Kombe la Dunia 2022: Mechi za Afrika zatarajiwa kushika kasi katika hatua za mchujo

Kombe la dunia

Chanzo cha picha, Getty Images

Safari ndefu ya Afrika kuelekea Kombe la Dunia mwaka 2022 itaamuliwa wakati nafasi zake tano nchini Qatar zitakapoamuliwa ndani ya siku tano zijazo.

Mataifa kumi yanashiriki katika mechi za mchujo za mpira wa soka, huku ikijitokeza kwamba jinsi mechi zingine zilivyopangwa ni kali mno.

Chini ya wiki saba tangu kumenyana katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Misri na Senegal zinakutana tena - safari hii kuwania kufuzu Qatar.

Sadio Mane alimshinda mchezaji mwenzake wa Liverpool, Mohamed Salah kunyakua taji la Afrika, na mmoja wa washambuliaji hao nyota sasa atakosa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa baadaye mwaka huu.

Mechi za kwanza zote tano zitachezwa Machi 25, na za marudiano siku nne baadaye.

Kwa mara ya kwanza, mechi za mchujo za Kombe la Dunia za Afrika zitakuwa na teknolojia ya video kusaidia marefa yaani (VAR).

Egypt v Senegal

Sadio Mane and Mohamed Salah

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ama Sadio Mane au Mohamed Salah atakosa kushiriki Kombe la Dunia la 2022

Mataifa yote mawili yalikuwepo kwenye Kombe la Dunia lililopita lakini hakuna iliyoweza kufuzu hatua ya makundi nchini Urusi.

Senegal inawania kucheza fainali kwa mara ya tatu huku Misri ikiwinda kwa mara ya nne katika michuano ya kimataifa, na ya pili mfululizo kwa mara ya kwanza.

Aliou Cisse amewabakisha wachezaji wengi walioisaidia Senegal kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza wakati 'Teranga Lions' ikipania kufuzu mfululizo kwa Kombe la Dunia baada ya kukosekana kwa miaka 16 iliyomalizika 2018.

Kocha wa Pharaohs Carlos Queiroz amesema hakuna nafasi ya pole au kesho kupitia akaunti yake ya twitter.

Misri watakuwa wenyeji wa mkondo wa kwanza, huku mchujo mpya wa Senegal uliozinduliwa Stade du Senegal ukiwa na mchezo wa marudiano Jumanne.

Ghana v Nigeria

Ghana coach Otto Addo and Nigeria coach Augustine Eguavoen

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ghana ilimteua Otto Addo (kushoto) baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika, huku Nigeria ikisalia na Augustine Eguavoen.

Mataifa hayo mawili ya Afrika Magharibi makubwa yatapambana kuelekea Qatar, huku sare yao ikiendelea kukumbukwa kutokana na ushindani wao.

Nigeria, ambao waliamua kumbakisha Augustine Eguavoen baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika, wanawinda kwa mara ya nne mfululizo Kombe la Dunia, huku Ghana wakitafuta kurejea baada ya kukosa michuano ya Urusi 2018.

Otto Addo aliteuliwa kuwa kocha wa muda baada ya Black Stars wakishika mkia katika kundi lao la Kombe la Mataifa ya Afrika, huku kocha wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza Chris Hughton akitajwa kuwa mkurugenzi wa ufundi, baada ya Milovan Rajevac kutimuliwa.

Ghana imekuwa timu ya tatu tu ya Afrika kutinga robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka wa 2010, ikifungwa na Uruguay kwa mikwaju ya penalti, na inalenga kupata nafasi ya kushiriki kwa mara ya nne kwenye michuano hiyo.

Cameroon v Algeria

Cameroon coach Rigobert Song and Algeria coach Djamel Belmadi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rigobert Song (kushoto) aliteuliwa hivi karibuni kuwa kocha wa Cameroon huku Djamel Belmadi akiwa ameiongoza Algeria tangu 2018.

Nchi zote mbili hazijafuzu tangu Brazil mwaka 2014 na zinatarajia kurejea baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa sababu tofauti.

Cameroon, wakiwa na kocha mpya Rigobert Song, walilazimika kumaliza katika nafasi ya tatu nyumbani na wanawania kufuzu kwa Kombe lao la nane la Kombe la Dunia - ikiwa ni mara nyingi zaidi kuliko taifa lolote la Afrika.

Utetezi wa Algeria wa taji lao la Kombe la Mataifa ya mwaka 2019 ulionekana kuwa mbaya, huku Desert Foxes wakifunga bao moja tu walipomaliza bila ushindi na mkiani mwa kundi lao.

Kocha Djamel Belmadi, ambaye alichukua usukani Agosti 2018, alikuwa amecheza mechi 35 bila kushindwa lakini alishangaza wengi pale alipopoteza rekodi hiyo dhidi ya Equatorial Guinea.

Mali v Tunisia

Mali's Abdoulaye Doucoure and Tunisia's Taha Yassine Khenissi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Abdoulaye Doucoure (kushoto) anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza nchini Mali huku Yassine Khenissi akirejeaTunisia baada ya kufungiwa kwa kutumia dawa za kulevya.

Mali ndiyo timu pekee kwenye raundi ya mchujo ambayo bado haijacheza fainali za Kombe la Dunia, na The Eagles wanaingia baada ya kutoka sare dhidi ya Tunisia wakiwa ndani ya hatua ya timu 16 bora kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika.

Pande hizo mbili zilikutana katika hatua ya makundi nchini Cameroon, huku wenyeji hao wa Afrika Magharibi wakishinda 1-0, lakini mechi hiyo ilizidiwa na mwamuzi wa Zambia, Janny Sikazwe aliyepuliza kipenga cha mwisho mapema baada ya kukumbwa na joto kali.

Tunisia ilimtimua kocha Mondher Kebaier kufuatia kuondolewa katika robo fainali, huku msaidizi wake Jalel Kadri akipewa jukumu la kusimamia michezo hizi miwili.

Wenyeji hao wa Afrika Kaskazini wanapania kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia mfululizo, baada ya kutolewa katika hatua ya makundi nchini Urusi miaka minne iliyopita.

DR Congo v Morocco

Morocco coach Vahid Halilhodzic and DR Congo coach Hector Cuper

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kocha wa Morocco, Vahid Halilhodzic na Kocha wa DR Congo, Hector Cuper wakutana

Baada ya kutolewa kwa hatua ya makundi kwenye Kombe la Dunia 2018, iliyojumuisha kipigo dhidi ya Iran na Ureno na kutoka sare na Uhispania, Morocco iko makini kurejea katika Kombe la Dunia na kuweka ahidi yao nchini Urusi.

Wachezaji hao wa Afrika Kaskazini wanatazamia kupata nafasi yao ya sita kwenye michuano hiyo, huku kufuzu kwao 2018 kukihitimisha miaka 20 ya kukosekana kwao kwenye hatua hiyo kubwa zaidi.

Atlas Lions ilitolewa katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika na Misri mapema mwaka huu, lakini wapinzani wao waliotinga Qatar hawakufanikiwa kuona lango kwa Cameroon.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imecheza Kombe la Dunia mara moja tu hapo awali, na kutolewa kwao pekee kunawadia kama vile Zaire mwaka 1974 walipopoteza michezo yote mitatu ya makundi.

Leopards ndio timu iliyo katika nafasi ya chini zaidi katika mchujo, ikishika nafasi ya 66 duniani, na mwenyeji wa mechi ya kwanza mjini Kinshasa siku ya Ijumaa.