Wabunge wa chama tawala cha Korea Kusini cha People Power Party
(PPP) 107
kati ya 108
wa chama tawala, 107 wameondoka bungeni kabla ya kura ya kumuondoa madarakani
tais wa nchi hiyo. Wabunge sasa waliztarajiwa kupigia
kura hoja ya kumuondoa madarakani Rais Yoon Suk Yeol anayezongwa na kashfa.
Huenda chama hicho
kilitumia mkakati wa kususia upigaji kura ili kuzuia watu kuasi, kwani kura ya kumuondoa ni kupitia kura
zisizojulikana.
Ahn
Cheol-soo, profesa aliyegeuka kuwa mwanasiasa ambaye aliwania urais mwaka wa
2012, 2017 na 2022, ndiye mwanachama pekee wa PPP ambaye amesalia katika kiti
chake.
Ahn amekuwa
akisema mara kwa mara kuwa atapiga kura ya kufunguliwa mashtaka ikiwa rais
hatajiuzulu kwa hiari kabla ya upigaji kura.
Wabunge wa wengi wa vyama vya upinzani wamekusanyika
bungeni . Walikimbia mara tu wabunge walipoanza kuondoka, wakijaribu kuwazuia kuondoka.
Walikuwa wakiimba "wasaliti" na "rudi tena
kupiga kura".
Kuna hasira kubwa. Ni mwanachama mmoja tu au wawili wa chama tawala ambao
bado wamesalia ndani ya ukumbi, ikimaanisha kuwa kura hii sasa haitapigwa,
amesema mwandishi wa BBC mjini Seol.
Nje ya bunge, kulikuwa na umati wa watu huku Wakorea wengi zaidi wakikusanyika kwenye
barabara ya bunge la ttaifa. Polisi wameimarisha hali ya usalama.
Maandamano hayo yapo karibu na kituo cha treni ya chini
ya ardhi, na vizuizi vikubwa vinaweza kuonekana kwenye kituo cha usafiri mapema huku watu wakimiminika.
Mamlaka iliamua kufunga kituo hicho, na polisi wamepanga
mistari kwenye maeneo mbalimbali kuongoza umati wa watu wanaoandamana.