Je ungependa kwenda anga ya mbali? Nauli ni dola milioni 28

Chanzo cha picha, Reuters
Mzabuni ambaye jina lake halijafahamika amelipia dola milioni 28 kwa ajili ya kupata kiti katika chombo cha anga cha Blue Origin kinachomilikiwa na muasisi wa kampuni ya mtandaoni ya Amazon.
Mshindi aliyeshinda mnada huo siku ya Jumamosi , hakutajwa jina bali kampuni ya Blue Origin iliandika kwenye kurasa ya tweet kuwa itamtangaza hivi karibuni.
Mchakato wa kupata mzabuni wa kusafiri katika chombo hicho ulivutia zaidi ya mataifa 140.
Watu wengine wawili wa chombo hicho kinachotarajiwa kuruka siku ya Julai 20, ni kaka yake Bezo , Mark na mtalii mwingine ambaye hakutajwa jina.
Baada ya takribani mwezi mzima wa mchakato wa kupata mnunuzi wa bei ya juu isiyoshuka dola milioni tano- lakini mnada wa Jumamosi uliibua mapya kwa malipo kuongezeka kwa zaidi ya mara tano.
"Fedha ya atakayotoa aliyeshinda itachangiwa katika taasisi ya Blue Origin'" Blue Origin iliandika kwenye tweeter.
Bwana Bezos ana utajiri wa thamani ya dola bilioni $186. (£131.5bn), kwa mujibu wa Jarida la Forbes, na kumfanya kuwa miongoni mwa watu tajiri zaidi duniani.
"Julai 20, nitasafiri na kaka yangu ," aliandika kwenye kurasa ya Instagram mapema wiki hii.
"Mtu muhimu sana na rafiki yangu wa karibu."

Kaka yake Bezos, Mark ameelezea chombo ambacho wana mpango wa kukitumia katika safari yao kitawapa fursa nzuri ya kujionea mengi.
Kwa mujibu wa mtandao wa Blue Origin, kampuni ina mpango wa kuzindua abiria wake kwa zaidi ya kilomita 100 juu ya uso wa dunia na hivyo kutoa fursa ya kuona vitu vipya vya anga.
Na watarudi duniani kwa kutumia parachuti.
Safari hiyo inategemewa kutumia dakika 10 hivi.
New Shepard booster ,kitakuwa chombo kipya kitakachoweza kutua wima kutoka kwenye anga. Jina lake lililotolewa baada ya Alan Shepard, mtu wa pili na raia wa kwanza wa Marekani kufanya ziara angani.

Wafanyakazi wa kwanza wa chombo hicho cha anga wamekuja wiki chache baada ya Bwana Bezos kuacha kuwa Mkurugenzi wa Amazon.
Badala yake kuhudumu kama mwenyekiti mkuu wa kampuni kubwa wa biashara ya mtadaoni iliyobuniwa miaka 30 iliyopita katika karakana yake , ili kumpatia muda na nguvu ya kuangazia mambo mengine kwa ukaribu.
Wakati huo huo mpinzani wake wa masuala ya anga Richard Branson anaweza kujumuika kwenye jaribio la chombo hicho cha anga Julai 4.













