Kesi ya nyaraka za siri iliyomkabili Trump yafutiliwa mbali na jaji wa Florida
Jaji wa Florida ametupilia mbali kesi ya nyaraka za siri za Wizara ya Sheria dhidi ya Donald Trump katika ushindi mkubwa wa rais huyo wa zamani siku chache tu baada ya mtu mwenye silaha kujaribu kumuua.
Muhtasari
Trump asema "ataleta nchi pamoja" baada ya kunusurika jaribio la mauaji
Mshukiwa mkuu wa mauaji ya wanawake jijini Nairobi akamatwa
Watu kadhaa wahofiwa kufariki baada ya bomu lililotegwa kulipuka Mogadishu
Polisi wanamsaka meya anayetuhumiwa kuwa jasusi wa China
Waziri wa Uingereza ahimiza kusitishwa kwa mapigano mara moja wakati wa ziara yake Israel
Argentina yaishinda Colombia na kutwaa taji la 16 la Copa America
England yavunjwa moyo baada ya kushindwa na Uhispania katika fainali ya Euro 2024
Mshawishi wa Instagram afungwa jela kwa ulanguzi na utumwa
IDF yasema kamanda mkuu wa Hamas aliuawa katika shambulio la anga la Israel
'Tunahitaji wamarekani kutuliza joto la kisiasa', Biden asema
Moja kwa moja
Asha Juma
Ruto ashutumu shirika la Kimarekani kwa kufadhili maandamano ya vurugu nchini Kenya
Chanzo cha picha, Getty Images
Rais William Ruto ameushutumu wakfu wa Ford, ambao ni wakfu wa binafsi wa Marekani, kwa kufadhili ghasia wakati wa maandamano dhidi ya serikali.
Akiongea mjini Nakuru siku ya Jumatatu, Ruto alidai kuwa Wakfu huo ulikodi watu kusababisha ghasia wakati wa maandamano yaliyosababisha uharibifu wa mali na uporaji wa biashara.
"Nataka niulize watu wa Ford Foundation watuambie hio pesa wanatoa, wanatoa ifanye fujo ndio wapate faida gani?"
"Tutawaita na tutawaambia kama hawapendi demokrasia nchini Kenya, kama watafadhili vurugu na machafuko tutawaita na tutawaambia wao pia kujirekebisha au waondoke." Alisema Rais Ruto.
Alisema kuwa serikali yake haitamwacha yeyote anayewasajili vijana wa Kenya ili kusababisha ghasia barabarani wakati wa maandamano ya amani.
Habari za hivi punde, Kesi ya nyaraka za siri iliyomkabili Trump yaondolewa na jaji wa Florida
Jaji wa Florida ametupilia mbali kesi ya nyaraka za siri za Wizara ya Sheria dhidi ya Donald Trump katika ushindi mkubwa wa rais huyo wa zamani siku chache tu baada ya mtu mwenye silaha kujaribu kumuua.
Jaji Aileen Cannon amekubali ombi la Trump la kutupilia mbali kesi hiyo kwa msingi kwamba uteuzi wa Wizara ya Sheria wa Mwendesha Mashtaka Maalum Jack Smith unakiuka Kipengele cha Uteuzi cha Katiba ya Marekani.
Trump alikana mashtaka kadhaa katika kesi hiyo ya kushughulikia nyaraka za siri, ikiwa ni pamoja na kuhifadhi kwa makusudi taarifa za ulinzi wa taifa.
Makumi ya makablasha yaliyoainishwa yalipatikana katika hoteli ya Trump ya Mar-a-Lago huko Florida, pamoja na kwenye bafu na chumba cha kuhifadhia, baada ya Trump kuondoka Ikulu ya White House mnamo 2021.
"Mahakama ina hakika kwamba mashtaka ya Wakili Maalum Smith kuhusu hatua hii yanakiuka misingi miwili ya kimuundo ya mpango wetu wa kikatiba, jukumu la Congress katika uteuzi wa maafisa wa kikatiba, na jukumu la Congress katika kuidhinisha matumizi kwa mujibu wa sheria,"
Kwa nini Trump aliulizia viatu vyake baada ya shambulio la risasi?
Chanzo cha picha, Reuters
Wacha tuangalie maelezo mengine tuliyobaini kutoka kwenye mahojiano ya Trump na New York Post.
Katika moja ya video za jaribio la mauaji, Trump alisikika akisema: "Nahitaji viatu vyangu." Aliielezea New York Post kwamba maafisa usalama waliomrukia baada ya kupigwa risasi walitumia nguvu sana hadi viatu vyake kudondoka.
"Na viatu vyangu vilikuwa vimenibana," aliambia gazeti hilo. Trump pia aliwapongeza wafanyakazi wa usalama kwa hatua zao na akawasifu kwa kumpiga risasi mtu aliyejihami kwa silaha.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema "ilikuwa awe amekufa" baada ya jaribio la kumuua Jumamosi usiku katika mkutano wa hadhara huko Pennsylvania.
Katika mojawapo ya mahojiano yake ya kwanza tangu kisa hicho, Bw Trump aliambia vyombo vya habari vya kihafidhina vya Marekani kuwa alihisi kuwa ameokolewa "kwa bahati na Mungu".
"Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba sikugeuza tu [kichwa changu] lakini kugeuka kwa wakati ufaao na kwa kiwango kinachofaa," alisema, akiongeza kuwa risasi ilivyogusa sikio lake ingeweza kumuua kwa urahisi.
"Ninapaswa kufa, sitakiwi kuwa hapa," alisema.
Mtazamaji mmoja aliuawa katika shambulio hilo, huku watu wengine wawili wakijeruhiwa vibaya.
Mshambuliaji, ambaye pia alikufa, ametajwa kwa jina Thomas Matthew Crooks.
Trump asema "ataleta nchi pamoja" baada ya kunusurika jaribio la mauaji
Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa
zamani Donald Trump ametoa moja ya mahojiano yake ya kwanza tangu jaribio la kumuua
Jumamosi usiku, akisema ameandika upya kabisa hotuba yake ya mkutano ili
kuzingatia ujumbe wa "umoja" badala ya kumkosoa Joe Biden.
"Hotuba
ambayo ningetoa Alhamisi itakuwa ya kufurahisha," aliiambia Washington
Examiner.
"Kama
haya hayangetokea, hii ingekuwa mojawapo ya hotuba za kushangaza," alisema
pia, akiongeza kuwa ingelenga zaidi sera za Rais Biden.
"Kusema
kweli, itakuwa hotuba tofauti kabisa sasa. Ni nafasi ya
kuleta nchi pamoja. Nilipewa nafasi hiyo.”
Trump pia alisema kwamba "ukweli" wa kile
kilichotokea Jumamosi " ndio unaanza tu," na akaelezea wakati
alipotazama umati wa watu baada ya kugundua kuwa alikuwa amepigwa risasi.
“Nguvu iliotoka kwa watu waliokuwepo wakati huo, walisimama tu;
ni vigumu kuelezea jinsi nilivyohisi, lakini nilijua ulimwengu ulikuwa
unatazama. Nilijua kuwa historia ingehukumu hili, na nilijua lazima
niwafahamishe tuko sawa,” alimwambia Mkaguzi.
Donald Trump amesema "alitakiwa kuwa amefariki",
akitaja jaribio la mauaji kuwa "kitu kibaya" kukipitia.
"Sitakiwi
kuwa hapa, ninapaswa kuwa nimekufa," Trump alisema, akizungumza na New
York Post alipokuwa akielekea Milwaukee kwa Kongamano la Kitaifa la Republican.
Trump alivaa
bandeji nyeupe iliyofunika sikio lake la kulia lakini wasaidizi wake
hawakuruhusu picha zozote kupigwa, lilisema Post.
"Daktari
katika hospitali alisema hajawahi kuona kitu kama hiki, alikitaja kuwa muujiza," Trump aliongeza.
'Mshukiwa mkuu' akamatwa baada ya miili kupatikana jalalani Kenya
Chanzo cha picha, AFP
Polisi nchini Kenya wamemkamata mwanamume ambaye wamemtaja kama "muuaji wa watu wengi" anayeshukiwa kuhusika na mauaji ya kutisha ya wanawake tisa ambao miili yao iliyokatwakatwa ilipatikana kwenye machimbo ambayo yanatumika kama jalala.
Mshukiwa alikamatwa katika baa mapema Jumatatu asubuhi alipokuwa akitazama fainali ya Euro.
Kumekuwa na mshtuko na ghadhabu nchini Kenya tangu maiti ya kwanza ya miili kupatikana siku ya Ijumaa katika mji mkuu, Nairobi.
"[Ali]kiri kuwarubuni, kuwaua na kutupa miili ya wanawake 42 katika eneo hilo la taka .Wote waliuawa kati ya 2022 na hivi majuzi Alhamisi," alisema Mohamed Amin, mkuu idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Alisema wamepata ushahidi muhimu katika nyumba ya mtuhumiwa, zikiwemo simu 10, tarakilishi bebe , panga, vitambulisho na mavazi ya kike.
Somalia: Bomu lililotegwa garini laua watu 9 waliokuwa wakitazama fainali ya Euro
Chanzo cha picha, BARAHA BULSHADA
Watu kadhaa wameuawa baada ya bomu lililotegwa ndani ya gari
kulipuka nje ya mkahawa maarufu uliokuwa umejaa mashabiki wa soka katika mji
mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Bomu hilo lililipuka Jumapili usiku saa 22:28 kwa saa za
huko wakati walinzi wa Top Coffee walikuwa wakitazama fainali ya kandanda ya
Euro 2024 kati ya Uhispania na England.
Polisi wamesema takriban watu watano waliuawa katika mlipuko
huo na wengine 20 kujeruhiwa. Vyanzo vya usalama baadaye vililiambia shirika la
habari la AFP kwamba idadi ya waliofariki imeongezeka hadi tisa.
Kundi la wanajihadi la al-Shabab lilisema lilitekeleza
shambulio hilo.
"Tulisikia mlipuko mkubwa na wa kutisha katika kipindi
cha kwanza cha mchezo tuliokuwa tukiutazama. Kila mtu alilazimika kufikiria
jinsi ya kujiokoa," mmoja wa walionusurika, Mohamed Muse, aliiambia BBC.
"Niliona watu katika hatari, watu waliojeruhiwa
wakipiga kelele kuomba msaada, na wengine kuchanganyikiwa – ilikuwa hali ya kutisha," aliongeza.
Mlipuko huo pia uliharibu magari kadhaa na kuharibu majengo pia.
Al-Shabab, kundi ambalo ni sehemu ya al-Qaeda, linaripotiwa kusema
lililenga mahali ambapo maafisa wa usalama na wafanyikazi wa serikali hukutana
usiku.
Eneo hilo liko karibu na Villa Somalia, makazi rasmi ya
rais.
Kundi hilo la kijihadi limefanya mashambulizi mengi ya
mabomu katika mji huo na maeneo mengine ya Somalia katika kipindi cha miaka 17
iliyopita.
Hata hivyo, kumekuwa na utulivu katika miezi ya hivi
karibuni huku kukiwa na kuendelea kwa mashambulizi ya vikosi vya usalama vya
Somalia dhidi ya kundi hilo ambalo bado linadhibiti maeneo makubwa ya nchi.
Polisi wanamsaka meya anayetuhumiwa kuwa jasusi wa China
Chanzo cha picha, Facebook
Meya wa mji
mdogo nchini Ufilipino ambaye ameshutumiwa kuwa jasusi wa China, ameenda
mafichoni, maafisa walisema.
Polisi
hawakuweza kutekeleza kibali cha kukamatwa kwa Alice Guo mwishoni mwa juma kwa
kuwa hakupatikana katika anwani zake zote zinazojulikana.
Vituo vya kulaghai
watu vilifichuliwa katika mji wa Bi Guo wa Bamban mnamo mwezi Machi,
vikiwa vimefichwa kwenye kasino za mtandaoni zinazohudumia Wachina wa bara.
Simulizi
yake imekuwa kama mchezo wa kuigiza wa televisheni, kwa vile pia aliwahi
kuhojiwa kuhusu kuwa mzazi nchini China na tuhuma kwamba alikuwa akifanya kazi kama
jasusi wa Beijing.
Bunge la
Seneti liliamuru kukamatwa kwa Bi Guo na baadhi ya watu wa familia yake Ijumaa
iliyopita baada ya kupuuza mara mbili wito wa kufika kwenye vikao vya kesi
inayomkabili.
"Jitokeze.
Kujificha hakuwezi kufuta ukweli," Seneta Risa Hontiveros, anayeongoza
uchunguzi wa bunge kuhusu Bi Guo, alisema kwenye taarifa.
Bi Guo
amekana kutenda makosa hayo. Anadai baba yake Mchina na mama yake Mfilipino
walimlea kwenye shamba lao la nguruwe.
Waziri wa Uingereza ahimiza kusitishwa kwa mapigano mara moja wakati wa ziara ya Israel
Chanzo cha picha, FCDO
Waziri wa
Uingereza David Lammy ametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja huko
Gaza wakati wa ziara yake ya kwanza nchini Israel na maeneo ya Palestina kama
waziri wa mambo ya nje.
"Niko
hapa kushinikiza kusitishwa kwa mapigano," alisema. "Kupoteza maisha
katika miezi michache iliyopita... ni ya kutisha. Inabidi ikome."
Bw Lammy pia
alihimiza kuachiliwa kwa mateka wote wanaoshikiliwa Gaza na kuongezeka kwa
misaada katika eneo hilo.
Waziri huyo
mpya aliyechaguliwa alifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin
Netanyahu na Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Palestina Mohammad Mustafa siku ya
Jumapili.
Baadaye
anatarajiwa kukutana na Rais wa Israel Isaac Herzog na familia za baadhi ya
mateka wenye uhusiano na Uingereza.
"Ni
muhimu kwamba, wakati tuko kwenye vita, vita hivyo viendeshwe kwa mujibu wa
sheria za kimataifa za kibinadamu," Bw Lammy alisema.
"Bila
shaka nitakuwa nikisisitiza viongozi wa Israel juu ya suala hilo katika siku
zijazo."
Waziri huyo
wa mambo ya nje pia alionyesha kufadhaika kutokana na ukosefu wa malori ya misaada
ya Uingereza inayoingia Gaza "baada ya miezi na miezi ya kuomba" hilo
kufanyika, akirejelea malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa mashirika ya kutoa misaada
kuhusu kuzuiwa au kucheleweshwa kwa ukaguzi tata uliowekwa na jeshi la Israel.
Alisema hali
ya kibinadamu huko Gaza ilikuwa "ya kutisha" na kwamba Uingereza
itakuwa ikitoa pauni milioni 5.5 za ziada kwa shirika la matibabu la UK-Med
kufadhili kazi yake katika eneo hilo.
Chama cha
Labour hivi majuzi kimekabiliwa na msukosuko kutoka kwa baadhi ya wapiga kura
Waislamu kuhusu jibu lake kwa mzozo huo, ambao wengi wanauona kuwa hautoshi
kuikosoa Israel.
Serikali
mpya sasa inakabiliwa na maamuzi juu ya masuala kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja
na kuweka kikomo au kusimamisha uuzaji wa silaha kwa Israel kutokana na raia
kupoteza maisha.
Argentina yaishinda Colombia na kutwaa taji la 16 la Copa America
Chanzo cha picha, Getty Images
Argentina
iliishinda Colombia 1-0 na kunyakua taji
la kuvunja rekodi la 16 la Copa America lakini mchezo huo ulitatizwa kwa kucheleweshwa kwa dakika 80 kwa sababu ya
matatizo nje ya uwanja huko Miami.
Lautaro Martinez alifunga bao katika kipindi cha pili cha
muda wa nyongeza kutoka kwa krosi ya Giovani lo Celso .
Nahodha Lionel Messi alitokwa machozi alipolazimika kubadilishwa katikati ya
kipindi cha pili baada ya kuumia alipokuwa akiutafuta mpira - lakini alikuwa
akisherehekea michuano mikuu ya tatu mfululizo ya nchi yake wakati wa kipenga cha mwisho.
Mchezo wa kwanza ulicheleweshwa kwa sababu ya fujo nje ya
Uwanja wa Hard Rock.
Waandalizi walisema mashabiki wasio na tiketi walijaribu
kuingia uwanjani, na kuwaacha mashabiki wengine wakisubiri kwa saa nyingi
kwenye joto la Miami ili milango ifunguliwe.
Mashabiki na maafisa wa polisi na usalama walikabiliana na
kuwakamata kwa watu kadhaa. Wafuasi kadhaa walihitaji matibabu kutoka kwa
wahudumu wa afya.
England yavunjwa moyo baada ya kushindwa na Uhispania katika fainali ya Euro 2024
Chanzo cha picha, Getty Images
Harakati za England kumaliza maumivu na kukatishwa tamaa kwa miaka
58 ziliishia pabaya walipofungwa na Uhispania kwenye fainali ya Euro 2024
kwenye uwanja wa Olympiastadion mjini Berlin baada ya kufungwa mabao 2-1.
Kikosi cha Gareth Southgate kilizamishwa na bao la dakika za
mwisho la Mikel Oyarzabal na kuwaacha wakiwa wamevunjika moyo tena katika fainali ya
pili mfululizo ya Ubingwa wa Ulaya .
Mawinga chipukizi wa Uhispania walishirikiana kuwapa bao la kuongoza dakika mbili baada ya
kipindi cha mapumziko huku pasi ya Lamine Yamal ikifungua nafasi kwa Nico
Williams kumshinda kipa wa Uingereza Jordan Pickford na kumaliza kwa kasi
ndogo.
Nahodha wa England Harry
Kane hakuwa katika hali nzuri kimchezo akatolewa baada ya saa moja na Cole Palmer -
akachukua Kobbie Mainoo - ambaye aliibua matumaini ya kurejea tena kwa bao la
mguu wa kushoto baada ya dakika 73.
Ilikuwa ni Uhispania, hata hivyo, walionyakua ushindi huo dakika
nne kabla ya mchezo kumalizika Oyarzabal alipofunga krosi ya Marc Cucurella na
kuwaacha England katika hali nyingine ya kungoja taji kuu
Mshawishi wa Instagram afungwa jela kwa ulanguzi na utumwa
Wakati wasichana wawili wa Kibrazili waliporipotiwa
kutoweka mnamo Septemba 2022, familia zao na Shirika la Upelelezi la Marekani
– FBI, walianzisha msako mkali kote Marekani ili kuwapata. Walichojua
ni kwamba walikuwa wakiishi na mshawishi wa Instagram Kat Torres.
Torres sasa amehukumiwa kifungo cha miaka minane jela kwa
ulanguzi wa binadamu na utumwa wa mmoja wa wanawake hao.
BBC pia imeambiwa kuwa mashtaka yamewasilishwa dhidi yake
kuhusiana na mwanamke wa pili.
Je, mwanamitindo huyo wa zamani ambaye aliwekwa kwenye jalada
la magazeti ya kimataifa alianzaje kuwahadaa wafuasi wake na kuwarubuni katika ulanguzi
wa kingono?
"Alikuwa kama mwenye kunipa tumaini," anasema
Ana, akielezea hisia zake baada ya kuona ukurasa wa Instagram wa Torres mnamo
2017.
Ana hakuwa
mmoja wa wanawake waliopotea waliolengwa katika msako wa FBI - lakini yeye pia
alikuwa mwathirika wa kulazimishwa na Torres na angekuwa muhimu kwa uokoaji
wao.
Anasema
alivutiwa na historia ya Torres kutoka kuwa mtu masikini wa Kibrazili hadi mwanamitindo
wa kimataifa, akishirikiana na waigizaji mashuhuri wa Hollywood.
"Alionekana
kama alikuwa ameshinda ghasia katika utoto wake, unyanyasaji, matukio yote ya
kutisha," Ana aliambia Uchunguzi wa BBC Eye na BBC News Brasil.
Ana mwenyewe
alikuwa katika mazingira magumu. Anasema aliteseka utotoni kwa vurugu, alihamia
Marekani peke yake kutoka kusini mwa Brazili, na awali alikuwa katika uhusiano
wa unyanyasaji.
Torres
alikuwa amechapisha hivi majuzi wasifu wake uitwao A Voz [The Voice], ambamo
alidai kuwa angeweza kutabiri kutokana na nguvu zake za kiroho, na alikuwa
amehojiwa kwenye vyombo vya habari maarufu vya Brazili.
“Alikuwa kwenye jalada la magazeti. Alionekana na watu
maarufu kama vile Leonardo DiCaprio. Kila kitu nilichoona kilionekana kuwa cha
kuaminika, "anasema.
Ana anasema alivutiwa hasa na mtazamo wa Torres wa
kiroho.
Kitu ambacho Ana hakujua ni kwamba simulizi ya kutia moyo
aliyosimulia Torres ilitokana na nusu ukweli na uwongo.
IDF yasema kamanda mkuu wa Hamas aliuawa katika shambulio la anga la Israel
Chanzo cha picha, IDF
Jeshi la
Israel linasema kamanda mkuu wa Hamas Rafa Salama aliuawa katika shambulio la
anga huko Gaza siku ya Jumamosi. Hata hivyo, Hamas haijathibitisha ripoti hiyo.
Wizara ya
afya inayosimamiwa na Hamas huko Gaza ilisema kuwa shambulio la Israel lilishambulia
kambi ya watu waliokimbia makazi yao katika eneo lililotengwa huko Khan Younis,
na kuua Wapalestina 90 huku wengine 289 wakijeruhi.
Israel
imesema shambulizi hilo lilikuwa linalenga viongozi wakuu wa Hamas, lakini
Hamas inasema madai hayo ni ya "uongo" na yanasaidia
"kuhalalisha" shambulio hilo.
Walioshuhudia
walisema waliona takriban "ndege kubwa za kivita tano zikishambulia kwa
mabomu katikati ya eneo la Al Mawasi, magharibi mwa Khan Younis".
Wengi wa
waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali ya karibu ya Nasser.
Hata hivyo,
kulingana na maafisa na madaktari, kituo hicho "hakina uwezo tena wa
kufanya kazi" kwani madaktari "wamezidiwa na idadi kubwa ya
majeruhi".
Akizungumza
na kipindi cha Newshour kwenye BBC World Service, Dkt Mohammed Abu Rayya,
ambaye yuko katika hospitali inayoshughulikia matokeo ya shambulio hilo,
alisema wengi wa waliojeruhiwa walikuwa wakiuguza majeraha ya vipande vya mabomu.
Aliongeza ni
kama kuwa "kuzimu", kwani wengi wa waathiriwa walikuwa raia, haswa
wanawake na watoto.
Jeshi la
Israel lilisema Salama, kamanda wa Brigedi ya Khan Younis, alikuwa mmoja wa
"wapangaji" wa shambulio la Oktoba 7 na mshirika wa karibu wa
Mohammed Deif, kamanda mkuu wa tawi la kijeshi la Hamas.
Msemaji wa
jeshi alisema kifo cha Salama "kinazuia kwa kiasi kikubwa uwezo wa kijeshi
wa Hamas".
Haijulikani
ikiwa Deif aliuawa. Jeshi la Israel lilisema pia alilengwa katika shambulio
hilo.
Deif amekuwa
miongoni mwa watu wanaosakwa sana na Israel kwa miongo kadhaa na analaumiwa na
mamlaka ya Israel kwa mauaji ya raia na wanajeshi wengi.
Wamarekani wanafaa kupunguza joto la kisiasa-Biden
Chanzo cha picha, Getty Images
Biden ametoa
hotuba kwa taifa baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Donald Trump kuponea
chupu chupu jaribio la mauaji.
Biden
alianza hotuba yake kwa kuwaambia "Wamarekani wenzake" juu ya
"haja ya kutuliza joto la siasa zetu".
"Milio
ya risasi jana kwenye mkutano wa hadhara wa Donald Trump huko Pennsylvania
inatutaka sote kurudi nyuma," alisema.
Biden anamwita
mtu aliyefariki kwa kupigwa risasi 'shujaa'
Katika
hotuba yake, Joe Biden kwa mara nyingine tena anatoa rambirambi zake kwa
familia ya Corey Compatore, mtu aliyeuawa kwa kupigwa risasi Jumamosi.
"Corey
alikuwa mume, baba, wazima moto wa kujitolea na shujaa, akiilinda familia yake
kutokana na risasi hizo," anasema, akiongeza kuwa umma unapaswa kumuweka
yeye na familia yake katika maombi yao.
'Hakuna mahali nchini Marekani kwa vurugu ' - Biden
Rais Biden amekariri kwamba "vurugu kamwe sio jibu"
katika siasa za Marekani, akiorodhesha msururu wa matukio ikiwa ni pamoja na
jaribio la mauaji ya Rais wa zamani Donald Trump, shambulio la Januari 6 bungeni
na shambulio la spika wa zamani Nancy Pelosi.
"Hakuna mahali nchini Marekani kwa aina hii ya
vurugu - kwa vurugu yoyote ile milele," alisema.
"Siasa katika nchi hii zimepamba moto, ni wakati wa
kuzituliza."