Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Simulizi ya Timbuktu, moja ya miji iliyokuwa tajiri zaidi duniani kabla ya kuzama ndani ya mchanga wa janjwa la Sahara
Kabla ya jua kuchomoza, AG Mohammed alianza safari yake ya usiku kwa miguu kupitia mitaa ya mchanga ya Timbuktu nchini Mali.
Njiani, alijiunga na rafiki, na wakaanza kutembea kwa pamoja.
Kwa muda muda mrefu waliendelea kukaribishana na wakaulizana kuhusu marafiki na familia zao.
Marafiki hao walivuka mitaa ya Timbuktu, na wakaendelea hadi kwenye eneo lenye rundo la mchanga lililopo viungani mwa mji huo upande wa magharaibi, huku wakiwa wamevaa mavazi ya kitamaduni ya watu wa eneo hilo.
AG Muhammad Ali anasema: Kikombe cha kwanza cha chai ni kigumu kama kifo, huku cha pili kikuwa na ugumu wa kati , na cha tatu ni kizuri kama mapenzi, lazima uvinywe vyote vitatu.
Sawa na Watuareg wengi, wafugaji hawa wa kuhamahama walioishi katika jangwa la Sahara, AG Muhammad Ali alizaliwa katika jangwa sio mbali na Timbuktu.
Cheti chake cha kuzaliwa kinaonesha alizaliwa mwaka 1970, lakini hayo ni makadiriio ya tarehe rasmi kwa ajili ya cheti cha kuzaliwa , na hakuna yeyote anayefahamu ni tarehe gani aliyozaliwa. Katika hilo, AG''Muhammad anasema :''Ninadhani alizaliwa kabla ya tarehe hii.
AG Muhammad Ali, ambaye wakati wa utoto wake alikulia jangwani, anasema kwamba hatari kwake pale haikuwa zaidi ya kuona kimbunga kikubwa cha mchanga kikija kwa mbali.
Anasema ''Siku moja nilipokuwa kijana, nilienda kutafuta maji akiwa juu ya ngamia , na nilipokuwa njiani nikirudi, kimbunga cha mchanga kilipaa juu na kuacha anga likiwa jeusi, kiasi kwamba sikuweza hata kuona mikono yangu. Katika kipindi cha dakika sikujua ni nini kilichotokea kabisa. Kilidumu kwa muda wa saa tano. Halafu nikarejea nyumbani lakini sikumkuta baba yangu, ambaye alikuwa ameondoka nyumbani kunitafuta.
Tangu wakati huo Hajj Muhammad Ali hakuwahi kuuona mji tena hadi alipofikia umri wa kubalehe, na katika mji huo alikuwa amejenga nyumba yake, anasema''hakuamini ukubwa wa mwanga.
Haja ya kutafuta maisha ilimfanya AG Muhammad Ali aende Timbuktu, ambako alianza kazi yake kama muongozaji wa watalii kwa wale ambao walitaka kufahamu zaidi kuhusu eneo la magharijbi mwa ujangwa la Sahara.
Moyo wa Ag Muhammad Ali uliendelea kukumbuka jangwa licha ya kwamba alikuwa mjini. Wakati kulipokuwa hakuna kazi ya mjini, alikuwa akirudi jangwani na kuijshi jhuko kwa miezi kunywa chai na marafiki zake.
Takriban watu 100,000 waliishi katika Timbuktu katka karne ya kumi na sita.
Wakati mmoja Timbuktu ilikuwa na karibu shule mia mbli na vyuo vikuu ambavyo viliwavutia wasomi kutoka maeneo ya mbali kama vile Granada na Baghdad.
Mji huo ulifahamika kwa maktaba zake za thamani na hati.
Siri hizi hutolewa na AG Mohammad kwa njia ya uchangamfu mara nyingi kwa watalii na za binafsi za kifamilia na huwaonesha watu hati nadra za maandishi ya kale.
Miongoni mwa hati hizo kuhusu taarifa za Mtume Muhammad( Amani iwe kwake) zilizoandikwa kwenye matawi ya dhahabu pamoja na mikataba ya kisayansi ya Waislamu walioishi enzi ile.