Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Hatari wanayokabiliana nayo walinzi wa sokwe katika mbuga ya wanyama ya Virunga DRC
Kulinda mbuga ya kitaifa ya Virunga Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - ambayo ni makazi ya sokwe wa milimani - imetajwa kuwa kazi ngumu sana duniani.
Katika kipindi cha miezi 12 iliopita, zaidi ya wafanyakazi 20 wameuawa - na wiki iliyopita waasi walilaumiwa kwa kumuua balozi wa Italia nchini DR Congo, pamoja na mlinzi na dereva wake katika shambulio lililofanywa ndani ya mbuga hiyo.
"Kiwango cha kujitolea ambacho kinahusika katika kuendeleza kazi hii ni kikubwa sana," anasema Emmanuel de Merode, msimamizi mkuu wa zaidi ya walinzi 800 wa Virunga, mbuga ya kitaifa kongwe zaidi barani Afrika.
Mbuga hiyo ilibuniwa karibu miaka 100 iliyopita kuwalinda sokwe wa milimani, ambao idadi yao imeongezeka katika kipindi cha miongo kadhaa iliyopita, ijapokuwa ni 1,000 tu waliosalia duniani.
Bw. De Merode ameishi DR Congo kwa karibu miaka 30, lakini bado anakumbuka siku alipofika nchini humo mara ya kwanza.
"Nilinunua pikipiki mjini Kampala na kuiendesha kutoka Uganda hadi Congo, na unapovuka mpaka moja kwa moja unakaribishwa ukubwa wa mbuga hii na mandhari ya kupendeza ajabu."
Bw. De Merode, alizaliwa Afrika Kaskazini na kulelewa Kenya, lakini ni mwanamfalme wa Ubelgiji ijapokuwa hatumii cheo chake.
IMAGE COPYRIGHTGETTY IMAGES
Anaonekana mtulivu licha ya changamoto zinazomkabili yeye na wafanyakazi wake kila siku.
Mashambulio mawili mabaya katika muda wa mwaka mmoja uliopita umewatikisa wote vibaya sana:
- Mwezi Aprili mwaka jana,walinzi 13 waliuawa katika kile maafisa wa mbuga hiyo walisema yalikuwa ''makabiliano makali'' kati yao na kundi lililojihami.
- Mwezi Januari mwaka huu, walinzi sita, waliokuwa wakishika doria ndani ya mbuga hiyo waliviziwa kuuawa na wanamgambo. Wote walikuwa na umri wa kati ya miaka 25 na 30.
"Inasikitisha sana kupoteza vijana wengi wadogo wakati mmoja," anasema mmoja wa walinzi Gracien Muyisa Sivanza, ambaye ni msimamizi wa maziwa ya mbuga hiyo.
"Walinzi wenzangu waliouawa walipenda sana kazi yao na walijitoa mhanga katika juhudi za kuhifadhi mazingira."
Lakini anasema vifo hivyo vimewapa motisha ya "kuendelea na juhudi hizo kwa pamoja… kwa heshima yao.
"Nadhani wanajivunia jinsi tunavyowawakilisha."
Bw. De Merode pia aliwahi kupigwa risasi na kujeruhiwa mwaka 2014.
"Lazima ukubali kwamba [kuna hatari. Ni mbuga ya kitaifa ambayo ni sehemu ya nchi ya Congo iliyoathiriwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe katika historia yake ya hivi karibuni ," anasema.
'Tumeleta uhai mbugani'
Lakini pia ameangazia ufanisi uliopatikana katika mbuga hiyo licha ya changamoto zinazowakabili.
"Tumekuwa na panda shuka nyingi… tumeathirika sana, lakini changamoto hizo zimesaidia mbuga hii kuwa hai."
Shambulio dhidi ya Bw. De Merode lilikuja wakati kulikua na vurugu zilizosababishwa na wanamgambo wa M23 katika eneo hilo. Wakati huo pia , kampuni ya mafuta ya Uingereza inayojulikana kama Soco ilikuwa imepewa idhini na serikali ya Kinshasa kuchimba mafuta katika ardhi ya buga.
Hali tete iliyoshuhudiwa katika eneo hilo wakati huo iliangaziwa katika filamu ya ya mwaka 2014 kuhusu Virunga ambayo iliteuliwa katika tuzo za Oscar.
"Tunapigana dhidi ya kampuni ya mafuta ya Uingereza … tulikuwa tukikabiliana na watt kadhaa. Siku hiyo, Nilikuwa nimewasilisha ripoti ya uchunguzi kuhusu shughuli za kampuni hiyo ya mafuta."
Alishambuliwa alipokuwa akiendesha gari peke yake kupitia msitu huo kurudi nyumbani: "Nilipigwa risasi ya kifua na tumbo."
Mlinzi wa mbuga Rachel Masika Baraka aliuawa mwaka 2018 baada ya watalii wawili wa Uingereza kutekwa nyara.
Kampuni hiyo Mililani shambulio hilo na kukana kuhusika nalo. Tangu wakati huo ilibadili jina lake na kujiondoa DR Congo .
Bw. De Merode anasema alikua na "bahati".
"Watu kutoka kijiji kimoja walinisaidia, kwa hio juhudi zangu zinaendelea kutokana na usamaria wao. Baadhi ya wafanyakazi hawana bahati."
Watu wanapofariki wakitekeleza amri yake katika mbuga hiyo, anasema "inaniacha na majonzi kupita maelezo kwani siwezi kuelezea familia zao mazingira ya vifo hivyo".
Inakadiriwa kuwa makumi ya makundi ya wanamgambo waliojihami kwa silaha wanajikimu kutokana na raslimali za mbuga hiyo kupitia shughuli za- uwindaji haramu, kukata miti na kuuza mbao au kuuza mafuta.
Raslimali asili ya DR Congo imezozaniwa kwa miongo kadhaa. Nchi hiyo ambayo ukubwa wake ni eneo la magharibi mwa Ulaya - ina utajiri mkubwa wa madini, ikiwa na almasi, mafuta, cobalt na shaba, kuliko mahali pengine popote duniani.
IMAGE COPYRIGHTAFP
image captionVirunga's Mount Nyiragongo is an active volcano - seen here in the distance - last erupting in 2002.
Unaweza pia kusoma:
Baadhi ya mad ini hizo zina muhimu kwa teknolojia ya kisasa, inayounda vitu muhimu katika magari ya umeme na simu za rununu za kisasa.
Virunga pia ina raslimali nyingi asililia na wanyama pori. Lakini watu milioni mbili wanaoishi katika eneo hilo wanaishi kwa chini ya dola 1.50 (£1.08) kwa siku.
Dola zinazotokana na Utalii
Mzozo unaokumba eneo hilo Sio mambo la kushangaza kwa Bwana De Merode amabaye anachukulia kulinda mbuga kama suala la haki ya kijamii.
"Tatizo sio kama dogo kama suala dogo kama kulinda sokwe na tembo; bali ni kupata ufumbuzi wa changamoto ya kiuchumi ambayo imekuwa chanzo cha vita vya wenyewe kwa wenyewe katika historia," anasema.
"Zaidi ya Wacongo milioni saba wanaaminiwa kufariki katika kipindi cha miaka 30 kutokana na mzozo wa kiuchumi.
"Tunaamini kwa Virunga kupata ustawi, kwanza lazima tutilie maanani maslahi ya wakazi. Lazaima tufanye mbuga hii kuwa mali… ili tuweze kupata faida."
Anatoa mfano na nchi jirani ya Rwanda ambayo kabla ya janga la corona ilikuwa na uwezo wa kukusanya dola milioni 500 kwa mawaka kutokana na shughuli za utalii. Nchini Kenya thamani ya septa ya utalii ni karibu dola bilioni 3.5.
"Hiyo ni zaidi ya bajeti ya kitaifa ya DR Congo," anasema akiongeza kuwa: "Utalii sio mchezo, ni sekta ambayo inahitaji mikakati. Tunahitaji kutafuta mbinu ya kuzalisha mali bila kuharibu mbuga''.