Ufaransa na Kenya zalalamikia kushambuliwa kwa balozi zao DRC

Umati wa watu wenye wanaolalamikia shambulio la waasi dhidi ya Goma pia walishambulia balozi za Rwanda, Uganda, na Ubelgiji.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Dinah Gahamanyi & Asha Juma

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya mubashara kwa leo, tukutane tena hapo kesho.

  2. Habari za hivi punde, Waasi wa M23 wautwaa uwanja wa ndege wa Goma

    Shirika la habari la AFP sasa linanukuu chanzo cha usalama kikisema kuwa uwanja wa ndege wa Goma uko mikononi mwa M23.

    "Wamechukua udhibiti wa uwanja wa ndege, wapiganaji wa M23 wapo," AFP inanukuu chanzo kisichojulikana kikisema.

    "Zaidi ya wanajeshi 1,200 wa Congo wamejisalimisha na wameshikiliwa katika [kambi ya Umoja wa Mataifa] katika uwanja wa ndege."

    Saa chache zilizopita, tulikununulia habari kwamba waasi walidai kuteka uwanja wa ndege wa Goma .

    Vyanzo vya kidiplomasia na usalama sasa vimethibitisha unyakuzi huo, shirika la habari la Reuters pia linaripoti.

  3. Wafanyakazi wa ubalozi wa Kenya mjini Kinshasa walilazimika kutoroka baada ya kuchomwa kwa ubalozi

    f

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Waandamanaji pia walilenga ubalozi wa Uganda na kuchoma bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

    Wafanyakazi wawili katika ubalozi wa Kenya katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kinshasa, walilazimika kutoroka na kutafuta hifadhi kwingine huku waandamanaji wakilenga jengo hilo mapema leo, serikali ya Kenya imesema.

    Umati wa watu wenye hasira wakilalamikia shambulio la waasi dhidi ya Goma pia walishambulia balozi za Rwanda, Uganda, Ufaransa na Ubelgiji.

    Katika taarifa yake, wizara ya mambo ya nje ya Kenya ilisema inasikitishwa sana na mashambulizi hayo ikiyataja kuwa "hayafai".

    Iliongeza kuwa kumekuwa na uporaji, na uharibifu wa mali.

    Taarifa hiyo ilidai kuwa wakati shambulio dhidi ya ubalozi huo lilitokea "mchana" huku maafisa wa usalama wa Congo wakishuhudia na, "hawakuchukua hatua yoyote kuzuia hali hiyo".

    Ilielezea kile kilichotokea kama ukiukaji wa sheria za kimataifa kwani serikali za nchi wenyeji zinahitajika kulinda balozi.

  4. Ikulu ya Marekani imesitisha misaada na mikopo kutoka serikali kuu

    Jk

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Marekani Donald Trump amesitisha misaada, mikopo na usaidizi mwingine kutoka serikali kuu ya shirikisho, kulingana na taarifa iliyovuja ya serikali na kuthibitishwa na CBS News.

    Katika taarifa hiyo, kaimu mkuu wa Ofisi ya Usimamizi na Bajeti (OMB) anatoa wito kwa mashirika ya serikali kuhakikisha matumizi yanaendana na vipaumbele vya Trump.

    Athari ya usitishwaji huu bado hazijabainika, ingawa taarifa hiyo inabainisha kuwa bima ya afya ya Medicare na Usalama wa Jamii havitaathirika. Inakuja siku chache baada ya Marekani kusitisha karibu misaada yote ya kigeni.

    Hatua hiyo imekosolewa na wanachama wa chama pinzani cha Democratic ambao wanaonya juu ya "athari mabaya" kwenye programu ambazo watu hutegemea misaada na mikopo.

    Seneta wa Washington, Patty Murray na Mbunge wa Connecticut Rosa DeLauro - walituma barua kwenda Ikulu ya Marekani siku ya Jumatatu jioni wakielezea:

    "Tunawaandikia leo kuwasihi kwa nguvu zote mzingatie sheria na Katiba na kuhakikisha rasilimali zote za shirikisho zinatumika kwa mujibu wa sheria."

    Naye Diane Yentel wa Baraza la Kitaifa la Mashirika Yasiyo ya Faida anasema agizo hilo linaweza kukwamisha utafiti wa saratani, usaidizi wa chakula na simu za dharura za kuomba msaada wa ushauri.

    Waraka huo, uliotiwa saini na kaimu mkuu wa OMB, Matthew Vaeth, unatoa wito kwa mashirika ya serikali kusitisha kwa muda programu zao za usaidizi wa kifedha, ili waweze kukagua matumizi ambayo yanaweza kuathiriwa na maagizo ambayo Trump ameyatia saini.

    Ikulu ya Marekani bado haijatoa kauli rasmi kuhusu waraka huo uliovuja.

    Pia unaweza kusoma:

  5. DRC: Haya ndio yanayojiri hadi sasa kuhusiana na vita vya Goma huku mzozo ukiendelea kuchacha

    h

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Wakazi wanatumai kuwa usitishaji mapigano utaanza kutumika

    Iwapo unajiunga nasi, haya ndio matukio yanayojiri punde katika Jamhuri ya Kidemokrasia wakati waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wakishiriki katika vita vikali na vikosi vya serikali na walinda amani wa kimataifa kuwania udhibiti wa mji wa mashariki wa Goma.

    • Umoja wa Mataifa unasema mamia ya watu wamejeruhiwa na miili imetanda katika mitaa ya Goma
    • Mkazi mmoja aliyekimbia aliambia BBC kwamba bomu lilimuua jirani yake na watoto sita
    • Imethibitishwa kuwa Waasi hao wameuteka uwanja wa ndege wa Goma
    • Shirika la misaada linasema kuwa maabara ya utafiti wa Ebola iko hatarini mjini Goma baada ya kupoteza nguvu
    • Afrika Kusini imepoteza askari wengine wanne wa kulinda amani katika mapigano hayo
    • Balozi za kigeni zikilengwa na umati wa watu katika mji mkuu , Kinshasa, huku watu wakiwa na hasira kwamba jumuiya ya kimataifa imeshindwa kusitisha mapigano.
    • Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika kwa sasa linakutana kujadili mgogoro huo.

    Soma zaidi:

  6. DRC: Ufaransa yalaani shambulio la ubalozi wake Kinshasa

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Waandamanaji wakikabiliana na maafisa wa usalama nje ya ubalozi wa Ufaransa mjini Kinshasa

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot amelaani shambulizi dhidi ya Ubalozi wa Ufaransa mjini Kinshasa na waandamanaji Jumanne asubuhi.

    "Mashambulizi haya hayakubaliki," alisema katika chapisho kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), akiongeza kwamba waandamanaji "waliwasha moto ambao sasa umedhibitiwa".

    Moshi mwingi ulionekana ukifuka kutoka kwa ubalozi wa Ufaransa, baada ya sehemu yajengo lake lake kuchomwa moto.

    "Juhudi zote zinafanywa ili kuwahakikisha usalama mawakala na raia wetu," Barrot aliongeza.

    Waandamanaji pia walilenga balozi za Rwanda, Kenya, Uganda, Ubelgiji, Uholanzi na Marekani.

    Soma zaidi:

  7. DRC: Umoja wa Mataifa wasema hospitali zimezidiwa na idadi ya majeruhi Goma

    g

    Chanzo cha picha, AFP

    Umoja wa Mataifa unasema hospitali zimezidiwa na mamia ya majeruhi kufuatia makabiliano kati ya jeshi la Congo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda ambao wanaodaiwa kuuteka mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo..

    Wito wa kuzitaka Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuanzisha tena mazungumzo ya amani inazidi kuongezeka.

    Waasi wa M23 wanasema kuwa sasa wameuteka uwanja wa ndege wa Goma. Wamekuwa wakikabiliwa na upinzani lakini wanaonekana kukaribia kuudhibiti mji wote.

    Umoja wa Mataifa unasema kuna miili ya watu waliokufa mitaani na kuna ripoti za ubakaji uliofanywa na wapiganaji.

    Zaidi ya kilomita elfu mbili kutoka mji mkuu wa Congo, Kinshasa, watu wamekasirishwa na shambulio hilo la waasi.

    Majirani wa nchi hiyo Uganda na Rwanda wana historia ndefu ya kuunga mkono makundi ya waasi mashariki mwa Congo.

    Balozi zao ni miongoni mwa zile ambazo zilishambuliwa na kuporwa.

    Kuna hatari ya kutokea mzozo wa kikanda, huku marais wa Congo na Rwanda wakitakiwa kuanzisha mazungumzo ya amani.

  8. Tazama: Waandamanaji wa Kinshasa wakiandamana kuonyesha hasira yao kuhusu vita vya Goma

    Maelezo ya video, DRC: Waandamanaji wazuia shughuli za usafiri kuonyesha hasira yao kuhusu vita vya Goma

    Waandamanaji katika mji mkuu wa DRC Kinshasa wamechoma , huku wakiendelea kuonyesha kutoridhishwa na mashambulizi ya kundi la M23 mjini Goma. Waandamanaji hao wamechoma sehemu ya ubalozi wa Ufaransa mjini humo. Walivamia mitaa, kuzuia matembezi na mizunguko , na kuchoma matairi barabarani. Moshi ulionekana ukifuka hewani wakati sehemu za ubalozi huo uliokuwa ukiwaka moto.

    Soma zaidi:

  9. DRC: Waandamanaji wauchoma ubalozi wa Ufaransa

    h

    Waandamanaji katika mji mkuu wa DRC Kinshasa wamechoma moto sehemu za ubalozi wa Ufaransa, huku wakiendelea kuonyesha kutoridhishwa na mashambulizi ya kundi la M23 mjini Goma.

    Walivamia mitaa, kuzuia matembezi na mizunguko , na kuchoma matairi barabarani.

    Moshi ulionekana ukifuka hewani wakati sehemu za ubalozi huo zilipokuwa zikiwaka moto.

    Siku ya Jumatatu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot alielezea mshikamano wa Ufaransa na DRC na uadilifu wake wa eneo "wakati Goma inajiandaa kuangukia."mikononi mwa waasi. Amewataka M23 kuacha mashambulizi yake.

    Aliwataka M23 kuacha mashambulizi yake.

    Soma zaidi:

  10. DRC: Miito ya amani yaongezeka huku kukiwa na mzozo Goma

    g

    Chanzo cha picha, AFP

    Kuna kuongezeka wito wa kimataifa wa mazungumzo ya amani ili kukomesha kuongezeka kwa ghasia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Hatima ya kitovu cha uchumi na biashara cha Goma bado haijulikani wazi. Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema hali ni ya machafuko huku mapigano yakiendelea katika baadhi ya maeneo ya mji huo.

    Afisa wa serikali ya Congo amesema jeshi bado linadhibiti sehemu kubwa ya mji mkuu wa eneo hilo, lakini waasi wa M23 ambao wameushambulia mji huo wanapinga hilo.

    Ripoti zinasema takriban watu 17 wameuawa na karibu 400 kujeruhiwa.

    Siku ya Jumanne, Afrika Kusini ilisema kuwa wanajeshi wake wengine wanne, ambao wako DRC kama sehemu ya juhudi za kulinda amani, walikufa kutokana na mapigano na M23.

    Hii inafanya jumla ya idadi ya waliopoteza maisha nchini Afrika Kusini kufikia 13. Malawi na Uruguay pia zimepoteza askari wa kulinda amani.

    Soma zaidi:

  11. Trump asema DeepSeek ni 'mwamko mpya' kwa makampuni ya teknolojia ya Marekani

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Marekani Donald Trump ametaja kujitokeza kwa kampuni ya Kichina ya DeepSeek kuwa "mwamko mpya" katika tasnia ya teknolojia ya Marekani, baada ya kuibuka na muundo wake wa akili mnemba (AI).

    Hisa katika makampuni makubwa ya teknolojia kama vile Nvidia zilishuka sana, huku kampuni kubwa ya chipu ikipoteza karibu $600bn (£482bn) katika thamani ya soko.

    Kilichotikisa tasnia hiyo ni madai ya DeepSeek kwamba modeli yake ya R1 ilitengenezwa kwa gharama ndogo sana ikilinganishwa na programu za wapinzani wake - na kuibua maswali kuhusu mustakabali wa utawala wa AI wa Marekani na ukubwa wa uwekezaji ambao makampuni ya Marekani yanapanga.

    DeepSeek imekuwa programu isiyohitaji malipo iliyopakuliwa zaidi nchini Marekani wiki moja tu baada ya kuzinduliwa.

    Akijibu habari hiyo, Trump alisema maendeleo ya hivi punde katika tasnia ya AI ya Uchina yanaweza kuwa "chanya" kwa Marekani.

    "Kama ungeweza kuifanya kwa bei nafuu, kama ungeweza kuifanya kidogo [na] kufikia matokeo yale yale. Nadhani hilo ni jambo zuri kwetu," aliwaambia waandishi wa habari akiwa kwenye ndege ya Air Force One.

    Pia alisema kuwa hatiwi wasiwasi na mafanikio hayo, na kuongeza kuwa Marekani itasalia wenye kumiliki tasnia hiyo.

    Kuibuka kwake kunajitokeza wakati Marekani inazuia uuzaji wa teknolojia ya hali ya juu ya chipu ambayo inawezesha AI kwa Uchina.

    Ili kuendelea na shughuli yao bila ugavi thabiti wa chipu za hali ya juu zilizoagizwa kutoka nje, wawezeshaji wa AI wa China wameshirikisha kazi zao na kujaribu mbinu mpya za teknolojia.

    Inamaanisha pia kuwa gharama ni kidogo kuliko ilivyodhaniwa hapo awali, ambayo ina uwezo wa kuleta mabadiliko katika tasnia hiyo.

  12. Mfungwa aliyebadili jinsia ashtaki agizo la Trump la 'kukandamiza' haki za LGBTQ

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mwanamke aliyebadilisha jinsia yake ambaye yuko gerezani amewasilisha kesi mahakamani akisema kwamba agizo la Rais Donald Trump lenye kueleza Serikali ya Marekani kutambua jinsia mbili tu, zisizobadilika na inayohitaji wafungwa kama yeye kuwekwa katika magereza ya wanaume inakiuka Katiba ya Marekani na sheria za nchi.

    Katika kesi iliyowasilishwa Jumapili katika Mahakama ya Shirikisho la Boston, mfungwa huyo, ambaye anawakilishwa na mawakili katika vikundi vya kutetea haki za binadamu ikiwa ni pamoja na Mawakili na Watetezi wa LBTQ, alilenga agizo la Trump lililosainiwa siku yake ya kwanza kurudi ofisini Januari.

    Kuhamishwa kwa mlalamikaji katika gereza la wanaume pia kutakiuka marufuku ya Marekebisho ya Nane ya Katiba ya Marekani dhidi ya adhabu ya kikatili na isiyo ya kawaida, na kumnyima mlalamishi huduma ya afya inayohitajika kitakiuka sheria ya shirikisho inayojulikana kama Rehabilitation Act of 1973, kulingana na kesi hiyo.

  13. Microsoft iko katika mazungumzo ya kununua TikTok - Trump

    /

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa Microsoft iko kwenye mazungumzo ya kununua TikTok na kwamba angependa kuona "ushindani wa zabuni" katika uuzaji wa programu hiyo ya mitandao ya kijamii.

    Alipoulizwa na waandishi wa habari iwapo kampuni hiyo kubwa ya teknolojia ya Marekani ilikuwa ikijitayarisha kuiuza, Trump alijibu: "Naweza kusema ndiyo" - kabla ya kuongeza kuwa "kuna hamu kubwa na TikTok" kutoka kwa makampuni kadhaa.

    Trump na mtangulizi wake Joe Biden wamekuwa wakijaribu kwa miaka mingi kulazimisha kampuni mama ya TikTok ya Uchina, ByteDance, kuuza shughuli za TikTok Marekani kwa misingi ya usalama wa kitaifa.

    Hatua hii inawadia wakati Trump alitia saini agizo kuu wiki iliyopita kutengua marufuku ya Utawala wa Biden kwa TikTok ambayo iliondoa programu hiyo kwa muda mfupi kwa watumiaji wake wa milioni 170 nchini Marekani.

    Soma zaidi:

  14. DRC inasema bado inadhibiti GOMA licha ya M23 kusonga mbele

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mamlaka ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo inasema vikosi vya serikali na washirika wao wanaopigana katika eneo la Mashariki ya nchi hiyo bado wana udhibiti wa baadhi ya maeneo huko Goma, licha ya kuingia kwa M23 jijini siku ya Jumatatu.

    Rais Felix Tshisekedi alifanya mkutano na viongozi wa taasisi kadhaa za serikali mwishoni mwa Jumatatu, ili kutathmini hali ilivyo huko Goma - mji mkuu wa Mkoa wa Kivu Kaskazini ambao kikundi cha M23 kinadai kuwa imeuteka.

    "Wanajeshi wetu na Wazalendo wanaendelea kushikilia maeneo fulani jijini" alisema Vital Kamerhe, msemaji wa Bunge la Kitaifa la DRC baada ya mkutano na rais.

    Serikali ya Kongo ilisema wanajeshi walifanya mashambulizi ya kujilinda kushinikiza waasi kurejea nyuma ambayo bado inasisitiza kuwa, waliungwa mkono na vikosi vya Rwanda.

    Ndani ya DRC, shutuma dhidi ya mashambulizi ya M23 huko Goma zimeongezeka. Chama cha vikundi tofauti vya asasi za kiraia viliwasihi watu kote nchini humo kutofika mjini leo, wakati kiongozi wa upinzaji Martin Fayulu akitaka wananchi kuandamana siku ya Jumamosi kukemea vitendo vya M23.

    Kupitia mazungumzo ya simu hapo awali, Waziri mpya wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio "alilaani mashambulizi katika mji wa Goma yanayotekelezwa na M23 yenye kuungwa mkono na Rwanda na kudhibitisha kuwa Marekani inaheshimu uhuru wa DRC," kulingana na taarifa kutoka kwa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Tammy Bruce.

    Kikao cha pili cha Baraza la Usalama la UN juu ya hali ya mashariki mwa DRC kitafanyika leo, pamoja na mkutano tofauti wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika.

    Soma zaidi:

  15. Refa Coote alificha jinsi yake kwa kuogopa unyanyasaji

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Refa wa zamani wa Ligi ya Primia David Coote amesema alificha jinsi yake wakati wa taaluma yake, akihofia unyanyasaji ambao angepata kwa kuwa mpenzi wa jinsi moja.

    Coote, 42, alisema shinikizo la kazi yake lilichangia tabia iliyosababisha kutimuliwa na Kampuni ya Professional Game Match Officials Limited (PGMOL) mwezi Desemba.

    Akizungumza na gazeti la The Sun katika mahojiano yaliyochapishwa Jumatatu usiku, alisema: "Mimi ni mpenzi wa jinsi moja na nimekuwa na wakati mgumu kujivunia kuwa 'mimi' kwa muda mrefu.

    "Nimepitia unyanyasaji mbaya wakati wa taaluma yangu kama refa na kuongeza jinsi yangu kwa hilo hali ingekuwa ngumu zaidi."

    Coote, ambaye aliongoza zaidi ya michezo 100 ya ligi kuu, alitoa mahojiano yake ya kwanza kwa gazeti la Sun, ambalo liliongoza kuripoti utovu wake wa nidhamu.

    Katika taarifa tofauti iliyotolewa Jumatatu jioni, aliomba radhi kwa tabia iliyosababisha kufutwa kwake kazi, akisema: "Hiki kimekuwa kipindi kigumu sana cha maisha yangu. Ninawajibika kikamilifu kwa matendo yangu, ambayo yalikuwa chini ya kile kilichotarajiwa kutoka kwangu.

    "Ninasikitika sana kwa kosa lolote lililosababishwa na matendo yangu na kwa uangalizi hasi niliouweka kwenye mchezo ninaoupenda. Natumai watu wataelewa kuwa ni matukio ya faragha yaliyochukuliwa wakati hali yangu ikiwa chini sana kimaisha. Hayaakisi mimi ni nani leo au ninachofikiria."

    Akiongea juu ya jinsi yake kwa gazeti la Sun, Coote alisema alihisi "aibu" wakati wa miaka yake ya ujana na aliwaambia wazazi wake alipokuwa na umri wa miaka 21 na marafiki zake wakati alikuwa na miaka 25.

    "Jinsi yangu sio sababu pekee iliyosababisha mimi kuwa katika hali hii, "alisema. "Lakini sisemi simulizi halisi ikiwa sitasema kuwa mimi ni mpenzi wa jinsi moja, na kwamba nimekuwa na kipindi kigumu kujaribu kuficha ukweli.

    "Nilificha hisia zangu kama refa chipukizi na nilificha jinsi yangu pia – Refa mzuri lakini mtenda maovu kama mwanadamu," alisema. "Na hilo lilisababisha nididimie kwenye mwenendo na tabia."

    Refa wa zamani wa Ligi ya Primia David Coote amesema alificha jinsi yake wakati wa taaluma yake, akihofia unyanyasaji ambao angepata kwa kuwa mpenzi wa jinsi moja.

    Coote, 42, alisema shinikizo la kazi yake lilichangia tabia iliyosababisha kutimuliwa na Kampuni ya Professional Game Match Officials Limited (PGMOL) mwezi Desemba.

    Akizungumza na gazeti la The Sun katika mahojiano yaliyochapishwa Jumatatu usiku, alisema: "Mimi ni mpenzi wa jinsi moja na nimekuwa na wakati mgumu kujivunia kuwa 'mimi' kwa muda mrefu.

    "Nimepitia unyanyasaji mbaya wakati wa taaluma yangu kama refa na kuongeza jinsi yangu kwa hilo hali ingekuwa ngumu zaidi."

    Coote, ambaye aliongoza zaidi ya michezo 100 ya ligi kuu, alitoa mahojiano yake ya kwanza kwa gazeti la Sun, ambalo liliongoza kuripoti utovu wake wa nidhamu.

    Katika taarifa tofauti iliyotolewa Jumatatu jioni, aliomba radhi kwa tabia iliyosababisha kufutwa kwake kazi, akisema: "Hiki kimekuwa kipindi kigumu sana cha maisha yangu. Ninawajibika kikamilifu kwa matendo yangu, ambayo yalikuwa chini ya kile kilichotarajiwa kutoka kwangu.

    "Ninasikitika sana kwa kosa lolote lililosababishwa na matendo yangu na kwa uangalizi hasi niliouweka kwenye mchezo ninaoupenda. Natumai watu wataelewa kuwa ni matukio ya faragha yaliyochukuliwa wakati hali yangu ikiwa chini sana kimaisha. Hayaakisi mimi ni nani leo au ninachofikiria."

    Akiongea juu ya jinsi yake kwa gazeti la Sun, Coote alisema alihisi "aibu" wakati wa miaka yake ya ujana na aliwaambia wazazi wake alipokuwa na umri wa miaka 21 na marafiki zake wakati alikuwa na miaka 25.

    "Jinsi yangu sio sababu pekee iliyosababisha mimi kuwa katika hali hii, "alisema. "Lakini sisemi simulizi halisi ikiwa sitasema kuwa mimi ni mpenzi wa jinsi moja, na kwamba nimekuwa na kipindi kigumu kujaribu kuficha ukweli.

    "Nilificha hisia zangu kama refa chipukizi na nilificha jinsi yangu pia – Refa mzuri lakini mtenda maovu kama mwanadamu," alisema. "Na hilo lilisababisha nididimie kwenye mwenendo na tabia."

    Soma zaidi:

  16. Nyota wa Nigeria 2baba atangaza kutengana na mkewe

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mwanamuziki na mwigizaji maarufu wa Nigeria Innocent Idibia, anayejulikana sana kama 2Baba au Tuface, ametangaza kutengana na mke wake, Annie Idibia.

    Mmoja wa wanandoa mashuhuri wa Nigeria, Annie na Tuface walifunga ndoa mwaka wa 2012 na kupata watoto wawili wa kike pamoja.

    Katika ujumbe kwenye Instagram, mwimbaji huyo wa African Queen alisema walikuwa wametengana kwa muda na wamechukua hatua katika mchakato wa talaka.

    Ujumbe huo ulifutwa baadaye lakini 2Baba kisha akatoa video kuthibitisha kuwa maudhui yake yalikuwa sahihi.

    Mwimbaji huyo anaonekana kuwa mmoja wa waanzilishi wa tasnia ya muziki ya Nigeria ambayo sasa inajulikana kote ulimwenguni, akifungua njia kwa wanamuziki kama Wizkid, Davido na Burna Boy.

    Wanandoa hao walikuwa na sherehe kubwa iliyojaa wasanii tajika mwaka wa 2013, hafla ambayo ilifuatiliwa sana nchini Nigeria ingawa ilifanyika Dubai.

    Nyota huyo bado anajulikana sana kwa jina la Tuface japo alitangaza mwaka 2014 kuwa amebadilisha jina na kuwa 2Baba.

    Habari za kutengana kwao zimewashtua mashabiki na wapenzi wao kote barani kwani wanandoa hao walikabiliana na matatizo ya awali na ni miongoni mwa wanandoa mashuhuri waliodumu kwa muda mrefu nchini Nigeria.

    Mwanamuzi huyo wa zamani wa Plantashun Boyz anasema anapanga kufanya mkutano na waandishi wa habari ili kutoa maelezo zaidi, akiongeza kuwa amejitolea kushirikisha mtazamo wake moja kwa moja na mashabiki zake na wapenzi wa muziki kote ulimwenguni.

    Pia unaweza kusoma:

  17. Idadi kubwa ya watu wakamatwa katika msako wa wahamiaji wasio na vibali Marekani

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Msako mkali wa wahamiaji ulifanyika nchini Marekani siku ya Jumapili na kusababisha kukamatwa kwa watu 956, idadi hiyo ikiwa kubwa zaidi tangu Donald Trump arejee mamlakani, kulingana na shirika la Uhamiaji na Utekelezaji wa Forodha (ICE).

    Mashirika kadhaa ya serikali yenye mamlaka mapya ya kuwaweka kizuizini wasio na vibali yalihusika katika kamata kamata hiyo kwenye miji kadhaa ikiwa ni pamoja na Chicago, Newark na Miami.

    Moja ya ahadi alizotoa Donald Trump wakati wa kampeni yake, ni kuwafukuza nchi Marekani wahamiaji wasio na vibali.

    Mtangulizi wake Joe Biden aliwarejesha makwao wastani wa wahamiaji 311 kila siku, kulingana na ICE, wengi wao wakiwa watu ambao walikuwa wamefanya uhalifu.

    Tangu aingie madarakani, Trump ametekeleza maagizo 21 kurekebisha mfumo wa uhamiaji wa Marekani.

    Huko Miami siku ya Jumapili, vyombo vya kutekeleza sheria vya serikali vilichukua "hatua kadhaa za uhamiaji," Uchunguzi wa Usalama wa jiji hilo ulisema kwenye mitandao ya kijamii.

    Hii ilijumuisha afisi ya eneo la ICE Miami kuwazuilia wahamiaji wasio na vibali kwa makosa mbalimbali.

    Mwanamume ambaye jina lake halikutajwa aliiambia CBS News , mshirika wa habari wa BBC wa Marekani, kwamba ICE alimchukua mkewe wakati wa kamata kamata ya Miami wikendi hii.

    "Inachukiza wanachofanya hivi sasa," aliiambia CBS. "Inatia aibu sana."

    Alisema mke wake alikuwa katika harakati za kupata uraia wakati ICE ilipofika nyumbani kwake: "Walikuja tu na kumchukua."

  18. Mateka wanane wa Israel wanaotakiwa kuachiliwa katika awamu ya kwanza wamekufa

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Israel inasema mateka wanane kati ya 26 waliosalia wanaotakiwa kuachiliwa na Hamas wakati wa awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza wamefariki dunia.

    Msemaji wa serikali David Mencer aliwaambia waandishi wa habari kuwa Israel imepokea orodha kutoka kwa kundi la wapiganaji wa Palestina usiku kucha ambayo ilitoa taarifa kuhusu hali ya mateka hao.

    "Orodha kutoka kwa Hamas inalingana na ujasusi wa Israeli, kwa hivyo naweza kuwafahamisha kwamba... wanane wameuawa na Hamas," alisema, bila kuwataja. "Familia hizo zimefahamishwa kuhusu hali ya jamaa zao."

    Wanawake saba tayari wameachiliwa wakiwa hai kwa mabadilishano ya zaidi ya wafungwa 290 wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za Israel tangu usitishaji wa mapigano uanze tarehe 19 Januari.

    Siku ya Jumapili usiku, ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ilitangaza Hamas imekubali kuwaachilia raia wa kike Arbel Yehud, mwanajeshi wa kike Agam Berger na mateka mwingine mmoja siku ya Alhamisi.

    Mateka wengine watatu wangeachiliwa na kundi la siku ya Jumamosi, alisema.

    Jeshi la Israel lilianzisha kampeni ya kuiangamiza Hamas kujibu shambulio la kuvuka mpaka ambalo halijawahi kutokea tarehe 7 Oktoba 2023, ambapo takriban watu 1,200 waliuawa na 251 walichukuliwa mateka.

    Zaidi ya watu 47,310 wameuawa huko Gaza tangu wakati huo, kulingana na wizara ya afya ya eneo hilo inayoendeshwa na Hamas.

    Israel inasema 87 kati ya mateka hao wamesalia utumwani, 34 kati yao wakidhaniwa kuwa wamefariki dunia. Aidha, kuna Waisraeli watatu waliotekwa nyara kabla ya vita, mmoja wao amefariki.

    Soma zaidi:

  19. Baraza la Usalama la UN kufanya mkutano mpya juu ya hali ilivyo DRC

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo inasema kikao cha pili cha Baraza la Usalama la UN kitafanyika leo kujadili mgogoro unaoendelea katika mkoa wake wa mashariki.

    Mkutano mpya ulioitishwa na viongozi wa Kongo unafuatia mapigano ya kundi la waasi la M23 huko Goma Jumatatu, huku hofu ikiendelea kuongezeka kwamba jiji hilo litaangukia mikononi mwa waasi.

    Waziri wa mambo ya nje wa DRC Therese Kayikwamba Wagner alisema hakufurahishwa na taarifa ya Baraza la Usalama la UN iliyotolewa Jumapili, ambayo ilitaka kujiondoa kwa "vikosi vya nchi za nje" kutoka nchi yake ambayo ni tajiri ya madini.

    "Serikali yangu inaeleza kufadhaishwa na jinsi Baraza la Usalama limetoa taarifa rahisi, isiyo wazi, na isiyo na maana," alisema, na kuongeza kuwa Rwanda inahitajika kutambuliwa wazi kama "mshambuliaji."

    Wengine katika DRC wanatumai kuwa machafuko na uharibifu unaosababishwa na kuingia kwa waasi wa M23 katika sehemu za Goma Jumatatu utasukuma Baraza la Usalama la UN kuchukua hatua kali wakati wa mkutano siku ya Jumanne.

    Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika pia litakutana siku hiyo hiyo kujadili hali ilivyo mashariki mwa DRC.

    Soma zaidi:

  20. Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja ikiwa ni tarehe 28/01/2025