Chombo cha Nasa cha anga za mbali kinasherehekea siku 100 za kwanza (sols) tangu kilipotua katika sayari ya Mars, ambako kinachunguza ishara za uhai wa vijidudu vya zamani, jiolojia ya sayari hiyo na hali ya hewa ilivyokuwa zamani.
Tangu ilipotua katika sayari ya Mars Februari, chombo hicho(roboti) kimenasa picha za kuvutia katika ardhi, inayofahamika kama Jezero Crater, kilomita 49 (maili 30) kaskazini mwa ikweta ya Sayari Nyekundu.
Helikompta hiyo ndogo pia imetuma picha za muonekano wa angani, baaa ya kuandikisha historia ya kuwa chombo cha kwanza kinachoongozwa na binadamu kutua katika sayari nyingine.
Hizi ni picha zilizotumwa na chombo hicho kutoka sayari ya Mars kufikia sasa.
Chanzo cha picha, NASA/JPL-Caltech/MSSS
Maelezo ya picha, Tarehe 6 Aprili, Chombo hicho kilitumia ( sensa pana ya Mfumo wa Juu wa Uendeshaji na uhandisi wa kidijitali) kupiga picha ya selfie karibu na helikopta yake. Picha hii imeundwa kutokana na picha 62 za kibinafsi ambazo ziliunganishwa pamoja wakati zilipotumwa duniani.
Chanzo cha picha, NASA/JPL-Caltech/MSSS
Maelezo ya picha, Siku tatu kabla ya hapo, kifaa hicho chenye muundo wa helikopta kilikuwa chini ya chombo hicho
Chanzo cha picha, NASA/JPL-Caltech/ASU
Maelezo ya picha, Helikopta hiyo iliyo na uzani wa kilo 1.8 inachukuliwa kama onyesho la ishara ya uwezekano wa vitu kuondoka sehemu moja hadi nyingine katika anga nyembamba ya Matian.
Chanzo cha picha, NASA/JPL-Caltech
Maelezo ya picha, Aprili 19, chombo hicho kiliandikisha historia ya kuwa kifaa cha kwanza kinachoelekezwa na binadamu kutua katika sayari nyingine. Helikopta hiyo ambayo inaonekana kati kati ya picha hi, ilipanda juu kwa mita 3(futi 10) jyuu ya chombo hicho na kuenda kwa sekunde chache kabla ya kutua.
Chanzo cha picha, NASA/JPL-Caltech
Maelezo ya picha, Chombo hicho kilipiga picha ya kwanza ya rangi ilipokua katika safari yake ya pili. Ndege hiyo ndogo ilipaa kidogo kwa karibu mita 5 (futi 16), kabla ya kurejea katika eneo iliyoanzia. Njia iliyopitiwa na chombo hicho na kivuli chake zinaonekana katika ardhi (Matian) iliyo chini.
Chanzo cha picha, NASA/JPL-CALTECH
Maelezo ya picha, Kifaa hicho kilipiga picha kilipokuwa katika safari yake ya tatu. Wakati huo helikopta hiyo ndogo ilikuwa umbali wa karibu mita 85 kutoka kwa roboti huku ikiruka urefu wa mita 5(futi 16).
Chanzo cha picha, NASA/JPL-Caltech
Maelezo ya picha, Mei 7, chombo hicho kilifika urefu wa mita 10 kabla ya kupaa mita 129 hadi eneo lingine jipya.
Chanzo cha picha, NASA/JPL-Caltech
Maelezo ya picha, Chombo hicho kilicho na uzani wa tani moja ikiwa imebeba vifaa vya kukusanya maelezo kuhusu jiolojia ya Mars, hali ya hewa na mazingira yake.
Chanzo cha picha, NASA/JPL-Caltech/ASU
Maelezo ya picha, Chombo hicho pia kina kifaa ambacho kimeundwa kukusanya data kuhusu jiolojia ya sayari hiyo. Wakati ikichunguza jiwe hili la senti mita 15, kifaa hocho kiliacha alama zinazoonekana kwa mbali.
Chanzo cha picha, NASA/JPL-Caltech/ASU
Maelezo ya picha, Chombo hicho pia kina kamera tofauti. Picha hii ilipigwa kupitia ''jicho la kulia'' la kamera ya Mastcam-Z ambayo inatoa muonekano sawa na ule wa jicho la mwanadamu.
Chanzo cha picha, NASA/JPL-Caltech/ASU
Maelezo ya picha, Picha hii ilipigwa kwa kutumia kamera ya kushoto na ilichaguliwa kupitia kura ya wasomaji kutumiwa kama ''picha ya wiki'' katika wiki ya sita ya chombo hicho katika sayari ya Mars.
Chanzo cha picha, NASA/JPL-Caltech/ASU/MSSS
Maelezo ya picha, Picha hii inaonesha Santa Cruz, mlima uliyo karibu maili 1.5( 2.2km) kutoka kwa chombo hicho. Muonekano wote uko ndani ya ardhi ya Jezero; ukingo wa sehemu inayoweza kuonekana katika upeo wa macho zaidi ya kilima.
Chombo hiki kina ufadhili wa awali wa kufanya kazi kwa mwaka mmoja wa Mars, tariban miaka miwili ya Dunia.