Herlinda Bobadilla: Je mwanamke huyu mkuu wa genge la mihadarati la Montes Bobadilla aliyekamatwa Honduras ni nani?

Ni kama athari kubwa: mara baada ya mmoja kukamatwa, baadhi ya wahusika wakuu katika biashara ya dawa za kulevya nchini Honduras wameanza kunaswa mmoja baada ya mwingine.

Wa kwanza Juan Antonio Hernández, ambaye 2020 alipatikana na makosa ya ulanguzi wa dawa na silaha.

Tony, kama anavyofahamika kwa jina la utani, alikuwa kaka wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo ya Amerika ya kati wakati huo.

Hata hivyo Juan Orlando Hernández, ambaye alikamatwa mapema mwaka huu akituhumiwa kwa uhalifu huo huo na kusafirishwa Marekani.

Na Jumapili hii, picha za kukamatwa kwa Herlinda Bobadilla, maarufu La Chinda, ambaye serikali ya Marekani ilitangaza zawadi ya dola milioni tano kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwake.

Bobadilla anasadikiwa kwa kiongozi wa kundi la Montes Bobadilla, linalotuhumiwa kudhibiti eneo la Caribbean la Hundurus, ambako kupitia uhusiano wao na magenge ya ulanguzi wa dawa za kulevya nchini Colombia na Mexico, waliweza kusafirisha maelfu ya kilo za cocaine kwenda Marekani.

Mmoja wa wanawe wa kiume, Tito Montes, alifariki katika oparesheni, huku mwingine, Juan Carlos, akifanikiwa kutoroka kutoka mikononi mwa maafisa wa usalama na bado anasakwa.

Lakini picha ya Herlinda - mwenye umri wa miaka 61 akiwa amevikwa pingu na kusafirishwa kwa helikopta kutoka eneo la Colón, alikokamatwa, hadi mji mkuu wa Tegucigalpa - iliibua maswali kuhusu utambulisho wake.

"Ukweli ni kwamba uwepo wa wanawake katika magenge ya ulanguzi wa dawa za kulevya ni jambo la kawaida kuliko inavyodhaniwa, kinachofanyika ni kwamba hawaonekani kutokana na usiri unaozunguka ulimwengu wa biashara ya dawa za kulevya" Deborah Bonello, mtaalamu anayeangazia wanawake katika ulimwengu wa uhalifu na mhariri Amerika Kusini wa Vice World News, laielezea BBC Mundo.

"Wengi wanatarajia kuona 'Chapa' wanapozungumza kuhusu wanawake ambao ni walanguzi wa dawa, wakati ki uhalisia wanashikilia nyadhifa zilizo na malka makubwa, lakini kimya kimya," aliongeza.

Lakini "la Chinda" nani na aliweza vipi kuwa kiongozi mwenye ushawishi mkubwa katika magenge makubwa ya walanguzi wa dawa za kulevya Amerika ya Kati?

Familia ya kipekee

Genge la Montes Bobadilla lina kizazi chake nchini Colombia, na ina ufungamano na genge maarufu la Cali ambalo sasa limetokomea.

Pedro García Montes, raia wa Honduras anayesimamia malipo na biashara zingine, aliwafanyia kazi. Wakati akiendeleza kazi hiyo, alianza kubuni eneo la kupakia na kupakua dawa za kulevya na kuifanya Caribbean zone ya nchi yake.

Kadri muda ulivyosonga, biashara hiyo ilienddelea kukua. Mwaka 2004, García Montes aliuawa huko Cartagena na udhibiti wa oparesheni ya Honduras ulichukuliwa na jamaa zake, Alex Adán Montes Bobadilla.

Ili kumsaidia kuimararisha nafasi yake ndani ya genge hilo, Alex Adán aliamua kuwajumuisha jamaa yake anayemuamini: Herlinda Bobadilla.

Manamke aliyezaliwa mnamo Oktoba 1961 katika mji wa Macuelizo, karibu kilomita 290 kutoka Tegucigalpa, lakini aliishi na familia yake katika eneo la Colón kaskazini, ambako shughuli za genge hilo zilikuwa zikiendeshwa.

Kulingana na mamlaka za Honduras, Herlinda aliolewa na Alejandro Montes Alvarenga na kujaaliwa na watoto sita. Watatu kati yao -Alejandro (maarufu Tito), José Carlos na Noé- walifanya kazi kikamilifu katika kundi hilo la kihalifu.

Herlinda naye alihusika pakubwa katika oparesheni za ndani za kundi hilo katika eneo la Colón.

Mmamlaka nchini Honduras, Herlinda Bobadilla anamiliki makumi ya nyumba katika manispaa ya Limón, eneo lenye ushawishi mkubwa wa kundi hilo.

Mtandao wa habari wa Insight Crime umethibitisha kuwa eneo hilo la Honduras ni muhimu kimkakati katika usafirishaji wa dawa za kulevya zinazoletwa na magenge yaAmerika Kusini, hasa kutoka Colombia, na kupeleka Guatemala, ambako inachukuliwa na magenge ya Mexico na hatimaye kuepelekwa Marekani.

Mwaka 2014 usimamizi wa kundi hilo ulifanyiwa mabadiliko kufuatia kifo Alex Adán akiwa gerezani. Huko alichukua nafasi ya Noé Montes Bobadilla, mwana wa kiume wa tatu wa Herlinda, lakini alikamatwa mwaka 2017 nakupelekwa Marekani kufunguliwa mashataka miaka miwili baadaye.

Huu ndio wakati, kulingana na mamlaka nchini Marekani, yeye na wanawe wakiume Tito na José Carlos, walichukua uongozi wa kundi hilo. Si hilo tu: saliongeza shughuli za usafirishaji na hata, akulingana na nyaraka za serikali ya Honduras, alijihusishwa na ukuzaji wa mmea wa coca ili kuanzisha biashara yake mwenyewe.

"Uongozi wake katika genge la ulanguzi wa dawa za kulevya la Montes ulikuwa kwa kwango kikubwa tangu mwaka 2017 hadi alipokamatwa 2019 na kupelekwa Marekani ambako mwana wa tatu wa Herlinda son, Noé Montes Bobadilla, alikuwa akisakwa," taarifa ya mwezi Mei ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema kuwa nchi hiyo imetoa zawadi ya dola milioni tano kwa yeyete atakayetoa taarifa itakayosaidia kukamatwa kila mmoja wa viongozi hao watatu.

Upanuzi na mateso

Ijapokuwa Noé alikamatwa na kupelekwa Marekani kufunguliwa mashtaka, na Herlinda Bobadilla (ambaye pia anafahamika kama Erlinda Montes Bobadilla au La Chinda) kupandishwa cheo katika kundi hilo, ukweli ni kwamba serikali ya Marekani tayari ilikuwa inamchunguza.

Mwaka 2015, mahakama ya Marekani katika jimbo la Virginia ilimfungulia mashataka yeye na wanawe kwa usafirishaji wa cocaine na uhalifu mwingine unaohusiana na mihadarati.

Ni hapo ambapo kundi hilo lilianza kulengwa. Mwaka 2017, Noé alikamatwa mchakato wa kutaifisha mali ya Herlinda Bobadilla nchini Honduras ilianza.

Karibu nyumba 40, zilizopo hususan katika mkoa wa Colón, zilichukuliwa na serikali ya Honduras.

Lakini hatua kubwa dhidi ya kundi hilo ilichukuliwa wakati zawadi ya dola milioni tano za Kimarekani zilipotolewa kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa kila mmoja wa wa jamaa wa familia hiyo, akiwemo Herlinda, Mei 2.

Ua lilianza kuporomoka weekendi hii kufuatia oparesheni kali iliofanywa na kikosi maalumu cha Honduras kuwanasa wanawe wawili wa kiume wa Herlinda wanoafahamika kama Tito na José Carlos.

Kulingana na ripoti ya maafisa, Tito alifariki katika makabiliano na vikosi maalum, huku José Carlos akifanikiwa kutoroka.

Mamlaka hatimaye ilimkamata mama yao, kumvisha pingu na kumpeleka Tegucigalpa, ambako atafunguliwa mashtaka ya ulanguzi wa mihadarati, ufisadi na utakatishaji fedha.

Bi Herlinda pia anasubiri kupelekwa Marekani, ambako mwanawe Noé anahudumia kifungo cha miaka 39.

Tangu mwaka 2014, Honduras imewapeleka takriban raia wake 31, ikiwa ni pamoja na watu kundi la Montes Bobadilla na Mkurugenzi wa zamani wa Polisi wa Kitaifa Juan Carlos Bonilla, ambaye alipelekwa Marekani wiki iliyopita kufunguliwa mashataka kwa tuhuma za kupokea rushw na kuruhusu uingizaji wa dawa za kulevya nchini humo.