Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Iran yaishambulia Israel kwa makombora
Katika taarifa ya video, msemaji wa IDF Daniel Hagari anawaambia watu wafikie eneo lililo salama zaidi katika maeneo yao na kusubiri maagizo zaidi.
Muhtasari
- Mwanamke wa China akamatwa Ujerumani kwa tuhuma za ujasusi
- Iran inajiandaa kuishambulia Israel kwa makombora - Marekani
- Kwa sasa hatupigani moja kwa moja nchini Lebanon - IDF
- Seneta wa Kenya awasilisha hoja ya kujadili mienendo ya Rais
- Kenya: Wabunge waanza mchakato wa kumwondoa naibu rais afisini
- Zaidi ya watoto 20 wahofiwa kufariki katika ajali ya basi nchini Thailand
- Watu milioni moja wamekimbia makazi yao nchini Lebanon - Waziri Mkuu
- 'Wakati mwingine nahisi heri tufe,' mtu aandika kwenye kikundi chetu cha WhatsApp
- Je hii inaweza kuwa Gaza nyingine?, BBC yahoji jeshi la Israel
- Israel yasema Hezbollah inawatumia raia kama 'ngao za binadamu'
- Israel na Hezbollah: Uvamizi wa ardhini unakuja na hatari kwa Israel
- Mbivu na mbichu kujulikana Kenya huku wabunge wakijiandaa kuwasilisha hoja ya kumtimua naibu rais
- Tazama: Milipuko yaonekana kwenye mpaka wa lsrael na Lebanon
- Nyota wa mpira wa kikapu katika NBA Dikembe Mutombo amefariki dunia kutokana na saratani ya ubongo akiwa na umri wa miaka 58
- Israel yasema operesheni ya ardhini "yenye mipaka, na inayolenga" maeneo inaendelea nchini Lebanon
Moja kwa moja
Na Ambia Hirsi & Dinah Gahamanyi
Katika picha: Makombora yaliyorushwa na Iran huko Tel Aviv
Awali tuliripoti kuwa Iran imefanya mashambulizi ya makombora dhidi ya Israel. Hizi ni baadhi ya picha zinazoonyesha hali ilivyokuwa wakati huo mjini Tel Aviv.
Habari za hivi punde, Iran yathibitisha kuishambulia Israel kwa makombora
Televisheni ya taifa ya Iran imeangazia taarifa kutoka kwa IRGC (lslamic Revolution Guard Corps) ikithibitisha kuwa "makumi" ya makombora yamerushwa kuelekea Israel, na kutishia shambulio jingine iwapo Israel itajibu.
Iran inasema shambulio hilo la makombora ni la kulipiza kisasi mauaji ya mwezi Julai ya kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh, pamoja na kiongozi wa Hezbollah, Hassan Nasrallah, siku ya Ijumaa - na kwa mauaji ya watu wa Lebanon na Wapalestina.
Inasema jeshi lake la anga lilikuwa limeazimia kulenga "kambi muhimu" na litatangaza maelezo baadaye.
Habari za hivi punde, Iran yaishambulia Israel kwa makombora
Jeshi la Israel, linasema kuwa Iran imerusha makombora mjini Tel Aviv.
Kikosi cha Ulinzi cha Israel (IDF) kinawahimiza Waisraeli "kuchukuwa tahadhari na kuzingatia maagizo ya amri ya kusalia majumbani".
"Ukisikia sauti ya king'ora kimbilia eneo eneo salama na ukae hapo hapo hadi taarifa maelezo zaidi yatakapotolewa," inaongeza.
Milipuko unayoisikia ni ya mifumo ya kuzuia makombora yaliyorushwa," taarifa ya Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) inasema.
Pia inaongeza kusema kuwa jeshi "kwa sasa linatathmini hali ilivyo".
Mwanamke wa China akamatwa Ujerumani kwa tuhuma za ujasusi
Mwanamke mmoja raia wa China amekamatwa mjini Leipzig Ujerumani kwa tuhuma za kutoa habari kuhusu uwanja wa ndege wa Leipzig/Halle, ambao unatumika kama kitovu muhimu cha usafirishaji wa vifaa vya ulinzi vya Ujerumani, kwa majasusi wa China.
Waendesha mashtaka wa Ujerumani walisema Yaqi X, 38, amekuwa akifanya kazi katika kampuni inayotoa huduma za usafirishaji katika uwanja wa ndege.
Waendesha mashtaka pia wanasema mwanamke huyo mara kwa mara alituma maelezo juu ya ndege, abiria na usafirishaji wa shehena ya kijeshi kwa mtu mwingine ambaye anasadikiwa kufanya kazi katika idara ya ujasusi ya China.
Uwanja wa ndege wa Leipzig/Halle unachukuliwa kuwa kituo muhimu cha mauzo ya nje ya vifaa vya ulinzi, hususan kwa taifa la Ukraine.
Mshukiwa wa pili, Jian G, alikamatwa mapema mwaka huu.
Habari za hivi punde, Iran inajiandaa kuishambulia Israel kwa makombora-Marekani
Afisa mkuu wa Ikulu ya White House ameiambia CBS mshirika wa BBC kwamba Iran inajiandaa "kuzindua shambulio la kombora la balestiki dhidi ya Israel".
"Shambulio la moja kwa moja la Iran dhidi ya Israel litakuwa na madhara makubwa kwa Iran," afisa huyo anaonya, akiongeza kuwa Marekani inaunga mkono "maandalizi ya kujihami ili kuilinda Israel dhidi ya shambulio hilo".
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametoa wito kwa Waisraeli kuzingatia maagizo ya usalama ya maafisa wa nchini.
Katika hotuba kwa njia ya video kwa taifa, Netanyahu anasema Israel "imo katikati ya kampeni dhidi ya mhimili wa uovu wa Iran".
Anasema Israel "imedhamiria" kuwarejesha wakazi wake katika makazi yao kaskazini mwa nchi, lakini anaongeza "changamoto kubwa" zinazotarajiwa kufikia hilo.
Netanyahu amewataka Waisraeli "kufuata kikamilifu maagizo" kamandi ya jeshi la nyumbani na "kusimama pamoja". “Kwa pamoja tutapambana na kwa pamoja tutashinda,” aliongeza kusema.
Kwa sasa hatupigani moja kwa moja nchini Lebanon - IDF
Msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari anasema: "Kwa sasa hatukabiliani moja kwa moja [na Hezbollah] lakini tunaichukulia kwa uzito,"
Hagari ameongeza kuwa vikosi vya Israel "viko tayari kupigana" na vikosi vya Hezbollah, lakini pia anasema Israel haina mpango wa kufika Beirut, au miji yoyote ya kusini mwa Lebanon.
Hagari kisha alipoulizwa kuhusu kile kitakachotokea wakati wa "uvamizi" huo katika siku zijazo alisisitiza kuwa huo sio uvamizi.
."Huu ni uvamizi uliodhibitiwa," akiongeza kuwa "tutafanya haraka iwezekanavyo, kukabiliana na tishio hilo".
Hagari pia amedokeza kuwa vikosi vya Israel vimefanya kazi ndani ya Lebanon mara kadhaa katika miezi iliyopita, na kuharibu mahandaki.
Kama tulivyoripoti hapo awali Israel ilitangaza kuhusu operesheni yake "ndogo" ya ardhini huko Lebanon mapema Jumanne.
Hezbollah yadai Israel haijaingia Lebanon
Huku hayo yakijiri Hezbollah inasema kuwa madai ya Israel kwamba majeshi yake yameingia Lebanon ni ya uongo.
Katika taarifa. kundi hilo pia linasema kuwa hakuna mapigano ya moja kwa moja yaliyotokea kati ya wapiganaji wao na vikosi vya Israel lakini wako "tayari kwa makabiliano ya moja kwa moja".
Mapema leo, afisa mkuu wa usalama aliiambia BBC kwamba vikosi vya ardhini vya Israel vimefika "karibu sana" na Lebanon. Chanzo pia kilisema "hakuna mapigano" kwa sasa.
Seneta wa Kenya awasilisha hoja ya kujadili mienendo ya Rais
Seneta wa Makueni Daniel Maanzo amewasilisha hoja ya kujadili utenda kazi wa Rais William Ruto.
Hayi yanajiri wakati bunge la kitaifa limeanza mchakato wa kumuondoa madarakani naibu wake Rigathi Gachagua.
Hoja ya Maanzo, inayoangazia ukiukwaji wa katiba unaodaiwa kufanywa na rais, iliwasilishwa huku polisi wakiimarisha usalama nje ya Bunge na katikati ya jiji la Nairobi.
Katika hoja hiyo Rais Ruto inamshtumu Ruto kwa kukosa kuwalinda Wakenya, ikiangazia ukosefu wa usalama katika maeneo kadhaa ya nchi na mauaji ya makumi ya watu wakati wa maandamano ya vijana wa GenZ mwezi Juni, ambayo yalikuwa maandamano ya kupinga Mswada tata wa Fedha.
Seneta huyo wa Makueni pia alitoa wito wa kukaripiwa kwa Rais kwa kutekeleza sera kali katika sekta ya elimu na afya bila kuwashirikisha Wakenya kikamilifu.
"Rais William Ruto amewatenga baadhi ya Wakenya na anaendelea kuzidisha mivutano kati ya sekta tofauti kutokana na sera zake tata," Maanzo alisema.
Maelezo zaidi:
Kenya: Wabunge waanza mchakato wa kumuondoa Naibu Rais madarakani
Wabunge nchini Kenya wameanza harakati za kumwondoa madarakani naibu rais wa nchi hiyo.
Wanamshutumu Rigathi Gachagua kwa kuhusika katika maandamano ya ghasia yaliyoshuhudiwa nchini Kenya miezi mitatu iliyopita, kuhusika katika ufisadi, kuhujumu serikali na kuendeleza siasa za migawanyiko ya kikabila.
Hatua hiyo ni kilele cha mzozo mkubwa kati ya rais wa Kenya na naibu wake.
Mchakato huo unatarajiwa kupitia mabunge yote mawili kwa urahisi, baada chama kikuu cha upinzani kuamua kushirikiana na chama cha Rais Ruto kufuatia maandamano ya hivi majuzi.
Polisi pia wamewashutumu wabunge wanaoshirikiana na naibu rais kwa kufadhili na kuhamasisha magenge kupora na kusababisha ghasia wakati wa maandamano ya kupinga ongezeko la kodi mwezi Juni.
Rigathi Gachagua hata hivyo amewatetea na kudai kuwa mashtaka hayo yanalenga kuchafua jina lake na kuwashutumu wafuasi wake kwa kujaribu kupindua serikali.
Juhudi nyingi za kukupitia mahakama zilishindwa.
Maelezo zaidi:
Zaidi ya watoto 20 wahofiwa kufariki katika ajali ya basi nchini Thailand
Basi lililokuwa limebeba makumi ya watoto wa shule ya msingi limeanguka na kuwaka moto nje kidogo ya mji mkuu wa Thailand wa Bangkok.
Watoto 16 na walimu watatu wanaripotiwa kutoroka, lakini wanafunzi 22 na walimu watatu bado hawajulikani waliko, kulingana na waziri wa uchukuzi wa nchi hiyo.
Waziri mkuu wa Thailand alisema ajali hiyo ilisababisha "vifo na majeruhi" - lakini idadi kamili ya waliofariki bado haijathibitishwa.
Picha zinaonyesha basi hilo likiwa limeharibiwa kabisa na moto huo.
Wachunguzi wanasemekana hawakuweza kuingia ndani ya gari kwa sababu ya joto, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.
Watu milioni moja wamekimbia makazi yao nchini Lebanon - Waziri Mkuu
Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Makati, anasema nchi yake inakabiliwa na "mojawapo wa awamu hatari" katika historia yake.
Takriban watu milioni moja wamekimbia makazi yao kote Lebanon tangu mashambulizi ya anga ya Israel kuanza mwezi uliopita, anaongeza.
"Tunaomba kwa dharura misaada zaidi ili kuimarisha juhudi zetu zinazoendelea za kutoa msaada wa kimsingi kwa raia waliokimbia makazi yao," anasema.
Makati alikuwa akizungumza wakati wa mkutano na mashirika ya Umoja wa Mataifa, ambapo alizindua ombi la msaada wa kibinadamu la zaidi ya dola milioni 426.
Huku hayo yakijiri, afisa mkuu wa usalama ameiambia BBC kwamba vikosi vya ardhini vya Israel vimefika "umbali wa mwendo wa miguu" hadi Lebanon na mpaka sasa "hakuna mapigano".
"Tunalenga vifaa kuharibu vifaa vya Hezbollah, miundombinu ya Hezbollah ambayo imehifadhiwa katika makazi ya watu kaskazini mwa Israel," afisa huyo anasema.
"Siwezi kutoa idadi kamili ya wanajeshi wanaoshiriki operesheni hiyo, lakini sio idadi yao sio kubwa kwa uvamizi wa ardhini," afisa huyo anasema, akielezea kama idadi "ndogo" ikilinganishwa na operesheni ya Israeli huko Gaza.
Soma zaidi:
'Wakati mwingine nahisi heri tufe,' mtu aandika kwenye kikundi chetu cha WhatsApp
"Haya yatakuwa maisha yetu ya kila siku kuanzia sasa."
Huo ulikuwa ujumbe kutoka kwa mmoja wa majirani zangu katika kundi letu la WhatsApp jana usiku, baada ya kusikia mlipuko mkubwa wa kwanza.
Mtaa mzima ulikuwa macho usiku kucha hadi asubuhi.
Dahieh, sehemu ya kusini mwa Beirut inayolengwa na mashambulizi ya anga ya Israel usiku kucha, haipo karibu, lakini pia sio mbali.
Tunaweza kuona sehemu yake kutoka kwa madirisha na roshani zetu.
Kila mlipuko katika eneo hilo, unasikika hapa kwa nguvu.
Jana usiku, tulisikia milipuko saba mikubwa iliyotikisa majengo yetu.
"Siwezi kuvumilia tena," jirani mwingine anaandika kwenye kikundi.
Baada ya milipuko kadhaa mikubwa, tuliona moshi mzito na moto ukitoka Dahieh.
Jirani yangu inachukuliwa kuwa salama na haijalengwa katika vita vya zamani kati ya Hezbollah na Israeli, lakini licha ya hili, watu wengi hapa hawajisikii salama.
Majengo ya kitongoji hicho - ikiwa ni pamoja na ninayoishi - yaliharibiwa vibaya wakati wa mlipuko wa bandari ya Beirut miaka minne iliyopita na kuua zaidi ya watu 200 na kuwaacha zaidi ya 7,000 kujeruhiwa.
Kila mlipuko tunaosikia hapa, unatukumbusha wa kiwewe ambacho bado, ni kinatuhangaisha.
Kwa sababu ya mzozo wa kifedha ambao Lebanon imekuwa ikikabiliana nao tangu 2019, ilichukua muda mrefu kwa wengi hapa kukarabati nyumba zao zilizoharibiwa.
"Hatuwezi kuanza tena upya. Wakati mwingine nahisi bora tufe. Tumepitia mengi.Jamani inatosha," mkazi mwingine anaandika kwenye kikundi.
Asubuhi ya leo, baada ya mvua, Dahieh anaonekana kuwa tulivu kutoka hapa.
Moshi mdogo tu bado unafuka. Kuna harufu ya ajabu hewani.
Kikundi chetu cha WhatsApp kimejaa habari kuhusu kuanza kwa uvamizi wa ardhini. "Tumeingia rasmi kusikojulikana," jirani anaandika.
Pia unaweza kusoma:
Je hii inaweza kuwa Gaza nyingine?, BBC yahoji jeshi la Israel
Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel amezungumza na wenzetu katika kipindi cha BBC Radio 4 cha Leo.
Luteni Kanali Peter Lerner anasema Hezbollah ina "vituo vya mapigano" kusini mwa Lebanon ambavyo vilikusudiwa kutumika katika "mashambulizi kama ya Oktoba 7".
Ndio maana jeshi la Israeli lilihamia huko na kufanya mashambulizi usiku kucha, anasema, "ili kuvunja miundombinu hiyo".
Amesema maelezo ya Israeli ya mashambulizi "madogo na yanayoyenga " [maeneo] ni sawa na lugha iliyotumiwa kabla ya vikosi vyake kuishambulia Gaza mwaka jana.
Lerner anasema kuna tofauti: huko Gaza, lengo ni kuivunja Hamas kama mamlaka inayotawala, na kwamba nchini Lebanon operesheni yake "inalenga zaidi vitisho dhidi vya haraka vinavyotolewa kwa raia wa Israeli".
Alipoulizwa mbona Israel imevamia nchi huru, Lerner amesema Hezbollah ilianza "vita vyao" mnamo 8 Oktoba, na kuwasambaratisha maelfu ya Waisraeli kwa roketi mpakani.
Hatua ya hivi karibuni inafuatia "mwaka wa mazungumzo" kujaribu kuwarudisha watu nyumbani salama, anasema.
"Hakuna mpango wa kuikalia [Lebanon], mpango ni kuvunja miundombinu ambayo Hezbollah iliianzisha kuua Waisraeli," Lerner amesema.
Unaweza pia kusoma:
Israel yasema Hezbollah inawatumia raia kama 'ngao za binadamu'
Akizungumza kwa lugha ya kiarabu msemaji wa jeshi la llinzi la Israel Avichay Adraee amesema Hezbollah inatumia raia kama ngao kuanzisha mashambulizi kusini mwa Lebanon.
Amesema kwamba "mapigano makali" yanaendelea kusini mwa Lebanon, akawaonya raia wa Lebanon dhidi ya kutumia magari kusafiri kusini kuvuka mto Litani.
Mto Litani hutiririka kutoka mashariki hadi magharibi karibu maili 20 kaskazini mwa mpaka wa Israeli na Lebanon.
Hezbollah inasema imewashambulia wanajeshi wa Israel katika mji wa mpakani wa Israel wa Metula asubuhi.
Hezbollah ilifyatua "msururu wa roketi" na kufyatua risasi, taarifa kutoka kwa kikundi ilisema.
IDF inasema arifa kadhaa ziliwashwa katika eneo hilo, ambazo ziligundua "takriban milipuko mitano".
Hapo jana, jeshi la Israel lilitangaza maeneo yanayozunguka Metula, Misgav Am, na Kfar Giladi kaskazini mwa Israel kuwa "eneo lililofungwa la kijeshi", na kuwazuia kuingia katika eneo hilo.
Unaweza pia kusoma:
Israel na Hezbollah: Uvamizi wa ardhini unakuja na hatari kwa Israel,
Mapema usiku wa kuamkia leo kulikuwa na msururu wa milipuko mikubwa iliyosikika hapa Israel ikithibitisha kuwa Israel imeanzisha mashambulizi ya ardhini " madogo, ya ndani na yanayolenga" maeneo ya Hezbollah, huko Lebanon.
Bado haijabainika ni kiwango gani au aina gani ya mashambulizi haya lakini kumekuwa na mkusanyiko wa wanajeshi hapa kwa siku kadhaa na hapo awali tuliona mizinga 24 ikiwa imewekwa umbali mfupi kutoka mpakani.
Israel imefanya mashambulizi ya mfulurizo kwa Hezbollah katika wiki kadhaa zilizopita lakini uvamizi wa ardhini kama huu ni wa aina tofauti ya vita, na hatari mpya kwa vikosi vya Israeli na utulivu wa kikanda, pamoja na Lebanon yenyewe.
Unaweza pia kusoma:
Mbivu na mbichu kujulikana Kenya huku wabunge wakijiandaa kuwasilisha hoja ya kumtimua naibu rais
Wabunge nchini Kenya wanatazamiwa kuwasilisha hoja ya kumg'oa madarakani Naibu Rais Rigathi Gachagua katika bunge la taifa baadaye leo.
Kiongozi wa Wengi na Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung'wah alithibitisha kuwa hoja dhidi ya Gachagua itawasilishwa mbele ya Bunge saa nane unusu leo kwa saa za Afrika mashariki.
Uwasilishaji wa hoja hiyo utahitaji kuungwa mkono na wabunge 233 na kuna taarifa zinazodai kuwa wajumbe 302 tayari wametia saini.
Wanaomshitaki Gachagua wanadai kuwa amekiuka Kifungu cha 10 cha katiba, wakisema matamshi yake hadharani yamekuwa ya uchochezi na yanaweza kuibua chuki za kikabila.
Pia anatuhumiwa kukiuka vifungu vya 147, 148,174,186 na 189 vinavyozungumzia mwenendo na wajibu wake kama msaidizi mkuu wa Rais.
Pia atajitetea dhidi ya madai ya kujipatia mali kwa ufisadi na kutumia pesa za walipa kodi kwa njia isiyo halali. Mali hiyo inasemekana kusambazwa katika kaunti za Nyeri, Nairobi na Kilifi.
Ikiwa hoja hiyo itakamilika, spika wa bunge la taifa Moses Wetangula atawasilisha azimio hilo kwa spika wa bunge la seneti Amason Kingi ndani ya siku mbili ili achukuliwe hatua.
Hoja ya kumuondoa madarakani Gachagua inakuja huku kukiwa na uhusiano mvutano baina yake Rais William Ruto. Viongozi hao wawili wamekuwa wakitupiana lawama kila mmoja akidai mwenzake anakwamisha utendaji wa mwenzake.
Unaweza pia kusoma:
'Madhara makubwa' kwa Iran itashambulia moja kwa moja kijeshi Israel
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alizungumza na mwenzake wa Israel Yoav Gallant siku ya Jumatatu, ambapo "walikubaliana juu ya umuhimu wa kubomoa miundombinu ya mashambulizi kwenye mpaka" ili kulinda jamii za kaskazini za Israel dhidi ya Hezbollah, kulingana na taarifa iliyotolewa na Marekani. Idara ya Ulinzi.
Hata hivyo, taarifa hiyo pia ilitaja umuhimu wa "mwishowe kutoka kwa operesheni za kijeshi hadi njia ya kidiplomasia".
Pande zote mbili pia zilionya juu ya "madhara makubwa" kwa Iran ikiwa itajaribu kuishambulia Israel moja kwa moja.
Unaweza pia kusoma:
Tazama: Milipuko yaonekana kwenye mpaka wa lsrael na Lebanon
Video iliyochukuliwa kutoka kaskazini mwa Israel inaonyesha miale ya moto na milipuko kwenye mpaka na Lebanon Jumatatu usiku na Jumanne asubuhi.
Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilisema operesheni ya ardhini "yeney mipaka, ya ndani na inayolenga" maeneo inaendelea dhidi ya Hezbollah kusini mwa Lebanon.
Maeneo hayo yanapatikana katika vijiji vilivyo karibu na mpaka ambavyo "vinaleta tishio la mara moja kwa Waisraeli kaskazini mwa Israeli", iliongeza.
Unaweza pia kusoma:
Nyota wa mpira wa kikapu katika NBA Dikembe Mutombo amefariki dunia kutokana na saratani ya ubongo akiwa na umri wa miaka 58
Nyota huyo aliyetunukiwa tuzo ya NBA All-Star mara nane, ambaye alistaafu mwaka wa 2009, alichezea ligi hiyo miaka 18 akicheza katika timu za Denver Nuggets, Atlanta Hawks, Philadelphia 76ers, New Jersey Nets, New York Knicks na Houston Rockets.
Mutombo alianza matibabu ya uvimbe wa ubongo Oktoba 2022.
"Dikembe Mutombo alikuwa mkubwa kuliko maisha," alisema kamishna wa NBA Adam Silver.
"Uwanjani alikuwa mmoja wa walinzi wakubwa waliozuia mashoti na wachezaji wa ulinzi katika historia ya NBA. Nje ya uwanja, alimimina moyo wake na roho katika kusaidia wengine."
Akiwa na urefu wa futi 7 na inchi 2 (m 2.18), kipaji cha Murombo, mzaliwa wa Jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo kiligunduliwa alipokuwa akisoma katika Chuo Kikuu cha Georgetown na alichaguliwa na baadaye kuchaguliwa na Nuggets na alichaguliwa kama mshindi wa jumla mara nne katika NBA ya 1991.
Uchangamfu wake na mtindo wake wa kutikisa vidole aliposhinda ilimfanya kuwa kipenzi cha mashabiki.
Akijulikana kwa mchezo wake wa ulinzi, aliiongoza NBA kwa kuzuia mashuti kwa misimu mitano mfululizo na kufunga kwa kila mechi kwa rekodi ya misimu mitatu mfululizo.
Kufuatia kustaafu kwake, Hawks na Nuggets walistaafisha shati lake la nambari 55, na mnamo 2015 aliingizwa kwenye orodha ya Umaarufu ya NBA.
Mutombo alikuwa balozi wa kimataifa wa NBA na alifanya kazi ya kibinadamu katika nchi yake.
Unaweza pia kusoma:
Israel yaanza uvamizi wa ardhini kusini mwa Lebanon
Israel imeanza operesheni ya ardhini kusini mwa Lebanon, kwa "mashambulizi madogo, ya ndani na yanayolenga" maeneo ya Hezbollah, jeshi la Israel limesema.
Maeneo, yaliyo karibu na mpaka, yanasababisha "tisho la haraka kwa jamii za Israeli", Jeshi la Ulinzi la Israeli limesema katika taarifa, iliyotumwa kwenye mtandao wa X.
"Jeshi la anga la Israel na mizinga ya jeshi la Israel ( IDF) vinasaidia vikosi vya ardhini kwa mashambulizi sahihi dhidi ya maeneo ya kijeshi katika eneo hilo," taarifa hiyo iliongeza.
Siku ya Jumatatu, kulikuwa na ripoti kwamba Israel ilikuwa ikijiandaa kwa operesheni ya ardhini kwenye mpaka na Lebanon ili kulinda maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo, ambayo yanakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa wanamgambo wa Hezbollah.
Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Galant alidokeza uwezekano huu jioni, afisa wa utawala wa Marekani ambaye hakutajwa jina aliwaambia waandishi wa habari kwamba operesheni hiyo inaweza kuanza Jumatatu.
Jumatatu jioni, kikao cha baraza la mawaziri la kijeshi kilifanyika nchini Israel, ambapo kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel, hatua inayofuata ya operesheni dhidi ya Hezbollah iliidhinishwa.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Matthew Miller alisema katika kikao fupi kwamba viongozi wa Israel wameifahamisha Washington kuhusu "operesheni kadhaa," ikiwa ni pamoja na operesheni za ardhini, nchini Lebanon.
Unaweza pia kusoma: