IDF yasema inaendeleza oparasheni "kwa nguvu kubwa" kusini mwa Lebanon
Jeshi la Israel IDF limetoa ilani ya watu kuhama kusini mwa Lebanon huku mashambulizi ya anga yakiendelea.
IDF imesema imeongeza nguvu yake ya mashambulizi karibu na eneo la mto Zahrani.
"Yeyote aliyekaribu na miundombinu ya Hezbollah au magari yao ya kijeshi anahatarisha maisha yake” taarifa ya IDF ilisema.
Israel na Hezbollah wamekuwa wakishambuliana siku moja tu baada ya Israel na Lebanon kufanya mazungumzo ya ana kwa ana baada ya miongo kadhaa.
Israel imesisitiza itaendelea na oparesheni yake dhidi ya Hezbollah, huku kundi hilo linaloungwa mkono na Iran limesema litaendelea na mashambulizi yake hadi pale Israel na Marekani watasitisha uvamizi wao.
Zaidi ya watu 2000 wamefariki tangu oparesheni ya jeshi la Israel kuanza nchini Lebanon tarehe 2 mwezi Machi, hii ni kulingana na wizara ya afya ya Lebanon.
Rais Trump amesema kuna uwezekano wa mazungumzo kati ya Iran na Marekani kufanyika katika muda wa siku mbili zijazo.
Soma pia: