Afghanistan: Kiongozi wa Taliban Mullah Abdul Ghani Baradar amepotelea wapi?

Msemaji Taliban wa masuala ya siasa Dkt. Mohammad Naeem siku ya Jumatatu alitumia mtandao wa WhatsApp kuelezea kutoweka kwa Mullah Abdul Ghani Baradar, Naibu Waziri Mkuu wa serikali ya Taliban na mkuu wa ofisi ya siasa.

Katika ujumbe huo, Mulla Abdul Ghani Baradar alisema, "Taarifa hizi zimekuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii kwa siku kadhaa. Nilikuwa safari na siku hizo nilikuwa mahali. Namshukuru Mungu..mimi na marafiki zangu tuko salama. Mara nyingi vyombo vya habari vinaeneza taarifa za uwongo dhidi yetu.

Mapema Septemba 12, barua iliyotolewa na Musa Kaleem, msemaji wa Mullah Abdul Ghani Baradar ilisema, "Taarifa iliyodaiwa katika mitandao ya WhatsApp na Facebook kwamba makundi mawili ya Taliban yalikabiliana katika eneo la Rashtrapati Bhavan nchini Afghanistan na Mullah Abdul Ghani Baradar kujeruhiwa vibaya na baadaye kufariki kutokana na majeraha hayo, Ni uwongo."

Taarifa hizo zilipata nguvu baada ya Mullah Abdul Ghani Baradar kukosekana katika mkutano wa viongozi wa Taliban na waziri wa mambo ya nje wa Qatar katika kanda ya video iliyoachiwa kutoka eneo la Rashtrapati Bhavan Arg siku ya Jumapili.

'Mulla Baradar hakujeruhiwa lakini ana hasira'

Kulingana na Taliban, Mullah Abdul Ghani Baradar yuko mjini Kandahar ambako anakutana na kiongozi wa Taliban, Mullah Hebtullah Akhundzada, na kwamba atarudi mjini Kabul hivi karibuni.

Lakini vyanzo viwili vya Taliban mjini Doha na Kabul vimeambia BBC kwamba usiku wa Alhamisi au Ijumaa iliyopita kulizuka mabishano makali kati ya Mullah Abdul Ghani Baradar na Khalil-ur-Rahman, waziri wa mtandao wa Haqqani ambao pia uliingiliwa na wafuasi wao.

Baada ya mvutano huo Mullah Abdul Ghani Baradar, aliyekasirishwa na serikali mpya ya Taliban alienda Kandahar.

Kulingana na vyanzo vya habari, kabla hajaondoka, Mulla Baradar alisema hataki kuwa katika serikali kama hiyo.

Hata hivyo BBC haikuweza kuthibitisha madai hayo.

Ni serikali gani itakua na Baradar

Kulingana na vyanzo hivyo, 'Mtandao wa Haqqani, kwa upande mwingine, unasema 'kwa mara ya pili Utawala wa Kiislamu umebuniwa kutokana na juhudi zao, kwa hivyo mtandao huo una haki zaidi katika serikali.'

Vyanzo vya habari mjini Doha na Kabul vinasema baada ya kuundwa kwa serikali mpya, Mullah Abdul Ghani Baradar alisema hataki serikali iliyojaa na viongozi wa kidini pekee na Taliban.'

Kulingana na vyanzo hivyo, Mullah Baradar alisema alipata uzoefu mkubwa katika miaka hiyo 20 na kwamba alikuwa ameahidi jamii ya kimataifa katika ofisi ya kisiasa nchini Qatar kuwa ataunda serikali itakayojumisha wanawake na makundi ya walio wachache kutoka kwa jamii.

Chanzo kingine cha Taliban mjini Kabul pia kinasema tofauti hizi zilikuwepo hata kabla ya kuundwa kwa serikali, lakini wakati majina ya mawaziri yalipowasilishwa na viongozi wao, kila mmoja alikubaliana nayo.

Tofauti kati ya Mtandao wa Haqqani na Taliban wa Kandahar umedumu kwa muda mrefu na tofauti hizo zimeongezeka zeidi baada ya Taliban kuchukua udhibiti wa Kabul.

Kulingana na vyanzo hivyo, 'Mtandao wa Haqqani, kwa upande mwingine, unasema 'kwa mara ya pili Utawala wa Kiislamu umebuniwa kutokana na juhudi zao, kwa hivyo mtandao huo una haki zaidi katika serikali.'

Vyanzo vya habari mjjini Doha na Kabul vinasema baada ya kuundwa kwa serikali mpya, Mullah Abdul Ghani Baradar alisema 'hataki serikali iliyokwa na viongozi wa kidini pekee na Taliban.'

Kulingana na vyanzo hivyo, Mullah Baradar alisema alipata uzoefu mkubwa katika miaka hiyo 20 na kwamba alikuwa ameahidi jamii ya kimataifa katika ofisi ya kisiasa nchini Qatar kwamba ataunda serikali itakayojumisha wanawake na makundi ya walio wachache kutoka kwa jamii.

Chanzo kingine cha Taliban mjini Kabul pia kinasema tofauti hizi zilikuwepo hata kabla ya kuundwa kwa serikali, lakini wakati majina ya mawaziri yalipowasilishwa na viongozi wao, kila mmoja alikubaliana nayo.

Hali ya serikali mpya huko Kabul

Kwa mijibu wa waandishi wa habari walioko mjini Kabul, licha ya baraza la mawaziri kutangazwa , shughuli katika ofisi nyingi za serikali hazijaanza kwani kufikia sasa ni waziri mmoja tu aliyewasilisha sera zake.

Hata hivyo Taliban inasema mawaziri wote wameanza kufanya kazi, lakini bado taasisi nyingi za serikali zikiwemo za elimu zimefungwa na hata zile ofisi zilizofunguliwa ni wafanyakazi wachache wanaofika kazini.

Kulingana na Tahir Khan, mwandishi wa habari wa Pakistan aliyeo mjini Kabul, mawaziri wameanza kufanya kazi lakini kufikia sasa ni Waziri wa Elimu Abdul Baqi Haqqani pekee ambaye ametoa taarifa ya sera itakayoongoza wizara hiyo

Kulingana na sera hiyo wanafunzi wa kike wanaweza kusoma kwa kuvalia hijab na walimu wa kiume wanaweza kufunza nyuma ya pazia: Taliban

Hali ilivyo mjini Kabul

Mwandishi wa BBC mjini Kabul Malik Mudassir, anasema benki bado zimefungwa mjini humo lakini mitambo ya ATM zinafanya kazi katika baadhi ya maeneo, lakini wateja wamewekewa kiwango cha pesa za kutoa.

Kuhusu hali ya uwanja wa ndege, Malik Mudassir amesema maafisa wa Qatar wamekuwa wakisimamia shughuli katika uwanja huo na Qatar imekuwa na jukumu muhimu la kuhakikisha uwanja wa ndege wa Kabul unarejelea shughuli zake.

Masomo yameanza katika baaadhi ya vyuo Vikuu vy akibinafsi mjini Kabul, lakini vyuo vikuu vya serikali na taasisi zingine za elimu na shule za upili bado zimefungwa.

Kulingana na Malik Mudassir, walimu hawajapokea mishahara yao kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita.