Jinsi wasichana wa shule wanavyoombwa picha za utupu kwa kutishiwa kudhalilishwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Baadhi ya wasichana wanaweza kuwasiliana na wavulana 11 majira ya usiku wakitaka kutumiwa picha za utupu huko England.
Utafiti uliofanyika , unaeleza kuwa wasichana wanasema kuwa iwapo wakifunga mawasiliano na wavulana hao kwenye mitandao ya kijamii, wanafungua akaunti nyingine nyingi kuwadhalilisha.
Ripoti zimebaini kuwa kati ya wasichana 10 , tisa kati yao wamekumbwa na changamoto- labda kwa kupigiwa simu au kutumiwa picha au video za utupu.
Utafiti umeonya juu ya unyanyasaji wa kijinsia wa namna hiyo kuchukuliwa kuwa kitu cha kawaida kwa watoto wa shule.
Mara nyingi wanafunzi hawaoni umuhimu wa kutoa taarifa kuhusu unyanyasaji wa aina hii wakiogopa kuongeza tatizo, utafiti wa Ofsted unasema.
Utafiti huo unasema wavulana hawakubali jibu la hapana wanapotaka kutumiwa picha ya utupu.
Katika shule moja, wasichana walimweleza mkaguzi kuwa wanaweza kuwasiliana na wanaume 10 au 11 na wavulana tofauti tofauti wanaotaka picha za utupu.
Makundi ya kutetea haki za wanawake wanataka wafanyakazi wa shule kubadili mtazamo wao na kupatiwa mafunzo.
Mawaziri wanasema shule na vyuo wanapaswa kupata mafunzo ili kusaidia kuzuia unyanyasaji wa kingono.
'Nilitumiwa picha za utupu 50 au 60'

Cerys, mwenye miaka 21, alisema wasichana wengi walipokea picha za utupu kutoka kwa wavulana au wanaume.
Alisema: "Wakati a lipokuwa mdogo shuleni alipokea picha 50 au 60 kwenye mtandao wa Instagram, Facebook Snapchat, zilikuwa picha za utupu ambazo nilikuwa staki kuziona.
Nadhani mtu wa kwanza kumwambia ni mama yako lakini unahisi kama hutaki kuona anajua hilo, Sikujua nini napaswa kukifanya na kumuuliza nani.
Si vizuri kwa kweli kupata picha kama hizo."
Lucy, mwenye miaka 18, alisema kupokea picha za utupu limekuwa jambo la kawaida na ukipokea kwenye mitandao ya kijamii inabidi ufute tu.
Alisema : "Baadhi ya wasichana huwa wanatumiwa mara kwa mara jambo ambalo si la kawaida na hawana cha kufanya."
Lucy alisema hadhani kama walimu wanafahamu kuhusu matatizo kama hayo.
Cerys alisema: "Walisema kama tutawataarifu basi polisi wanapaswa kuhusishwa pia.
Inatisha na kusikitisha sana kupokea picha za aina hiyo.

Amy, ambalo si jina lake la asili ameiambia BBC kuwa alipokuwa kidato cha sita alibakwa baada ya sherehe.
Sasa ana miaka 25, anaamini kuwa kuna unyanyasaji mkubwa wa kijinsia ambao ulipelekea kufikia hapo alipo.
Alisema: "Changamoto kubwa ilikuwa ni kuzungumzia suala hilo, kila nilipojaribu kuwaambia marafiki , hata kama lawama zilienda kwa mvulana kwa 80% lakini bado 20% ulikuwa unalaumiwa na kuhojiwa kama nina uhakika sikumrubuni kufanya hivyo kwangu?'
Alisema kuna wasichana wengi ambao walimwambia kuwa walipitia changamoto kama hiyo na alifahamu kuwa alipaswa kuiambia shule.
Alisema: "Haikuwa mvulana mmoja peke yake na mimi, ilikuwa wasichana wengi ambao waliathirika kutokana na vitendo vya wavulana wengi ambao walikuwa wanafanya mambo ya aina hiyo.
Amy alisema aliweza kuongea na mwalimu na alisaidiwa kwa kiasi kikubwa.
Lakini anaamini kuwa kutumiana picha za utupu ni suala ambalo limekuwa baya zaidi tangu aache shule.
"Sasa naongea na vijana wadogo ambao wanasema wanatarajia kuona picha za utupu tu. Wakati ukiwa katika mahusiano ndio wapenzi hufanya kuonesha mapenzi na kama hufanyi hivyo basi huna mapenzi ya kweli," alisema.

Chanzo cha picha, Getty Images

Utafiti wa Ofsted ,wa majimbo 30 na shule za umma na vyuo vingine viwili na kuongea na vijana zaidi ya 900 kuhusu unyanyasaji wa ngono.
Asilimia 64% ya wasichana walisema walishikwa bila ridhaa yao mara nyingi , wakati wasichana nane kati ya 10 walisema wanasukumwa kutuma picha zao za utupu .
Watoto walisema unyanyasaji wa jinsia mara nyingi hutokea eneo la nje ya shule kama kwenye sherehe.
Wanafunzi katika shule mbalimbali walisema unyanyasaji wa kijinsia hutokea katika sherehe za nyumbani , bila ya kuwa na usimamizi wa watu wazima huku kukiwa na pombe na dawa za kulevya.

Wanafunzi wengi wanahisi kama mahusiano , ngono na elimu ya afya wanayopata shuleni hayawapi taarifa au ushauri wanaohitaji katika hali yao ya uhalisia.
Wasichana haswa hupata msongo wa mawazo kuwa hakuna elimu ya uwazi kuhusu tabia gani zinaruhusiwa na zipi haziruhusiwi.
Walimu wengi walisema hawana uelewa kuhusu mada za mahusiano , afya na picha za ngono.
Kila mtu alialikwa
Utafiti wa Ofsted' umetoka baada ya ushaidi wa maelfu ambao waliandika kwenye mtandao wa - Everyone's Invited yaani kila mtu anakaribishwa- na serikali ikataka uchunguzi ufanyike kuangalia sera na mambo ambayo wanafunzi wanakutana nayo shuleni au vyuoni.
Mwezi Aprili , waziri alitaka kuwe simu ambayo inaweza kusaidia kusikiliza unyanyasaji sehemu za limu mpaka mwezi Oktoba.

Chanzo cha picha, Getty Images
Msimamizi wa utafiti anasema , ilikuwa inashangaza sana kuwa vijana wadogo wanakutana na changamoto kubwa katika kila shule.
Ni suala la tamaduni na mtazamo ambao umechukuliwa kuwa wa kawaida , shule na vyuo hawawezi kutatua suala hilo wenyewe.












