Rais wa Korea Kusini Yoon amesimamishwa kazi rasmi

Maelfu ya waandamanaji wamesherehekea baada ya Bunge kupitisha hoja ya kumuondoa madarakani huku waziri mkuu akihudumu kama kaimu rais.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Asha Juma

  1. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu ya moja kwa moja. Kwaheri.

  2. Golikipa wa West Ham, 15, afariki baada ya kuugua saratani

    .

    Chanzo cha picha, West Ham United

    Golikipa wa shule ya michezo ya West Ham amefariki akiwa na umri wa miaka 15 baada ya kuugua saratani.

    Oscar Fairs kutoka Benfleet, Essex, aligundulika kuwa na aina ya uvimbe usio wa kawaida kwenye ubongo wenye ukubwa wa 7cm (2.8in) unaofahamika kama ependynoma, mwezi Agosti 2023.

    Alifanyiwa upasuaji mara saba, raundi moja ya matibabu ya mionzi yanayofahamika kama chemotheraphy na radiotherapy, lakini aliambiwa kuwa kitu pekee anachoweza kufanya ni kupata matibabu ya kupunguza maumivu na msongo wa mawazo unaotokana na kuugua maradhi makubwa.

    Mkurugenzi wa klabu hiyo ya michezo Mark Noble amesema kuwa “alikuwa na maisha mazuri kwa siku za baadaye, na inasikitisha sana kuwa ameondoka kwa familia na marafiki zake katika umri mdogo.”

    Salam za pole kutoka kwa vilabu vingi na wachezaji wengi wa mpira zimekuwa zikitolewa kwenye mitandao ya kijamii, ikiwemo kipa wa Real Madrid Thibaut Courtois na nyota wa Liverpool aliyestaafu, Jamie Carragher.

    Ukurasa wa kusaidia familia kukusanya £100,000 kwaajili ya gharama za matibabu nchini Ufaransa umefunguliwa.

    Kulingana na familia yake, Wachezaji wa timu ya West Ham wamechangia £27,000, huku mwenyekiti wao David Sullivan akichangia £10,000 na mchezaji wa Arsenal na mchezaji wa zamani wa West Ham Declan Rice wakitoa £5,000.

    Ratiba zote za shule hiyo ya michezo za mwishoni mwa wiki zimeahirishwa ikiwa kama ishara ya heshima kwa marehemu.

  3. Marekani yasema uhusiano wake na Korea Kusini ni kama ‘chuma’

    .

    Chanzo cha picha, Picha za Getty

    Balozi wa Marekani nchini Korea Kusini ameandika kwenye ukurasa wake wa X kuwa amekutana na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo, baada ya hatua ya kumuondoa madarakani Rais Yoon.

    Philip Goldberg amesema “Kama kawaida, Marekani inaunga mkono Jamhuri ya Korea na hatua ya kidemokrasia na kikatiba ipo pamoja na raia wake.”

    “Waziri wa mambo ya nje Cho na mimi tumehakikisha kuwa uhusiano wetu utaendelea kuwa imara kama chuma. Ahadi zetu kuhusiana na amani kwenye rasi ya eneo hili zipo thabiti.”

    Korea Kusini ni mshirika muhimu wa Marekani katika eneo la Asia – nchi hizo mbili zinashirikiana kwa karibu sana hususan, kwenye masuala yanayo husiana na Korea Kaskazini.

    Pia unaweza kusoma:

  4. Mlipuko wa bomu waua watu watatu na kujeruhi wengi kwenye tamasha Thailand

    .

    Chanzo cha picha, Umphang Rescue Group

    Takriban watu watatu wameuawa na wengi kujeruhiwa baada ya bomu kurushwa kwenye kundi la watu waliokusanyika katika tamasha nchini Thailand.

    Shambulio hilo lilitokea muda mfupi kabla ya saa sita usiku saa za eneo hilo, siku ya Ijumaa, katika tamasha la Red Cross Doi Loyfa, linalofanyika kila mwaka kwenye wilaya ya Umphang, Kaskazini mwa jimbo la Tak.

    Watuhumiwa wawili wanashikiliwa, lakini kulingana na vyombo vya habari nchini humo na shirika la habari la AP wakinukuu kile ambacho polisi wa Thai wamekisema, ni kuwa, hakuna mashtaka yoyote yaliyotolewa hadi sasa.

    Polisi wanasema karibu watu 48 wamejeruhiwa, ambao sita kati yao wamejeruhiwa vibaya sana.

    Polisi walipewa taarifa majira ya 23:30PM usiku saa za Thailand siku ya Ijumaa.

    Timu ya uokoaji ya Umphang imesema kuwa bomu lilirushwa na kutua mbele ya jukwaa lililokuwepo nje ambapo wahudhuriaji wa tamasha hilo walikuwa wakicheza densi.

    Waziri mkuu Paetongtarn Shinawatra ametoa salamu za pole kwa familia za wale walioathirika na tukio hilo kupitia mtandao wa kijamii wa X.

    Pia aliongeza kwa kusema ameagiza polisi na mashirika ya kiusalama kuchunguza chanzo cha mlipuko huo na kuwasaidia wale walioathirika na tukio hilo. Pia ameagiza kuwepo kwa idadi kubwa ya polisi kwenye matukio yote ya matamasha.

    Ripoti kadhaa zinaashiria kuwa mlipuko huo ulisababishwa na bomu lililotengenezwa nyumbani kwa kutumia vifaa ambavyo ni rahisi kupatikana.

    Pia unaweza kusoma:

  5. Ghasia nchini Georgia zaongezeka huku aliyekuwa mchezaji soka akitarajiwa kuwa rais

    .

    Chanzo cha picha, Picha za Getty

    Mchezaji wa mpira wa miguu wa zamani kutoka timu ya mpira ya Manchester City, anatarajiwa kuapishwa kuwa rais siku ya Jumamosi na bunge la Georgia, lenye mgawanyiko mkubwa, baada ya siku 16 za maandamano yanayounga mkono umoja wa ulaya, EU, ambayo yamegubika miji ya nchi hiyo.

    Mikheil Kavelashvili, 53, ni mbunge wa zamani kutoka chama cha Georgian Dream ambacho kimeshutumiwa kwa kuwa na misimamo mikali na ndiye mgombea pekee wa nafasi hiyo.

    Waandamanaji walianza kukusanyika nje ya bunge Jumamosi asubuhi.

    Vyama vikuu vinne vya upinzani vimemkataa Kavelashvili na kususia bunge, wakisisitiza kuwa uchaguzi uliofanyika mwezi Oktoba 2024, ulikuwa wa hila.

    Rais anayeondoka madarakani ambaye anashirikiana kwa karibu na mataifa ya Magharibi, Salome Zourabichvili, ameshutumu kitendo cha Kavelashvili kuibuka mshindi na kudai kuwa kulikuwa na udanganyifu, na kusisitiza kuwa yeye ndiye anayeshikilia nafasi pekee ya Georgia inayofuata kanuni za demokrasia.

    Maandamano dhidi ya chama cha Georgian Dream yalianza mara tu baada ya uchaguzi wa Oktoba, lakini yaliibuka tena mnamo Novemba 28 wakati serikali ilipotangaza kuwa inasimamisha mazungumzo ya kujiunga na umoja wa ulaya, EU, hadi mwaka 2028.

    Pia unaweza kusoma:

  6. Mahakama ya katiba Korea Kusini yatarajia kukutana siku ya Jumatatu

    .

    Chanzo cha picha, Picha za Getty

    Vyombo vya Habari nchini Korea Kusini vimeripoti kuwa, Mahakama ya Kikatiba inatarajia kukutana siku ya Jumatatu kuzungumzia ratiba ya kusikilizwa kwa kesi ya kumuondoa Yoon madarakani.

    Mahakama pia itapanga tarehe ya kusikilizwa kwa kesi hiyo hadharani, licha ya kuwa haijulikani ikiwa Yoon mwenyewe atahudhuria.

    Kiongozi wa chama cha Yoon amekubali matokeo ya kura ya kumuondoa madarakani

    Kiongozi wa chama cha Yoon cha People’s Power, Han Dong-hoon, anasema anakubali matokeo ya leo na anayachukulia kwa umakini sana.

    Kabla ya wabunge kupiga kura ya kutaka kumuondoa Yoon madarakani, Han alijaribu kumuomba rais kufikiria kujiuzulu.

    Han amewaambia waandishi wa habari bungeni muda si mrefu kuwa, chama cha People’s Power “kitarekebisha makosa yaliyotokea na kulinda katiba na demokrasia.”

    Pia unaweza kusoma:

  7. Yoon anasema 'Nasimamisha kwa muda safari yangu'

    .

    Chanzo cha picha, AFP

    Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol ametoa taarifa kufuatia kura ya kumuondoa madarakani.

    "Ninasimamisha safari yangu kwa muda," alisema rais, ambaye mamlaka yake yatasitishwa mara moja.

    "Ingawa kwa muda huu nasitisha hili, safari ya siku zijazo niliyotembea kwa miaka miwili na nusu iliyopita lazima iendelee. Sitakata tamaa kamwe. Nitapokea ukosoaji, sifa na uungwaji mkono wenu kwa moyo mkunjufu na kufanya kila niwezalo kwa nchi hii hadi mwisho.”

    Prime Minister Han Duck-soo, who will assume the role of acting president once Yoon receives a copy of the impeachment resolution, has commented on the impeachment vote.

    Waziri Mkuu aapa 'uendeshaji thabiti wa masuala ya serikali'

    Waziri Mkuu Han Duck-soo, ambaye atachukua nafasi ya kaimu rais mara Yoon atakapopokea nakala ya azimio la kumuondoa madarakani, ametoa maoni yake kuhusu kura hiyo.

    "Nitatumia nguvu na juhudi zangu zote katika utendakazi thabiti wa mambo ya serikali," amesema baada ya Bunge la Kitaifa kupitisha kura ya kumuondoa rais madarakani.

    Anatarajiwa kufanya mkutano wa baraza la mawaziri leo, kulingana na shirika la habari la Yonhap.

  8. Habari za hivi punde, Raia washerehekea baada ya Bunge kumuondoa rais wa Korea Kusini madarakani

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Bunge limepiga kura ya kumuondoa madarakani Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol, huku wabunge 204 wakiunga mkono hoja hiyo.

    Ina maana kwamba Yoon atasimamishwa kazi mara moja, na waziri mkuu atakuwa kaimu rais.

    Hata hivyo, hatu hiyo sio hakikisho kwamba ataondolewa kabisa ofisini.

    Mchakato mzima wa kumuondoa madarakani unaweza kuchukua wiki kadhaa, kwasababu kesi bado inabidi ifanyike katika Mahakama ya Kikatiba.

    Iwapo wajumbe sita kati ya tisa wa mahakama hiyo watapiga kura kuunga mkono kuendelezwa na hatua hiyo, basi rais ataondolewa madarakani.

    Na ikifikia hatua hii, uchaguzi wa rais ajaye utaitishwa ndani ya siku 60 baada ya uamuzi huo.

    Yoon atasimamishwa kazi atakapopokea ilani ya kuondolewa madarakani

    Kulingana na spika wa bunge la Korea Kusini Woo Won-shik, mamlaka na majukumu ya urais ya Yoon yatasitishwa baada ya nakala za hati kuhusu kuondolewa madarakani kuwasilishwa kwake na kwa Mahakama ya Kikatiba.

    Soma zaidi:

  9. Daktari wa mwisho wa upasuaji wa mifupa kaskazini mwa Gaza ameuawa - maafisa wa Palestina

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Daktari wa upasuaji wa mifupa anayeaminika kuwa wa mwisho aliyesalia kaskazini mwa Gaza ameuawa na Israel, kwa mujibu wa maafisa wa Palestina.

    Dkt Sayeed Joudeh alifariki siku ya Alhamisi alipokuwa akielekea kazini.

    Alikuwa daktari wa upasuaji katika hospitali za Kamal Adwan na al-Awda kaskazini mwa Gaza.

    Jeshi la Israel lilisema kuwa halifahamu tukio hilo, lakini linafanya uchunguza.

    Daktari huyo ambaye alikuwa amestaafu alijitokeza ili kusaidia wakati wa vita kati ya Israel na Hamas.

    Mwezi uliopita akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika Hospitali ya Kamal Adwan, alishikilia bango lililosomeka "Tuokoe".

    "Akiwa njiani kuelekea Hospitali ya al-Awda kuangalia mgonjwa, alifyatuliwa na kifaru moja kwa moja kuelekea upande wake," kulingana na Dk Hussam Abu Safiya, mkurugenzi wa Hospitali ya Kamal Adwan.

    "Kwa bahati mbaya, aliuawa papo hapo."

    Lakini baadhi ya walioshuhudia wanasema Dkt Joudeh alipigwa risasi na ndege isiyo na rubani.

    Israel haiwaruhusu waandishi wa habari wa kigeni kuingia Gaza.

    Soma zaidi:

  10. Jeshi la Israel linajiandaa kusalia mpakani katika eneo la amani majira ya baridi

    ,

    Chanzo cha picha, IDF kupitia Reuters

    Waziri wa ulinzi wa Israel amewaagiza wanajeshi kujiandaa kusalia kwenye eneo la amani katika kilele cha Mlima Hermoni wakati wa majira ya baridi, ulio kwenye mpaka kati ya Syria, Lebanon na eneo salama la Umoja wa Mataifa lililoko Milima ya Golan.

    Tangazo hilo linawadia baada ya Israel kutwaa udhibiti wa eneo hilo tarehe 8 Disemba baada ya kuangushwa kwa utawala wa Rais wa Syria Bashar al-Assad.

    Ofisi ya Waziri wa Ulinzi Israel Katz ilisema katika taarifa kwamba "kutokana na kile kinachotokea nchini Syria, kuna umuhimu mkubwa wa kuwepo kwa usalama katika eneo la mlimani".

    Katz aliweka picha kwenye mtandao wa X ikimuonyesha Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu akitumia darubini na kuandika maneno haya: "Ninaangalia kilele cha Syria cha Mlima Hermoni, ambao ulirudi kwa udhibiti wa Israel baada ya miaka 51."

    Umoja wa Mataifa umeitaka Israel kujiondoa katika eneo salama, ambalo liko kati ya Syria na Milima ya Golan inayokaliwa na Israel.

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alisema katika taarifa yake kwamba "anatiwa wasiwasi sana na ukiukwaji mkubwa wa maeneo ya Syria".

    Umoja wa Mataifa umesema Israel inakiuka makubaliano ya mwaka 1974 ya kujiondoa kati ya Israel na Syria ambayo yalianzisha eneo la salama.

    Israel imesema makubaliano ya mwaka 1974 ya kujiondoa "yaliisha" na kuporomoka kwa serikali ya Syria.

    Soma zaidi:

  11. Waandamanaji wa Korea Kusini wakusanyika kabla ya kura ya kumuondoa rais madarakani

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Wabunge wa Korea Kusini watapiga kura ya iwapo watamuondoa rais Yoon Suk Yeol madarakani saa chache zijazo kwa jaribio lake lililoshindwa la kutekeleza sheria ya kijeshi.

    Nchi hiyo ilitumbukia katika machafuko mabaya zaidi ya kisiasa kuwahi kutokea kwa miaka mingi kufuatia tamko la rais la kuanza kutekelezwa kwa sheria ya kijeshi wiki iliyopita.

    Hata hivyo, sheria hiyo iliondolewa kwa haraka saa kadhaa baadaye.

    Mamia ya waandamanaji wanaotaka kuondolewa madarakani kwa Yoon tayari wamekusanyika mbele ya Bunge la Kitaifa, ambapo upigaji kura unatarajiwa kufanyika. Waandamanaji zaidi wanatarajiwa kujiunga.

    Wito wa kumtaka aondolewe madarakani umekuwa ukiongezeka.

    Yoon alinusurika katika kura ya kwanza ya kuondolewa madarakani Jumamosi iliyopita, wakati hoja hiyo ilipokuwa na pungufu ya kura tano kati ya 200 zilizohitajika ili iweze kupitishwa. Hii ilitokea baada ya wabunge wa chama cha Yoon kususia mswada huo.

    Wabunge wa upinzani, hata hivyo, wameapa kupiga kura ya kumuondoa madarakani kila Jumamosi hadi Yoon atakapoondoka.

    Wabunge wengi wa chama cha Yoon, People Power Party (PPP) sasa wamependekeza kuwa watapiga kura kuunga mkono hoja hiyo.

    Soma zaidi:

  12. Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja ikiwa ni tarehe 14/12/2024