Love Has Won: Familia yaomboleza kifo cha kiongozi wa kiroho aliyeongoza dhehebu lenye imani ya ajabu

Ilikuwa ni siku ya Jumatano usiku wakati mkuu wa polisi wa Kaunti ya alilpomtaka afisa wa polisi Koplo Steven Hansen kuchunguza ripoti ya kifo.

Mwili wa marehemu , aliambiwa ulikuwa umepatikana kwenye nyumba moja iliyokuwa katika eneo la mbali karibu na mlima wa Moffat, unaokaliwa na watu wapatao 100.

Katika kipindi cha saa kadhaa, aliamua kutekeleza kazi aliyopewa kulingana na kibali na hivyo kuisaka nyumba alikoelekezwa kulikuwa na mwili. Alichokiona ndani ya nyumba ile kilikuwa ni cha kutisha.

Katika moja ya vyumba vaya kulala vya nyumba ile kulikuwa kumetengenezwa kaburi ambalo Bw Hansen analielezea kuwa mlikuwemo mwili uliokuwa umenyofolewa viungo ulionekana kuwa ni wa mwanamke.

Ukiwa umewekwa kwenye kitanda, mwili wa mwanamke huyo ulikuwa umefungwa ndani ya karatasi ya plastiki na kuzingirwa na mishumaa na taa za vimulimuli za Krismasi, huku ukiwa umepakwa vipodozi vya kumetameta vilivyozingira macho yake.

Mwili huo unaaminiwa kuwa ulikuwa ni wa Amy Carlson, kiongozi wa kiroho mwenye umri wa miaka 45 aliyeongoza vuguvugu la kiimani linalojiita Mapenzi yameshinda( Love Has Won), kikundi cha kidini kilichoelezewa kama dini ya kishetani na polisi pamoja na wakosoaji wake.

Kuhakikisha hilo, polisi alihitaji kuhesabu rekodi ya meno yake, kwasababu mwili ukikuwa umeoza sana, hakuweza kupata alama za vidole. Anaamini kuwa huenda mwanamke huyo alikuwa ameuawa tangu mwezi Machi.

Huku kukiwa hakuna ushahidi kuwa aliuawa, wajumbe saba wa vuguvugu la Love Has Won walikamatwa katika nyumba hiyo na kushitakiwa kwa kutumia vibaya mwili wa mfu.

"Sijawahi kuona kikundi cha watu ambacho kinaishi na maiti bila kuwa na wasi wasi wowote ," Polisi Hansen aliviambia vyombo vya habari vya Corolado.

Hakuna lolote kati ya haya lililoishangaza familia ya Carlson, ambayo iilikuwa na uhakika wa mwili wa wake

"Tulifahamu kuwa hakuwa mtu ambaye hakuwa na makosa katika hali yote hii, kwasababu aliamua kujiunga na kikundi hiki cha imani ya kiajabu," dada yake mdogo Carlson ,Chelsea Renninger, aliiambia BBC. "Lakini wakati huo huo, hastahili kufanyiwa kile alichofanyiwa katika mwisho wake. Hakuna binadamu anayestahili hayo ."

Kwa miaka, Bi Renninger alikuwa na uhakika kuwa uongozi wa dada yake wa kiroho wa kikundi cha Love Has Won ungeishia katika kifo.

Machache sana yanajulikana kuhusu asili ya kikundi cha Love Has Won, ambacho kinaaminiwa kuibuka katika miaka ya 2000 chini ya kikundi kingine.

Mfuasi wake mmoja alimshawishi Bi Carlson kujiunga na vuguvugu lao, na hivyo kufungua njia yay eye kuwa kiongozi wa Love Has Won. Wafuasi wake wanaonekana kutokuwa na imani inayojulikana.

Badala yake, hutoa mahubiri kuhusu theolojia isiyo na mwelekeo inayohusisha falsafa ya nyakati mpya, dhana potofu, na ibada ya mesia.

Mesia wao alikuwa ni Bi Carlson aliyefahamika kama "Mama mungu ".

Mafundisho yake yalikuwa matakatifu, na madai yake yalikuwa hata ya kiajabu kuliko cheo chake. Alijiita ''Yesu Kristo'' katika moja ya maisha yake ya miaka 534 iliyopita, aliweza kutibu saratani, angeweza kunena na roho ya mchezaji filamu wa zamani Robin Williams, alikuwa anadai hivyo mara kwa mara.

Madai haya yasiyo ya kweli yalienezwa na kuamniwa miongoni mwa waamini wa dhehebu hilo nchini Marekani na maeneo mengine dunaini kupitia matangazo ya moja kwa moja ya mtandao wa YouTube. Katika video hizi, wafuasi wa Bi Carlson wanaomba msaada kwa ajili ya kiongozi wao.

Katika kamera, wafuasi wanaonekana kuridhishwa na maisha yao.

Katika waraka wa kesi kuhusiana na mauaji yake, ambao BBC imeuona, Ofisi ya mkuu wa polisi ilisema ili "pokea malalamiko mengi kutoka katika familia za watu nchini Marekani wakisema kuwa kikundi hicho kinawalaghai watu na kuwaibia pesa ".

Hakuna hata mmoja katika kikundi hicho, ambaye wavuti wake unaweza kufikiwa, hawakuweza kuhojiwa.

Ukugrasa wa Facebook wenye uhusiano na kikundi cha Love Has Won haukujibu ombi la kutaka waelezee kisa hiki .

Mmoja wa watot watatu wa Bi Carlson, Cole Carlson, alisema kuwa yalikuwa ni madai ambayo yalimuumiza zaidi.

Walikuwa ni sehemu ya sababu ya Bw Carlson, 25, ya kujitenga kwa kiasi kikubwa na mama yake kwa kipindi kikubwa cha maisha yake.

"Maisha yangu ni ya kawaida, kuliko ukweli kwamba mama yangu aliondoka na kujiunga na dhehebu la ajabu," Bw Carlson aliiambia BBC.

Alikuwa na umri wa miaka 12 wakati mama yake, aliyekuwa mfanyakazi wa zamani wa kampuni ya McDonald kutoka Texas, alipoamua kufuata njia yake ya kiimani. Sauti yake ilisikika kutetemeka alipoelezea vile alivyobaini maisha aliyoyaingia mama yake katika kikundi hicho cha kiimani.

Alikuwa amepanga kwenda Krismas kuwa na familia yake iliyoko Houston pamoja na mama yake, baba yake akamwambia kile kilichotokea. Mama yake alikuwa ameenda na kuwaacha watoto wake- akiwemo mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka miwili-chini ya uangalizi wa baba yake.

Licha ya kumbukumbu ya kusikitisha, Bw Carlson anasema alimpenda mama yake sana.

"Hakuwa mama bora, hata alipokuwa akiishi na sisi.

Lakini nilimpenda sana,"Bw Carlson, ambaye anaishi na kusomea baiolojia katiuka chuo cha Portland, Oregon alisema.

Hakukuwa na ukosefu wa upendo katika maisha Bi Carlson, anasema dada yake Bi Renninger. Walikuzwa katika mazingira mazuri na wazazi waliowapenda mjini Dallas.

Shuleni, Bi Carlson alikuwa ni mwanafunzi wa kupata alama-A na kiongozi wa kwaya akiwa na sauti tamu kama ya malaika. Ni tu baada ya kuanza kuwa mtu mzima ambapo alianza kuongea na watu wasiojulikana kwenye intaneti, ambapo alianza kuonesha maisha tofauti ya kiroho.

Alipoondoka nyumbani kuishi na watu hao wasiojulikana, wengi miongoni mwa watu wa familia yake hawakuwahi kumuona wala kuzungumza naye tena.

Familia yake inasema ilijaribu sana kumsaidia mara nyingi lakini haikufanikiwa. Hata waliwahi kumuomba mtangazaji wa kipindi cha mazungumzo cha telebvisheni ya CBC Dr Phil, ambaye alimhoji Bi Carlson na wafuasi wake katika mahojiano ya televisheni mwaka jana.Lakini haikusaidia. Alisalia kuwa katika vuguvugu hilo mpaka mwisho wa maisha yake.

Mazingira ya kifo chake bado yanachinguzwa.

Wiki iliyopita, mwendesha mashitaka alisema anapanga kuwasilisha mashitaka makubwa ya uharibifu mkubwa wa mwili dhidi ya watu saba waliokamatwa kuhusiana na kifo cha Bi Carlson.

Watu hao saba walikuwa wakiishi katika nyumba ya Miguel Lamboy, mtu anayeshukiwa kuwa mjumbe wa kikundi cha Love Has Won, ambako mwili wa Carlson ulipatikana tarehe 28 Aprili.

Mwili ulikuwa katika hali mbaya, ukiwa na ngozi ya rangi ya kijivu, ukiwa hauna macho, na meno yalikuwa yametoka nje ya mdomo, Lamboy aliiambia Polisi.

Melezo ya kutisha kuhusu mwili huo yameishitua familia ya Carlson na wakatoa wito wa kufahamika kwa hatma za mesia wengine -Kuanzia Shoko Asahara na David Koresh, hadi Charles Manson na Jim Jones.

Maisha yao yanapaswa kusaidia kama njia ya kumfanya yeyote anayefikiria kujiunga na kikundi hiki ajiahadhari na kikundi hiki cha imani cha ajabu, mama yake Carlson, Linda Haythorne, aliiambia BBC.

"Ingawa alifanya mambo mabaya, bado alikuwa ni binadamu ,"alisema. "Ninataka kutuma ujumbe kwa watu kuwa kikundi hiki cha kiimani ni hatari na natumai, tunamsaidia mama mwingine, dada au mtoto ."