Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Uvaaji wa barakoa na kutosogeleana kwa watu 'kunaweza kudumu kwa miaka '
Watu wanaweza kuhitaji kuvaa barakoa na kukaa mbali hadi tutakaporejea katika hali ya ya kawaida, amebashiri Mary Ramsay, mtaalamu anayeongoza wa magonjwa yanayoambukiza nchini Uingereza.
Mary Ramsay, ambaye ni mkuu wa kitengo cha chanjo katika wizara ya afya ya umma nchini Uingereza, amesema kuwa hatua hizo za kimsingi za kudhibiti maambukizi zinaweza kuendelea kuwepo hadi pale nchi zote zitakapofanikiwa katika utoaji wa chanjo kwa watu wake.
Amesema pia kwamba kurejea kwa matamasha makubwa kunahitaji ufuatiliaji wa makini na maagizo ya wazi kuhusu usalama wa watu.
Waziri wa ulinzi hajazuia safari za mapunziko za watu katika mataifa ya kigeni baada ya kupigwa marufuku.
Ben Wallace amemwambia mwandishi wa kipindi cha BBC One Andrew Marr hatahivyo kwamba kupanga safari za nje ya nchi za mapumziko kwa sasa litakuwa ni jambo la "mapema sana " na lenye "uwezekano wa hatari".
Uingereza imeweka rekodi nyingine ya idadi ya watu waliopata dozi za chanjo ya vortusi vya corona kwa kuwachanja watu 844,285 kwa siku moja tu ya Jumamosi.
Dkt Ramsay amesema kuwa sheria kama vile kuvaa barakoa katika ameneo yenye umati wa watu na kukaa mbali imekubaliwa na wengi na zinawawezesha watu kuendelea na shughuli zao za kiuchumi.
Amesema "wamezoea sasa viwango vya chini vya maagizo ya kukabiliana na maambukizi, na watu wanaweza kuishi nazo, na uchumi unaweza kuendelea huku watu wakitekeleza hizo sheria".
"Kwahiyo ninadhani kwa miaka michache, walau mpaka maeneo mengine ya dunia yachanjwe vyema kama ilivyo kwetu, hapo ndipo tunaweza kurejea taratibu katika hali ya kawaida ," aliongeza.
Alitahadharisha kuwa ni "muhimu sana kwamba watu wasilegeze hatua za kujikinga na maambukizi haraka sana ",Dkt Ramsay amesema kuzunguka kokote kwa virusi kunaweza kuwadhuru walio katika hatari ya kupata maambukizi hayo.
"Tunapaswa kuangalia kwa uangalifu sana kabla ya kuondoa sheria yoyote ya kukabiliana na corona ,"alisema.
Profesa Chris Whitty, Msahuri wa mkuu wa masuala ya tiba wa Serikali ya Uingereza , aliwaambia wabunge wa nchi hiyo wiki hii kwamba inatumainiwa kuwa "matumizi ya hatua rahisi kama vile kunawa mikono, kuvaa barakoa pale inapofaa, kupima na kuwatafuta waliokutana na wwenye maambukizi, na zaidi ya hayo chanjo " kutadhibiti virusi hata baada ya msimu wa kiangazi.
Sir Patrick Vallance, mshauri mkuu wa masuala ya sayansi, pia amesema kuwa barakoa zinaweza kuhitajika katika hali fulani kama idadi ya maambukizi itaongezeka katika majira ya baridi, lakini inawezekana kwamba watu watakuwa na mienendo ambayo itawawezesha kutokaribiana.
Kikundi cha wasahuri wa serikali wa masuala ya kisayansi kilisema mwezi uliopita kwamba "kuendeleza sera za kimsingi zinazopunguza maambukizi "kutakuwa muhimu katika kipindi fulani kijacho.
Wataalamu hao walisema kuwa sera hizo ni pamoja na kuendela kuwapima watu na kuwatafuta waliokutana na waliopata maambukizi, kujitenga binafsi kwa wenye maambukizi na ujumbe wa umma unowashauri watu kuchukua " hatua za kujitolea wenyewe kupunguza hatari za maambukizi ".
Unaweza pia kutazama:
Mpango wa serikali wa kulegeza sheria ya kukaa nyumbani ''lockdown'' au ukomo wa watu kuwa pamoja itaondolewa nchi Uingereza sio kabla ya tarehe 21 Juni.
Katika sheria za pili zitakazotangazwa Jumatatu tarehe 29 Machi, watu hadi watano wataweza kukutana nje ya nyumba zao katika kurejea kwa kile kilichoita "sheria ya sita".
Taarifa zaidi kuhusu corona:
Michezo ya maeneo ya wazi na maeneo ya burudani pia vinawza kufunguliwa, michezo ya maeneo ya wazi iliyopangwa pia itaruhusiwa tena , makundi ya wazazi na watoto wao wataruhusiwa kukutana tena wakiwa sio zaidi ya watu 15.
Katika Scotland, inbada za kijamii zitafunguliwa tena tarehe 26 Machi. Wales Maduka ya bidaa mbalimbali supermarkets yanaweza kuuza bidhaa muhimu kuanzia Jumatatu, na vituo vya bustani za umma vinaweza kufunguliwa. Na Katika Ireland Kaskazini, watu sita kutoka nyumba moja wanaweza kukutana katika bustani ya kibinafsi kuanzia Aprili Mosi.