Ukatili:Tazama vifaa vilivyotumiwa kuwaangamiza na kuwaua watumwa weusi

Watumwa weusi waliotekwa Afrika na sehemu nyingine duniani ni baadhi ya kundi la watu waliopitia ukatili ,ubwa sana kuwahi kurekodiwa .

Ubinadamu ulijaribiwa katika enzi hizo na baadhi ya walioishi kupitia mateso hayo walisimulia na kuacha kumbukumbu ambazo zinautisha ulimwengu kurudi katika enzi kama hizo.

Ingawaje unyanyasaji na mateso ya kila aina yanaenelea kushuhudiwa katika sehemu mbali mbali duniani ,kusahau historia ya ukatili waliopoitia mababu zetu ni jambo lisiloweza kusameheka.

Kufikia wakati utumwa ulipopigwa marufuku maelfu ya Watu weusi walikuwa wamenyanyaswa na hata kuuawa katika sehemu za dunia zilizokuwa bado zinashabikia utumwa .

Picha hizi za baadhi ya mbinu na vifaa vilivyotumiwa kuwaadhibu watumwa weusi zitakupa tasira ya safari ndefu ya watu weusi kujinasua kutoka minyororo ya utumwa na mateso .

'Screw ya Pamba'

Moses Roper, mtu Mweusi ambaye alizaliwa katika utumwa huko North Carolina na mwishowe alitoroka utumwa mnamo 1835, alisimulia mateso aliyopitia katika simulizi ya " Narrative of the Adventures and Escape of Moses Roper, from American Slavery."

Mashine iliyotumika kufunga pamba ikawa kifaa cha kutoa adhabu. Wakati Roper, ambaye alifanya majaribio mengi ya kutoroka shamba la South Carolina ambalo alikuwa mtumwa, alikimbia tena, wakati mwingine, kukwepa vifaa vya mateso vilivyotumiwa dhidi yake.

Kifaa hicho cha 'screw ya pamba," kilitumiwa kupakia pamba.

'Screw ya vidole'

Thumbscrew ni chombo cha mateso ambacho kilitumika kwa watu weusi waliokamatwa ndani ya meli za wafanyabiashara wa watumwa kwenye Bahari ya Atlantiki.

Kifaa hicho cha mateso kilitumiwa mara nyingi dhidi ya Waafrika waliohusika katika ghasia na uasi wakati wa biashara ya watumwa ya Atlantiki kutoka karne ya 16 hadi 19. Kiongozi alilazimika kuweka vidole vyake vya gumba kati ya vipande viwili vya chuma vyenye vilivyounganishwa na skrubu moja au zaidi.

Vyuma hivo vilikuwa na miiba mikali, ambayo ingetiwa ndani ya vidole vya gumba vya mwathiriwa, na kuvunja mifupa yake katika ukatili uliozua uchungu mkali sana kwa mwathiriwa .

Maski

Maski aina mbali mbali zilitumika dhidi ya Waafrika waliotekwa ambao walijaribu kutoroka utumwa wao. Katika makala kuhusu Waafrika waliotoroka nchini Brazil, "Esclave Marron wa Rio de Janeiro" Bwana Bellel anabainisha kuwa maski zilitumika kwa mateso zaidi:

"Wakimbizi waliotekwa walilazimika kufanya kazi ngumu zaidi na kali. Kwa kawaida waliwekwa katika minyororo na kuongozwa kwa vikundi kupitia vitongoji vya jiji ambapo walibeba mizigo au kufagia takataka mitaani.

Watumwa wengi walipoteza matumaini yote ya kukimbia tena, hawakufikirii chochote isipokuwa kujiua. Walijipa sumu kwa kunywa au kumeza kiasi kikubwa cha pombe kali, au kwa kula uchafu / udongo

Ili kuwazuia kujiua walilazimishwa kuvalia maski hizo na kuachiwa shimo dogo la kuingia kinywani mwao

Kola ya chuma shingoni

Kola ya chuma iliwekwa shingoni mwa Waafrika waliotekwa kwa miezi kwa wakati mmoja kuwakumbusha makosa yao.

Kola kama hizo zilikuwa nene na nzito; mara nyingi zilikuwa na miiba iliyowadunga wakifanya kazi za shambani .Mara nyingi ilichukua saa moja kuifungua na kuondoa kola hizo shingoni .

Kola ya mbao

Hili lilikuwa bao kubwa lenye shimo la kuingia shingoni ambalo lilikuwa nzito.kola hii ya mbao ilikuwa mbinu inayotumiwa sana kuwatesa na kuwapa adhabu watumwa wa kike . Licha ya uzito wake ,mtumwa aliyevalishwa kifaa hicho alilazimika kuendelea kufanya kazi .