Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Putin asema Urusi itatumia tena kombora jipya katika vita

Urusi ina akiba ya makombora mapya yenye nguvu "tayari kutumika", Rais Vladimir Putin amesema, siku moja baada ya nchi yake kurusha kombora jipya la masafa marefu katika mji wa Dnipro nchini Ukraine.

Moja kwa moja

Seif Abdalla

  1. Gachagua amwambia Ruto: 'Sasa tunakujua wewe ni mtu wa aina gani'

    Naibu Rais aliyetimuliwa madarakani nvhini Kenya Rigathi Gachagua amedokeza kurejea kwa kishindo kisiasa mwezi Januari 2025 baada ya kufanya mashauriano na wakaazi wa eneo la Mlima Kenya.

    Akizungumza wakati wa ibada ya kanisa mjini Murang'a siku ya Jumapili, Gachagua amesema kuwa mgogoro wake na Rais William Ruto umemruhusu kupanga upya mikakati yake ijayo ya kisiasa.

    Kulingana na The Citizen Digital , Naibu huyo wa zamani alisema kwamba alibaini rasmi Rais Ruto ni mtu wa aina gani ilipodhihirika kwamba ndiye aliyechangia kuondolewa kwake na kwamba atafanya maamuzi ya busara wakati atakaporejea katika siasa.

    "Sisi kama watu wa Mlima Kenya tunachukia mambo mawili; uongo na usaliti. Januari hii ijayo baada ya mazungumzo tutatoa mwelekeo wetu..

    Hatutajikuta tena kwenye shimo tulimo,” alisema Gachagua.

    “Rais Ruto, rafiki yangu, alifanya jambo jema kuleta vita hivi dhidi yangu na watu wa mlimani kwa sababu sasa tunamjua.

    Sasa tumekuelewa (Ruto) na tutakuhutubia jinsi tunavyokujua wewe ni nani. Sasa tutakuwa na mazungumzo kwa heshima."

    Gachagua alisema kuwa amekuwa akifanya mazungumzo na viongozi wa makanisa, wafanyabiashara, wataalamu na viongozi wenye nia moja "wanaopenda watu wetu".

  2. 'Sijuti kuyapatia makanisa fedha' - Rais Ruto

    Rais William Ruto ameshikilia kuwa hataacha kutoa misaada ya kifedha kwa makanisa huku kukiwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa makasisi na Wakenya.

    Akizungumza wakati wa ibada ya kanisani mjini Kericho siku ya Jumapili, Rais Ruto alibainisha kuwa amejitolea kuunga mkono maendeleo ya makanisa na kuenea kwa Ukristo kwa kutoa pesa.

    Ruto alisema hatasitisha utamaduni wake kwa vile yeye ni "amezoea kutoa", akiongeza kuwa hatanyamazishwa na wachochezi.

    “Hatuna msamaha kabisa tunapomtolea Mungu kwa sababu Mungu alitoa kwanza, tunalielewa neno la Mungu kiasi cha kujua kwamba ni heri kutoa kuliko kupokea na ndicho tunachokwenda kufanya,” alisema. .

    "Tutajenga makanisa yetu na tutashirikiana kueneza neno la Mungu. Nimesaidia kujenga makanisa 30 ndani ya miaka 30 na sijawahi kukosa maana najua siri ya kutoa na najua inafanya nini."

    Hisia za Ruto zinatokana na uhusiano mbaya na kanisa huku Dayosisi Kuu ya Nairobi ikirudisha Ksh.2.8 milioni zilizotolewa na Rais na Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja mnamo Novemba 17.

  3. COP29: Makubaliano ya $300bn ni makubwa kimaendeleo lakini bado ni fedha kidogo - mtaalam wa tabianchi Uingereza

    Nigel Topping, mjumbe wa Kamati ya Uingereza ya Mabadiliko ya Tabianchi (CCC), anasema ahadi ya mataifa tajiri kulipa $300bn (£239bn) kwa mwaka ifikapo 2035 ni ishara ya maendeleo lakini bado ina mapungufu.

    "Kwa upande mwengine, ni mara tatu ya kiwango cha awali," anaongeza, akimaanisha ahadi ya awali ya $100bn kwa mwaka.

    Topping anasema anaona ufadhili zaidi ukiongezeka katika mazungumzo yajayo ya hali ya hewa.

    “Kila nchi ambayo inakubali kuongeza ufadhili inafikiria pia hoja za ndani, jambo ambalo si rahisi kila wakati,” anasema.

    "Tayari tunaona mageuzi makubwa katika mfumo wa fedha wa kimataifa," anasema, akiongeza kuwa ingawa mpango huo unakatisha tamaa kwa nchi maskini, bado unaashiria hatua kubwa zilizopigwa.

  4. Ukraine yatangaza kuilipua rada ya mfumo wa kulinda anga wa Urusi S - 400

    Mkuu wa jeshi nchini Ukraine ametangaza uharibifu wa rada ya mfumo wa kulinda anga wa S-400 katika eneo la Kursk

    Kulingana na jeshi la Ukraine, usiku wa Jumapili lilifanya mashambulizi ya mfululizo katika kitengo cha jeshla Urusi katika mkoa wa Kursk.

    Mashambulizi hayo yanadaiwa kuharibu rada ya mfumo wa ulinzi wa anga wa S-400.

    "Kitengo kilichotajwa cha vikosi vya jeshi la Urusi kilikuwa kikiendesha operesheni za kivita katika hali ya ardhi hadi ardhini, yaani, kushambulia maeneo kutoka ardhini ," Mkuu jeshi la Ukraine alisema katika taarifa.

    Katika hali ya wakati wa vita, BBC haiwezi kuthibitisha mara moja taarifa kutoka kwa wawakilishi wa pande zinazozozana.

    Uongozi wa jeshi la Urusi haukutoa tamko lolote kuhusu mashambulizi ya mfumo wa anga ya Urusi wa S-400.

    Siku ya Jumapili usiku, Gavana wa Mkoa wa Kursk Alexey Smirnov aliandika kuhusu makombora mawili ya Ukraine na droni 27 zilizorushwa kwenye eneo hilo.

    Na chaneli ya Telegraph ya "Kursk" ilichapisha video yenye mwangaza mkali na sauti za mlipuko mkali.

  5. Sudan iko katika hatari ya kuwa taifa lililofeli - Mkuu wa misaada aonya

    Sudan iliyokumbwa na vita iko katika hatari ya kuwa taifa jingine lililofeli kwa sababu mashirika ya kiraia yanasambaratika huku kukiwa na ongezeko la makundi yenye silaha, mkuu wa shirika la kimataifa la misaada ameiambia BBC.

    Pamoja na pande mbili kuu zinazopigana nchini Sudan - jeshi na Vikosi vya RSF - kuna "vikoso vingi vya kikabila" vinavyowapora na "kuwadharau" raia, Jan Egeland, mkuu wa Baraza la Wakimbizi la Norway (NRC), alisema.

    "Vikosi hivyo vinaharibu nchi yao wenyewe kupitia mauaji ya raia wao," alisema.

    Kwa muda wa miezi kumi na tisa, kumekuwa na mzozo mkali wa madaraka kati ya jeshi na RSF, ambao umewalazimu zaidi ya watu milioni 10 kukimbia makazi yao na kusukuma nchi katiuka njaa.

    "Yote niliyoyaona yanathibitisha kwamba hii kwa hakika ndiyo dharura kubwa zaidi ya kibinadamu mbele yetu, janga kubwa la njaa, janga kubwa zaidi la watu kuyahama makazi yao," Bw Egeland alisema, alipozuru nchini Sudan.

    Mwezi Septemba, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema njaa nchini Sudan "iko karibu kila mahali".

    Jiko la chakula limelazimika kufungwa kutokana na kutofadhiliwa. Egeland alisema kukosekana kwa mwitikio wa kibinadamu kunamaanisha kuwa vyanzo vilivyobaki vya misaada ni "vinachelewesha vifo badala ya kuvizuia."

    "Eneo kubwa la Sudan Sudan lina njaa, lina njaa," alisema, akiongeza kuwa njaa imekuwa ikitumika kama njia ya vita.

    Baadhi ya wataalam wa usalama wa chakula wanahofia kwamba takriban raia milioni 2.5 wanaweza kufariki kutokana na njaa mwishoni mwa mwaka huu.

    Bw Egeland alionya kwamba ulimwengu "unashindwa kuiangazia Sudan" kwa kutofanya vya kutosha.

  6. COP29: 'Makubaliano ni machache na yamepitwa na wakati wasema wawakilishi wa Afrika'

    Baadhi ya mataifa yanayoendelea yamekuwa yakikosoa ofa ya ufadhili wa hali ya hewa ya $300bn, yakisema ofa hiyo inashindwa kuafikia kiwango cha changamoto wanazokabiliana nazo katika miaka ijayo.

    Muda mfupi baada ya makubaliano hayo kupitishwa mapema huko Azabajani, Kundi la Afrika la Wapatanishi, kambi ya mataifa yanayoendelea yenye ushawishi, ilielezea ahadi hiyo kama "imechelewa sana, kwa bara hilo.

    "Tumesikitishwa sana na hatua finyu zilizopigwa katika masuala muhimu kwa Afrika," Ali Mohamed, mwenyekiti wa kundi hilo tawi la Kenya, aliuambia mkutano wa COP29.

    "Afrika ina na itaendelea kutoa tahadhari juu ya uhaba wa fedha za hali ya hewa."

    Akiwahutubia washiriki wa mazungumzo hayo, Simon Stiell, mkuu wa Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, alikiri kwamba makubaliano hayo yalikuwa hayajatimia kama ilivyotarajiwa.

    "Hakuna nchi iliyopata kila walichotaka. Na tunaondoka Baku na mrundiko wa kazi ya kufanya," alisema.

  7. Kiongozi wa dini ya Kiyahudi aliyetoweka UAE aliuawa - Israel

    Israel inasema kiongozi mmoja wa dini ya Wayahudi aliyetoweka katika Umoja wa Falme za Kiarabu ameuawa.

    Zvi Kogan, mjumbe wa shirika la Kiyahudi la Othodoksi Chabad, alitoweka tangu Alhamisi, ofisi ya waziri mkuu wa Israel ilisema, na kuibua uchunguzi kutoka kwa shirika la kijasusi la Israel Mossad na mamlaka za UAE.

    "Mauaji ya Zvi Kogan ni tukio la kigaidi dhidi ya Wayahudi. Taifa la Israel litachukua hatua katika uwezo wake wote kuwafikisha mahakamani wahalifu waliohusika na kifo chake,” ilisema taarifa ya ofisi ya Waziri Mkuu.

    Maafisa wa Israel wamekuwa wakiwasiliana na familia ya Bw Kogan, raia wa Israel-Moldova, tangu alipotoweka, taarifa hiyo iliendelea.

    Shirika la habari la serikali ya UAE limesema wizara ya mambo ya ndani imekuwa ikimtafuta mtu huyo aliyetoweka na kuchunguza kutoweka kwake.

    Abu Dhabi ilianzisha uhusiano rasmi na Israel chini ya makubaliano yaliyosimamiwa na Marekani, yanayojulikana kama Mkataba wa Abraham.

    Imedumisha uhusiano wakati wa vita vya Israel na Hamas huko Gaza. Huduma ya ushauri wa usafiri ya serikali ya Israel inaonya raia kusafiri tu hadi UAE kwa "sababu muhimu", kwani inasema kuna "shughuli za kigaidi" katika UAE, ambazo ni "hatari kwa Waisraeli wanaokaa/kutembelea nchini hiyo" .

    Chabad UAE haikujibu mara moja ombi la BBC la kutoa maoni.

  8. Ndege zisizo na rubani zaonekana kwenye kambi tatu za jeshi la Marekani nchini Uingereza

    Ndege zisizo na rubani ambazo hazijatambuliwa zimeonekana juu ya kambi tatu za anga nchini Uingereza, Jeshi la Wanahewa la Marekani (USAF) limethibitisha.

    Matukio hayo, yaliyotokea kati ya Jumatano na Ijumaa, yalionesha "ndege ndogo zisizo na rubani katika kambi za kijeshi za Uingereza za RAF Lakenheath na RAF Mildenhall, huko Suffolk, na RAF Feltwell katika kaunti jirani ya Norfolk.

    Jeshi la Marekani la USAF, ambalo hutumia kambi hizo, lilisema haijulikani kwa wakati huu ikiwa ndege hizo zisizo na rubani zilikuwa na nia mbaya.

    Pia ilikataa kutoa maoni kuhusu iwapo njia zozote za ulinzi zilitumika, lakini ilisema inahifadhi "haki ya kulinda" mali yake.

    Msemaji wa USAF barani Ulaya alisema: "Tunaweza kuthibitisha kwamba mifumo midogo ya angani isiyo na rubani [UASs] ilionekana katika maeneo ya karibu na RAF Lakenheath, RAF Mildenhall na RAF Feltwell.

    "Idadi ya ndege hizo ilibadilika mbali na kutofautiana katika ukubwa.

    Ndege hizo ndogo zilifuatiliwa kikamilifu na maafisa waliamua kuwa hakuna uvamizi wowote ulioathiri wakaazi au miundombinu muhimu.

    "Ili kulinda usalama wa uendeshaji, hatujadili hatua zetu maalum za ulinzi lakini tunahifadhi haki ya kujilinda.

    "Tunaendelea kufuatilia anga yetu na tunafanya kazi na mamlaka za nchi hii na washirika wa misheni ili kuhakikisha usalama wa wafanyikazi, vifaa na mali."

  9. Urusi iko tayari kuanzisha vita vya mtandaoni dhidi ya Uingereza - Waziri

    Urusi iko tayari kufanya mashambulizi ya mtandaoni dhidi ya Uingereza na washirika wengine katika jitihada za kudhoofisha uungaji mkono kwa Ukraine, waziri mwandamizi ataonya baadaye.

    Kansela Pat McFadden, ambaye jukumu lake ni pamoja na lile la usalama wa kitaifa, anatazamiwa kuuambia mkutano wa Nato kwamba Kremlin inaweza kulenga biashara za Uingereza na kuacha mamilioni bila nguvu za umeme.

    Ni onyo la hivi punde zaidi katika mfululizo wa maonyo kuhusu uwezo wa vita vya mtandaoni vya Urusi, ambavyo McFadden anavitaja "vita vilivyofichwa" vinavyoendeshwa dhidi ya Ukraine.

    Anatarajiwa pia kutaja kitengo cha 29155 cha Urusi, ambacho serikali inasema kimefanya mashambulizi kadhaa nchini Uingereza na Ulaya.

    Katika hotuba kwa Mkutano wa Ulinzi wa Mtandao wa Nato katika jumba la Lancaster House huko London, waziri huyo ataonya kwamba"vita vya mtandao vinaweza kudhoofisha" na kuelezea Urusi kama "mchokozi asiyejali" katika eneo hili.

    McFadden atazingatia tishio la uwezo wa Urusi kuzima gridi za umeme na " kwa mamilioni ya raia", pamoja na nia yake ya kulenga biashara za Uingereza "katika kutekeleza malengo yake mabaya".

    "Kwa kuzingatia ukubwa wa uhasama huo, ujumbe wangu kwa wanachama leo uko wazi: hakuna mtu anayepaswa kudharau tishio la mtandao wa Kirusi kwa Nato. Tishio ni la kweli," atawaambia washirika waliokusanyika wa Nato.

    Atadai kuwa makundi ya wadukuzi wanaohusishwa na serikali ya Urusi yamehusika kwa angalau mashambulizi tisa tofauti ya mtandao dhidi ya mataifa ya NATO, ikiwa ni pamoja na mashambulizi yasiyo ya msingi dhidi ya miundombinu muhimu ya kitaifa.

    Maoni ya McFadden ni ya hivi punde zaidi katika mfululizo wa maonyo kuhusu ongezeko la vitisho vya vita vya mtandao vya Urusi.

    Mwezi Septemba, mkutano wa utetezi wa pamoja wa mashirika ya kijasusi ya Magharibi ulishutumu Kitengo cha 29155 kwa kufanya mashambulizi yaliyopangwa kuvuruga juhudi za kuisaidia Ukraine kupinga uvamizi kamili wa Urusi.

  10. Putin asema Urusi itatumia tena kombora jipya katika vita

    Urusi ina akiba ya makombora mapya yenye nguvu "tayari kutumika", Rais Vladimir Putin amesema, siku moja baada ya nchi yake kurusha kombora jipya la masafa marefu katika mji wa Dnipro nchini Ukraine.

    Katika hotuba aliyoitoa katika runinga ambayo haijaratibiwa, kiongozi huyo wa Urusi alisema kuwa kombora la Oreshnik halikuweza kuzuiwa na kuahidi kufanya majaribio zaidi, ikiwa ni pamoja na "hali ya mapigano".

    Utumizi wa Urusi wa kombora la Oreshnik ulimaliza wiki moja ya kuongezeka kwa vita ambavyo pia vilishuhudia Ukraine ikirusha makombora ya Marekani na Uingereza hadi Urusi kwa mara ya kwanza.

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitoa wito kwa viongozi wa dunia kutoa "jibu zito" ili Putin "ahisi matokeo halisi ya matendo yake".

    Taifa lake lilikuwa likiwataka washirika wake wa Magharibi kuipatia nchi hiyo mifumo imara ya ulinzi wa anga, aliongeza.

    Kulingana na shirika la habari la Interfax-Ukraine, Kyiv inatafuta kupata mfumo wa ulinzi wa Marekani wa (THAAD), au kuboresha mifumo yake ya ulinzi wa anga dhidi ya makombora ya masafa marefu.

    Katika hotuba ya Ijumaa Putin alisema makombora ya Oreshnik hypersonic yaliruka mara 10 ya kasi ya sauti na kuamuru yaendelee kuzalishwa. Hapo awali alisema kuwa matumizi ya kombora hilo ni jibu kwa matumizi ya Ukraine ya makombora ya Storm Shadow na Atacms.

    Shambulio la siku ya Alhamisi mjini Dnipro lilielezewa kuwa la kawaida na kwa mujibu wa walioshuhudia lilisababisha milipuko ambayo iliendelea kwa saa tatu.

    Shambulio hilo lilikuwa na nguvu sana hali ambayo iliwafanya maafisa wa Ukraine kusema linafanana na kombora la masafa marefu (ICBM).

    Justin Crump, Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa kampuni ya ushauri wa hatari ya Sibylline, aliiambia BBC kwamba Moscow huenda ilitekeleza shambulio hilo kama onyo, akibainisha kuwa kombora hilo - ambalo ni la kasi na la kisasa zaidi ya mengine lina uwezo wa kukabiliana na Ukraine anga ya Ukraine.

  11. Natumai hujambo