Matokeo ya uchaguzi wa Marekani 2020: kati ya Trump na Biden ni nani anayeweza kushinda kwa urahisi?

Biden and Trump

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni siku ya pili tangu kura za uchaguzi wa Marekani kupigw , na mshindi bado hajaamuliwa.

Huku masunduku ya kupiga kura kutoka kwa zaidi ya raia milioni 160 zikiendelea kuhesabiwa, hatahivyo, kuna picha ambayo inaanza kujitokeza.

Tayari rais Donald Trump amejitangaza kuwa mshindi na kuwashutumu wapinzani wake kwa kuiba kura.

Amechapisha msururu wa jumbe za twitter , ambazo zimedaiwa kupotosha na zisizo na ukwelia akidai kwamba wapizani wake wanaiba kura. Hatahivyo huo si ukweli kufikia sasa. Kuna mamilioni ya kura ambazo zinaendelea kuhesabiwa.

Na sasa Michigan inaelekea upande wa Biden, huku vyombo vya habari vya Marekani vikiwa vinatabiri kwamba atashinda jimbo hilo , kinyanganyiro hicho kinaelekea wakati ambapo kitaamuliwa na majimbo machache yaliosalia-Arizona, Nevada Georgia na Pennsylvania.

Jinsi Biden anavyoweza kushinda

Kufikia sasa Biden amejishindia wajumbe 243 huku Trump akijishindia wajumbe 214, huku wakikaribia kuwa wapangaji wapya wa Ikulu ya White House iwapo watafikia wajumbe 270.

Hivi ndivyo wagombea hao wanapaswa kupata ili kuibuka washindi.

Kwa urahisi , mgombea wa Democrat Joe Biden lazima aendelee kuongoza katika majimbo ya Arizona , Nevada na Wisconsin , majimbo ya buluu katika ramani.

Iwapo atafanya hivyo atafikisha wajumbe 270, ikiwa ndio kiwango cha chini kinachohitajika kwa mgombea kuibuka mshindi.

Katika jimbo la Michigan, Biden alimuongoza Trump mapema wakati kura zinazopigwa kwa njia ya posta zilipoanza kuhesabiwa katika mji wa Detroit ambao una wafuasi wengi wa Democrat , na kufikia majira ya jioni alitarajiwa kuchukua ushindi katika jimbo hilo.

Katika jimbo jirani la Wisconsin, hali katika jimbo hili imeamuliwa kumpendelea yeye. Wanachama wa Republican wanataka kura kuhesabiwa tena.

Biden ameimarisha uongozi wake katika jimbo la Arizona huku kura nyingi zilizopigwa kwa njia ya posta zikiwa bado hazijahesabiwa.

Tofauti katika jimbo la Nevada ni elfu chache za kura lakini ni kura zilizopigwa siku ya uchaguzi ambazo zinaelekea katika kapu la Trump na kura zilizopigwa kupitia njia ya posta ndizo zilizosalia na ambazo zinaelekea katika kapu la democrats.

Kwa sasa Biden anaonekana kuwa katika mwelekeo ambao ni rahisi kuibuka mshindi.

Jinsi Trump anavyoweza kushinda

Kama Biden, ili kusalia katika Ikulu ya Whitehouse anapaswa kushinda majimbo machache yaliosalia ambapo anaongoza.

Iwapo ni Pennsylvania na Georgia majimbo yalio mekundu katika ramani.

Baadaye Republican italazimika kuvuna jimbo moja ambapo Biden anadaiwa kuongoza.

Nevada kuna ushindani wa karibu na sio vigumu kulibadilisha jimbo na kuingia katika kapu la Trump.

La sivyo watapata wajumbe sawa na majdala wa nani mshindi kupelekwa bungeni.