Miili ya waathiriwa wa mafuriko Libya yasombwa na maji ufuoni umbali wa maili 60

Mamia ya waathiriwa bado wanaopolewa kutoka kwenye matope, huku takriban watu 30,000 wakiachwa bila makao.

Moja kwa moja

  1. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu kwa leo. Kwaheri

  2. Rubiales apigwa marufuku kwa kumpiga busu mchezaji wakati wa Kombe la Dunia

    .

    Chanzo cha picha, MARCOS DE MAZO/PA

    Jaji amempiga marufuku aliyekuwa mkuu wa soka wa Uhispania Luis Rubiales kwenda umbali wa mita 200 kutoka kwa mwanasoka Jenni Hermoso.

    Waendesha mashtaka waliomba amri ya zuio wakati mahakama ya kitaifa huko Madrid ikizingatia malalamiko ya uhalifu ya unyanyasaji wa kijinsia na kulazimishwa.

    Akiwa amefikishwa mahakama kwa mara ya kwanza, Bw Rubiales alikana kumnyanyasa Bi Hermoso kwa kumbusu midomoni baada ya ushindi wa Kombe la Dunia la Wanawake la Uhispania.

    Wakili wa Bi Hermoso alisisitiza kuwa lilikuwa "busu lisilo la ridhaa".

    Bw Rubiales alijiuzulu wadhifa wake kama mkuu wa shirikisho la kandanda mapema wiki hii na kufika katika kikao cha mahakama siku ya Ijumaa kukana makosa mawili ya uhalifu.

    Jaji anayechunguza kesi hiyo Francisco de Jorge aliombwa amzuie kufika umbali wa mita 500 (futi 1,600) kutoka kwa Jenni Hermoso au asiwasiliane naye.

    Baadaye alikubali agizo hilo lakini akaweka vizuizi vya mita 200 (futi 650), akiongeza kuwa Bw Rubiales hapaswi kuwasiliana na mchezaji huyo wakati wa uchunguzi.

    Ombi zaidi kwamba afike mbele ya hakimu kila baada ya siku 15 lilikataliwa.

    Uhispania ilishinda Kombe la Dunia la Wanawake nchini Australia mnamo 20 Agosti, lakini mafanikio ya timu hiyo hayakushabikiwa vile tangu wakati huo kutokana na vitendo vya Bw Rubiales wakati wa sherehe baada ya firimbi ya mwisho.

    Suala la kususia timu ya taifa bado halijatatuliwa, wiki moja kabla ya mchezo wao ujao, na wachezaji 39 wametia saini barua wakisema kwamba mabadiliko yaliyofanywa na shirikisho la soka "haitoshi kwa wachezaji kujisikia wako mahali salama".

    Baada ya kukanusha madai dhidi yake, aliondoka mahakamani pamoja na wakili wake Olga Tubau.

    Pia unaweza kusoma:

    • Rubiales mahakamani kwa kumpiga busu mchezaji wakati wa Kombe la Dunia la Wanawake
  3. Makumi ya wanamgambo wauliwa na jeshi la Burkina Faso

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Ripoti kutoka Burkina Faso zinasema kuwa jeshi limewaua idadi isiyojulikana ya wapiganaji wa Kiislamu baada ya kushambulia eneo la wanajeshi katika eneo la Kati-Kaskazini.

    Haya yanajiri huku maafisa wakithibitisha kuwa watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo waliwauwa watu wanane katika shambulizi dhidi ya kambi ya wakimbizi wa ndani katika jimbo la kaskazini la Seno mapema wiki hii.

    Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Serikali, karibu wanamgambo 300 walishambulia kituo cha jeshi huko Sogodin.

    Wakati wakijaribu kutoroka washambuliaji hao inasemekana waligawanyika katika makundi kadhaa lakini helikopta za kivita ziliwafuatilia na kuwalenga, na kuua makumi kadhaa.

    Tangu mwaka wa 2015, Burkina Faso imekumbwa na wimbi la ghasia zinazoongezeka kuhusishwa na makundi yenye silaha yanayoshirikiana na al-Qaeda na Islamic State.

    Maelfu ya raia wameuawa huku zaidi ya milioni mbili wakikimbia makazi yao.

    Jeshi nchini Burkina Faso lilimpindua rais wake, Roch Kabore Januari mwaka jana likimtuhumu kwa kushindwa kudumisha usalama.

    Lakini tangu kipindi hicho mgogoro huo umeongezeka.

    Wataalamu wanahofia kuwa huenda nchi hiyo ikageuka kuwa kitovu cha mzozo katika eneo la Sahel.

    Pia unaweza kusoma:

    • Vita dhidi ya wanamgambo wa kiislamu Burkina Faso
  4. Miili ya waathiriwa wa Derna inasongea kwenye ufukwe umbali wa maili kadhaa

    .

    Chanzo cha picha, EPA

    Waathiriwa wa mafuriko ya Derna ambayo ilisombwa na maji hadi baharini inaelea kwenye ufuo umbali wa zaidi ya kilomita 100 (maili 60), anasema mkazi wa jiji la Tobruk upande wa mashariki.

    Nasir Almnsori, mhandisi anayeishi katika jiji hilo zaidi ya kilomita 150 kutoka Derna, aliambia BBC Breakfast kwamba waathiriwa wa mafuriko walikuwa wakisombwa hadi eneo lililo karibu.

    Baadhi ya familia ya Almnsori walifariki huko Derna, na wale watatu walionusurika walifunga safari hadi Tobruk ili kukaa na jamaa zao.

    Anasema kiasi kikubwa cha jiji hilo limeharibiwana hakuna kitu kilichosalia kwao huko Derna.

    "Hawana nyumba huko za kuishi, ndio maana walihamia mji wangu," alisema.

    Soma zaidi:

    • 'Tukio lisilofikirika': Walionusurika waelezea mafuriko ya Libya
    • Tazama :Kijiji kizima kilivyosombwa na mafuriko mpaka baharini Libya
  5. Raia wa Poland akamatwa Kenya akiwa na heroini yenye thamani ya $22,000

    .

    Chanzo cha picha, Directorate of Criminal Investigations/X

    Maafisa wa upelelezi nchini Kenya wamemkamata mshukiwa wa ulanguzi wa dawa za kulevya kutoka Poland akiwa na heroini yenye thamani ya $22,000 (£18,000) katika uwanja mkuu wa ndege kwenye mji mkuu, Nairobi.

    Arkadiusz Stanislaw, mshukiwa, alikamatwa muda mfupi kabla ya kupanda ndege ya shirika la Misri inayoelekea Hungary katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.

    Polisi wamemzuilia mshukiwa huyo ambaye anasubiri kufikishwa mahakamani.

    Mkurugenzi wa idara ya kupambana na madawa ya kulevya nchini Kenya Margaret Karanja anaonya kuwa washukiwa wote wa dawa za kulevya watashughulikiwa "vilivyo" kulingana na sheria, bila kujali majukumu yao katika biashara hiyo.

    Nchi hiyo ya Afrika Mashariki ni kituo kikuu cha kupitisha dawa za kulevya kutoka Mashariki ya Kati hadi Magharibi.

    Pia unaweza kusoma:

    • Bangi za kutengeneza maabara zina madhara gani mwilini?
  6. Taarifa za kutatanisha zaibuka kuhusu usalama wa mabwawa mengine ya Libya

    Picha ya satelaiti inaonyesha bwawa la juu huko Wadi kabla ya mafuriko huko Derna

    Chanzo cha picha, Maxar Technologies / Reuters

    Tangu kuporomoka kwa mabwawa mawili katika mji wa Derna nchini Libya, vyombo vya habari vya Libya na vile vya kikanda vimeangazia wasiwasi unaozunguka mabwawa mengine, wasema wenzao wa BBC Monitoring.

    Shirika la habari la Lana na tovuti ya Afrigate News liliripoti maoni ya meya wa mji wa Tocra kaskazini-mashariki mwa nchi, ambapo alionya kwamba mifumo ya kusukuma maji ya bwawa la Wadi Jaza haifanyi kazi, na kwamba kizuizi cha maji kati ya bonde na bwawa hilo kimeanza. kupasuka.

    Alisema hii inaweza kuwa tishio kubwa kwa wakazi wa Bersis, eneo la mashariki mwa Benghazi, na miji jirani ya pwani.

    Jana, ripoti ya kituo cha televisheni cha Al Arabiya ilisema kuwa kuna hofu kwamba bwawa la Wadi Jaza na bwawa la Wadi Qattara linaweza kupasuka.

    Hata hivyo, pia ilinukuu kuwa utawala huo wenye makao yake mashariki mwa nchi ukisema kuwa hali imedhibitiwa na kwamba mabwawa hayo mawili yanafanya kazi kama kawaida.

  7. Rubiales mahakamani kwa kumpiga busu mchezaji wakati wa Kombe la Dunia la Wanawake

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Luis Rubiales amefika katika mahakama ya Madrid kujibu lalamiko la uhalifu la kumpiga busu mchezaji wa Uhispania Jenni Hermoso, siku chache baada ya kujiuzulu kama mkuu wa shirikisho la soka la Uhispania.

    Hakusema lolote alipokuwa akiingia katika mahakama ya kitaifa kukabiliana na tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia na kulazimishwa.

    Bw Rubiales, 46, anasisitiza kwamba alikuwa amepata ruhusa kutoka kwa mwanasoka huyo alipokuwa akisherehekea Uhispania kushinda Kombe la Dunia la Wanawake.

    Mahakama itaamua iwapo kesi hiyo itasikilizwa.

    Waendesha mashtaka wa serikali ya Uhispania wamewasilisha rasmi malalamiko ya jinai dhidi ya rais wa zamani wa shirikisho la kandanda (RFEF), ambayo yatasikilizwa na Jaji Francisco de Jorge.

    Uhispania ilishinda Kombe la Dunia la Wanawake nchini Australia mnamo 20 Agosti, lakini ushindi wa timu hiyo haujavuma inavyostahili kutokana na vitendo vya Bw Rubiales wakati wa kusherehekea baada ya firimbi ya mwisho.

    Hata hivyo Bw Rubiales, ameshikilia kuwa alipoweka mikono kwenye kichwa chake na kumbusu kwenye midomo ilikuwa ya kuheshimiana na kuridhiana.

    Bw Rubiales hatimaye alijiuzulu siku ya Jumapili kama rais wa shirikisho hilo, na kutangaza: "Nina imani na ukweli na nitafanya kila niwezalo ili ubainike."

    Hermoso, 33, anasema kwamba busu hilo halikuwa la makubaliano. Waendesha mashtaka waliwasilisha malalamiko yake ya awali ya unyanyasaji wa kijinsia na kuongeza ni moja ya kulazimishwa, wakisema kwamba alikuwa ameweka shinikizo kwa mshambuliaji huyo wa Uhispania kumtetea huku kukizuka vurugu siku chache baada ya kumbusu.

    Serikali ya mrengo wa kushoto ya Uhispania ilifanyia mageuzi sheria kuhusu ridhaa katika miaka miwili iliyopita baada ya kesi maarufu ya ubakaji mwaka 2016 iliyopelekea wanaume watano kuondolewa kesi ya ubakaji.

    Chini ya sheria inayoitwa "Only Yes is Yes", Bw Rubiales anaweza kukabiliwa na faini au hata kifungo jela iwapo kesi hiyo itasikilizwa na kupatikana na hatia ya unyanyasaji wa kingono.

    Jaji ataamua iwapo kesi hiyo itasikilizwa baada ya kuchunguza msururu wa video kabla, wakati na baada ya sherehe.

    Ameomba kuona wakati wa kupigwa busu "kutoka pembe zote".

    Jaji pia ameomba video ya sherehe hiyo kwenye chumba cha kubadilishia nguo na kutoka kwa basi la timu wakati timu hiyo ikiondoka kwenye uwanja wa Sydney.

    Pia unaweza kusoma:

    • Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 15.09.2023
  8. Je, miili ya wahanga wa mafuriko ya Libya ni tishio kwa afya?

    Mamlaka ya afya inatarajiwa kufanya uamuzi juu ya tishio la janga linalowezekana

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Bado kuna mamia ya miili chini ya majengo yaliyoporomoka huko Derna na mingine imeletwa na maji hadi kwenye fuo za umbali wa maili 60, na mamlaka za afya za Libya zinafuatilia hatari ya magonjwa.

    Lakini "dhana kwamba maiti zitasababisha magonjwa ya mlipuko haijathibitishwa", anasema Pierre Guyomarch, mkuu wa kitengo cha uchunguzi wa mahakama cha Msalaba Mwekundu.

    "Miili ya watu ambao wamekufa kufuatia majeraha katika janga la asili au vita karibu kamwe haileti hatari ya kiafya kwa jamii.

    "Wale wanaoponea tukio kama janga la asili wana mkubwa wa kueneza magonjwa kuliko maiti."

    Miili iliyo karibu au iliyo kwenye maji inaweza kusababisha hatari za kiafya, hata hivyo, kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni, na ndivyo wengine wana wasiwasi juu ya Derna, ingawa hali halisi bado haijajulikana.

  9. Kiongozi wa RSF wa Sudan atishia kuunda serikali yake

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Hemedti analishutumu jeshi kwa kuongoza mpango unaolenga kuigawanya Sudan

    Kamanda wa Kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) ametishia kuunda serikali yake, Khartoum ikiwa mji mkuu wake ikiwa jeshi litaanzisha utawala katika mji wa mashariki wa Port Sudan.

    Katika ujumbe kwenye mtandao wa X (zamani ukifahamika kama Twitter), Luteni Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo, anayejulikana pia kama Hemedti, alisema RSF imeonyesha "uvumilivu mkubwa kuhusiana na maamuzi ya kibinafsi ya al-Burhan licha ya kwamba sio halali", akimaanisha mkuu wa jeshi Luteni Jenerali Abdel Fattah al- Burhan.

    "Hatutaruhusu mtu yeyote kuzungumza kwa niaba ya Sudan na kudai halali kwake kufanya hivyo," aliongeza kiongozi huyo wa RSF.

    Tishio la kiongozi huyo wa RSF lilifuatia ripoti za vyombo vya habari vya serikali kwamba serikali inayoongozwa na jeshi ina mpango wa kujenga ikulu ya rais na makao makuu ya wizara yake ya mambo ya nje katika bandari ya Sudan kwenye jimbo la Bahari Nyekundu.

    Jiji hilo limekuwa likitumika kama kituo cha uendeshaji wa serikali tangu mzozo mbaya ulipozuka kati ya jeshi la kawaida na RSF mjini Khartoum katikati ya mwezi Aprili.

    Pia unaweza kusoma:

    • Mzozo wa Sudan: 'Niliona miili ikitupwa kwenye kaburi la pamoja Darfur'
  10. Wanadiplomasia wa Marekani nchini Urusi watakiwa kuondoka mara moja - kunani?

    Rais Putin

    Chanzo cha picha, EPA

    Wanadiplomasia wa Ubalozi wa Marekani nchini Urusi, Jeffrey Sillin na David Bernstein, wametangazwa kuwa watu wasiofaa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi ilisema.

    Sillin na Bernstein wanatakiwa kuondoka Urusi ndani ya siku saba. Kulingana na Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi, Sillin na Bernstein "walifanya shughuli haramu" na kudumisha mawasiliano na mfanyakazi wa zamani wa Ubalozi Mkuu wa Marekani huko Vladivostok, Robert Shonov, ambaye FSB ilimshtaki kwa kukusanya habari kuhusu vitendo vya wanajeshi wa Urusi huko Ukraine.

    Robert Shonov alifanya kazi katika Ubalozi wa Marekani huko Vladivostok kwa zaidi ya miaka 25 hadi Urusi ilipoamuru kufukuzwa kwa wafanyikazi wa misheni ya Marekani mnamo 2021.

    Unaweza kusoma;

  11. Taiwan yamwambia Elon Musk kuwa 'haiuzwi'

    Musk

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Taiwan imemwambia bilionea Elon Musk "haiuzwi" baada ya kusema kuwa kisiwa hicho ni sehemu ya China.

    "Sikiliza, Taiwan si sehemu ya PRC [Jamhuri ya Watu wa Uchina] na hakika haiuzwi!," waziri wa mambo ya nje Joseph Wu alisema kwenye ukurasa wa mtandao wa X wa Bw.Musk.

    Katika mkutano wa kilele wa biashara wiki hii, Bw Musk alilinganisha Taiwan na Hawaii, akiiita "sehemu muhimu" ya China.

    Beijing imedai Taiwan inayojitawala yenyewe na mivutano kati ya pande hizo mbili imeongezeka katika kipindi cha mwaka uliopita.

    Wiki hii tu, China ilifanya mazoezi ya anga na majini kuzunguka Taiwan, katika kile ambacho kimekuwa onesho la kawaida la nguvu za kijeshi kuzunguka kisiwa hicho.

    Taiwan ilisema kuwa imegundua zaidi ya ndege 40 za kijeshi za China na takribani meli 10 kwenye maji yake.

    Hii si mara ya kwanza kwa Bw Musk, ambaye ana maslahi ya kibiashara nchini China, kukasirisha serikali ya Taiwan kwa maoni yake.

    Mnamo Oktoba, alisema kuwa mvutano kati ya Beijing na Taipei unaweza kutatuliwa kwa kuipa China udhibiti fulani juu ya Taiwan.

    Alisema kisha katika mahojiano na Financial Times kwamba anaamini kuwa serikali hizo mbili zinaweza kufikia hatua "inayopendeza". Balozi wa China nchini Marekani alimsifu Bw Musk lakini mwenzake wa Taiwan alisema kitu sawa na Bw Wu - kwamba uhuru "hauuzwi".

    Unaweza kusoma;

  12. UN yataka msaada zaidi wa matibabu maeneo yaliyoathirika zaidi Libya

    Derma

    Chanzo cha picha, EPA

    Shirika la Afya Duniani (WHO) limeiambia BBC kwamba vifaa vya matibabu vinahitajika haraka katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na jiji lililoathiriwa zaidi la Derna na "itahitajika kuongezeka haraka sana".

    Rick Brennan, mkurugenzi wa masuala ya dharura wa WHO katika eneo la Mashariki ya Mediterania linalojumuisha Libya, alisema vituo vingi vya afya vimekuwa havifanyi kazi vizuri hata kabla ya kimbunga hicho.

    "Sehemu kubwa ya vituo hivyo vya afya tayari vilikuwa haba, na wafanyakazi duni," alisema. WHO, alisema, ilikuwa katika nafasi ya kuongoza juhudi za ushirikiano za mashirika mengine ya misaada lakini hilo linacheleweshwa kwa sababu ya serikali mbili za Libya za magharibi na mashariki.

    Kulikuwa na masuala ya kupata kibali kutoka kwa serikali ili kupata misaada ya kwenda inapohitajika, alibainisha.

    "Suala la kushughulikia mapema kwa changamoto yoyote kubwa kama hii hufanywa na jumuiya ya ndani ... lakini sisi ... jumuiya ya kimataifa, tunahitaji kuja nyuma yao na kutoa msaada kwa kiwango ambacho kinalingana na mahitaji haya makubwa, " alisema.

    Unaweza kusoma;

  13. Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kuendelea na vikwazo vya nyuklia kwa Iran

    Muonekano wa ndege zisizo na rubani wakati wa mazoezi ya kijeshi katika eneo lisilojulikana nchini Iran

    Chanzo cha picha, Reuters

    Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimetangaza kuendelea kuiwekea Iran vikwazo katika jaribio la kuizuia nchi hiyo kuiuzia Urusi ndege zisizo na rubani na makombora.

    Mnamo mwaka wa 2015 Iran ilikubali makubaliano ya nyuklia na, chini ya masharti, vikwazo vingine vinapaswa kuondolewa mwezi ujao.

    Lakini mataifa ya Ulaya yanaamini Iran ilikiuka makubaliano hayo kwa kurutubisha na kuhifadhi madini ya uranium.

    Iran inasema hatua yao ni "haramu na ya uchochezi". Ikirutubishwa sana, uranium inaweza kutumika kutengeneza silaha ya nyuklia.

    Mataifa ya Ulaya yalitangaza kwamba yatajumuisha vikwazo vya Umoja wa Mataifa vilivyokwisha muda wake katika sheria zao.

    Baadhi ya hatua hizo zinatakiwa kuzuia Iran kutengeneza na kusafirisha nje makombora na ndege zisizo na rubani.

    Lakini licha ya vikwazo hivyo, ndege nyingi zisizo na rubani zinazotengenezwa nchini Iran zimetumiwa na Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine.

    Iran ilikubali makubaliano hayo, yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Utekelezaji wa Pamoja (JCPOA), na kundi la madola yenye nguvu duniani yanayojulikana kama P5+1 - Marekani, Uingereza, Ufaransa, China, Urusi na Ujerumani -miaka minane iliyopita.

    Chini ya makubaliano hayo, Iran ilikubali kupunguza shughuli zake nyeti za nyuklia na kuruhusu wakaguzi wa kimataifa kama malipo ya kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi.

    Makubaliano hayo yanazuia mtu yeyote kununua, kuuza au kuhamisha ndege zisizo na rubani na makombora kwenda na kutoka Iran.

  14. Kanda ya video ya CCTV yaonesha jinsi wafanyakazi wa Uwanja wa ndege wanavyoibia abiria mabegi yao Marekani

    Maelezo ya video, Tazama : Kanda ya video ya CCTV ikionesha jinsi wafanyakazi wa Uwanja wa ndege wanavyoibia abiria mabegi yao

    Picha za uchunguzi zinaonyesha maafisa wawili wa Usalama wa Uchukuzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami huko Florida wakidaiwa kuchukua pesa kutoka kwa mifuko kwenye kituo cha ukaguzi cha usalama.

    Maafisa hao walikamatwa mwezi Julai na wanakabiliwa na mashtaka ya wizi.

    Wamekana mashtaka hayo.

  15. Mauaji ya Sara Sharif: Baba yake ni kati ya watu 3 walioshtakiwa kwa mauaji ya msichana

    .

    Chanzo cha picha, Handout

    Maelezo ya picha, Sara Sharif alikuwa amepata "majeraha mengi na makubwa", uchunguzi wa maiti ulifichua

    Baba, mama wa kambo na mjomba wa Sara Sharif wameshtakiwa kwa mauaji ya msichana wa miaka 10, Polisi wa Surrey wamesema.Urfan Sharif, 41, mpenzi wake Beinash Batool, 29, na kakake Urfan, Faisal Malik, 28, wote kutoka Hammond Road, Woking, wamefunguliwa mashtaka.

    Pia kila mmoja ameshtakiwa kwa kusababisha au kuruhusu kifo cha mtoto.

    Mwili wa Sara ulipatikana nyumbani kwao tarehe 10 Agosti.Uchunguzi wa baada ya maiti uligundua alikuwa amepata "majeraha mengi na makubwa".

    Watu wazima watatu waliondoka Uingereza kwenda Pakistan tarehe 9 Agosti.Walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Gatwick Jumatano jioni baada ya kushuka kutoka Dubai.

    Mapema Ijumaa asubuhi, Polisi wa Surrey walithibitisha kuwa wamefunguliwa mashtaka.Wamerejeshwa rumande ili kufika katika Mahakama ya Guildford baadaye siku ya Ijumaa.

    .

    Chanzo cha picha, SURREY POLICE

    Maelezo ya picha, Urfan Sharif, Binash Batool na Faisal Malik
  16. Bei ya mafuta yapanda na kupita kiwango cha ksh 200 kwa lita Kenya

    Gharama za mafuta

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Gharama ya mafuta imepita rekodi ya kiasi cha sh 200 kwa mara ya kwanza katika Historia ya Kenya, huku bei ikiwa imepanda kwa sh 20 kwa kila lita.

    Ongezeko la bei ya mafuta itawaathiri watumiaji hasa kwenye gharama za chakula na kila bidhaa.

    Serikali iliweka ruzuku ili kudhibiti kupanda kwa bei hiyo tarehe 15 Septemba mpaka tarehe 14 Oktoba.

    Bei ya Petroli, Dizeli na mafuta ya taa yalipanda kwa sh 16.96, 33.13, mtawalia na kuuzwa kwa sh 211.64, 200.9 na 202.61 jijini Nairobi.

    Ongezeko hili kubwa litakuwa na athari kubwa kwa mtumiaji ambaye tayari ana maumivu ya ongezeko la kodi na mazingira magumu ya kiuchumi.

    Unaweza kusoma;

  17. 'Tukio lisilofikirika': Walionusurika waelezea mafuriko ya Libya

    Athari za mafuriko

    Chanzo cha picha, Reuters

    Ishara ya kwanza ya kuwa kuna kitu kibaya ilikuwa sauti ya mbwa wakibweka.

    Ilikuwa 2.30 asubuhi na giza nje. Wakati Husam Abdelgawi, mhasibu mwenye umri wa miaka 31 katika mji wa Derna, mashariki mwa Libya, alipoinuka na kwenda akiwa na usingizi, alihisi maji chini ya miguu yake.

    Husam alifungua mlango wa mbele wa nyumba aliyoishi pamoja na mdogo wake, Ibrahim. Maji zaidi yalifurika, yakivuta mlango kutoka kwenye bawaba zake.

    Ndugu walikimbilia mlango wa nyuma, ambapo walikutana na "tukio la kutisha, lisilofikirika, baya zaidi kuliko kifo chenyewe kushuhudia", Husam alisema, katika mahojiano ya simu kutoka mji wa Al-Qubbah.

    "Miili ya wanawake na watoto ilikuwa ikielea nyuma yetu. Magari na nyumba zote zilinaswa kwenye mkondo. Baadhi ya miili ilisombwa na maji hadi ndani ya nyumba yetu."

    Maji yaliwafagia Husam na Ibrahim juu pia, yakiwapeleka mbali zaidi na kwa kasi kuliko walivyofikiria. Ndani ya sekunde chache, walikuwa wametengana kwa mita 150.

    Ibrahim, mwenye umri wa miaka 28, alifaulu kushika nyaya za umeme zinazoelea ambazo bado zimefungwa kwenye nguzo zao na kujibana nyuma kuelekea pale ambapo Husam alikuwa amekwama.

    Wanandugu walitumia nyaya kama kamba kujivuta kuelekea kwenye jengo lililo karibu na kupitia dirisha la orofa ya tatu, na kutoka hapo wakafika kwenye paa la orofa ya tano ambapo walingoja mafuriko yapite.

    Unaweza kusoma;

  18. Habari, karibu katika taarifa za moja kwa moja