Uimara wa jeshi wa nchi 10 zenye watu wengi zaidi duniani

Kufikia mwaka 2021, China imeweka rekodi kwa kuwa na vikosi vingi zaidi duniani, miongoni mwa nchi zenye vikosi vingi ni pamoja na India, Marekani na Urusi.

Lakini pia ni muhimu kujua kwamba uimara wa jeshi la nchi hautathminiwi tu na maafisa waliopo jeshini lakini pia idadi na uimara wa vifaa vya jeshi.

BBC imepigia darubini nchi 10 zenye idadi kuwa ya watu ambazo pia jeshi lake ni imara kupitia data za tovuti ya Global Fire Power GFP ambayo inafuatilia usalama wa dunia.

China

Ni nchi yenye idadi kubwa ya watu duniani ikiwa na jumla ya watu 1,439,323,776.

Inakadiriwa kwamba vikosi vya usalama vya China vimefikia 3,355,000. Tovuti hiyo inasema China ni nchi ya tatu yenye vikosi vya usalama imara zaidi duniani.

India

India ni ya pili yenye idadi kubwa ya watu duniani ambayo ni bilioni 1,326,093,247.

Idadi ya vikosi vya usalama vya India imefikia 5,127,000. Ni vikosi vya nne vya usalama kwa idadi kubwa zaidi duniani,

Marekani

Ni nchi ya tatu yenye idadi kubwa zaidi duniani ikiwa na watu 332,639,102.

Ni nchi yenye vikosi imara zaidi dunianina jumla ya idadi ya wanajeshi wake ni 2,245,500.

Indonesia

Ni ya nne yenye idadi kubwa ya watu ya 267,026366.

Vikosi vya usalama vinakadiriwa kuwa 1.080,000 na ni nchi ya 16 kwenye orodha hiyo.

Pakistan

Ina jumla ya idadi ya watu 223,500,636, na kuifanya kuwa ya tano yenye watu wengi duniani.

Idadi ya vikosi vya usalama ni 1,704,000. Pakistan inaorodheshwa kuwa ya 10 kati ya zile zenye vikosi vilivyo imarika.

Nigeria

Nigeria ina idadi ya watu 214,328,302. Hii inafanya kuwa nchi ya sita yenye watu wengi zaidi duniani.

Vikosi vyake vya usalama ni 200,000 na ni ya 35 katika orodha ya nchi zenye wanajeshi wengi.

Brazil

Brazil ni nchi ya saba dunia yenye kwa zenye idadi kubwa ya watu ikiwa na idadi jumla ya watu 211,715,973.

Idadi ya vikosi vyake ni 2,074,500. Ni ya 9 kwa nchi zenye nguvu duniani.

Bangladesh

Bangladesh ni nchi ya nane kwa zile zenye idadi kubwa ya watu ikiwa na raia milioni 162,650,853.

Idadi ya vikosi vyake ni 7,004,000. Inaorodheshwa ya 45 katika nchi zenye vikosi imara vya usalama.

Russia

Urusi ni ya tisa ikiwa na idadi ya watu 141,722,205. Idadi ya wanajeshi wake ni 3,569,000.

Ni nchi ya pili kwa vikosi vya usalama imara zaidi duniani baada ya Marekani.

Mexico

Idadi ya watu nchini Mexico ni milioni 128,649,565.

Idadi jumla ya wanajeshi wake ni 417,000. Inaorodheshwa kuwa ya 46 katika orodha ya nchi zenye vikosi imara.