'Mfalme wa Khoisan' wa Afrika Kusini akamatwa kwa kupanda bangi katika ofisi ya rais

King Khoisan covered in cannabis being dragged away

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Familia ya Mfalme wa Khoisan imekasirika kutokana na kukamatwa kwake, vyobo vya habari nchini humo vimeripoti.

Polisi ya Afrika Kusini imeng'oa mimea kadhaa ya bangi iliyopandwa karibu na ofisiya Rais Cyril Ramaphosa mjini Pretoria.

Mimea hiyo ni mali ya wanaharakati kutoka jamii ya wazawa ya Khoisan, ambao baadhi yao wamekita kambi katika eneo hilo kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kiongozi wao, ambaye hujiita Mfalme wa Khoisan, alianguka ndani ya mmea wa bangi wakati polisi walipokuwa wakimburuza kumlazimisha atoke wamkamate na kumpeleka kituo cha polisi.

"Polisi ... mmetangaza vita?," shirika la habari la AFP lilimnukuu Mfalme wa Khoisan akipaza sauti akisema.

"Tumekuwa hapa kwa amani. Tunawajia," aliendelea. Baada ya matamshi hayo alikamatwa.

Yeye na baadhi ya wanaharakati waliokamatwa kwa "kuhusika na dagga (bangi), upandaji na uvunaji haramu wa bangi na kukataa kuvaa barakoa wanapokuwa katika maeneo ya umma wakati walipoamrishwa na afisa wa polisi kufanya hivyo," taarifa ya AFP ilisema.

King Khoisan shielding cannabis plants from police

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Jamii ya Khoisan ni wakazi wa zamani zaidi wa Afrika Kusini ,lakini mara kwa mara wamekuwa wakijipata nyuma kimaendeleo katika kanda nzima ya Kusini mwa Afrika.

Mnamo mwaka 2018, kikundi hicho kiliweka kambi yao katika eneo la bustani nje ya ofisi ya rais, karibu na sanamu kubwa ya Nelson Mandela, kufanya kampeni ya kutambuliwa rasmi kwa lugha yao.

Mke wa Mfalme wa Khoisan ameelezea kukasirishwa kwake na tukio hilo katika mahojiano na wavuti wa habari wa Afrika Kusini wa IOL.

Unaweza pia kusoma:

"Niko karibu sana, karibu sana ," Malkia Cynthia alisema. "Rais hataki kuja," kuzungumza nao, alisema. Aliuambia wavuti wa habari wa IOL kuwa watu wa jamii ya Khoisan wanataka tu kutambuliwa.

Watu wamekuwa wakitumia mimea ya bangi kwa sababu za kimatibabu, kama vile saratani na shinikizo la damu, aliendelea kusema. Bangi imekuwa ikipandwa katika bustani ya mboga.

Matumizi ya watu binafsi ya bangi katika maeneo ya kibinafsi yalikubalika kisheria katika nchini Afrika Kusini mwaka 2018.

Jamii ya Khoisan ni wakazi wa zamani zaidi wa Afrika kusini lakini sasa ni jamii yenye watu wachache zaidi nchini humo.

Bangi hutambuliwa kama "dagga" nchini Afrika Kusini

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Bangi hutambuliwa kama "dagga" nchini Afrika Kusini