa idara ya zima moto, alisema timu zinategemea mambo kadhaa kusaidia kutambua abiria.

    Hizi ni pamoja na hati na nafasi zao walizokuwa wameketi, pamoja na simu za mkononi zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya walioathirika.

  7. Habari za asubuhi, karibu katika taarifa zetu