Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jeshi la Madagascar lasema limenyakua mamlaka - ripoti
Hii ni baada ya Wabunge kupiga kura kumuondoa madarakani Rais Andry Rajoelina.
Muhtasari
- DRC yafikia utaratibu wa ufuatiliaji usitishaji mapigano na AFC/M23
- Jeshi laahidi uchaguzi ndani ya miaka miwili
- Madagascar ilifikaje hapa?
- Jeshi la Madagascar lasema limenyakua mamlaka
- Rais Rajoelina apinga kura ya kumuondoa madarakani Madagascar
- Jeshi lakanusha madai ya kutaka kumdhuru Rajoelina
- AU yaonya dhidi ya jaribio la mapinduzi Madagascar
- Upinzani nchini Madagascar unataka kumvua urais Rajoelina
- Unyongaji hadharani wazidisha hofu na mgawanyiko huko Gaza
- Wafungwa wa Kipalestina waripoti unyanyasaji katika magereza ya Israel
- Rais wa Madagascar avunja bunge ili kuzuia kuondolewa madarakani
- Afisa Kenya auawa katika shambulio la upinde na mshale kwenye lango la makazi ya rais
- Familia za mateka zaghubikwa na hasira wakiendelea kusubiri kurudi kwa miili ya wapendwa wao
- Korea Kaskazini huenda ilitumia teknolojia ya Urusi kwa kombora la Hwasong-20 ICBM, asema mwenyekiti wa (JCS)
- Mgombea wa upinzani nchini Cameroon adai ushindi akimtaka Rais Biya kukubali
- Marekani yashutumu China kufuatia makabiliano ya baharini na Ufilipino
- Shirika la kijasusi la Uingereza laonya wanasiasa ni walengwa wa ujasusi wa Urusi na China
- Mkuu wa Nato atania akisema nyambizi ya Urusi 'inachechemea' baharini
- Rais wa Madagascar asema 'nimejificha mahali salama' huku akionya kuhusu jaribio la mapinduzi
- Trump atangaza mwisho wa vita vya Gaza
Moja kwa moja
Na Asha Juma, Lizzy Masinga & Ambia Hirsi
Katika picha: Raia wa Madagascar washangilia mabadiliko ya uongozi
Wakaazi katika mji mkuu wa Antananarivo wamekuwa wakishangilia matukio ya kisiasa nchini humo.
Tumeangazia msururu wa taarifa tangu Wabunge walipopiga kura kumtimua Rais Andry Rajoelina na jeshi kutangaza kuchukua madaraka nchini humo.
Ingawa hali bado haijaimarika, baadhi ya raia wanahisi wamepiga hatua:
DRC Congo yafikia utaratibu wa ufuatiliaji usitishaji mapigano na AFC/M23
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Muungano wa Mto Kongo (AFC) wamefikia Utaratibu wa Ufuatiliaji na Uthibitishaji wa mpango wa Kusitisha mapigano.
Itasimamia utekelezwaji wa usitishaji vita wa kudumu, kuchunguza ukiukaji, na kushirikisha pande husika ili kudhibiti uhasama ulioanzishwa upya.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar ilitangaza makubaliano hayo leo kupitia mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter), na kuyataja makubaliano hayo kuwa "hatua muhimu kuelekea upatikanaji wa amani kati ya pande zote".
Taarifa hiyo pia imethibitisha kuwa Qatar, Marekani na Umoja wa Afrika watakuwa waangalizi katika utaratibu huo, wakiunga mkono uwazi na kuimarisha juhudi za amani za kikanda na kimataifa katika eneo la Maziwa Makuu.
Licha ya tamko lililotiwa saini mnamo Julai 19, 2025, na serikali ya DRC na AFC, ambayo ilijumuisha kundi la M23) - sehemu ya Muungano wa Mto Kongo - mapigano yameendelea katika Mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini, ambapo vikosi vya Waasi vilianzisha mashambulizi yaliyosababisha kuanguka kwa miji ya Goma na Bukavu ,miji miwili muhimu ya mashariki.
Jeshi laahidi uchaguzi ndani ya miaka miwili
"Tutaunda serikali na kufikia muafaka", Kanali Michael Randrianirina amewaambia waandishi wa habari nchini Madagascar baada ya kutangaza kuwa kitengo maalum cha jeshi maarufu CAPSAT, kimetwaa mamlaka.
Alipoulizwa kama watafanya uchaguzi, alijibu, "bila shaka". Hii itafanyika ndani ya "miezi 18 hadi miaka miwili" ijayo, alisema.
Mkuu wa CAPSAT alisema waandamanaji wa Gen Z watakuwa sehemu ya mageuzi hayo kwa sababu "vuguvugu hilo liliundwa mitaani kwa hivyo tunapaswa kuzingatia matakwa yao".
Alisema yeye na maafisa wenzake hawakuwa na budi ila kuung'oa madarakani utawala uliopo.
"Hakukuwa na rais, wala serikali ... hakuna kinachofanya kazi hapa."
Unaweza kusoma:
Madagascar ilifikaje hapa?
Zaidi ya wiki mbili zilizopita, vuguvugu linaloongozwa na vijana lilianza kupinga kukatika maji na umeme kote nchini
Maandamano hayo yaliongezeka hivi karibuni, huku waandamanaji wakionesha hasira juu ya masuala kama vile gharama ya maisha, na kumtaka Rais Andry Rajoelina kujiuzulu.
Siku ya Jumamosi, wanajeshi kutoka kitengo chenye nguvu cha jeshi kinachojulikana kama CAPSAT bila kutarajia waliondoka kwenye kambi zao na kujiunga na waandamanaji.
Siku mbili baadaye, ripoti ziliibuka kuwa Rajoelina alihamishwa na jeshi la Ufaransa na huenda alielekea Dubai.
Hatahivyo, hakuna uthibitisho rasmi wa hii Jumatatu usiku Rajoelina alisema alikuwa alijihifadhi "mahali salama" baada ya jaribio la kutaka kumuua.
Saa chache kabla ya wabunge kuanza kupiga kura ya kumshtaki Rajoelina kwa kuutelekeza wadhifa wake, alitangaza kulivunja bunge la taifa.
Kura iliendelea bila kujali hilo, huku wabunge wakipiga kura kwa wingi kumvua urais. CAPSAT kisha ikatangaza kuchukua mamlaka.
Unaweza kusoma;
Habari za hivi punde, Jeshi la Madagascar lasema limenyakua mamlaka
Kufuatia kura ya kumvua madaraka Rajoelina, kikosi maalumu cha kijeshi cha CAPSAT kinasema kinachukua mamlaka, shirika la habari la Reuters linaripoti.
AFP inaripoti kwamba "kanali wa jeshi" anasema jeshi limechukua jukumu.
Wanachama wa chama cha Rajoelina, IRMAR, walikuwepo kwenye kura ya kuondolewa madarakani katika bunge la kitaifa na hata walipiga kura nyingi dhidi yake, na hivyo kuongeza shinikizo kumtaka ajiuzulu.
Wabunge wa Madagascar walipiga kura ya kumvua Rais Rajoelina kwa kura 130 za ndio.
Mahakama Kuu ya Kikatiba lazima sasa ithibitishe kura hiyo.
Wabunge walimshutumu rais kwa kutelekeza wadhifa wake.
Siku ya Jumatatu, Rais Rajoelina alithibitisha kuwa ameondoka nchini, akisema anahofia maisha yake baada ya jeshi la CAPSAT kujiunga na maandamano yaliyoongozwa na vijana dhidi ya serikali yake.
Lakini kanali wa CAPSAT alipuuzilia mbali madai ya Rajoelina kuwa hayana msingi, akisema jeshi halijawahi kuwa na nia yoyote ya kudhuru hata unywele mmoja kichwani mwake.
Rais sasa bado hajulikani aliko.
Baada ya kutangaza kuwa CAPSAT, imechukua mamlaka, Kanali Michael Randrianirina amekuwa akizungumza zaidi kuhusu kile kinachofuata.
Alisema kuwa CAPSAT itaunda kamati na maafisa kutoka jeshi na polisi wa kitaifa. "Labda kwa wakati itajumuisha washauri wakuu wa kiraia. Ni kamati hii ambayo itatekeleza kazi ya urais,"
Kanali Randrianirina alinukuliwa na shirika la habari la AFP akisema. "Wakati huo huo, baada ya siku chache, tutaunda serikali ya kiraia."
Unaweza kusoma;
Rais Rajoelina apinga kura ya kumuondoa madarakani Madagascar
Rais Rajoelina amelaani kura ya kumuondoa madarakani inayoendelea hivi sasa. Anabainisha kuwa mkutano huo umefanyika licha ya yeye kuvunja bunge la kitaifa na kusema kura hiyo ni kinyume cha katiba.
Matokeo ya mkutano huo vyovyote vile, "utachukuliwa kuwa ni batili", Rajoelina anasema katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Facebook.
Muda mfupi uliopita, wabunge katika bunge la kitaifa la Madagascar wanapiga kura ya kutaka kumshtaki rais Andry Rajoelina.
Hii ni licha ya kuwa Rajoelina akutangaza mapema kuwa amevunja bunge la taifa ambalo ni baraza la chini la bunge.
Unaweza kusoma;
Jeshi lakanusha madai ya kutaka kumdhuru Rajoelina
Kikosi chenye nguvu cha kijeshi nchini Madagascar kimetupilia mbali madai ya Rais Andry Rajoelina kwamba walikusudia kumdhuru.
Kanali Randrianirina Michael wa kitengo cha CAPSAT aliiambia BBC madai hayo hayana msingi, akisema jeshi halijawahi kuwa na nia yoyote ya kudhuru "hata unywele mmoja kichwani mwake".
Katika matangazo ya moja kwa moja kwa taifa kwenye Facebook, Rajoelina, 51, alisema "kundi la wanajeshi na wanasiasa walipanga kuniua", na kumlazimisha kujificha.
Maandamano makubwa yalianza nchini Madagascar tarehe 25 Septemba kutokana na hasira ya kukatwa mara kwa mara kwa maji na umeme, kisha yakaongezeka kuakisi kutoridhika zaidi na serikali ya Rajoelina juu ya ukosefu mkubwa wa ajira, rushwa na mgogoro wa gharama ya maisha.
Siku ya Jumamosi, wanajeshi kutoka CAPSAT waliondoka kwenye kambi zao, na kujiunga na waandamanaji, na kuleta changamoto kubwa kwa mamlaka ya Rajoelina.
Alijibu kwa kusema kulikuwa na jaribio la kunyakua mamlaka kinyume cha sheria nchini Madagascar.
Rajoelina hajaonekana hadharani tangu wiki iliyopita, huku ripoti ambazo hazijathibitishwa zikisema ameikimbia nchi.
Unaweza kusoma;
AU yaonya dhidi ya jaribio la mapinduzi Madagascar
Jumuiya ya Umoja wa Afrika umetoa wito kwa jeshi nchini Madagascar "kutoingilia" masuala ya kisiasa na kuonya kuwa "unapinga jaribio lolote la kubadilisha serikali kinyume na katiba".
Tunafuatilia matukio nchini Madagascar kwa "wasiwasi mkubwa", Baraza la Amani na Usalama la jumuiya hiyo ya Afrika nzima lilisema katika kikao cha dharura siku ya Jumatatu.
Rais wa Madasgacar anayekabiliwa na shinikiza la kuachia madaraka yuko mafichoni "mahali salama", na hapo awali alitoa agizo la kuvunja bunge la kitaifa ili kuzuia jaribio la wabunge kuidhinisha kura ya kutokuwa na imani naye.
Maandamano makubwa yalianza nchini Madagascar tarehe 25 Septemba kutokana na hasira ya huduma ya maji na umeme kukatwa mara kwa mara, lakini maandamano hayo yakageuka kuwa uasi dhidi ya serikali ya Rajoelina.
Waandamanaji wanalalamikia ukosefu mkubwa wa ajira, rushwa na kupanda kwa gharama ya maisha.
Upinzani nchini Madagascar unataka kumvua urais Rajoelina
Agizo la Rais Rajoelina la kuvunja bunge la kitaifa lilikuja wakati wabunge walipokuwa wakijiandaa kwa kikao ya kupiga kura ya kumvua urais kwa kutelekeza majukumu yake, shirika la habari la AFP linaripoti.
Rais wa zamani na kiongozi wa upinzani Marc Ravalomanana alisema kuwa bunge la taifa - limeitisha kikao hicho kisicho cha kawaida "kutambua kukosekana kwa mamlaka nchini Madagascar", AFP iliongeza.
"Kuna ombwe la madaraka. Suluhisho si kulipiza kisasi, wala kufanya maamuzi yasio na busara, bali ni kufikia mpito wa amani, kwa ushirikiano na uwajibikaji," Ravalomanana alinukuliwa akisema.
Ravalomanana aliondolewa mamlaka na Rajoelina kufuatia mapinduzi ya mwaka 2009.
Unyongaji hadharani wazidisha hofu na mgawanyiko huko Gaza
Ripoti za wapiganaji wa kundi la Hamas waliojifunika nyuso zao wakiwaua Wapalestina wanane hadharani zimezua hofu na hasira miongoni mwa wakazi wa Gaza, eneo ambalo tayari limechoshwa na miaka miwili ya vita, kufurushwa na uharibifu.
Mauaji hayo, ambayo Hamas inasema yalilenga "wahalifu na washirika na Israel", yanakuja siku chache baada ya mapigano makali kati ya wapiganaji wa Hamas na wanachama wa ukoo wenye nguvu wa Dughmush katika mji wa Gaza na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 50, ikiwa ni pamoja na wanachama 12 wa Hamas.
Wakati familia zilipokuwa zikiendelea kusherehekea kuachiliwa kwa wafungwa 2,000 wa Kipalestina badala ya mateka 20 wa Israel, milio ya risasi mpya ilizuka Jumanne asubuhi katika wilaya ya Shejaiya mashariki mwa Gaza.
Wakati Hamas ikisisitiza kuwa wapiganaji wake wanafanya kazi ya "kurejesha usalama" na "kuondoa uvunjaji wa sheria," wengi wanahofia kuwa kundi hilo linatumia machafuko kulipa kisasi dhidi ya wapinzani na wakosoaji wa kuwanyamazisha wakiwemo wale waliohoji shambulio lake la tarehe 7 Oktoba ambalo lilisababisha vita.
Mumen al-Natoor, mwanasheria anayeishi Gaza, analaani mauaji hayo kama vitendo vya uvunjaji sheria: "Kwa nini watu wanashangilia machafuko?.
Mtu aliyejifunika uso anaua mtu mwingine aliyefunika uso bila uthibitisho wowote, bila uchunguzi, bila mahakama, bila hata muda wa kusubiri wa kukata rufaa tunaitaje hii? Upinzani? Hapana, huu ni uvunjaji wa sheria," anasema.
"Wale wanaoua bila sheria ni wahalifu. Tutawawajibisha. Sisi ni mashahidi wa sura mbaya zaidi katika historia yetu." Mwanaharakati wa haki za binadamu Khalil Abu Shammala aliiambia BBC kwamba Gaza imeingia katika "hatua mpya na hatari." "Ninaona hofu, kushindwa na kukata tamaa machoni pa watu," anasema.
"Ndiyo, vita vimesimama, lakini changamoto zilizopo mbele ni kubwa. Isipokuwa watu wataona hatua za kweli zinazowapa matumaini, wengi wataendelea kuondoka Gaza si kwa hiari, lakini kwa sababu wanahisi hawana mustakabali hapa." Ibrahim Faris, mwanaharakati anayeishi katikati mwa Ukanda wa Gaza, anayaita mapigano ya ndani kuwa "dhambi." "Huwezi kusahihisha kosa moja na jingine," anasema.
Unaweza kusoma;
Wafungwa wa Kipalestina waripoti unyanyasaji katika magereza ya Israel
Familia za wafungwa wa Kipalestina zilishtushwa jana kuona hali ya wapendwa wao waliorejea kutoka jela za Israel.
Wafungwa walipotoka kwenye basi huko Ramallah, walionekana wamelegea na kupauka, huku wengine wakihangaika kutembea.
Niliona wanaume kadhaa wakisaidiwa au kubebwa na wanafamilia.
Ushahidi umeanza kujitokeza wa unyanyasaji mkubwa katika magereza ya Israel - ikiwa ni pamoja na mateso, kunyimwa chakula, na kupigwa.
BBC haiwezi kuthibitisha madai haya kwa uhuru. Lakini mahakama kuu ya Israel ilisema mwezi uliopita kuwa wafungwa wa Kipalestina walikuwa hawapewi chakula cha kutosha.
BBC pia hapo awali iliripoti juu ya Wapalestina kuteswa katika kizuizi cha Israeli.
BBC imewasiliana na Huduma ya Magereza ya Israel (IPS) kwa maoni. Serikali ya Israel hapo awali ilikataa shutuma za kuenea kwa unyanyasaji na mateso kwa wafungwa, na kusisitiza kuwa "imejitolea kikamilifu kwa viwango vya kisheria vya kimataifa".
Baadhi ya madai ambayo tumesikia ni ya kuongezeka kwa unyanyasaji katika siku chache kabla ya kuachiliwa kwa wafungwa.
Kuachiliwa kwa wafungwa wa Kipalestina kulihusisha wapatao 250 ambao walikuwa wamepatikana na hatia ya uhalifu ikiwa ni pamoja na mauaji na mashambulizi mabaya dhidi ya Waisraeli na wafungwa wapatao 1,700 kutoka Gaza ambao walikuwa wakishikiliwa na Israel bila kufunguliwa mashtaka.
Nje ya ukumbi wa mkutano huko Ramallah ambapo familia nyingi zilikusanyika kuwapokea wapendwa wao, Aya Shreiteh, 26, kutoka Klabu ya Wafungwa wa Palestina aliniambia: "Haki zao zilikiukwa kwa njia mbaya zaidi". "Wengi wa wafungwa katika mwaka uliopita walikabiliwa na njaa ya kimakusudi na kukabiliwa na magonjwa," alisema. "Miili yao ni dhaifu kutokana na njaa."
Habari za hivi punde, Rais wa Madagascar avunja bunge ili kuzuia kuondolewa madarakani
Rais wa Madagascar Andry Rajoelina amelivunja Bunge la nchi hiyo saa chache kabla ya upinzani kuwasilisha mswada wa kumjadili kwa kuacha wadhifa wake.
Jumatatu usiku, Rais Rajoelina alithibitisha kuwa ameondoka nchini lakini hakufichua mahali alipo.
Mara baada ya kutangaza hatua hiyo Rais Rajoelina amemteua Lova Tahina Rajaoarinelina kuwa mshauri maalum wa rais. Kabla ya uteuzi huo Bi Rajaoarinelina alikuwa mshauri wa spika wa bunge la kitaifa.
Huku hayo yakijiri kiongozi wa upinzani bungeni amesema agizo la Rais Andry Rajoelina la kuvunja bunge la taifa - "si halali kisheria", shirika la habari la Reuters linaripoti.
"Amri hii si halali kisheria... rais wa bunge la taifa anasema hakushauriwa," Siteny Randrianasoloniaiko alinukuliwa akisema.
Maelezo zaidi:
Afisa Kenya auawa katika shambulio la upinde na mshale kwenye lango la makazi ya rais
Polisi walisema siku ya Jumatatu asubuhi, mzee wa miaka 56, akiwa na upinde na mishale, alikaribia maafisa kwenye lango la Ikulu na kuamriwa kujisalimisha. Badala yake, alisonga mbele na kumdunga mshale afisa Ramadhan Matanka kwenye mbavu.
Polisi huyo alipelekwa hospitali mara moja lakini alifariki alipokuwa akipata matibabi, kwa mujibu wa taarifa ya polisi.
Shambulio hilo limeibua maswali kuhusu uwezekano wa kudorora kwa usalama kwani Ikulu ni mojawapo ya maeneo yenye ulinzi mkali zaidi nchini Kenya.
Mwili wa PC Matanka sasa uko katika chumba cha kuhifadhia maiti na uchunguzi wa maiti utafanywa baadaye.
Uchunguzi pia unaendelea kubaini chanzo cha shambulio hilo.
Vyombo vya habari vya ndani vinaripoti kwamba polisi aliyekufa alikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakichunguza magari yaliyokuwa yakiingia Ikulu.
Familia za mateka zaghubikwa na hasira wakiendelea kusubiri kurudi kwa miili ya wapendwa wao
Familia za mateka waliokufa ambao miili yao imesalia Gaza wameonyesha hasira baada ya Hamas kurejesha miili minne pekee kati ya 28 inayoaminika kuwa bado imesalia Gaza.
Chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano, Hamas walikuwa na hadi saa sita mchana (1:00 BST) jana kuwarudisha mateka wote kwa Israeli - wakiwa hai na waliokufa.
Jeshi la Israel limethibitisha kuwa limepokea mabaki ya mateka wanne, na litafanya uchunguzi wa kitaalamu kuthibitisha utambulisho wao.
Hamas walisema ni miili ya Guy Illouz, Yossi Sharabi, Bipin Joshi na Daniel Peretz. Imesema maeneo ya maziko ya wengine 24 hayajulikani, na itachukua muda kupatikana.
Hapo jana Baraza la Familia za Mateka za Israel liliitaka serikali ya Israel kusitisha makubaliano ya kusitisha mapigano, likisema "ukiukaji wa Hamas wa makubaliano hayo lazima ukabiliwe na jibu kali."
Waziri wa ulinzi wa Israel Israel Katz alisema kuwa kuachilia miili minne pekee itakuwa "kushindwa" kwa Hamas kutimiza ahadi zake.
Soma zaidi:
Korea Kaskazini huenda ilitumia teknolojia ya Urusi kwa kombora la Hwasong-20 ICBM, asema mwenyekiti wa (JCS)
Korea Kaskazini huenda ilitumia teknolojia ya Urusi katika kutengeneza kombora jipya la masafa marefu (ICBM) ambalo lilionyeshwa kwa mara ya kwanza wakati wa gwaride la kijeshi la hivi majuzi, mwenyekiti wa Majeshi ya Pamoja ya Wafanyakazi (JCS) wa Korea Kusini amesema.
Korea Kaskazini ilizindua kombora la Hwasong-20 ICBM, ambalo ililielezea kama "mfumo wa kimkakati wenye nguvu wa nyuklia," katika gwaride la kijeshi lililofanyika kuadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Chama tawala cha Korea Kaskazini.
Muundo wa chombo cha usafirishaji wa Hwasong-20 ulionekana kuwa tofauti ikilinganishwa na cha awali cha Hwasong-19 lililorushwa kwa mara ya kwanza Oktoba mwaka jana, na kuzua uvumi kwamba huenda Korea Kaskazini ilipata teknolojia ya Urusi katika kutengeneza kombora hilo jipya la masafa marefu wakati mshikamano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili umeendeela kuwa thabiti.
"Ninaamini kuna uwezekano wa kutosha," Mwenyekiti wa JCS Jenerali Jin Yong-sung alisema katika kikao cha ukaguzi wa bunge, alipoulizwa kuhusu uwezekano huo.
Mbali na kombora la Hwasong-20 ICBM, Korea Kaskazini pia silaha kadhaa kuanzia kombora jipya la hypersonic hadi magari yaliyoundwa kurusha droni kadhaa.
Mgombea wa upinzani nchini Cameroon adai ushindi akimtaka Rais Biya kukubali
Mgombea wa upinzani wa Cameroon Issa Tchiroma alijitangazia ushindi Jumatatu jioni katika uchaguzi wa rais wa Oktoba 12 nchini humo, akimtaka Rais Paul Biya kukubali kushindwa na "kuheshimu maamuzi ya wapiga kura".
"Ushindi wetu uko wazi. Ni lazima uheshimiwe," Tchiroma alisema katika hotuba yake kwenye ukurasa wake wa Facebook kutoka mji alikozaliwa wa Garoua kaskazini mwa
Tchiroma, 76, msemaji wa zamani wa serikali na waziri wa ajira, aliachana na Biya mapema mwaka huu na kuanzisha kampeni iliyovuta umati mkubwa wa watu na ridhaa kutoka kwa muungano wa vyama vya upinzani na vikundi vya kiraia.
Biya, 92, kiongozi wa nchi mwenye umri mkubwa zaidi duniani anayehudumu, anawania muhula wa nane baada ya miaka 43 madarakani.
Soma zaidi:
Marekani yashutumu China kufuatia makabiliano ya baharini na Ufilipino
Marekani imeshutumu China siku ya Jumatatu baada ya Ufilipino na Uchina kushutumiana juu ya makabiliano ya baharini karibu na visiwa vinavyozozaniwa katika Bahari ya Kusini ya China.
"Marekani inalaani kitendo cha China cha kufanya mashambulizi Oktoba 12 na kurusha maji kwa meli ya Uvuvi na Rasilimali za Majini ya Ufilipino karibu na Kisiwa cha Thitu katika Bahari ya China Kusini," Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema katika taarifa yake.
"Tunasimama na washirika wetu Ufilipino wanapokabiliana na vitendo vya hatari vya China ambavyo vinadhoofisha utulivu wa kikanda," iliongeza idara hiyo.
Pia unaweza kusoma:
Shirika la kijasusi la Uingereza laonya wanasiasa ni walengwa wa ujasusi wa Urusi na China
Shirika la kijasusi la Uingereza laonya wanasiasa ni walengwa wa ujasusi wa Urusi na China
Shirika la kijasusi la ndani la Uingereza MI5 limetoa onyo nadra hadharani kwa wabunge Jumatatu kwamba wanalengwa na majasusi kutoka China, Urusi na Iran katika jaribio la kudhoofisha demokrasia ya nchi hiyo.
Onyo hilo linakuja wiki moja baada ya waendesha mashtaka kusema kuwa walilazimika kuachana na kesi ya wanaume wawili wa Uingereza wanaoshtakiwa kwa ujasusi kwa wabunge kwa ajili ya China kwa sababu serikali ya Uingereza haikuwa imetoa ushahidi unaoonyesha China ni tishio kwa usalama wa taifa lake.
MI5 iliwaonya wanasiasa na wafanyakazi wao kuwa makini na majasusi wanaotaka kupata taarifa kutoka kwao kwa ulaghai au mashambulizi ya kuwahadaa, kukuza uhusiano wa muda mrefu na wa kina nao, au kutoa michango ili kuathiri maamuzi yao.
"Mataifa ya kigeni yanapoiba taarifa muhimu za Uingereza au kuendesha michakato yetu ya kidemokrasia sio tu kwamba inaharibu usalama wetu kwa muda mfupi, yanaharibu misingi ya uhuru wetu," Mkurugenzi Mkuu wa MI5 Ken McCallum alisema.
MI5 iliwasihi wanasiasa "kuwa makini na mawasiliano ya kijamii yasio ya kawaida", ikiwa ni pamoja na maombi ya mara kwa mara ya kukutana kwa faragha, na kuwa waangalifu ikiwa kuna "kubembeleza kwa wazi".
Pia unaweza kusoma:
Mkuu wa Nato anatania kuhusu 'kuchechemea' kwa nyambizi ya Urusi
Mkuu wa Nato Mark Rutte ametania kuhusu hali ya nyambizi ya wanamaji ya Urusi siku ya Jumatatu huku Moscow ikikanusha kuwa nyambizi hiyo imekumbwa na matatizo ya kiufundi.
Meli yake katika Bahari Nyeusi ya Urusi ilisema nyambizi hiyo inayotumia dizeli ya Novorossiysk ilijitokeza nje ya Ufaransa ili kufuata sheria za urambazaji katika kivuko, ambapo ilifuatwa na meli ya kivita ya Uingereza na helikopta.
Mamlaka ya Uholanzi ilisema Jumamosi nyambizi hiyo ilikuwa katika mkondo wa maji ya Bahari ya Kaskazini.
"Ni mabadiliko yaliyoje kutoka kwa riwaya ya Tom Clancy ya 1984 The Hunt for Red October. Leo, inaonekana zaidi kama kuwinda fundi wa karibu," Rutte alisema katika hotuba yake huko Slovenia, akisema chombo "chenye matatizo" kilikuwa "kikichechemea" kuelekea nyumbani.
Rutte alisema "hakuna uwepo wa jeshi la wanamaji la Urusi katika Bahari ya Mediterania waliosalia".
Pia unaweza kusoma: