Thomas Sankara na Patrice Lumumba: Mashujaa waliouawa katika hali za kutatanisha

Thomas Sankara in 1986

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Thomas Sankara waliripotiwa kuwa rafiki na majirani zake Ghana

Hatua ya jopo la majaji wa mahakama ya kijeshi kwamba rais wa zamani wa Burkina Faso Blaise Compaoré, anafaa kushtakiwa kwa mauaji ya mtangulizi wake Thomas Sankara, kiongozi ambaye Compaore alimpindua mwaka wa 1987, imefungua matumaini ya uwezekano wa kupatikana kwa haki kuhusu mauaji yake .

Bw Compaoré alilikimbia kwenda mafichoni mwaka wa 2014 baada ya kufeli katiaka jaribio lake la kutaka kubadilisha sharia ili kuendeleza muda wake madarakani .Waranti ya kukamatwa kwake ilitolewa mwaka wa 2015 .

Mahakama hiyo ya kijeshi imesema jumanne kwamba rais huyo wa zamani anafaa kushtakiwa kwa 'kushambulia asasi za usalama wa kitaifa ,kuhusika na njama ya mauaji ya Sankara na kuuficha mwili wake'

T-shirts (L) reading President Thomas Sankara, already 20 years, and Che Guevara (R) are pictured on 14 October 2007 in Ouagadougou on the eve of the 20th anniversary of the assassination of Burkina Faso's former President Thomas Sankara

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Sankara alifananishwa na Guevara Che Guevara (kulia)

Sankara, ambaye huitwa kuwa 'Che Guevara wa Afrika alipendwa sana katika nchi yake na kote barani Afrika . Uamuzi huo wa korti ya kijeshi umtarejesha tena katika mijadala mauaji Sankara na kiongozi mwingine wa bara la Afrika - Patrice Lumumba aliyekuwa na umaarufu kama wake miaka ya 60 huko DR Congo .Je,Ni nani aliyehusika na mauaji ya viongozi hao wawili ambao wanatajwa kuwa mashujaa wa bara hili na katika hali gani?

Thomas Sankara wa Burkina Faso

Marehemu rais wa Burkina Faso, Thomas Sankara - shujaa kwa vijana wengi wa Kiafrika katika miaka ya 1980 - amebaki katika kumbukumbu za wengi tangu alipouawa akiwa na umri wa miaka 37 .

Julius Malema in Johannesburg, South Africa - 29 April 2014

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Nchini Afrika Kusini, wakati wa uchaguzi Julius Malema kalivaa kofia yake nyekundu ya kijeshi iliyotambulika kama sehemu ya vazi maarufu la Sankara.

Wengi hadi sasa wanamuenzi Sankara kwa njia mbali mbali wakiwemo mwanasiasa wa Afrika kusini Julius Malema kupitia kofia yake nyekundu ya kijeshi iliyotambulika kama sehemu ya vazi tajika la Sankara.

Akisifiwa na wafuasi kwa uadilifu wake na kiongozi asiye na ubinafsi, nahodha wa jeshi na mwanamapinduzi anayepinga ubeberu aliongoza Burkina Faso kwa miaka minne kutoka 1983

Lakini anaonekana na wengine kama mtu aliyeingia madarakani kupitia mapinduzi na kuthamini nidhamu juu ya haki za binadamu.

Sankara alikuwa mtetezi mkali wa vitu vyote vilivyokuzwa nyumbani - kama pamba - lakini bado tasnia ya nguo za Kiafrika ilishindwa kumfanya kuwa nembo ya T-shati.

Ingawaje Sankara anaweza kuwa sio nembo ya mapinduzi, kama Che Guevara mzaliwa wa Argentina, teksi nyingi kote Afrika Magharibi zina stika ya picha yake kwenye vioo vya bagari yao .

Ushawishi wake hata baada ya kifo unaweza kutambulika hata katika nchi za mbali na Afrika Magharibi kama vile Afrika kusini .

Uwezekano wa kushtakiwa kwa Compaoré, kwa mauaji yake huenda ukamaliza jitihada za muda mrefu za wafuasi wake kupata haki .

Mnamo Disemba tarehe 7 mwaka wa 2015 aliyeongoza mapinduzi ya septemba mwaka huo jenerali Gilbert Diendere alishtakiwa kwa njama ya mauaji ya Sankara .Alikuwa ndiye afisa wa ngazi ya juu kushatakiwa kwa mauaji ya Sankara .

Rais Sankara aliuawa na kikundi cha wanajeshi lakini hali kamili iliyozingira mauaji yake bado haijulikani .

Uchunguzi wa maiti yake uligundua kwamba mwili wake ulikuwa umechanika kwa ajili kupigwa risasi ,wakili wa familia yake alisema.

Blaise Compaore alikuwa rais wa Burkina Faso kuanzia mwaka 1987 hadi 2014

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Blaise Compaore alikuwa rais wa Burkina Faso kuanzia mwaka 1987 hadi 2014

Nafasi yake kama rais ilichukuliwa na Blaise Compaore ambaye alisalia madarakani kwa miaka 27 kabla ya kuondolewa madarakani na waandamanaji mwaka wa 2014

Jenerali Diendere, ambaye baadaye alihudumu kama mkuu wa ujasusi wa Compaore alionekana kuwa mtu wa karibu sana na Sankara wakati wa mauaji yake .

Inaripotiwa alishirikiana kwa karibu na mashirika ya ujasusi ya Marekani na ufaransa na kusaidia kuachiliwa kwa mateka kutoka mataifa ya nchi za magharibi waliokuwa wakishikilia mara kwa mara na makundi ya kijihadi huko Afrika Magharibi .

Patrice Lumumba wa DR Congo

Waziri mkuu wa kwanza wa Congo aliyechaguliwa alikuwa Patrice Lumumba ambaye muda ,mfupi baadaye alikabiliwa kuvunjika kwa utaratibu na utiifu wa sheria. Kulikuwa na uasi wa jeshi wakati vikundi vya kujitenga kutoka mkoa wenye utajiri wa madini wa Katanga wakifanya harakati zao na wanajeshi wa Ubelgiji walirudi, ikidaiwa walikuwa wamekuja kurejesha usalama.

A picture taken in December 1960, shows soldiers guarding Patrice Lumumba

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Patrice Lumumba alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Congo mwaka 1960, baada ya uhuru

Lumumba alichukua hatua mbaya - aligeukia Umoja wa Kisovyeti kwa msaada. Hii ilileta hofu huko London na Washington, ambao waliogopa Wasoviet watapata nafasi katika Afrika kama vile walivyofanya nchini Cuba.

Katika Ikulu ya White House, Rais Eisenhower alifanya mkutano wa Baraza la Usalama la Kitaifa katika msimu wa joto wa 1960 ambapo wakati mmoja alimgeukia mkurugenzi wake wa CIA na kutumia neno "kuondolewa" kwa kile alichotaka kifanyiwe Lumumba.

CIA ilianza kufanya kazi. Ilikuja na mipango kadhaa - pamoja na kikosi maalum na dawa ya meno yenye sumu - ili kumwua kiongozi huyo wa Congo. Hayakufanyika kwa sababu ajenti wa CIA aliyekuwa Congo , Larry Devlin, alisema alikuwa anasita kuitekeleza mipango hiyo .

Lakini mnamo Januari 1961, Lumumba alikuwa amefariki.

Je, Uingereza na Marekani zilihusika na mauaji yake ? Sio moja kwa moja. Lumumba Aliendelea kukimbia, alikamatwa na kukabidhiwa kwa serikali mpya ambayo wlaijua fika kwamba ingemuua

Muaji yake yanadaiwa kutekelezwa na wapiganaji kutoka Congo pamoja na Wabelgiji na kwa usaidizi wa serikali yao ambayo ilimchukua sana .Hadi leo mauaji ya Lumumba yameghubikwa na taarifa nyingi na ukweli wa kilichotokea huenda hautajulikana hivi karibuni.

Unaweza pia kusikiliza:

Maelezo ya sauti, Ni kwanini jina la Patrice Lumumba Ubelgiji, limezusha hasira DRC