Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Zifahamu faida za kulala 'kiduchu' mchana
Sio rahisi kuwa na nguvu wakati wote kwa siku nzima, kutokana urefu wa siku yenyewe na hekaheka za skila siku, iwe ni lazima au hiari.
Ingekuwa vizuri kama na sisi tungekuwa kama kompyuta ambayo inaweza kujiongezea nguvu katikati ya siku kwa kubonyeza tu kitufe fulani, kujizima kuanza tena na kuwa na uwezo wa kuendelea kufanya kazi tena.
Kwa binadamu kuna kitufe pia ya aina hii, au angalau yenye utaratibu ambao unaweza kufanya ya aina hiyo (ya kompyuta), nacho ni usingizi mfupi.
Kulingana na kuongezeka kwa ushahidi wa kisayansi, usingizi kidogo, au kinachojulikana kama 'nap', ni kitu cha thamani ambacho kinaweza kurejesha kiasi sawa cha nguvu na uwepo wa akili ambao tunakuwa nao tunapoianza siku.
"Faida kuu ya usingizi kidogo ni kwamba inondoa athari za kisaikolojia zinazotokea baada ya kuamka" inaanzia wakati tunapoamka vizuri "kuongezeka kwa 'adenosine' kemikali inayopatikana katika ubongo ambayo husababishwa na metaboliki," anasema mwanasikolojia ya kulala, na mwanzilishi mwenza wa shule ya kulala huko London.
"Unapokaa macho muda mrefu, ndivyo kemikali ya 'adenosine' inavyozidi kujilimbikiza katika ubongo wako, ndivyo utakavyohisi usingizi zaidi," anaongeza. Lakini tunapolala usingizi wa muda mfupi au tunapolala kidogo, inapunguza kiasi cha adenosine na kupitia mfumo metaboliki, husaidia kuongeza viwango vya nguvu zetu na hufanya tujisikie kuchangamka na kuwa kwenye kumbukumbu nzuri.
"inasaidia kuboresha hisia zetu na kutufanya mwili kuchangamka;
Faida anayoizungumza huyu inatokana na usingizi mfupi wa dakika kati ya 10 hadi 20.
Sarah Madanik, mtafiti wa usingizi na mwandishi wa chapisho la "make a short sleep! Anasema "badilisha maisha yako, ikiwa unatafuta kuboresha kumbukumbu, ubunifu, kuimarisha mtazamo au akili, utahitaji kulala muda mrefu kiasi wa hadi dakika 90.
Madanik, mtafiti ambaye amekuwa akifanya utafiti wa madhara ya usingizi kwa zaidi ya miaka 20, anasema kwamba usingizi 'kiduchu' wa muda kati ya dakika 60 na 90, unatuingiza katika hatua ya usingizi mzito, yaani aina hiyo ya usingizi ni sawa na wa usiku na kwa hiyo kipindi hiki cha kulala nusu siku mchana kina faida sawa na usingizi wa usiku.
Jizoeshe kulala angalau 'kiduchu' mchana
Inawezekana ikawa ngumu kwa kila mtu kulala kwa lisaa limoja na nusu katikati ya siku, kama ni ngumu kwako basi ni bora kuzingatia kulala usingizi wa muda mfupi. Kwa nchi kama Hispania na kidogo Ugiriki, kulala mchana ni sehemu ya utamaduni wao na hilo linaonekana hata kwenye mikataba ya masaa ya kazi huzingatia muda wa kulala kidogo mchana.
Kulala usingizi mfupi ni kama kuogelea au kuendesha baiskeli: ujuzi ambayo unahitaji mazoezi lakini hilo linawezekana katika muda mfupi bila hata kufanya juhudi kubwa.
"Kama unataka kujifunza kulala kwa muda mfupi, kwanza tenga muda wako unaotaka kulala na kengele ya kukukumbusha (alarm) kuhakikisha unalala. Ikiwa unafanya mazoezi ya kulala kwa wakati fulani kila siku, mwili wako utazoea kulala kwa wakati maalumu. Inachukua miezi mitatu kuzoea usingizi huu mfupi."
Usijilazimishe kulala. Usingizwi huu mfupi haulazimishwi, hujengwa kwa mazoea. Jilaze kitandani ama kwenye kiti kazini ama popote unapoweza kujiegeza kidogo. Inashauriwa usishike na kushughulika na simu yako ama kopmyuta kutazama barua pepe angalau dakika 5 kabla ya kualala. Pia kuwa na pumzi za taratibu na kunywa maji kiasi kabla ya kuamua kulala usingizi huu 'mfupi' .
Kulala bila kutambua
Watu wengine wanasema kwamba kwa sababu hawawezi kulala kwa urahisi, haiwezekani kwao kulala angalau kwa dakika ya 15 katikati ya siku, lakini inaelewa, mara nyingi wakati mwingine tunalala bila kutambua.
"Wale ambao walikuwa wamelala usingizi mwepesi bila kujijua wakiwa katika hatua ya kwanza ukiwaamisha na kuwauliza kama walikuwa wamelala, asilimia 65 walisema walikuwa macho muda wote wakati ukweli hawakuwa macho. Inaonyesha kwamba hatuwezi kujielewa kama tunalala," anasema Madanik
Faida nyingine ya kulala ni kwamba tunafunga macho yetu kwa dakika 10 hadi 20. Kulala kwa muda mfupi ni muhimu kwa wale ambao hawajapata shida za usingizi kabla na kwa wale walio na matatizo ya usingizi, lakini ikiwa hatuhisi msongo wa mawazo na upweke baada ya kuamka, hatupaswi kuongeza muda wa kulala usingizi mfupi.
Ushauri mwingine unaotolewa ni angalau kunywa kikombe kimoja cha kahawa kabla ya kulala kwa sababu athari za 'caffeine' ndani ya kahawa huanza kujitokeza dakika 20 baada ya kunywa kahawa yenywe, yaani, wakati ambao pengine tutaamka kutoka usingizi mfupi.
Lakini kwa mujibu wa Sara Mendik, ushauri huu anauona sio wazo nzuri.