Ramani za Google : "shimo jeusi" katika bahari ya Pasifiki lagunduliwa na kifaa kikubwa cha teknolojia

Picha iliyochukuliwa na kifaa cha ramani za Google ilisambazwa sana kwenye mitandao baada kuchapishwa na mtandao wa kijamii wa Reddit na kuibua kila aina ya tetesi kutokana na muonekano wake wa ajabu.

Picha halisi ilichapishwa bila kuratibiwa na udadisi wa watumiaji muda mfupi baada ya kuanza kwa uvumi, kwani umbile lake la kijiografia lilionekana kama ''shimo jeusi''.

Baadaye, kutokana na uchunguzi wa kina wa watumiaji wengine waliobaini eneo halisi ramani hiyo ilipochukuliwa, ilifahamika kuwa muonekano wake halisi ulikuwa tu ni "athari ya macho".

Lakini mjadala katika mitandao ya kijamii ilikuwa imeibua dhana zisizohesabika kuhusu muonekano huo.

Nini unachoona?

Picha inaonyesha umbo linalofanana na la kijiografia kama na kuzingirwa na peasi mwitu za rangi ya bluu za baharini.

Umbo hilo limo katika kile kinachoonekana kama povu la maji ya bahari ambalo ''limemezwa'' na eneo jeusi la kati.

Wengi hawakuamini kuwa lilikuwa ni shimo jeusi la , lakini maelezo pia yalitolewa kwamba inaweza kuwa volkano ya chini ya ardhi ambayo miamba yake ilisababisha weusi wenye kina.

"Ni Dhahiri kuwa lango la kuingia katika shimo la Dunia ," aliandika mtumiaji mmoja wa mtandao wa kijami wa Reddit, na kuibua nadharia kwamba katika sayari yetu kuna ustaarabu chini ya ardhi.

Tafsiri moja ilikuwa kwamba ilikuwa ni rasi kubwa katikakati ya kisiwa, huku mtumiaji mwingine akisema ilikuwa ni eneo halisi la Bermuda Triangle.

Wazo kwamba kilikuwa ni kisiwa lilichukua mkondo katika mjadala wa mtandao, na mtu mmoja ambaye kwa mzaha alisema kwamba tayari msururu wa kipindi cha televisheni wa kuelezea eneo hilo umepangwa kipindi kitaitwa ''Lost had been found'', ambacho kitaelezea jinsi manusura wa ajali ya ndege walivyolazimishwa kuishi katika kisiwa cha ajabu.

Wenye dhana potofu walisema kuwa eneo jeusi la kisiwa lilitokana naupotoshaji ambao Google huufanya wakati haitaki kukuonyesha kitu fulani.

Vostok Island, Kiribati

Hatimaye, mtu mmoja alielezea kwamba ilikuwa ni picha mbaya ya setilaiti ya kisiwa ambacho hakikaliwi na watu katika Pacific na akaongezea kiunganishi cha mtandao wa GeoEye unaooyoonyesha wazi.

Ni kisiwa cha Vostok, sehemu ya Jamuhuri ya Kiribati iliyoundwa na msururu wa visiwa vya atoll na coral.

Vilipewa jina la meli ya mvumbuzi Mrusi Fabian Gottlieb von Bellingshausen ambaye alivumbua eneo hilo mwaka 1820, kisiwa hicho kinalindwa kama nyumbani kwa koloni la ndege wa baharini.

Mmoja wa watumiaji wa mtandao ambaye alitambua eneo hilo aliandika kwamba hakuna Ushahidi wowote kwamba kisiwa hicho kilikuwa koloni la binadamu katika wakati wowote wa kihistoria. "Hata Wapolynesia hawakukiona," aliongeza.

Kinaaminiwa kuwa nchi ya kwanza katika dunia kutoweka wakati viwango vya maji ya bahari vilipopanda, kutokana na ongezeko la joto duniani lililoyeyusha barafu.

Kulingana na data za hivi karibuni, kiwango cha maji kimepanda kwa milimita 3.2 kila mwaka tangu 1993, ongezeko ambalo, likiendelea kuimarika, itakuwa maafa kwa visiwa hivi na maeneo mengine ya mwambao kwa miongo.