Uchaguzi Ujerumani: Merkel amuunga mkono Laschet kuwa mrithi wake

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anamuunga mkono mgombea wa chama chake cha mrengo wa kati kulia bwana Armin Laschet ili amrithi nafasi yake, katika uchaguzi wenye ushindani mkali.

Katika kampeni za CDU katika eneo la mtaa wa nyumbani kwa bwana Laschet, ambapo bi.Merkel amemsifia kuwa mtu sahihi atayeweza kuunganisha watu".

Ikiwa watu wanakaribia kuanza kupiga kura , vituo vya kupigia kura vikiwa katika maandalizi ya mwisho.

Bi Merkel amekuwa akiongoza siasa za Ujerumani kwa kipindi cha miaka 16 akiwa na wadhifa kansela.

Bi Merkel aliahidi kutofanya kampeni siku ya uchaguzi ambayo ni Jumapili, lakini muungano wa CDU-CSU umepoteza kile ambacho walikuwa wanajiamini nacho katika kuongoza katika kura na sasa kiko nyuma ya SPD (Social Democrats) - washirika wapya katika serikali ya muungano .

Chama cha Green kinaonekana kuwa cha tatu, lakini bado kinaweza kuepo kwenye serikali ; wachambuzi wanasema muungano wao kwa kiasi kikubwa unaweza kuwa wa kitaaluma tu, kama kukiwa na ugumu kukubaliana kisiasa.

Mafanikio ya SPD yanachangiwa kiasi kikubwa na mgombea ambaye ni waziri wa fedha wa sasa Olaf Scholz, ambaye anapimwa tofauti na wengi ambao wanampenda Angela Merkel, anasema mwandishi wa BBC Jenny Hill katika mji mkuu wa Berlin.

Lakini kuna suala la wapiga kura wana mtindo wa kuwapima wagombea kwa masuala wanayoyapa kipaumbele, likiwemo suala la mabadiliko ya tabia nchi.

Siku ya Ijumaa, maelfu ya vijana wanaharakati walifanya maandamano ya nchi nzima wakitaka suala la mabadiliko ya tabia nchi lifanyiwe kazi.

Mabadiliko ya tabia nchi ndio imekuwa mada kuu katika kampeni za uchaguzi huu.

Mwanaharakati wa mazingira kutoka Sweden, Greta Thunberg aliwaambia wananchi mjini Berlin kuwa hakuna chama cha kisiasa kinachojitoa vya kutosha katika kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabia nchi.

Kura hizo katika uchumi mkubwa wa Ulaya, ambao ndio unasimama kama muhimili wa Umoja wa Ulaya, zinafuatiliwa kwa ukaribu katika bara zima na duniani kote.

Wajerumani wataweza kuchagua wabunge katika bunge la muungano huko Bundestag, na kuna viti vipatavyo 598 na mara nyingi zaidi ya hapo.

Wajerumani wapatao milioni 60.4 ambao wana umri zaidi ya miaka 18 wanaweza kupiga kura.

Ingawa chama kitakachoshinda kitaweza kuunda serikali mpya mara tu kitakapotangazwa ushindi na kuweza kuunda baraza lake.