Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini: Kombora kubwa zaidi lafyatuliwa tangu 2017
Korea Kaskazini imefyatua kile kinachodhaniwa kuwa ni kombora kubwa zaidi kuwahi kufyatuliwa tangu mwaka 2017.
Korea Kaskazini iliripoti kwamba ufyatuaji huo ulifanyika saa moja na dakika 55 asubuhi kwa saa za eneo au saa nne na dakika 52 kwa saa za Afrika Mashariki, tukio ambalo lilifanyika kwenye mwambao wa Korea Kaskazini.
Japan, Korea Kusini na Marekani kwa pamoja zimelaani ufyatuaji huo, likiwa ni jaribio la saba lililotekelezwa mwezi huu.
Umoja wa Mataifa umeizuwia Korea Kaskazini kufanya majaribio ya makombora ya ballistic na silaha za nyuklia na umeiwekea vikwazo.
Lakini taifa hilo la Mashariki mwa Asia mara nyingi hukiuka marufuku hiyo, na kiongozi wake Kin Jong-un ameapa kuimarisha ulinzi wa nchi yake.
Baraza la usalama la taifa la Korea Kusini limesea kuwa jaribio la Jumapili lilikuwa ni la kombora la masafa ya kati, aina ya ballistic (IRBM), ambalo litakuwa ndilo kombora kubwa zaidi kuwahi kufanyiwa majaribio, tangu Novemba 2017.
Maafisa wa Japan na Korea Kusini wanakadiria kuwa kombora hilo lilifika umbali wa kilomita 2,000 (au maili 1240 ) na lilipaa kwa dakika 30 kwa umbali wa kilomita 800 (au maili 500 ). Lilitua katika Bahari ya Japan.
Marekani imeitolea wito Korea Kaskazini "kujizuwia kufanya vitendo zaidi vya kuyumbisha usalama".
Januari ulikuwa moja ya miezi yenye shuguli nyingi zaidi katika rekodi ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini, ambapo makombora kadhaa ya masafa ya kati yalifyatuliwa ndani ya bahari.
Rais wa Korea Kusini , Moon Jae-in, alisema wingi wa majaribio ya makombora unakumbusha wasi wasi mkubwa uliooongezeka katika mwaka 2017, wakati Korea Kaskazini ilipofanya majaribio ya nyuklia na kufyatua makombora yake makubwa ya masafa, ikiwa ni pamoja na baadhi yake yaliyopaa juu ya Japan.
Kulingana na shirika la habari la Korea Kusini- Yonhap, kombora hilo linaonekana kuwa saw ana kombora la Hwasong-12 ambalo Korea Kaskazini lililifanyia majaribio katika mwaka 2017.
Mwaka 2018, Bw Kim alitangaza kusitishwa kwa majaribio ya silaha za nyuklia na makombora yake ya masafa marefu yenye uwezo wa kupiga kwenye bara lingine ya aina ya ballistic (au ICBMs).
Lakini kiongozi wa Korea Kaskazini mwaka 2019 kwamba hafungwi na usitishaji huo.
Marekani iliiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini mapema mwezi Januari, kujibu ufyatuaji wake wa awali wa makombora. Mazungumzo baina ya nchi mbili yamekwamba tangu rais wa Marekani Joe Biden achukue mamlaka.
Unaweza pia kusoma:
Makombora yaliyofanyiwa majaribio mapema mwezi huu yalionyesha kuwa Korea Kaskazini ilikuwa inatengeneza teknolojia ambayo inaweza kuishinda mifumo ya ghali na migumu ya ulinzi ambayo Marekani na Japan imekuwa ikiipeleka kote katika kanda hiyo.
Kamanda wa zamani wa vikosi vya majini wa Korea Kaskazini Profesa Kim Dong Yup alisema: "Wanataka kuwa na mifumo ya kuzuwia ambayo iko sawa na mkia wa wa nge."
"Lengu kuu la Korea Kaskazini sio kushambuliwa bali ni kujilinda wenyewe ," anasema Profesa Kim, na kuongeza kuwa nchi inajaribu "kupata uwezo wa aina mbali mbali wa kujikinga".