Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Urusi :Kesi ya uhalifu yafunguliwa kuhusiana na upigaji picha za nusu uchi karibu na msikiti wa Moscow Ijumaa
Kamati ya uchunguzi ya Urusi sasa imefungua kesi ya uhalifu chini ya sheria hiyo. Washukiwa wanasemekana kuchunguzwa. Dini ya Kiislamu ni dini ya pili kwa ukubwa zaidi nchini Urusi.
Kwanini tukio la upigaji picha limeibua mtafaruku?
Video ya msichana aliyekuwa amevalia barakoa nyeusi, koti refu, na nguo za ndani aliyekuwa akipigwa picha mbele ya msikiti unaofahamika kama Msikiti wa Ijumaa wa -Moscow Friday Mosque inasemekana ilipigwa siku ya Alhamisi. Video hiyo imekuwa ikisambaa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, huku wengi wakilaani kitendo hicho.
Video hiyo ilikuwa sababu ya kamati ya uchunguzi ya Urusi ya kufungua kesi ya uhalifu.
Kulingana na Kamati hiyo, "watu kadhaa mbele ya macho ya umma karibu na mtaa wa Vipolzov walitekeleza kitendo cha kuukosea umma heshima kwa lengo la kutusi hisia za Waislamu na waumini ."
Kitengo cha huduma za habari cha Wizara ya mambo ya ndani ya Urusi mjini Moscow pia kilishirikisha umma taarifa ya kamati hiyo.
Kulingana na huduma za habari, "wakati uchunguzi wake wa intaneti, polisi ilibaini video iambayo ilikuwa ya uchokozi wa kiroho.
Ilionyesha msichana aliyekuwa anapigwa picha nusu uchi mbele ya jingo la kidini .", ilisema taarifa hiyo.
Kamati ya uchunguzi ya Urusi inasema mshukiwa (aliyezaliwa mwaka 1981) atafikishwa mbele ya kitenge cha uchunguzi karibuni.
Imam wa Msikiti wa Moscow-Moscow's Grand Mosque, ambaye pia ni Mufti wa Moscow, Ildar Alyautdinov, alisema picha za aina hiyo mbele ya maeneo matakatifu zinaonyesha ukosefu wa maadili ya kijamii. Aliilezea video hiyo kama "kitendo kingine cha uchokozi ".
Kuwatusi watu wa dini ni kosa linaloadhibiwa nchini Urusi kwa faini ya hari robo to 300,000 au kifungo cha hadi mwaka mmoja nchini Urusi.
Kulingana na gazeti la Poster Daily, msichana huyo alikuwa akipigwa picha na mwanablogi Maria Katanova.
Katika mahojiano na gazeti hilo, mwanablogi huyo alisema kwammba "alipokuwa akipita karibu na msikiti ," aliwaona wasichana kadhaa wakipigwa picha pale.
Alisimama na akaomba kama anaweza kupigwa picha yake . "
Mwanablogi anasisitiza kuwa "hana nia ya kumtusi mtu yeyote na anapenda heshima na kuheshimiana kwa ujumla."
Visa vinavyoendelea wakati huu ? ...
Idadi ya kesi za aina hii zimekuwa zikiongezeka nchini Urusi katika miaka ya hivi karibuni. Kesi kama hizi zilitokea kuhusu picha zilizopigwa nje ya makanisa ya Wakristo.
Katika kila kesi, kesi ya uhalifu ilifunguliwa kwa kutusi hisia za waumini.
Baadhi ya wale waliopatikana na hatia katika kesi za aina hii waliripotiwa kufungwa kifungo cha miezi 10 gerezani.
Mwaka 2013, Kipengele 148 cha sheria ya uhalifu ya Urusi kilirekebishwa.
Uwajibikaji kwa ajili ya kutusi hisia za waumini umeimarishwa, na uwezekano wa kosa hili kuwa la jinai umeongezeka kwa kisa kama hiki.
Unaweza pia kusoma:
Kwa mujibu wa takwimu rasmi, kuna zaidi ya Waislamu milioni 20 nchini Urusi, Uislamu ni dini ya pili kwa ukubwa nchini Urusi.
Urusi ina idadi kubwa ya zaidi ya Waislamu kuliko taifa lingine lolote la Ulaya.