Mchungaji Mick wa Burnley: ‘Nikifunga huu mlango, anakufa’

Kila baada ya sekunde saba - mtu mmoja anaelekezwa kwenda kupata usaidizi wa afya ya akili katika taasisi ya usimamizi wa matibabu nchini Uingereza mnamo Septemba.

Huko Burnley, hilo sio jambo la kushangaza kwa Mchungaji Mick - mfanyabiashara wa dawa za kulevya-aliyegeuka-mwokozi wa maisha wakati wa Covid - ambaye kila siku hukutana na watu wanaohangaika kuishi.

Makala hii inarejelea mara kadhaavisa vya kujiua.

Joanne alipigwa na butwa miezi 18 iliyopita wakati mpenzi wake, Robert, alipofariki ghafla.

"Nilihisi kana kwamba nimekosea, kwa sababu sikuweza kumsaidia kwa wakati unaofaa," anasema.

Hali ya afya ya akili ya Robert ilizorota wakati amri ya kwanza ya kutotoka nje ilipowekwa. Alishindwa kustahamili wazo la kufungiwa nyumbani kwa muda mrefu. Hali iliyomfanya aingiwe na mawazo ya kutaka kujitoa uhai.

Joanne anasema alipigia simu kundi linalojishughulisha na masuala ya afya ya akili chake kutafuta usaidizi wiki mbili kabla ya kifo - na aliambiwakuwa kuna mtu atampigia simu Robert siku iliyofuata. Lakini simu hiyo haikuwahi kupigwa.

Wiki mbili baadaye, Robert alijitoa uhai.

Ni Joan alipata mwili wa Robert.Baadaye siku hiyo, alipokea simu kutoka kwa maafisa wa afya ya akili ambao walikuwa wapige simu wiki mbili zilizopita.

"Waliuliza: 'Vipi naweza kusema Robert?'

"Nilimwambia, 'Hayupo tena… amejitoa uhai.'"

Joanne anasema afisa aliyekuwa kwenye simu upande wa pili aliomba msamaha na kusema walikuwa nashughuli nyingi. "Aliniambia pole sana na nasikitika hatuuwasiliana haraka kama tulivyoahidi.'"

Ijapokuwa Joanne hawalaumu wataalamu wa afya, anaamini Robert angeweza kuokolewa kwa usaidizi wa mapema. "Nadhani angehudumiwa mapema - bado angekuwa hapa."

Zaidi ya mwaka mmoja, Joanne bado anahangaishwa na kifo hicho. Kila neno huleta kumbukumbu zenye uchungu, lakini anataka kuzungumzia jinsi anavyohisi.

Kanisa la Church on the Street limekuwa mkombozi kwa Joanne. Anasema ni mahali ambapo yeye na familia yake wanapata faraja - na sio yeye pekee. Mamia ya wengine huja hapa kila juma wakitafuta tumaini.

Cha kusikitisha ni kuwa, Joanne ni mmoja tu wa waathiriwa ambao Mchungaji Mick anahudumia. Wakati Robert alipokufa, anasema, vijana wengine wawili walijiua katika mitaa iliyo karibu na nyumbani kwa Robert. Wakati huo, Mick alikuwa akipeana vifurushi vya chakula mara kwa mara katika maegesho ya magari huko Burnley.

"Sikuweza kuamini kilichokuwa kikifanyika. Nilihisi nahitajika kuchukuwa hatua licha ya kwamba sikuwa na uwezo kutokana na athari za kiuchumi zilizosababishwa na janga la Covid- 19."

Ndani ya Kanisa la Mick - tulifarijiwa kwa mwezi mmoja - sera ya kumpokea kila mtubila kumhukumu inasaidia sana. Mick anataka wengine wanaokabiliwa na changamoto za maisha na wanatafuta pahali pa kupata tumaini wasisite kumtembelea ili kupata ushauri.

Mick anawasiwasi kuhusu kukosekana kwa huduma ya afya ya akili kwa walio hatarini zaidi - watu ambao wanaona vigumu kuwaona madaktari wao, kando na kupata kitanda katika kituo cha msaada.

Pia analaumu vikwazo vya miezi kadhaa vilivyowekwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona kwa kufanya hali kuwa mbaya. Mjini Burnley ,anasikia visa vya watu waliyotengwa kujiingiza katika utumizi wa dawa za kulevya na kunywa pombe.

Kanisa hilo linapanukwa kwa haraka -Linatoa chakulana nguo kwa waathirika. Mick pia anashirikiana na polisi, mashirika ya makazi na baraza la mitaa na taasisi zinazotoa huduma za kuwasaidia watu waliyoachana na utumizi wa dawa za kulevya.