Mzozo wa Ethiopia: Picha za kupotosha kuhusu mzozo wa Tigray zahakikiwa

    • Author, Peter Mwai
    • Nafasi, BBC Reality Check

Mamia ya watu wameripotiwa kuuawa katika mapigano ya wiki mbili kati ya vikosi vya Ethiopia na vikosi tiifu kwa utawala wa kisiasa jimbo la Tigray Kaskazini mwa nchi hiyo.

Mzozo unapoendelea kufukuta, kumeshuhudiwa majaribio ya watu kusambaza taarifa za uongo na kupotosha kuhusu hali ilivyo.

Picha haioneshi Waziri Mkuu wa Ethiopia akiwa katika uwanja wa mapigano

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anaonekana akiwa amevalia sare za kijeshi akizungumza kwa simu katika ujumbe uliowekwa Facebook ambao unaunga mkono oparesheni ya majeshi ya Ethiopia katika jimbo la Tigray.

Kuna picha tatu za Waziri Mkuu, ambazo zimesambazwa mitandaoni zaidi ya mara 1,000.

Ziliwekwa mtandaoni kupitia jina la Taye Dendea Aredo, msemaji wa chama tawala katika jimbo la Oromia, lakini kwa kutumia picha ya kutengenezwa.

Picha ilipotafutwa mara nyingine inaonesha picha yake ya kawaida alipokuwa anazungumza kwa simu, ambayo ishawahi kutumiwa awali katika taarifa kuhusu majeshi ya Marekani.

BBC imepata picha halisi iliyooneshwa hapo juu katika hifadhi ya picha zinazomilikiwa na Getty.

Ilipigwa nchini Ukraine mwaka 2017, lakini imefanyiwa ukarabati ili kumfanya askari kuonekana kama Bwana Abiy, na kuongezewa vinyweleo usoni.

Tulipowasiliana na Taye Dendea Aredo kuhusu picha hii, alituambia kuwa hakuitumia lakini hakufafanua jinsi ilivyotumika katika ujumbe huu.

Kanda feki ya video inayoonesha kudunguliwa kwa ndege ya kivita ya Ethiopia

Video inayoonesha ndege ya kijeshi ya Ethiopia ikidunguliwa kabla kuanguka imesambazwa sana mitandaoni kwa madai kwamba ilikuwa ikifanya mashambulio katika jimbo la Tigray.

Lakini video hilo sio halisi, inatoka kwa rekodi ya mchezo wa kuigiza wa video ya kijeshi unaoitwa Arma.

Kuna baadhi ya vita ambavyo vinaashiri video hii sio halisi, kama vile muonekano wa buluu ambao sio wa kawaida, na moshi kutoka kwa ndege kabla ianguke na kutoweka haraka katika eneo lisilojulikana.

Tulibaini kuwa video halishi ilikuwa mchezo wa vita katika kituo cha YouTube cha Japan.

Video inayosambazwa imefanyiwa marekebisho kwa kuondoa sehemu ya mwanzo na mwisho, mahali ambapo kuna iliani iliyotolewa kwa lugha ya Kijapani ikisema video hiyo ni ya maigizo.

Baadhi ya video zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii pia zina picha zinazoonesha upande wa juu wa ndege iliyoshika moto ambayo ni picha halisi, lakini sio kutoka Ethiopia.

Tumebaini kuwa pita hilo ni za ripoti ya mwaka 2016 kuhusu ndege ya jeshi ya Jordan F-16 ambayo ilianguka kutokana na hitilafu ya kimitambo

Picha kutoka kwingine

Kumekuwa na picha kasha za upotoshaji kuhusu mashambulio au athari za mashambulio ambazo ambazo zimekuwa zikisambazwa katika mitandao ya kijamii

Baadhi ya picha hizo ni za kutoka maeneo mengine ulimwenguni na zilipigwa kabla ya mzozo unaoendelea sasa nchini Ethiopia.

1. Ukurasa wa Facebook unaounga vikosi vya serikali umetupia picha kutoka Uzbekistan.

Inaonesha picha ambayo ilipigwa kutoka kwenye ndege angani ikifyatua roketi, na pia imetumiwa na akaunti nyingine za mitandao ya kijamii kuashiria kinachoendelea Tigray.

Lakini uchunguzi wa kina wa picha hiyo unaonesha ina alama ya "Uz Air Force A. Pecchi".

Uz ni ufupisho wa Uzbekistan, na A.Pecchi ni mpiga picha Anthony Pecchi. Mpiga picha huyo aliweka picha hiyo hiyo katika ukurasa wake wa Facebook mwezi Januari mwaka huu.

2. Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wametumia picha za kupotosha kuonesha matokeo ya shambulio lililofanywa na vikosi vya Tigray dhidi ya mji wa Bahir Dar katika jimbo la Amhara, huku wengine wakizitumia kuonesha mashambulio yaliyofanywa na vikosi hivyo dhidi ya Asmara, mii mkuu wa chi jirani ya Eritrea.

Picha inayotumiwa ni ya mlipuko uliyotokea katika bohari ya kemikali katika mji wa bandari wa Tianjin nchini China mwaka 2015.

BBC iliangazia taarifa hiyo na moja kati ya picha iliyotumiwa ni sawa na ile unayosambazwa kuhusu mzozo wa Ethiopia.

3. Ukurasa wa Facebook umeweka video ambayo mwenywe anasema inaonesha shambulio la kombora lililofanywa na na vikosi vya Tigray dhidi ya mji mkuu wa Eritrea, Asmara (ambayo wanadai inasaidia serikali ya Ethiopia katika mzozo- madai ambayo imekanusha).

Kumekuwa na taarifa ya Tigray kushambulia Asmara kwa roketi hivi karibuni lakini picha hizi hazioneshi tukio hilo

Akaunti hiyo ya Facebook iliweka video hiyo katika mfumo ambao uliifanya kujirudia kwa saa mbili kana kwamba ilikuwa tukio mubashara.

Lakini video, ambayo imesambazwa kwa zaidi ya mara 1,000, isiyo ya kutoka Eritrea hata kidogo, ilitolewa katika video ya shambulio la makombora ya Iran dhidi ya kambi ya jeshi ya Marekani nchini Iraq mwezi Januari mwaka huu.