Türkiye : Nchi tano zilizobadilisha majina yake na ni kwanini

Madaxweyne Erdogan

Chanzo cha picha, Adem Altan

Maelezo ya picha, Rais Erdogan anataka nchi yake iitwe Türkiye

Uturuki inataka dunia iite Türkiye. Umoja wa Matifa ulitangaza wiki iliyopita kwamba inaweza kubadili jina la na kuwa Türkiye.

Rais Recep Tayyip Erdoğan amesema kuwa jina jipya la nchi hiyo "litaonyesha taswira halisi ya utamaduni , ustaarabu na maadili a nchi yake."

Baadhi wanadai kwamba mabadiliko ya jina la nchi hiyo yametokana na dhana kwamba jina la nchi linapaswa kutokanganywa na jina la ndege Kware ambaye huitwa Turkey

Katika lugha ya Kiturkey, jina la nchi ni Türkiye. Wakati nchi hiyo ilipopata uhuru wake kutoka kwa mamlaka za Magharibi katika mwaka 1923, nchi hiyo iliitwa Turkey.

Turkey

Chanzo cha picha, Meleagris gallopavo

Maelezo ya picha, Ndege anayefahamika kama Turkey

Kuna nchi nyingine ambazo zimebadilisha majina. Baadhi zilifanya hivyo kwasababu za kisiasa, huku nyingine zikifanya hivyo kwa misingi ya historia iliyopita.

Eswatini

Mwezi Aprili, 2018, Mfalme Mswati III alibadilisha jina la nchi , kutoka Swaziland, na kuwa Eswatini, katika juhudi za kuondoa jina kikoloni.

Pia inasemekana kwamba mfalme huyo alikasirishwa na namna watu wanavyokanganya jina la nchi yake na Switzerland.

Tangazo hilo la jina jipya lilitolewa wakati nchi hiyo ilipokuwa ikiadhimisha miaka 50 ya nchi hiyo.

Eswatini, lilikuw ani jina la nchi hiyo kabla halijatawaliwa na wakoloni , likimaanisha "ardhi ya Swaziz".

North Macedonia

Katika mwaka 2019,. Jamuhuri ya Macedonia ilibadili rasmi jina lake na kuwa Northern Republic of Macedonia. Sababu za kuchukua uamuzi huo zikuwa ni za kisiasa.

Nchi hiyo ilitaka kuboresha uhusiano wake na Ugiriki, kwani ilitaka kujiunga na Muungano wa Ulaya pamoja na Jumiya ya kujihami ya kujihami ya nchi za Magharibi NATO.

Ugiriki ililalamika kuhusu jina la nchi ya Macedonia, kwani kuna jimbo la Ugiriki lenye jina linalofanana na hilo na kwamba kulikuwa na Himaya ya Ugiriki inayoitwa Macedonia.

Mzozo baina yan chi mbili ulifikia kiwango cha kusababisha kuyumba kwa usalama katika kanda hiyo.

Serikali ya Athens ilitaka nchi hiyo iachane na jina la Wamacedonia kabisa na kuipatia jina nchi yao " Vardar Republic" (Jamuhuri ya Vardar )au "Skopje Republic" (Jamuhuri ya Skopje).

Baada ya mazungumzo mare, ilikubaliwa kuwa nchi hiyo ibadilishe jina na kuitwa Northern Republic of Macedonia(Jamuhuri ya Kaskazini ya Macedonia)

The Netherlands ( Uholanzi)

Serikali ya Amsterdam imebadilisja jina lake na kuitwa Holland. Tangu mwaka 2020, viongozi wa kibiashara, watalii na mashirika ya kiserikali wamekuwa wakiita nchi hiyo Netherlands.

Nchi hiyo kwa sasa ina nchi mbili, North Holland (Holland Kaskazini) na South Holland (Holland Kusini).

Sababu ya ya kubadilishwa kwa jina la nchi inasemekana kuwa ni azma yake ya kujitenga na mihadarati na ukahaba katika mji mkuu , Amsterdam, uliokithiri katika eneo la North Holland (Holland kaskazini)

Czechia

Czech Republic( Jamuhuri ya Czech) imebadilisha jina lake kwa ajili ya sababu za kjitangaza. Mnamo mwaka 2016, Serikali ya Czech ilibadilisha rasmi jina lake na kuwa Czechia kuifanya kuwa ya kimataifa zaidi.

Maafisa wanasema jina jipya ni rahisi zaidi kuliko Czech Republic (Jamuhuri ya Czech na linaweza kutangazwa kwenye bidhaa kwemnye bidhaa za nchi hiyo zinazouzwa nje.

Ingawa Muungano wa Ulaya, Umoja wa Mataifa na badhi ya mashirika yanaiita nchi Czechia, bado jina hili halijafahamika katika maenepo mengine ya dunia.

Sababu ya kubadili jina hili inasema kwa sehemu moja ni kwamba Czechia inaweza kufananishwa kimakosa na Chechnya, ambalo ni jimbo la Urusi.

Katika mwaka 2020, Waziri mkuu wa Czechia Andrej Babis aliliambia jarida la Wall Street kwamba hakupenda jina Czech.

Soma taarifa zaidi kuihusu Türkiye Uturuki: