Yafahamu madhehebu ya imani za kutisha ,watu kujiita mungu na hata kuwaoza watoto

Madhehebu ya kidini yamekuwepo kwa miaka mingi sana na hadi hii leo bado bado yanaendelea kuchipuka na kuvutia wengi kuanzia vijana hadi watu wazima ikitegemea na malengo ya mtu binafsi.

Makundi ya aina hii kuna wale ambao huyachukulia kama ya dini fulani au kundi la watu linalojumuika pamoja kuendesha ndoto zao ingawa mara nyingi huwa yanapelekea kutengwa na jamii kwasababu ya maswali mengi yanayoibuka na ukosefu wa majibu kuwa wazi kwa kila mmoja katika jamii.

Fahamu baadhi ya madhehebu yaliyogonga vichwa vya habari duniani.

Tahadhari: Baadhi ya taarifa na picha huenda zikawa za kuogopesha.

Dhehebu la Love Has Won

Ni machache sana yanayofahamika kuhusu chimbuko la dhehebu la kidini la Love Has Won, ambalo linaaminika liliibuka miaka ya 2000 kwa mtindo tofauti.

Mfuasi alimhamasisha mwanamke Amy Carlson kujiunga na baadaye kuwa kingozi wa kundi hilo la Love Has Won.

Wafuasi wake hawaonekani kuwa na imani fulani walizoshikilia na badala yake, wanafuata na kuhubiri theolojia ya kizazi cha sasa, nadharia za kisiri na ibada ya messiah.

Messiah wao alikuwa Bi. Carlson, aliyefahamika kama "Mungu Mama".

Mafundisho yake yalichukuliwa kuwa matakatifu na wafuasi wake na madai yake yalikuwa ya ajabu zaidi hata kuliko cheo chake alichopewa na waliomuamini. Alichukuliwa kuwa Yesu Kristo katika moja ya maisha yake 534, angeweza kutibu ugonjwa wa saratani na pia aliweza kuzungumza na roho mtakatifu wa marehemu muigizaji Robin Williams, mara tu nyingi alidai hivyo.

Madai hayo ya uwongo yalielezwa waumini malimbali nchini Marekani na kote duniani kupitia mahubiri ya kila siku kwa njia ya mtandao wa Youtube. Katika video hizo, wafuasi wa Bi. Carlson waliomba msaada, wakaendeleza biashara za kisasa na kumuabudu kiongozi wao.

Mbele ya kamera, wafuasi wake walionekana kufurahia mtindo wao wa maisha lakini ushuhuda wa baadhi ya waliokuwa wafuasi wake ulioochukuliwa gizani, baadhi walionekana kuonesha madai ya unyanyasaji wa kimwili na kiakili ambayo wafuasi sugu wa Bi. Carlson waliyakanusha.

Nukupitia nyaraka za mahakamani zilizoshuhudiwa na BBC, ilisemekana kwamba "wamepokea malalamiko mengi kutoka kwa familia za Marekani zikisema kwamba kundi hilo limebadilsha akili za wafuasi wake ambao wanaiba pesa majumbani".

Wakati BBC ilitaka kuzungumza na angalau hata mfuasi mmoja, hakuna aliyekuwa tayari kwa mahojiano na pia ukurasa wao wa Facebook wa 'Love Has Won' haukujibu ombi lililotumwa.

Alivyofariki dunia

Mwili wa kiongozi wa dhehebu hilo la kidini ulipatikana katika nyumba moja huko cul-de-sac karibu na Moffat.

Inasemekana kwamba katika moja ya chumba cha nyumba hiyo, kulipatikana hekalu lililokuwa na kile kilichosemekana kuwa mabaki ya maiti aliyeonekana kuwa mwanamke.

Katika kitanda chake, kando kando ya mwili wa mwanamke huyo kulikuwa na vifuko vilivyokuwa na taa za Krismasi huku uso wake ukiwa umerembeshwa hadi macho yake.

Mwili huo uliaminika kuwa wa Amy Carlson, 45, kiongozi wa kundi hilo ambalo wakosoaji na polisi walilitambua kama dhehebu fulani la kidini.

Dhehebu la NXIVM

Mwasisi wa dhehebu la Nxivm, Keith Raniere alifungwa jela miaka 120 gerezani kwa makosa ya ulaghai, ulanguzi wa kingono, umiliki wa video za kingono dhidi ya watoto na makosa mengine ya uhalifu.

Kama kiongozi wa kundi hilo, alisajili wanawake kama watumwa na kuwalazimisha kufanya mapenzi naye.

Mwendesha mashitaka alisema kuwa Raniere, 60, anastahili kuishi maisha yake yote yaliyosalia akiwa gerezani kwa "maovu aliyotekeleza" dhidi ya waathirika wa dhehebu aliloendesha.

Mamlaka ya Marekani ilianza kumchunguza Nxivm baada ya kuchapishwa kwa taarifa zake kwenye gazeti la New York Times mwaka 2017.

Kauli mbiu ya dhehebu hilo ni "kujenga dunia iliyo bora zaidi".

Kundi hilo linasemekana kuwa na zaidi ya watu 16,000 na matawi yake huko Marekani, Canada, Mexico na Amerika Kusini.

Lakini kuhalisia dhehebu la Raniere lilikuwa pendwa na washiriki wanawake walichukuliwa kama watumwa.

Baadhi ya wanawake walikuwa wamewekwa alama kwenye nyonga zao kwa namba za awali za Raniere na kuonekana kwenye sherehe zao zilizotengenezewa filamu huku washiriki wakikusanyika kila mwaka kusherehekea na kulipia ada siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi huyo.

Ushuhuda

Mmoja wa wanachama alishuhudia kwamba alipewa mafunzo kwa wiki kadhaa kabla ya kutimu miaka 18 ili Raniere aweze kuvunja ubikira wake.

Akiwa anajulikana kwa jina la Daniela, aliambia mahakama kuwa yeye na dada zake walitiwa mimba na mwasisi huyo na kulazimshwa kuavya mimba hizo, na pia yeye pamoja na dada yake ambo walikuwa na umri wa chini ya miaka 18 walilazimishwa kushiriki ngono na mwanzilishi wa dhehebu hilo mara kadhaa.

Dhehebu hilo inasemekana kwamba lilijumuisha waigizaji wa kike wa Hollywood na hata kijana wa aliyekuwa rais wa Mexico - baadhi yao wakiwa miongoni mwa waliotoa ushahidi dhidi ya Raniere mahakamani.

Mwaka 2018, majasusi wa Marekani walimkamata Bwana Raniere nchini Mexico baada ya kuondoka Marekani kufuatia ufichuzi wa taarifa zake kupitia gazeti la New York Times.

Dhehebu la Angels' Landing

Lou Castro alikuwa mwanamume mwenye historia ya kutisha ambaye alishawishi idadi ya watu kadhaa kwamba yeye alikuwa malaika, angeweza kutibu wagonjwa na kutabiri ya siku za usoni.

Mwanamume huyo aliyesemekana kuwa "malaika," jina lake halisi lilikuwa Daniel Perez, na alipatikana na hatia Februari 2015 ya ulaghai, unyanyasaji dhidi ya watoto, ubakaji na mauaji ya kiwango cha kwanza.

Pia kuna vifo kadhaa vya ajabu vilivyotokea huko Wichita, Kansas, katika eneo ambalo Perez alikamatwa na kuzua maswali mengi.

Mara ya kwanza Perez kuvutia nadhari ni mwaka 2003 alipokuwa anaishi na kundi dogo la watu wa asili mbalimbali katika kipande cha ardhi cha hekari 20 kilichojulikana kama 'Angel's Landing'.

Kulikuwa na magari ya kifahari, kidimbwi cha kuogolea na nyumba kadhaa.

Inasemekana kuwa Perez aliwaambia wafuasi wake kwamba alihitajika kufanya mapenzi na wasichana wadogo ili aweze kuwa hai.

Pia kwa miaka mingi tu, Perez alikusanya mamilioni ya madola katika sera ya bima ya maisha kutoka kwa washiriki wake waliokuwa wamefariki dunia.

Ushuhuda

Sara McGrath aliletwa katika familia ya Perez na mama yake ambaye alikuwa ajenti wa majumba na ndiye aliyemsaidia "Lou Castro" kupata eneo la kumiliki alipoingia mjini.

McGrath, wakati huo alikuwa katika miaka ya kumi na kitu huku dada yake mdogo, Emily, akiwa karibu miaka 11.

Sara hakumpenda kabisa Perez kulingana na kauli zake lakini mama yake alikuwa na uhusiano wa karibu na Perez akiamini kabisa kwamba ni malaika ambaye angeweza kukuambia kwamba unafariki dunia lini.

Maisha katika eneo la 'Angel's Landing' yalianza kubadilika miezi michache baadaye.

Dhehebu la 'Watoto wa Mungu' Chukua picha hapa: Children of God cult was 'hell on earth'

Verity Carter anasema kukua katika dhehebu la kisiri ambalo lilihamasisha mahusiano ya mapenzi kati ya watoto na watu wazima ilikuwa kuishi kwenye "jehanamu duniani".

Msichana huyo, anasema alianza kunyanyaswa kingono akiwa na umri wa miaka minne na washiriki wa dhehebu la Children of God akiwemo baba yake mzazi.

Alexander Watt alihukumiwa baada ya kukiri kutekeleza makosa manne ya unyanyasaji dhidi ya Verity na mtoto mwingine huko Renfrewshire pamoja na mashariki ya pwani ya Scotland miaka ya 1980.

Verity alielezea BBC Scotland kwamba "Hakuwa peke yake aliyenitendea unyama kupitia mpango wa 'Kaye Adams' wakati ninakua"

"Nilitendewa mengi maovu na wengi tu."

Msichana huyo alisema kuwa anatumai kuhukumiwa kwa baba yake mzazi kuta hamasisha wengine kujitokeza na kuelezea matendo machafu ambayo wamepitia katika dhehebu hilo lililopo Scotland.

'Mapenzi ya Bure'

Dhehebu la Children of God lilianza nchini Marekani miaka ya 1960.

Mwanzilishi wake, David Berg, aliwaambia washirika kuwa Mungu alikuwa upendo na upendo ulikuwa mapenzi, kwahiyo hakutakiwi kuwa na mipaka kati ya hivyo viwili licha ya umri au uhusiano.

"Alihamasisha sana vitendo vya ngono miongoni mwao watoto wenye umri wa miaka miwili au mitatu," Verity amesema.

Dhehebu hilo lilisambaa na kusemekana kuwa na wanachama 10,000 katika jamii 130 kote duniani miaka ya 1970.

Nyota wa Hollywood Rose McGowan na Joaquin Phoenix walizaliwa katika dhehebu hilo.

Aidha, wazazi wote wa Verity walikuwa washirika wa karibu sana wa dhehebu hilo wakati anazaliwa.