Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Joe Biden aruhusu ufadhili kwa wanaotoa huduma za uavyaji mimba na kupanua bima ya afya ya Obamacare
Rais wa Marekani Joe Biden ametengua marufuku ya ufadhili wa fedha ambazo zimekuwa zikitumwa katika makundi ya kimataifa ya misaada ambayo husaidia katika suala la kuavya mimba.
Amesema kwamba kukamilika kwa sera ya mji wa Mexico kunatengua hatua ya rais Trump kuwanyima wanawake haki yao ya kiafya.
Barua hiyo inaagiza kubadilishwa kwa sera za enzi ya Trump iliozuia ufadhili katika kliniki za Marekani ambazo hutoa rufaa ya uavyaji mimba. Bwana Biden pia alisaini amri ya kupanua mpango wa bima ya afya ya Obamacare.
"Sianzisha sheria mpya yoyote, ama jambo jipya la sheria," alisema katika ofisi yake mnamo Alhamisi, akijibu kukosolewa kwamba alikuwa akiongoza kwa kutoa amri badala ya kufuata sheria za bunge.
''Hakuna kitu kipya tunachofanya hapa mbali na kurudisha bima ya afya ya bei nafuu ...kama ilivyokuwa hapo awali kabla Trump kuwa rais'', aliongezea.
Je sheria ya kuavya mimba inasemaje kote duniani?
Sera hiyo ya Mji wa Mexico kwa mara ya kwanza ilianzishwa na rais wa Republican Ronald Reagan mwaka 1984 na imekuwa ikiendelezwa na Republicans na kufutiliwa mbali na Democrats.
Kwa miongo kadhaa , Marekani imefutilia mbali fedha zinazotumwa kusaidia kuavya mimba ughaibuni lakini sera hiyo ya mji wa Mexico inaendeleza hatua hiyo.
Inazuia fedha zinazotoka katika majimbo kutopatiwa mashirika yanayotoa huduma ya kuavya mimba , ushauri wa kuavya mimba ama kupigania haki ya kuavya mimba.
Mpango huo ulipanuliwa chini ya uongozi wa rais Trump, ambaye alipiga marufuku fedha zinazoelekezwa katika mashirika yasio ya serikali ambayo binafsi yanatoa ufadhili wa kuavya mimba.
Katika taarifa mapema , Ikulu ya Whitehouse ilisema kwamba Biden alikuwa anatoa amri kama rais kusaidia afya ya uzazi ya wanawake na wasichana na haki zao nchini Marekani pamoja na duniani kwa ujumla.
Ripoti ya ofisi ya uwajibikaji katika serikali ya Marekani iliotolewa mwaka uliopita ilibaini kwamba 2017, mashirika yasio ya kiserikali yalishindwa kupokea takriban $153m (£112m) kwasababu yalikataa kufutilia mbali mipango ya kuavya mimba.
Ripoti hiyo iligundua kwamba mara 54 mashirika hayo yalikataa ufadhili huo kutokana na sera hiyo ya kutakiwa kufutilia mbali sera ya kuavya mimba.
Je ni nini chengine ambacho Biden amefanya kuhusu kuavya mimba?
Bwana Biden pia ameamrisha idara ya afya nchini Marekani kuondoa mara moja masharti ya enzi za Trump kuhusu mpango wa uzazi wa familia kwa raia wa Marekani wanaopokea pato la chini uliojulikana kama Title X.
Hatua ya rais Trump kufutilia mbali mpango wa uzazi wa Title X ulipelekea kuondolewa kwa ufadhili wa mamilioni ya dola kutoka katika vituo vya kiafya ambavyo vinatoa mpango wa uzazi kupitia njia nyengine mbali na uavyaji mimba.
Bwana Biden siku ya Alhamisi pia aliiondoa Marekani kutoka katika maamuzi ya 2020 kwa jina Geneva Consensus, makubaliano yasiolazimisha kati ya mataifa 30 ambayo yanapinga uavyaji mimba.
Ni nini kinachoendelea na bima ya afya ya Obamacare?
Bwana Biden siku ya Alhamisi alitia saini amri kufungua tena sheria ya afya ya bei nafuu - inayojulikana kama Obamacare kwa miezi mitatu.
Chini ya utawala wa rais Trump sheria hiyo ilitumika kwa wiki sita huku wanachama wa Republican wakijaribu kuondoa mpango huo wa afya.
Bwana Joe Biden amesema kwamba kutokana na mlipuko wa virusi vya corona , huu ndio wakati kwa raia kuweza kupata mpango wa afya ulio bei nafuu.