Rais wa
Marekani Donald Trump ameiambia Uingereza kuwa haihitaji meli zake za kubeba
ndege na kumshutumu Waziri Mkuu Sir Keir Starmer kwa kutaka "kujiunga na
vita baada ya sisi kushinda", huku Marekani na Israel zikiendelea
kushambulia Iran.
Katika
chapisho lake kwenye mitandao ya kijamii, Trump alisema Uingereza
"inafikiria kwa uzito" kutuma meli mbili za kubeba ndege Mashariki ya
Kati, kabla ya kusema kwamba Marekani "haihitaji". Uingereza haijajibu.
Wizara ya
Ulinzi ilithibitisha kuwa moja ya meli mbili za kubeba ndege za Uingereza
imewekwa katika hali ya utayari.
Matamshi ya
Trump yalikuja baada ya ndege za kivita za Marekani kuonekana zikitua Uingereza
huku Marekani ikianza kutumia kambi za Uingereza kwa "shughuli maalum za
kujilinda".
"Uingereza,
ambayo hapo awali ilikuwa mshirika wetu mkuu, labda mkubwa kuliko wote,
hatimaye inafikiria kwa uzito kutuma meli mbili za kubeba ndege Mashariki ya
Kati," Trump aliandika kwenye mtandao wa Truth Social Jumamosi. "Hiyo
ni sawa, Waziri Mkuu Starmer, hatuzihitaji tena - Lakini hili tutalikumbuka."
"Hatuhitaji
watu wanaojiunga na vita baada ya kushinda!"
Akizungumza
kwenye Air Force One akijibu swali kuhusu matumizi ya kambi za Uingereza katika
vita, Trump alirejelea chapisho lake kwenye Truth Social, akisema:
"Hatuzihitaji", akionekana kurejelea ndege hizo.
Aliongeza:
"Sio wakati mwafaka. Ingekuwa vizuri kuwa nao wiki mbili zilizopita."
Serikali ya
Uingereza ilisema wazi kwamba haina nia ya kujiunga na operesheni kubwa ya
mashambulizi Mashariki ya Kati.