Yajue Mataifa hasimu duniani kihistoria

Uhusiano mzuri wa taifa moja na lingine kidiplomasia ni jambo linalotajwa kusaidia sana kuepusha mifarakano na kurahisisha shuguhuli na utendaji wa kimataifa baina ya nchi husika. Licha ya juhudi za kimataifa, yapo mataifa machache ambayo hayajawahi kuwa na uhusiano mzuri baina yao, na kutikisa uhusiano wao kisiasa, kiuchumi na kijamii. Je unayajua mataifa hasimu duniani? BBC imekuandalia orodha ya mataifa hasimu ambayo kwa muda mrefu uhusiano wao kidiplomasia ni sawa na wa paka na panya.

Marekani vs. Urusi

Marekani inaonekana kuzozana na mataifa kadhaa, ukiacha China, inazozana pia kihistoria na Urusi. Walianza kuhasimiana tangu kujiingiza kwao kwenye migogoro ya nchi za Vietnam na Afghanistan. Hata baada ya vita baridi vya miaka ya hivi karibuni, kwa sasa kila nchi inajihami kwa silaha kali dhidi ya mwenzie.

Israel vs. Palestina

Uhasama huu unaoenaka kirahisi zaidi kwa kuwa uko wazi licha ya kuichanganya dunia. Mzozo wa kihistoria kati ya waarabu na wayahudi umedumu kwa muda mrefu sana hasa katika eneo la Jerusalem. Juhudi zinafanyika lakini historia urejesha machungu yanayoleta ugumu wa kupatikana kwa suluhu.

China vs. Japan

Nchi hizi zilianza uhasama na kupigana tangu mwaka 663. Hata baada ya vita kuu ya pili ya dunia, Japan iliivamia China na kutwaa maeneo mengi ya nchi hiyo. Katika uvamizi huu, inaelezwa ukatili mwingi ulifanyika ikiwemo matumizi ya silaha za kemikali, mauaji ya halaiki na ubakaji. Mpaka leo kuna mzozo wa mipaka baina ya nchi hizo, huku China ikiendelea kuituhumu Japan kwa kushindwa kukukiri makossa yake ya huko nyuma.

Iran vs Saudi Arabia

Mashariki ya kati kunawaka moto kutokana na mzozo wa kisiasa uliopo kati ya mataifa haya, ingawa uhusiano wa Iran na Iraq ukiwa na fukuto kubwa pia. Nchi hizi zote ni za kiislamu, ambapo Saudi Arabia ni chimbuko la Wasunni na Iran ni chimbuko la Washia. Kinachowazozanisha mataifa haya ni masuala matatu makubwa; mafuta, gesi na nani anahusiano gani ama anaungwa mkono na mataifa ya Magharibi. Saudi Arabia ina urafiki na nchi kama Uingereza na Marekani, ambao ni mahasimu wa Iran.

Korea Kaskazini vs. Korea Kusini

Hizi zilikuwa nchi moja, lakini baada ya vita ya pili ya dunia, nchi hizi zilitengana rasmi, huku Wasoviet wakiiunga mkono Korea Kaskazini na Marekani ikiisaidia Korea Kusini. Mwaka 1950, Korea Kaskazini ilitangaza viti dhidi ya Korea Kusini, vita ambayo iliwahusisha pia Marekani na China. Uhusiano wao kwa sasa umeimarika hasa katika miaka ya hivi karibuni, ila wengi wanatazama kama uhusiano wa paka na panya.

India vs. Pakistan

Uhasama wa mataifa haya unajengwa zaidi na mambo mawili; utofauti uliopo wa mitazamo na imani kati ya Wahindu na Waislamu pamoja na mgogoro wa mipaka. Mara kadhaa kumezuka mapigano baina ya nchi hizo ikiwemo vita kubwa ya mwaka 1965, na 1971. Kwa sasa nchi zote mbili zinamiliki kiwango kikubwa cha silaha za nyuklia, kwa lengo ni kujilinda dhidi ya mwenzake. Wataalamu wa masuala ya uasalama wana wasiwasi kwamba huenda kukazuka vita kubwa itakayohusisha silaha ya nyuklia baina ya nchi hizi.

Uingereza v Ufaransa

Uhasama wa nchi hizi ni wa kihistoria, ulianza tangu karne ya 10 ambapo watemi ama wafalme wa nchi zote walizozania ardhi ya upande wa pili. Katika Karne hiyo Mtemi William wa Normand, aliyekuwa chini ya Mfalme wa Ufaransa alivamia Uingereza, baadae waingereza walipaswa kuachia mali zote kutoka Urithi wa Wanormandi. Igawa kwa sasa uhusiano wao nje ya sura ya kimataifa si wa mashaka sana, lakini historia inawaweka kwenye mataifa hasimu yasiyokubaliana.

Uturuki vs Ugiriki

Uhasama wao ulianzia mwaka 1954, wakati himaya ya Byzantine ilipovamiwa na himaya ya kiflame ya kituruki ya Ottoman. Baada ya Ugiriki kupata uhuru, 1832. watu wa Ottoman, waliendelea kupambana kurejesha himaya hiyo kiasi cha kuwaingiza kwenye vita ya dunia ya kwanza. Hata baada ya vita ya kwanza ya dunia kumalizika, pande hizo ziliendelea kutwangana. Mpaka leo mihemko baina ya nchi hizo chembe za kihistoria zilizosalia mioyoi wmwa wananchi zinaendelea kutikisa mpaka leo mahusiano baina ya nchi hizo.

Uingereza vs. Ireland

Hawa ni ndugu wanaogombana chumbani, wakitoka nje wanatabasamu. Uhusiano wao ulianza kutetereka tangu miaka na miaka. Licha ya kuwa na mahusiano kisiasa tangu karne ya 16, na kuwa nchi moja mwaka 1801, kumekuwa na uhasimu unaotokana na Ireland kutaka kuwa huru zaidi. Ukiacha eneo la Ireland ya Kaskazini, eneo kitovu cha Ireland lilijitenga na Uingereza mwaka 1921. Uhasama haukuishia hapo umejitokeza hata hivi karibuni tu wakati Uingereza ikitangaza kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Ujerumani v Ufaransa

Nchi hizi ni majirani, kila mmoja akitupa lawama kwa kilichotokea miaka kede kede huko nyuma. Ufaransa inailaumu mpaka leo Ujerumani kwa kuwa sehemu ya chanzo cha vita kuu ya kwanza ya dunia. Katika kuu vita ya pili ya dunia ya, wafaransa wengi aliingia kwenye mtengo wa Ujerumani na kushikiliwa na vikosi vya jeshi chini ya Hitler. Hata hivyo mahusiano yao sasa yameimarika kiasi cha kusahau machungu yaliyojitokeza kihistoria.