Kanisa la Shetani: Fahamu jinsi wafuasi wa shetani wanavyomuabudu

Mahakama Kuu nchini Nigeria, iliyoko Umuahia, Jimbo la Abia, hivi karibuni ilimwachilia huru mwanzilishi wa Kanisa la Shetani nchini humo.

Yeye pamoja na wenzake 17 walikuwa wanashikiliwa na Polisi kutokana na vurugu zilizofanyika katika eneo la Ebem Ohafia.

Wanakijiji walikuwa wanamtuhumu jamaa huyo na Kanisa lake kwa kuwa mfano mbaya katika eneo hilo na kuharibu mali za Kanisa hilo

Pia alikuwa anatuhumiwa kwa kuhatarisha amani ya jiji hilo. Tayari serikali katika eneo hilo imesema hapaswi kuendelea na shughuli za Kanisa lake katika jiji hilo kwa sababu linajishughulisha na biashara ya kuuza mafuta mpakani.

Kanisa la Shetani ni nini hasa?

Kanisa la shetani lilianzishwa April 30, 1966, na Anton Szandor LaVey, huko San Francisco, Marekani.

Kwa mujibu wa mtandao wa kanisa hilo, LaVey awali alikuwa fundi seremala.

Kwa waumini, hawamuabudu, shetani, lakini wanamuona kama mfano wa mtu aliye mwema.

Wanasema anasimama kama kielelezo cha kiburi, uhuru, na kujitosheleza - sifa ambazo wengine huziita mbaya. Wafuasi wa Shetani wanaamini kwamba mtu, kwa akili yake, ndiye anayelilia miungu yote.

Yeyote anayeabudu miungu hiyo, wanamwabudu aliyeiumba.

Wanamuona kama mfano wa kile shetani anakitaka - "kiumbe anayejali haki."

Yule ambaye, badala ya kufanya dhambi, ili dhamiri ya mtu isiwe ya kibinadamu, badala yake huvumilia shinikizo la kujifurahisha.

'Yeye ndiye mungu pekee tunaweza kumuelewa.'

Mwanzo wa kanisa la Shetani:

Tangu mwaka 1950, waliokuwa wanaounga mkono dhana ya LaVey wamekuwa wakimuendea na kujiunga nae kwenye "Jumba jeusi" huko San Francisco

Majaribio ya LaVey juu ya roho ya giza, ilijiegemeza kwenye utumiaji wa mkufu mweusi na mwekundu, uliokuwa na picha ya popo. Kanisa pia lilisema kwamba baada ya miaka michache, LaVey alianza kazi ya uchawi na nguvu ya giza, akifanya kazi kwa kutangaza kutoa zawadi za bure, pesa, mapenzi ya kujifurahisha, na kuua na kukabiliana na maadui zake.

Ndani ya mwaka mmoja na nusu kanisa la Shetani lilianzishwa , huku kukiwa na tetesi kubwa tatu kuhusu Kanisa hilo. Ya kwanza kuhusu ndoa iliyofungwa kati ya mwandishi maarufu John Raymond, na Judith Case, binti wa aliyekuwa mwanasheria maarufu wakati huo. Wote walikuwa wafuasi wa Kanisa hilo, walialikwa na kiongozi wa Kanisa hilo, LaVey, kujiunga nao kwa jina la Shetani.

Vyombo vingi vya habari Marekani vikiwemo vya Ulaya, vilimtaka mwandishi huyo kuwawakailisha na kuandika kuhusu ndoa hiyo na sifa zake.

Kanisa la Shetani na viwango vya kimamlaka:

Mwanachama aliyeandikishwa

Mwanachama wa kawaida (Daraja la kwanza)

Mchawi (Daraja la Pili)

Padri Mwanaume / mwanamke (Daraja la tatu)

Mwalimu (Daraja la nne)

Namna ya kuabudu:

Jambo la kwanza kubwa ni uasi dhidi ya Ukristo.

Je! Wanakanusha madhabahu ya mwanamke uchi, na kuimba kwa siri. Utupu ulikuwa jambo la kawaida na wanasoma Sala ya Bwana kutoka mwisho. 'Maji matakatifu' wanayoweka yametiwa najisi, kwa kitu kitokanacho na uso wa mwanamke.

Chakula cha bwana wanachokula kinaenda na pombe kali aina ya whisky badala ya damu ya Yesu.

Wanaita majina ya miungu, badala ya Mungu wa Wakristo.

Jambo la pili ilikuwa wakati wa ubatizo wa binti wa LaVey kwa njia ya kishetani.

Badala ya kumtumbukiza mtoto ndani ya maji, anachokifanya ni kukaa mlangoni mwa madhabahu, na vitu anuwai vya kula.

Pia alivaa picha ya Shetani kichwani mwake, na kusoma maneno ya kumtukuza na kuomba msaada kwa shetani.

Wengi wao hawamwabudu Shetani:

Jambo la kushangaza ni kwamba waja wengi katika kanisa hhili awakuabudu Shetani - hawakuamini mungu yeyote.

Hawapingi sherehe ya Krismasi:

Kwa sababu wanaupinga Ukristo ulitegemea kuona hawasheherekei kuzaliwa kwake, lakini hilo ni tofauti. Ni mshangao mkubwa kuona kuwa wanasherehekea siku ya kuzaliwa ya Yesu.

Imani yao ni kwamba wakristo wamechukua muda kusherehekea. Sherehe za Christmas ni njia ya kujipendekeza, ambayo ni moja ya malengo yao makuu.

"Kwa sasa, tunafurahia maisha, na tuko pamoja na wapendwa wetu."

Hauwezi kupata kanisa lolote la Shetani katika eneo lako:

Kama ilivyo kwenye wavuti wao wa ulimwengu, kanisa la Shetani halina kanisa, kwa sababu "inapinga kanuni kwamba kila mmoja wetu hutumia maisha yake.

Mbali na nyumba yake iliyotumika kuanzisha Kanisa, walikuwa wamewahi kuwa na matawi ya kanisa, lakini walifukuzwa, kutokana na dhana kwamba hayafai. Mkuu wa kanisa aliondoka nyumbani kwa LaVey huko San Francisco, na sasa yuko New York City.

Hawakuruhusu mtu yeyote atembelee hapo. Jambo muhimu la kwanza kwao ni sherehe.

Baadhi ya masharti yao:

  • Kama mgeni amekuudhi, mtendee vile ambavyo wewe ungependa kutendewa.
  • Usishiriki mapenzi kama mtu unayetaka kushiriki nae hajaonyesha dalili ya kuhitaji mapenzi ama hataki kushiriki mapenzi na wewe.
  • Usiwadhuru watoto.
  • Usiue wanyama, isipokuwa kama ni kwa ajili ya kitoweo, ama anataka kukudhuru.
  • Usipigane na yoyote, lakini unaweza kumsambaratisha mtu ambaye anaingilia mapambano yako, baada ya kutolewa kwa onyo.
  • Vitu vinavyochukuliwa kuwa ni dhambi na Kanisa hilo ni pamoja na ujinga, ubinafsi na kujidanganya. Kanisa linapinga matumizi, na biashara ya dawa za kulevya.
  • Inaaminika kwamba mshirika yeyote wa kanisa anayekiuka sheria ya dawa za kulevya nchini mwake anajiua.

Kanisa hili la Shetani sio la maskini:

Mwanachama mpya analipa karibu dola 200 kujiunga. Hii inategemea jinsi mtu huyo anavyoweza kujibu maswali.

Wakati mwingine, wanaweza hata kumaliza uanachama wao.