Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kifo cha Rais John Pombe Magufuli: Salamu za rambirambi zaendelea kumiminika kufuatia kifo cha rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
Salamu za rambirambi zinaendela kutolewa kufuatia kifo cha Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Kilichotangazwa usiku wa Jumatano na Makamu wake Samia Hassan Suluhu.
Bi Samia amesema, Rais Magufuli amefariki dunia katika hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es Salam mwendo wa saa kumi na mbili jioni saa za Afrika Mashariki kutokana na matatizo ya moyo.
Kufuatia taarifa ya kifo hicho viongozi na watu mbalimbali wamekuwa wakitoa salamu za rambirambi.
Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi kupitia mtandao wa Twitter ameelezea masikitiko yake kufuatia kifo hicho:
Kiongozi wa upinzani wa chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania Bw. Zitto Kabwe amesema pia amezungumza kwa njia ya simu na Rais -Mteule wa Tanzania Samia Suluhu na kumtolea salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Rais John Pombe Magufuli:
Mbali na Tanzania viongozi wa Mataifa mbali mbali wameelezea kusikitishwa na kifo cha Rais Magufuli. Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo Felix Tschisekedi kupitia ukurasa wa Twitter wa Ofisi ya rais DRC amesema amehuzunishwa na kifo hicho:
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Domic Raab ameeleza pia kusikitishwa kwake na kifo cha Rais Magufuli, akisema anajiunga na wapendwa wake pamoja na watu wote wa Jumuiya ya Madola:
Aidha Rais wa Somalia Mohamed Farmaajo pia ametoa salamu za rambirambi kwa niaba ya raia wa Somalia kufuatia kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli:
Mbali na viongozi mbalimbali, watu binafsi wameelezea masikitiko yao kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, hizi ni baadhi ya jumbe za Twitter zilizotumwa na watu binafsi: