Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vita vya Afghanistan: Fahamu uwezo wa kijeshi wa kundi la Taliban
Taliban wamekuwa wakipata faida kubwa katika siku za hivi karibuni katika vita nchini Afghanistan na sasa wako katika hatihati ya kuchukua nchi hiyo.
Taliban, ambayo imechukua udhibiti wa miji muhimu ya nchi hiyo, iliangushwa mnamo 2001 na Marekani, ambayo ilivamia Afghanistan wakati huo.
Taliban kwa sasa wanadhibiti Kabul, mji mkuu wa Afghanistan.
Nguvu ya Taliban
Hakuna takwimu kamili za nguvu za jeshi la Taliban nchini Afghanistan.
Lakini wachunguzi wanakadiria kuwa karibu wapiganaji 150,000, ikiwa ni 50% chini ya jeshi la Afghanistan.
Wapiganaji wa Taliban wanatawaliwa na ukoo wa Bashtun.
Lakini pia kuna wapiganaji wengine kutoka makabila mengine na pia nchi nyingine za Kiislamu.
Taliban imeundwa tofauti na vikundi vingine vya wapiganaji na ina uongozi wa kimfumo.
Kundi hilo linaongozwa zaidi na makamanda ambao walipigana dhidi ya Umoja wa Kisovieti katika miaka ya 1990.
Makamanda hawa wana uzoefu wa jinsi ya kushambulia na njia rahisi za kushambulia miji muhimu nchini.
Wapiganaji wa Taliban walisemekana kuweza kushinda vita kwa sababu wanajua kupigana msituni na milimani.
Wapiganaji wa Taliban wana silaha ndogo ndogo, lakini pia kuna silaha nzito. Idadi kamili ya vifaa vyao vya kijeshi haijulikani.
Kiongozi wa Taliban
Hebatullah Akhundzada alichukua uongozi wa Taliban nchini Afghanistan mnamo Mei 26, 2016, wakati alipoteuliwa na baraza la ushauri la harakati hizo.
Alichukua nafasi ya kiongozi wa zamani wa kikundi hicho, Akhtar Mohamed Mansour, ambaye aliuawa katika shambulio la angani la Marekani mnamo Mei 22 mwaka 2016.
Hebatullah alizaliwa mnamo Oktoba 19, 1967, kulingana na tovuti rasmi ya Taliban.
Alizaliwa katika wilaya ya Bajway ya mkoa wa Kandahar na ana asili ya Bashtur.
Anaaminika kuwa mmoja wa wanachama waanzilishi wa Taliban na msaidizi wa karibu na mwanzilishi wake, Mulah Mohamed Omar.
Historia fupi ya Taliban
Wapiganaji wa Taliban waliibuka mwanzoni mwa miaka ya 1990 na kwanza walianzia kaskazini mwa Pakistan.
Kundi hilo liliibuka baada ya kumalizika kwa vita vya Umoja wa Kisovieti huko Afghanistan.
Washiriki wengi wa Taliban ni kutoka kabila la Pashtun, ambalo ni kabila kubwa zaidi nchini Afghanistan.
Inaaminika kuwa kwa mara ya kwanza, walifadhiliwa na Saudi Arabia.
Wakati Afghanistan ilichukua madaraka, Taliban iliweka sheria za Kiislamu juu ya nchi hiyo.
Wakati wa utawala wao nchini Afghanistan, Taliban walipiga marufuku kusikiliza muziki, kwenda kwenye sinema na kuruhusu wasichana wenye umri wa miaka 10 na zaidi kwenda shule.
Nchi zinazotambuliwa wakati wa utawala wa Taliban ni pamoja na Pakistan, Saudi Arabia na Falme za Kiarabu.
Zaidi ya vikosi vya usalama 45,000 vimeuawa nchini Afghanistan katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.