Tetesi za soka Ulaya 16.02.2022 Jumatano: Ronaldo, Savio, Ndidi, Bissouma, Bowen, Broja, Kounde

Mshambuliaji wa Manchester United na Ureno Cristiano Ronaldo, 37, anavivutia vilabu vya Paris St-Germain, Bayern Munich na Roma wakati huu akitafakari kama atimke Old Trafford msimu huu. (Sun)

Manchester City imetenga ofa ya £5.5m kwa ajili ya winga wa Atletico Mineiro, Savio. Kinda huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 17, anasakwa pia na Arsenal. (Guardian)

Aston Villa ilo tayari kutumia £50m kununua kiungo huku viungo walioko kwenye orodha ya juu kusakwa ni kiungo wa kimataifa wa Nigeria na Leicester Wilfred Ndidi, 25, na kiungo wa Brighton na Mali Yves Bissouma, 25. (Star)

West Ham wanapanga kuzungumza na kiungo Jarrod Bowen, 25, mwishoni mwa msimu kuhusu mkataba mpya ili kuzuia kusajiliwa na Liverpool wanaomsaka. (Evening Standard)

Bayern Munich na Borussia Dortmund ni vilabu vya hivi karibuni vinavyomfuatilia are mshambuliaji wa Chelsea na Albania Armando Broja, 20, ambaye anacheza kwa mkopo Southampton. (Sun)

Manchester United, Liverpool, Chelsea, Arsenal na Newcastle zinamfuatilia kinachoendelea kuhusu mkataba wa Kalvin Phillips pale Leeds. Mkataba wa kiungo huyo wa England mwenye umri wa miaka 26 unamalizika mwaka 2024. (90min)

Chelsea imejikita kumsajili mlinzi wa Ufaransa Jules Kounde, 23, kutoka Sevilla baada ya kutaarifiwa kuwa Paris St-Germain haitamuuza beki wake wa kati Marquinhos, 27. (Fabrizio Romano)

Kiungo wa Leicester Mbelgiji Youri Tielemans, 24, ametakiwa kukacha kuhamia vilabu vya Liverpool na Manchester United ili kujiunga na Chelsea, kwa mujibu wa kiungo wa zamani wa United na Brazil Kleberson. (Express)

Liverpool iko kwenye mazungumzo na kiungo wa zamani wa England James Milner, 36, kuhusu kumuongezea mkataba wa mwaka 1. (Fabrizio Romano)

Leicester City na Southampton zinamuwania kiungo mfaransa wa Bristol City Han-Noah Massengo, 20. (Football Insider)

Mlinzi wa zamani wa West Ham na Chelsea Glen Johnson anasema the Blues wanapaswa kumsajili nyota wa England Declan Rice, 23, kutoka West Ham kuziba nafasi ya kiungo wa kimataifa wa Italia Jorginho,30. (Mail)

West Ham iko kwenye mazungumzo na nahodha wake Mark Noble ili kiungo huyo muingereza, 34, achukue moja ya nafasi za juu za utendaju mwishoni mwa msimu. (Mail)

Aston Villa otasikiliza ofa msimu huu kwa ajili ya winga wake kutoka Burkina Faso Bertrand Traore, 26, ambaye ana mkataba unaokwenda mpaka mwaka 2024. (Football Insider)

Pep Guardiola anafikiria kumpa nafasi kiungo wa Brazil midfielder Fernandinho, 36, kuwa sehemu ya benchi la ufundi la Manchester City msimu ujao. (Sun)

Kiungo wa zamani wa Vissel Kobe mhispania Andres Iniesta, 37, hana tatizo kurejea Barcelona kama mchezaji, kama fursa hiyo itakuwepo. (Goal)