Waasi waanzisha mashambulizi mapya DR Congo
Waasi wa M23 wamefanya mashambulizi katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Moja kwa moja
Waasi waanzisha mashambulizi mapya DR Congo

Chanzo cha picha, AFP
Waasi wa M23 wamefanya mashambulizi katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Wanashambulia vijiji vitano nje ya mji wa Mweso, ambao uko kwenye barabara kuu ya jimbo hilo. Vyombo vya habari vya ndani vinasema mashambulizi hayo yalifuatia kuwasili kwa wanajeshi wa Rwanda.
Kigali, hata hivyo, inakanusha kuwa inaunga mkono waasi.
M23 inadhibiti eneo ndani ya Congo, lakini kasi yake kuelekea Goma, mji mkuu, imepungua katika siku za hivi karibuni.
Majaribio ya hivi majuzi ya kutekeleza usitishaji mapigano yameshindwa.
Unaweza kusoma;
Muuguzi aliye mafunzo akamatwa kwa tuhuma za jaribio la kuwabaka wagonjwa Uganda

Polisi wa Uganda wamemkamata muuguzi aliye mafunzo kwa njia ya vitendo kwa tuhuma za ubakaji na jaribio la ubakaji kwa wagonjwa wawili wajawazito katika hospitali ya Entebbe Grade B, kituo cha serikali kilicho umbali wa kilomita 40 kutoka mji mkuu wa Kampala.
Naibu Msemaji wa Polisi wa Jiji la Kampala, Luke Owoyesigire alisema mshukiwa, Kutesa Denis alikamatwa Jumamosi tarehe 18 Februari na kwa sasa anazuiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Entebbe.
Kutesa anadaiwa kuwatambua waathiriwa wake kutoka wodi ya magonjwa ya Wanawake na kuwawekea dawa kwa kutumia dawa inayoshukiwa kuwa chloroform kabla ya kuwanyanyasa kingono.
Klorofomu inayoshukiwa ilipatikana kutoka kwa makazi ya Kutesa baada ya upekuzi vile vile barua ambayo inadaiwa aliandika akiomba kuombewa juu ya mawazo machafu aliyokuwa nayo.
Polisi wanasema kunaweza kuwa na waathiriwa zaidi na wanawaomba watu kujitokeza.
Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk Peterson Kyebambe aliiambia BBC kwamba tukio hilo sasa limeongeza tahadhari na ufahamu wa hospitali hiyo ili kuimarisha usimamizi wa wafanyakazi na kufunga kamera zaidi za CCTV.
Naibu wa Rais akosolewa kwa kuashiria Kenya kama kampuni,

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Naibu Rais Rigathi Gachagua (Kulia) alikosolewa siku za nyuma kutokana na matamshi yake. Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua amekosolewa na kuashiria nchi hiyo kama kampuni yenye hisa ambayo kwanza itawanufaisha waliopigia kura serikali.
Bw Gachagua alitetea uteuzi wa hivi majuzi wa serikali akisema waliomuunga mkono na Rais William Ruto walistahili "kuvuna kwanza".
“Serikali hii ni kama kampuni iliyodhaminiwa na hisa. Wapo wamiliki wa kampuni, wapo wenye hisa nyingi, wenye hisa chache na wasio na hisa. " Kama uliwekeza serikalini na sasa ni wakati wako wa kuvuna," alisema.
“Wapo wanaonilaumu kwa kusema hivi lakini ni makosa? Hata wale wakosoaji na wale ambao hawakutuunga mkono watavuna, lakini watalazimika kusubiri kilichobaki ili watu wajue wanapopiga kura, inamaanisha kitu na ina matokeo.
Kauli hiyo ilizua gumzo kali miongoni wa Wakenya katika mitandao kijamii huku wanaopinga wakisema serikali inafaa kuwahudumia Wakenya wote bila kujali misimamo yao ya kisias.
Wengine waliongeza kuwa wananchi wote wanastahili uangalizi sawa kutoka kwa serikali, ikiwa ni pamoja na linapokuja suala la miradi ya maendeleo.
Soma:
- Cheche za maneno kati ya Rais William Ruto na Raila zinaashiria nini?
- Je Rais William Ruto atafanikiwa kumnyamazisha Raila Odinga?
- Je, Raila Odinga anataka nini haswa?
Watoto 12 wapoteza maisha kutokana na ugonjwa wa surua Tanzania,

Chanzo cha picha, Getty Images
Watoto 12 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na surua katika wilaya ya Mlele mkoani Katavi kusini magharibi mwa Tanzania .
Kati ya kipindi cha mwezi wa 12 mwaka jana hadi kufikia mwezi wa pili mwaka huu watoto 847 wameambukizwa surua kwenye wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Mlele Majid Mwanga ameiambia BBC hadi sasa wamefanikiwa kutoa chanjo kwa watoto 16480 na wanaendelea na zoezi hilo .
Pamoja na kutoa elimu wakiwataka wananchi wa eneo hilo kuachana na imani potofu kuwa vifo hivyo vimetokana na imani za kishirikina na badala yake wasikilize na kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya pamoja na kuwapelekea watoto kupata chanjo .
Ugonjwa wa surua huathiri watu wa rika zote japokuwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ndio huathiriwa zaidi na dalili zake ni homa kali, udhaifu wa mwili pamoja na upele.
Miezi mitano iliyopita Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alitangaza mlipiko wa ugonjwa wa surua nchini Tanzania na kuanza kampeni ya utoaji chanjo ya surua na rubela kwa watoto walio chini ya miaka mitano nchi nzima.
Katika picha: Ziara ya kihistoria ya Biden nchini Ukraine
Rais wa Marekani Joe Biden sasa ameondoka Kyiv baada ya kufanya ziara ambayo haikutangazwa na kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.
Kiongozi huyo wa Marekani alikariri kujitolea kwa nchi yake kusaidia Ukraine, na kuahidi silaha zaidi kwa taifa hilo na kuahidi kutangaza vikwazo vipya dhidi ya Urusi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Rais Biden alisisitiza dhamira ya Marekani ya kuiunga mkono Ukraine 
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Ziara ya Biden ilisifiwa na Rais Zelensky kama hatua muhimu sana katika vita vya Ukraine 
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Biden alisimulia usiku ambao alizungumza na Zelensky wakati Urusi ilipovamia nchi hiyo mwaka jana Kusini mwa Afrika yajiandaa kukabiliana na Kimbunga Freddy,

Chanzo cha picha, AFP
Kimbunga Freddy kimedhoofika katika saa chache zilizopita, lakini kinaendelea kukaribia Mauritius "kwa hatari" na kuwa "tishio la moja kwa moja kwa kisiwa hicho", ofisi ya hali ya hewa ya eneo hilo imeripoti. Bahari hiyo inatarajiwa kujaa hadi takriban mita saba zaidi ya miamba. Takriban watu 400 wanaishi katika mji mkuu, Port Louis.
Eneo la kusini mwa Afrika linajiandaa kukabiliana na Kimbunga Freddy ambacho kinatarajiwa kupiga nchini Madagaska siku ya Jumatatu na watu milioni mbili katika njia yake, kulingana na UN.
Nchini Msumbiji, Rais Filipe Nyusi alirejea nyumbani mapema kutoka kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika kwani dhoruba inaweza kuikumba nchi yake mwishoni mwa juma.
Madagascar imeonya juu ya madhara yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa, upepo mkali na mawimbi ya dhoruba. Ripoti zinaonesha kuwa kimbunga hicho kinaweza kuathiri mataifa ya pwani kutoka Tanzania hadi Afrika Kusini.
Safari za ndege za kuingia na kutoka nchi jirani ya Mauritius zimeahirishwa. Zimbabwe nayo imejiandaa kukabiliana na maafa.
Mapema mwaka jana nchi za kusini mwa Afrika zilikumbwa na dhoruba sita kali ambazo ziliua takriban watu 890.
Jinsi safari ya Biden kwenda Ukraine ilivyofanywa kisiri

Chanzo cha picha, Getty Images
Safari ya siri ya Biden kwenda Ukraine ilifanywa kupitia treni kutoka mpaka wa Poland, gazeti la New York Times linaripoti.
Ziara ya Kyiv ilifanywa kisiri kwa sababu ya tahadhari ya kiusalama.
Ripoti pia zinasema kwamba Biden aliondoka Washington bila taarifa baada ya yeye na mkewe Jill kula chakula cha jioni kwenye mkahawa Jumamosi usiku.
Maafisa walikuwa wamekanusha kuwa Biden angezuru Ukraine wakati wa safari yake ya kuelekea Ulaya mashariki.
Gazeti la The New York Times linasema: "Hakika, Ikulu ya Marekani Jumapili usiku ilitoa ratiba ya hadharani Jumatatu ikimuonyesha rais bado yuko Washington na kuondoka jioni kuelekea Warsaw, wakati alikuwa tayari ameanza safari."

Chanzo cha picha, EPA
Kabla ya mkutano na waandishi wa habari, Joe Biden alifanya mazungumzo na Volodymyr Zelensky na kusema kwamba "anatazamia kujadili ulimwengu" pamoja naye.
Pia aliwasifu raia wa Ukraine kwa mapigano yao ya "kishujaa" - licha ya ukosefu wa uzoefu wa kijeshi. Alisema: "Tena cha kustaajabisha ni kwamba watu wa Ukraine ni raia wa kawaida, wachapakazi, ambao hawakuwahi kupata mafunzo ya kijeshi, lakini jinsi walivyopiga hatua ya kishujaa ni jambo ambalo na ulimwengu wote unajivunia."
Habari za hivi punde, Biden afanya ziara ya kushtukiza mjini Kyiv kabla ya maadhimisho ya vita vya Ukraine

Chanzo cha picha, Telegram
Rais wa Marekani Joe Biden amewasili Kyiv - ziara yake ya kwanza nchini Ukraine tangu Urusi ilipovamia karibu mwaka mmoja uliopita.
Ziara hiyo ya kushtukiza imekuja wakati alipokuwa akisafiri kwenda nchi jirani ya Poland kukutana na Rais Andrzej Duda.
Dakika chache Rais wa Ukraine Zelensky ameshirikiaha picha kwenye akaunti yake rasmi ya Telegram akipeana mkono na rais wa Marekani.
Kulikuwa na uvumi mapema leo kwamba mgeni muhimu alikuwa akiwasili katika mji mkuu wa Ukraine, ambao mwanasiasa wa Ukraine Lesia Vasylenko amethibitisha kuwa Biden.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Zaidi ya watu 30 wamekufa katika dhoruba baya pwani ya Brazil

Mamlaka ya Brazil jimbo la São Paulo imesema watu wapatao 36 wamekufa katika mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi,tukio ambalo lilipelekea baadhi ya miji kufuta sherehe za kila mwaka za Carnival.
Video zinaonesha jinsi baadhi ya maeneo na barabara zilivyoharibika na maji.
Vikosi vya uokoaji vimekuwa vikijitahidi kuwafikia walionusurika na kufungua barabara ambazo zilijaa vifusi.
Zaidi ya milimita 600 (inchi 23.6) za mvua zilinyesha katika baadhi ya maeneo siku ya Jumapili, mara mbili ya kiwango kilichotarajiwa kwa mwezi huo.
"Timu za uokoaji zinashindwa kufika sehemu kadhaa; kutokana na hali kuwa mbaya," alisema Felipe Augusto, meya wa mji ulioathirika sana wa São Sebastião.
"Bado hatujajua ukubwa wa uharibifu. Tunajaribu kuwaokoa waathiriwa.
" Makumi ya watu walipotea katika mji huo na takriban nyumba 50 zilibomoka na kusombwa na maji, Bw Augusto aliongeza, akisema kuwa hali ilibaki kuwa "mbaya sana".
Serikali ya jimbo hilo iliripoti vifo 35 huko São Sebastião na meya wa Ubatuba, baadhi ya kilomita 80 (maili 50) kaskazini-mashariki, alisema msichana mdogo ameuawa.
Mamia wamekimbia makazi yao na wengine kuhamishwa katika makazi yao.
"Ni tukio baya, tutakuwa na vifo vingi zaidi," afisa wa ulinzi wa raia aliliambia gazeti la Folha de São Paulo.
Wakati huohuo, maafisa wanasema watu wengine 228 wameachwa bila makazi, huku wengine 338 wakihamishwa kutoka maeneo ya pwani kaskazini mwa São Paulo.
Mtoto wa Mugabe akamatwa kwa kuharibu mali - polisi

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Robert Mugabe (kushoto) akiwa na mtoto wake (kulia) Polisi nchini Zimbabwe wamethibitisha kukamatwa kwa mtoto wa kiume wa marehemu Rais Robert Mugabe kwa "uharibifu mbaya wa mali".
Katika ujumbe wa Twitter, polisi walisema kukamatwa huko kulifuatia malalamiko kwamba Robert Mugabe Junior alidaiwa kuharibu mali ya thamani ya $12,000 (£10,000) katika nyumba moja iliyopo kitongoji cha mji mkuu, Harare.
Malalamiko dhidi ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 31 yalitolewa na rafiki yake, Nkatazo Sindiso.
ZimLive imetuma kwenye mtandao wa twitter video yake akiwasili katika mahakama ya hakimu mjini Harare ili, inasema, kukabiliwa na mashtaka ya kuharibu magari na mali nyingine wakati wa tafrija ya wikendi.
Mugabe Junior ni mtoto wa pili wa marehemu Mugabe na mjane wake, Grace.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Nyota wa muziki wa Nigeria watumbuiza kwenye tamasha la NBA All-Stars

Chanzo cha picha, AFP
Wasanii watatu wakubwa wa muziki nchini Nigeria siku ya Jumapili walitumbuiza wakati wa mapumziko ya NBA All-Stars 2023, ambayo ni moja ya hafla kubwa zaidi za kimichezo nchini Marekani.
Burna Boy, Rema na Tems walitumbuiza kwa zamu maonyesho ya Afrobeat kwenye kipindi cha mapumziko.
Burna Boy alitumbuiza katika tamasha hilo kwa kuipa vibao vyake kali vikiwemo Anybody, It’s Plenty, Last Last na Alone.

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Rema alifuatia kwa kupiga nyimbo zake Calm Down na Holiday. 
Chanzo cha picha, Getty Images
Soma:
Umoja wa Afrika umesisitiza 'kutovumilia' mapinduzi

Chanzo cha picha, AFP
Umoja wa Afrika umesisitiza msimamo wake wa kutovumilia mabadiliko ya utawala wa kidemokrasia katika bara hilo.
Katika siku ya mwisho ya mkutano wa AU uliofanyika mjini Addis Ababa, Umoja huo ulisema utaendelea kuzisimamishwa kwa Burkina Faso, Guinea, Mali na Sudan - ambazo zote zinatawaliwa na viongozi wa kijeshi kufuatia mapinduzi.
Kamishna wa masuala ya kisiasa, Bankole Adeoye, alisema AU iko tayari kusaidia nchi hizo kurejea katika utaratibu wa kikatiba na kusaidia demokrasia kuota mizizi.
Viongozi katika mkutano huo pia walikubali kuendelea na mipango ya mpango wa biashara huria ikiwa ni pamoja na karibu kila nchi barani Afrika.
Soma zaidi:
- Kwanini Urusi inashangilia mapinduzi ya Burkina Faso
- Mapinduzi ya Sudan:Jeshi la Sudan lavunja serikali ya kiraia na kuwakamata viongozi
Naibu mkuu wa utawala kijeshi wa Sudan ayaita mapinduzi ya 2021 kuwa 'makosa'

Chanzo cha picha, AFP
Naibu mkuu wa baraza tawala la Sudan, Mohamed Daglo, amesema mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2021 yalikuwa "makosa".
Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni, Bw Daglo alisema imetoa mwanya kwa utawala wa zamani wa Omar al-Bashir, ambaye aliondolewa madarakani miaka miwili kabla.
Alisema alikosea kutoa msaada katika mapinduzi ya hivi karibuni ni mojawapo ya makosa hayo.
Mpango wa Disemba wa kuibadilisha Sudan kuwa na utawala wa kiraia, Bw Daglo aliahidi kutekeleza mageuzi ya usalama, ikiwa ni pamoja na kuunganisha kundi lake la kijeshi la RSF katika jeshi la taifa.
Sudan imekuwa katika msukosuko wa kiuchumi na kisiasa tangu mwaka 2021, wakati Jenerali Abdel Fattah al-Burhan alipopinduliwa na kuchukua madaraka kutoka kwa serikali ya mpito inayoongozwa kiraia na hivyo kuharibu mpito kwa utawala wa kiraia kufuatia kuondolewa kwa Bashir 2019.
Wanaharakati wanaounga mkono demokrasia wamekuwa wakiandaa maandamano dhidi ya mamlaka ya kijeshi tangu wakati huo
Soma zaidi:
- Mapinduzi ya Sudan: Waandamanaji wauawa na makumi wengine kujeruhiwa
- Viongozi Sudan wakamatwa, huku kukiwa na ripoti za mapinduzi ya Kijeshi
Habari za hivi punde, Waandamanaji nchini Moldova waitaka Urusi iwaokoe

Chanzo cha picha, EPA
Chini ya jengo la bunge la Moldova, gwaride linapita polepole - likiwa na watu elfu moja kutoka kote nchini, kila mmoja akiwa na hadithi yake ya kibinafsi ya umaskini na kufadhaika.
"Sisi ni kicheko - serikali inatudhihaki," wengine wanalia.
Akiwa amevalia kofia ya buluu, Ala anasogeza uso wake mpana uliopauka karibu na wangu, na kusema: "Kuna watu walio na watoto wanne au watano ambao hawana chochote cha kula."
Bili za nishati hapa sasa zinatumia zaidi ya 70% ya mapato ya kaya, kulingana na rais wa Moldova.
Ala ananiambia wanameza nusu ya pensheni yake.
"Tulipochagua serikali hii, waliahidi kuongeza mishahara na pensheni, lakini hadi sasa hatujaona hata senti," anasema.
Maandamano ya Jumapili, yaliyoandaliwa na chama cha Sor cha Moldova kinachounga mkono Urusi, yanafuatiliwa kwa karibu na serikali kote Ulaya na kwingineko. Waandamanaji wengi walisafiri hadi mji mkuu wa Chisinau kwa basi, na gharama zao ziliripotiwa kulipwa na chama cha Sor.
Siku chache kabla ya mkutano huo kufanyika, Rais Maia Sandu alionya kwamba Urusi inapanga njama ya kutuma wahujumu waliofunzwa kijeshi nchini humo, waliojigeuza kuwa raia, ili kuipindua serikali yake inayounga mkono Magharibi.
Urusi imesema kuwa shutuma hizo ni jaribio la mamlaka ya Moldova kutaka kuvuruga tahadhari kutokana na kushindwa kwao kijamii na kiuchumi..
Soma zaidi:
- Urusi yawafukuza wanadiplomasia wa Moldova
- Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter kupata huduma ya mwisho wa uhai

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter atasitisha matibabu yake hospitalini na kuanza kuhudumiwa nyumbani kwake Georgia, taasisi yake ilitangaza Jumamosi.
Kituo cha Carter kilisema Bw Carter ameamua "kutumia wakati wake uliobaki nyumbani na familia yake," lakini hakusema ni nini kilichosababisha uamuzi huo.
Bw Carter mwenye umri wa miaka 98, amekumbwa na matatizo ya hivi karibuni ya kiafya, ikiwa ni pamoja na melanoma ambayo ilisambaa kwenye ini na ubongo wake.
Kiongozi huyo mkongwe zaidi nchini Marekani, alihudumu kwa muhula mmoja madarakani kuanzia 1977-81.
Wakati wa uongozi wake kama rais, Bw Carter alikabiliwa na changamoto nyingi za sera za kigeni na chama cha Democrat kilishindwa kuchaguliwa tena na Ronald Reagan kuchukua wadhfa huo.
"Kwa sasa anaangaliwa kwa karibu na familia yake pamoja na timu yake ya matibabu.
Familia ya Carter inaomba faragha kwa wakati huu na inashukuru salamu za kheri zinazotumwa na watu wengi wanaompenda," Kituo cha Carter kilisema katika taarifa yake Jumamosi.
Wagonjwa walio katika hali mbaya ya karibu na kifo wanaweza kuomba huduma ya matibabu wakiwa nyumbani.
Kipaumbele si kutoa matibabu zaidi, bali kutoa faraja kuelekea mwisho wa maisha ya mgonjwa.
Mjukuu wa Bw Carter, Jason Carter, seneta wa zamani wa jimbo la Georgia, alituma ujumbe kwenye Twitter kwamba aliwatembelea "babu na babu zangu wote wawili jana." "Wana amani na kama kawaida nyumba yao imejaa upendo.
Asanteni wote kwa maneno yenu mazuri," alisema. Mnamo 2021, Bw Carter na mkewe Roslyn waliposherehekea kumbukumbu ya miaka 75 ya ndoa yao. Wana watoto wanne pamoja.
Katika ujumbe wa tweeter siku ya Jumapili, Rais wa Marekani Joe Biden aliandika kwamba yeye na mkewe, Jill Biden, walikuwa wakiwaombea "rafiki zao Jimmy na Rosalynn".
"Tunawapongeza kwa nguvu na unyenyekevu ambao mmeonyesha katika wakati mgumu," Bw Biden aliandika.
"Uendelee na safari yako kwa neema na heshima, na Mungu akupe amani."
Soma zaidi:
- Jimmy Carter: Nitaenda Korea Kaskazini kwa niaba ya Trump
- Jimmy Carter asema ana kansa
Mwili wa mchezaji soka Christian Atsu umerejeshwa Ghana

Chanzo cha picha, Reuters
Mwili wa mwanasoka Christian Atsu, aliyefariki katika tetemeko la ardhi lililotokea Uturuki wiki mbili zilizopita, umerudishwa nchini kwao Ghana.
Ndege iliyobeba mwili wa marehemu ilitua mjini Accra Jumapili jioni, na jeneza lake lilibebwa na wanajeshi wa Ghana.
Atsu alikutwa amefariki siku ya Jumamosi chini ya nyumba yake kusini mwa Uturuki.
Alikuwa akiichezea klabu ya Hatayspor.
Winga huyo aliichezea timu ya taifa ya Ghana mara 65 na kuisaidia timu yake kufika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2015.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 pia alichezea timu za Premier League Everton na Newcastle.
Akizungumza katika uwanja wa ndege wa Kotoka katika mji mkuu wa Accra, Makamu wa Rais wa Ghana Mahamudu Bawmia alisema:
"Tulikuwa na matumaini dhidi ya matumaini, kila siku iliyopita, tulisali na kuomba.
Lakini alipopatikana akiwa amefariki." Bw Bawmia aliongeza kuwa mwanasoka huyo alipendwa sana na atakumbukwa sana. "Ni maumivu makali mno kumpoteza." Na kuahidi kuwa Atsu atapewa mazishi "ya heshima".
Soma zaidi:
- Je, tutaweza kutabiri matetemeko ya ardhi?
- Mpenzi wa Christian Atsu atoa wito wa vifaa vya kusaidia uokoaji
Rais wa Ukraine asema Macron anapoteza muda kudhani kutakuwa na mazungumzo na Urusi

Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy alisema katika mahojiano yaliyochapishwa Jumapili kwamba kiongozi wa Ufaransa Emmanuel Macron alikuwa akipoteza wakati wake kwa kuzingatia aina yoyote ya mazungumzo na Urusi.
Zelenskiy, alihojiwa na gazeti la kila siku la Italia Corriere della Sera, alikuwa akijibu maoni ya Macron kwamba Urusi inapaswa "ishindwe lakini sio kwa kukosolewa" na kwamba mzozo wa Ukraine utalazimika kutatuliwa kwa mazungumzo.
"Hakutakuwa na maana ya kuwa na mazungumzo. Kiukweli Macron anapoteza muda wake. Nimefikia mwisho kuona kwamba hatuwezi kubadilisha mtazamo wa Urusi," Zelenskiy aliliambia gazeti la kila siku la Italia.
"Kama wameamua kujitenga wenyewe katika ndoto ya kujenga upya himaya ya zamani ya Sovieti, hatuwezi kufanya lolote kuhusu hilo. Ni juu yao kuchagua au kutoshirikiana na jumuiya ya mataifa kwa misingi ya kuheshimiana."
Alikataa pendekezo lolote kwamba ni vikwazo vya Magharibi vilivyomfanya Rais wa Urusi Vladimir Putin kutengwa. "
Badala yake ni uamuzi wa kuanzisha vita ambavyo vilimweka pembeni Putin," alinukuliwa akisema.
Siku ya Ijumaa, Macron aliwataka washirika kuongeza msaada wa kijeshi kwa Ukraine.
Pia alisema katika mahojiano na Jarida la du Dimanche haamini katika mabadiliko ya utawala, kwamba kulikuwa na nafasi ndogo ya suluhisho la kidemokrasia kutoka ndani ya mashirika ya kiraia ya Urusi na hakuna njia mbadala ya kumrudisha Putin kwenye meza ya mazungumzo.
Soma zaidi:
- Urusi lazima ishindwe lakini ‘isisambaratishwe’ asema Macron
Hujambo na karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya ukurasa wa BBC Swahili leo ikiwa tarehe 20.02.2023
