Moja kwa moja, Trump amtuhumu Starmer kwa kutaka 'kujiunga na vita baada ya sisi kushinda'

Wizara ya Ulinzi ilithibitisha kuwa moja ya meli mbili za kubeba ndege za Uingereza imewekwa katika hali ya utayari.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Asha Juma

  1. Idadi ya waliofariki Kenya kwa mafuruko yafikia 28 huku tahadhari ya hatari za kiafya ikitolewa

    .

    Chanzo cha picha, EPA

    Idadi ya waliofariki dunia imeonezeka hadi 28 kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha kote nchini huku wizara ya afya Kenya ikitoa tahadhari kuhusu hatari zinazoweza kutokea kiafya.

    Timu za uokozi bado zinatafuta manusura, polisi imesema.

    Mkuu wa polisi wa Nairobi George Seda alisema miili mitano zaidi ilipatikana Jumamosi jioni huku kukiwa na hofu kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka wakati shughuli za utafutaji zikiendelea.

    "Timu ziko huko tena kuendelea kutafuta manusura wanaoweza kupatikana lakini tunatarajia kupata miili zaidi," alisema.

    Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Afya nchini Kenya Mary Muthoni amesema kwamba mvua kubwa na mafuriko vinaweza kusababisha uchafuzi wa vyanzo vya maji, kuongezeka kwa uzalishaji wa vijidudu vya magonjwa kama vile mbu na kuvuruga mifumo ya usafi.

    Hali hizi, aliongeza, zinaweza kuchangia milipuko ya magonjwa ya kuambukiza na mengineo kama kipindupindu, homa ya matumbo, na kuhara ambayo yanaweza kutokea kutokana na unywaji wa maji au chakula kilichochafuliwa.

    Maafisa wa afya walitahadharisha zaidi kwamba hali ya hewa ya baridi na unyevunyevu inaweza kusababisha kuongezeka kwa maambukizi ya njia ya upumuaji, hasa miongoni mwa makundi yaliyo hatarini kama vile watoto, wazee na wenye kinga dhaifu.

    Majeraha yanayohusiana na mafuriko pia yaliorodheshwa miongoni mwa hatari zinazowezekana wakati wa msimu wa mvua.

    Wizara pia imetaka raia kuwa na tahadhari juu ya kuzama maji pamoja na kuumwa na nyoka kipindi hiki cha mafuriko.

    Soma zaidi:

  2. Trump amtuhumu Starmer kwa kutaka 'kujiunga na vita baada ya sisi kushinda'

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Marekani Donald Trump ameiambia Uingereza kuwa haihitaji meli zake za kubeba ndege na kumshutumu Waziri Mkuu Sir Keir Starmer kwa kutaka "kujiunga na vita baada ya sisi kushinda", huku Marekani na Israel zikiendelea kushambulia Iran.

    Katika chapisho lake kwenye mitandao ya kijamii, Trump alisema Uingereza "inafikiria kwa uzito" kutuma meli mbili za kubeba ndege Mashariki ya Kati, kabla ya kusema kwamba Marekani "haihitaji". Downing Street haijajibu.

    Wizara ya Ulinzi ilithibitisha kuwa moja ya meli mbili za kubeba ndege za Uingereza imewekwa katika hali ya utayari.

    Matamshi ya Trump yalikuja baada ya ndege za kivita za Marekani kuonekana zikitua Uingereza huku Marekani ikianza kutumia kambi za Uingereza kwa "shughuli maalum za kujilinda".

    "Uingereza, ambayo hapo awali ilikuwa Mshirika wetu Mkuu, labda Mkubwa kuliko zote, hatimaye inafikiria kwa uzito kutuma meli mbili za kubeba ndege Mashariki ya Kati," Trump aliandika kwenye mtandao wa Truth Social Jumamosi. "Hiyo ni sawa, Waziri Mkuu Starmer, hatuzihitaji tena - Lakini hili tutalikumbuka."

    "Hatuhitaji watu wanaojiunga na Vita baada ya kushinda!"

    Akizungumza kwenye Air Force One akijibu swali kuhusu matumizi ya kambi za Uingereza katika vita, Trump alirejelea chapisho lake kwenye Truth Social, akisema: "Hatuzihitaji", akionekana kurejelea ndege hizo.

    Aliongeza: "Sio wakati mwafaka. Ingekuwa vizuri kuwa nao wiki mbili zilizopita."

    Serikali ya Uingereza ilisema wazi kwamba haina nia ya kujiunga na operesheni kubwa ya mashambulizi Mashariki ya Kati.

    Soma zaidi:

  3. Mlipuko watokea nje ya ubalozi wa Marekani huko Norway – Polisi

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Polisi nchini Norway wamezingira eneo linalozunguka ubalozi wa Marekani mjini Oslo baada ya mlipuko kuripotiwa katika eneo hilo.

    "Idadi kubwa ya maafisa wa usalama" imetumwa katika eneo hilo takriban saa 1:00 usiku wa manane (GMT), polisi walisema.

    "Polisi wanafanya mazungumzo na ubalozi na hakuna majeraha yaliyoripotiwa," ilisema taarifa hiyo.

    "Kwa sasa hakuna taarifa kuhusu hasa kilichotokea au ni nani anayeweza kuhusika," polisi waliongeza.

    Michael Dellemyr, ambaye anaongoza kundi la polisi waliofika eneo la tukio, aliambia mtangazaji wa Norway NRK kwamba mlipuko huo ulitokea kwenye mlango wa umma wa jengo hilo.

    Ubalozi ulipata uliharibiwa kidogo, ripoti za vyombo vya habari zinasema.

    Ubalozi wa Marekani upo katika wilaya ya Morgedalsvegen ya Oslo, yapata kilomita 7 (maili nne) nje ya katikati mwa jiji.

    Soma zaidi:

  4. Moto mkubwa waunguza mnara wa jiji la Kuwait

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Ni siku nyingine tena tunapokutana, tukiwa tayari kukuletea habari kuhusu mzozo wa Mashariki ya Kati, ambao sasa umeingia wiki yake ya pili.

    Maghala ya mafuta mjini Tehran yameshambuliwa, maafisa wa Lebanon wanasema watu wanne wameuawa katika shambulio la Israel kwenye hoteli moja mjini Beirut, na Israel inasema iliwashambulia "makamanda wakuu" wa Kikosi cha Lebanon cha Wakurdi, ambacho ni tawi la operesheni za nje ya nchi la IRGC.

    Mataifa ya Ghuba pia yamekuwa yakiripoti makombora na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani.

    Moto mkubwa umeteketeza mnara huko Kuwait, ambapo jeshi linasema limekuwa likikabiliana na "wimbi la ndege zisizo na rubani za adui zilizovamia anga ya nchi hiyo".

    "Baadhi ya vituo vya raia vimeharibika kutokana na vifusi na vipande vya silaha vilivyoanguka wakati wa operesheni ya kuzuia ndege za adui," msemaji rasmi wa Wizara ya Ulinzi amenukuliwa akisema katika chapisho kwenye mtandao wa X, lililoshirikishwa na jeshi la Kuwait.

    Jeshi la anga la nchi hiyo "linaendelea kushambulia maeneo fulani angani ya maadui", msemaji huyo anasema, huku jeshi likiwahimiza raia na wakazi "kufuata maagizo ya usalama na usalama".

    Soma zaidi:

  5. Hujambo na karibu katika matangazo yetu mubashara ya tarehe 08/03/2026.